NI UPI USIKU WA LAYLATUL QADR ?
Jamii ya vilivyomo
Vyanzo
Full Description
NI UPI USIKU WA LAYLATUL QADR
Swahili
Imeandikwa na:
Daudi Abubakari
Imepitiwa na :
Abubakari Shabani Rukonkwa
ما هي ليلة القدر ؟
السواحلية
كتبه: دود أبوبكر
المراجع:
أبوبكر شعبان روكونكوا
بسم الله الرحمن الرحيم
Utangulizi:
Hadiyth kadhaa zimetaja kuhusu usiku wa Laylatul-Qadr. Imetajwa kuwa ni katika masiku kumi ya mwisho; siku ya ishirini na moja, au ishirini na tatu, au ishirini na tano au ishirini na saba kwa dalili zifuatazo:
عن عائشة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((تحروا ليلة القدر في الوتر من العشر الأواخر)) رواه البخاري
Hadiyth ya 'Aiashah (Radhiya Allaahu 'anhaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Utafuteni usiku wa Laylatul-Qadr katika siku za witiri kwenye siku kumi za mwisho)) [Al-Bukhaariy[
حديث ابن عباس رضي الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((التمسوها في العشر الأواخر من رمضان ليلة القدر في تاسعة تبقى ، في سابعة تبقى ، في خامسة تبقى)) رواه البخاري
Hadiyth ya Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Utafuteni usiku wa Laylatul-Qadr katika siku kumi za mwisho za Ramadhaan; katika (usiku wa) tisa, saba, na wa tano utakaobakia [mwisho wa Ramadhaan])) [al-Bukhaariy[
Imaam Ahmad amepokea kutoka kwa 'Ubaydah bin As-Swaamit kwamba alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kuhusu usiku wa Laylatul-Qadr akasema:
((فِي رَمَضَان فَالْتَمِسُوهَا فِي الْعَشْر الْأَوَاخِر فَإِنَّهَا فِي وِتْر إِحْدَى وَعِشْرِينَ أَوْ ثَلَاث وَعِشْرِينَ أَوْ خَمْس وَعِشْرِينَ أَوْ سَبْع وَعِشْرِينَ أَوْ تِسْع وَعِشْرِينَ أَوْ فِي آخِر لَيْلَة ))
))Katika Ramadhaan, utafuteni siku kumi za mwisho, hakika umo katika siku za witiri; siku ya ishirini na moja, au ishirini na tatu, au ishirini na tano, au ishirini na saba, au ishirini na tisa, au usiku wa mwisho)) [Ahmad[
Alama Zinazobainisha Laylatul-Qadr:
1. Usiku huo unakuwa na mwanga zaidi.
2. Upepo siku hiyo hutulia, yaani siku hiyo hautokei upepo mkali.
3. Hali ya hewa huwa nzuri.
4. Nyoyo za Waumini usiku huo huwa zina utulivu kuliko siku nyingine.
5. Baadhi ya watu wema huoteshwa usiku huo kama walivyokuwa wakioteshwa Maswahaba na Salafus-Swaalih (wema waliotangulia(
Asubuhi Yake:
حديث أبي بن كعب رضي الله عنه أنه قال: "أخبرنا رسول الله صلى الله عليه وسلم أنها تطلع يومئذ ٍ لا شعاع لها" رواه مسلم
Hadiyth ya ‘Ubay bin Ka'ab (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ametuambia kuwa, jua siku hiyo hutoka likiwa halina mishale (mikali)" [Muslim[
Pia:
ليلة القدر ليلة طلقة لا حارة ولا باردة ، تُصبح الشمس يومها حمراء ضعيفة)) صحيح ابن خزيمة
))Laylatul-Qadr ni usiku ulio katika hali ya ukunjufu, usio na baridi wala joto, asubuhi yake jua huwa jekundu na dhaifu)) [Swahiyh Ibn Khuzaymah[
ليلة القدر ليلة بلجة (أي مضيئة) لا حارة ولا باردة ، لا يرمى فيها بنجم)) (أي لا ترسل فيها الشهب) رواه الطبراني ومسند أحمد
))Laylatul-Qadr usiku wa kung'aa [yaani wenye mwanga] sio joto wala baridi, na vimondo (nyota za kufyatuliwa) havitotumwa)) [At-Twabaraaniy na Ahmad]
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atuwezeshe kukesha masiku kumi ya Ramadhaan ili tujaaliwe kuupata usiku huu mtukufu, tutoke katika Ramadhaan tukiwa tumeghufuriwa madhambi yetu yote. Aamiyn