×
Image

Sherhu Umdatul Ahkam 13 - (Kiswahili)

Shekh anazungumzia: ufafanuzi wa hadithi ya kwanza kazungumzia maana ya matendo, akaeleza tofauti baina ya niya na kuazimia, kisha akaeleza kusudio la kuhama katika uislam.

Image

Sherhu Umdatul Ahkam 26 - (Kiswahili)

Shekh anazungumzia: ufafanuzi wa hadithi ya sita na yasaba, kuhusu na najsi ya mbwa, kisha amebainisha mbwa anaefaa kufugwa, kisha akabainisha namna ya kusafisha najsi ya mbwa, na akasema kuwa hadithi ya sita na ya saba zinabainisha kuwa mbwa ni najsi.

Image

Sherhu Umdatul Ahkam 15 - (Kiswahili)

Shekh anazungumzia: marejeo mafupi ya hadithi iliyo tangulia kisha akaanza kufafanua hadithi ya pili katika hadithi za kitabu cha Umdatul Ahkam..

Image

Sherhu Umdatul Ahkam 16 - (Kiswahili)

Shekh anazungumzia: Maana ya hadithi kwa ujumla kisha historia fupi ya Swahaba Abuu Hurayra, kisha akabainisha maana ya kauli ya Mtume (s.a.w): (hakubali) katika hadithi, kisha akaweka wazi tofauti baina ya hadath na najsi.

Image

Sherhu Umdatul Ahkam 17 - (Kiswahili)

Shekh anazungumzia: Ufafanuzi wa hadithi ya pili na amenukuu maneno ya shekh Albassam katika kufafanua maana ya hadithi, kisha amebainisha hukumu za hadithi kisha akasisitiza uwajibu wa kutawadha vizuri.

Image

Sherhu Umdatul Ahkam 18 - (Kiswahili)

Shekh anazungumzia: umuhimu wa kujifunza mambo ya muhimu katika udhu kabla ya kuswali, kisha akataja faida zinazo tokana na hadithi: swala ya mwenye hadathi haikubaliwi, hadadhi ni katika vitenguzi vya udhu…

Image

Sherhu Umdatul Ahkam 19 - (Kiswahili)

Shekh anazungumzia: ufafanuzi wa hadithi ya tatu, amebainisha daraja ya hadithi hiyo na akafafanua baadhi ya maneno katika hadithi kama vile (waylu) na (aqaab).

Image

Sherhu Umdatul Ahkam 20 - (Kiswahili)

Shekh anazungumzia: umuhimu wa kutawadha vizuri, na uhatari wa kuharakisha kutia udhu, kisha amewahusia watu waoshe viungo vizuri wakati wa kutawadha, katika hadithi: Udhu ni katika matendo mema, miguu inaoshwa katika kutawadha, mwenye kuacha mabaka katika kutawadha ataadhibiwa.

Image

Sherhu Umdatul Ahkam 21 - (Kiswahili)

Shekh anazungumzia: Ufafanuzi wa hadithi ya nne, ameeleza maana ya hadithi kwa jumla, kisha akabainisha faida za hadithi: kwamba inafaa kupandisha maji puani na kuyatoa, na nisheria kuosha mikono miwili baada ya kuamka usingizini, aliye lala bila kuambatanisha makalio yake anatakiwa atawadhe upya.

Image

Sherhu Umdatul Ahkam 22 - (Kiswahili)

Shekh anazungumzia: Ufafanuzi wa hadithi ya tano ambayo imeelezea makatazo ya kuoga katika maji yalio tuwama mahala pamoja, kisha akabainisha maana ya maneno ya hadithi na tafsiri ya hadithi kisha akafafanua kuhusu upokezi wa hadithi hii.

Image

Sherhu Umdatul Ahkam 23 - (Kiswahili)

Shekh anazungumzia: ufafanuzi wa hadithi ya tano na amebainisha upotovu wa rai ya dhwahiriya katika hadithi hii, kisha amebainisha faida za hadithi hii ikiwemo: makatazo ya kukojoa katika maji yalio tuwama, na kwamba Uislam unalinda mazingira, uislam unapiga vita uchafuzi wa mazingira, na usafi nikatika imani.

Image

Sherhu Umdatul Ahkam 24 - (Kiswahili)

Shekh anazungumzia: Ufafanuzi wa hadithi ya tano ameleza faida za hadithi ikiwemo, kujuzu kujitwaharisha katika maji yanayo tembea na inajuzu kukidhi haja katika maji yanayo tembea kwa dharura. Kisha amebainisha hadithi ya sita inayo zungumzia namna ya kuosha chombo kilicho lambwa na mbwa na nguruwe kisha ametaja taratibu za kufuga....