×
Image

Miujiza Ya Mtume (s.a.w) 45 - (Kiswahili)

Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni mameno aliyosema kwamba kikikaribia kiyama zama zitakaribiana mwaka utakua kama mwezi, amali zitakua chache na ubakhili utakithiri, pia imezungumzia umuhimu wa kusoma dini.

Image

Miujiza Ya Mtume (s.a.w) 44 - (Kiswahili)

Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa watu waliodai Utume ni Milza Ahmadi Alkaadiyan aliyedai kwamba anapata wahyi kutoka mbinguni, pia imezungumzia muujiza wa Mtume (s.a.w) aliposema kwamba utakithiri ujinga katika zama hizi na elimu itashuka.

Image

Miujiza Ya Mtume (s.a.w) 43 - (Kiswahili)

Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa watu waliodai utume baada ya kufa Mtume (s.a.w) ni mwanamke aitwae Sajjaha bintul-Harith, na wengineo.

Image

Miujiza Ya Mtume (s.a.w) 42 - (Kiswahili)

Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni maneno aliyosema kwamba hakitosimama kiyama ila watatokea watu waongo watakaodai Utume, pia imezungumzia vita aliyopigwa Musailama Al-kadhaab baada ya kudai Utume.

Image

Miujiza Ya Mtume (s.a.w) 41 - (Kiswahili)

Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni mambo ya shari aliyomwambia Swahaba Hudhayfa bunil-Yamany (r.a) kwamba yatatokea katika zama hizi, pia imezungumzia ushauri na wasia wa Mtume (s.a.w) kwa Hudheyfa (r.a).

Image

Miujiza Ya Mtume (s.a.w) 39 - (Kiswahili)

Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni maneno aliyosema wakati wa uhai wake Mtume (s.a.w) na yakatokea baada ya kufa kwake, miongoni mwa hayo ni maneno aliyosema kwamba zitakuja zama za fitna na watu watauana sana.

Image

Miujiza Ya Mtume (s.a.w) 38 - (Kiswahili)

Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni muujiza uliotokea kwa Abuu Jahli alipotaka kumdondoshea jiwe Mtume (s.a.w) wakati akiswali, lile jiwe likamng’ang’ania mikononi, pia imezungumzia muujizaa Mtume (s.a.w) uliotokea kwa Fudhwaala bin Ubaad (r.a).

Image

Miujiza Ya Mtume (s.a.w) 37 - (Kiswahili)

Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni maneno aliyombashiria mwanae Fatwima (r.a) kwamba baada ya kufa Mtume (s.a.w) yeye ndiye atakaekuwa wa kwanza kumfuata katika familia yake, pia imezungumzia muujiza wa Mtume (s.a.w) kwa Abuu Jahli baada kumdhulum mtu ngamia.

Image

Miujiza Ya Mtume (s.a.w) 36 - (Kiswahili)

Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni Muujiza uliotokea kwa Khaatwib bin Abi Balta’a (r.a) alipoandika barua na kuituma Mkka ili kutoa siri ya kivita, Mtume (s.a.w) akajua kabla barua haijafika Makka.

Image

Miujiza Ya Mtume (s.a.w) 35 - (Kiswahili)

Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni kuzungumzia mambo ambayo ni ya ghaibu kama alivyo wabashiria Maswahaba pepo na kuwaeleza fitna zitakazo wapata waka wa ukhalifa, pia imezungumzia umuhimu wa muislam kujiepusha na fitna.

Image

Miujiza Ya Mtume (s.a.w) 34 - (Kiswahili)

Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni kwamba aliyomuombea dua Qaisi bin Zaidi (r.a) kisha akapangusa kichwa chake sehem ile aliyoigusa Mtume (s.a.w) haikuota mvi mpaka anakufa, pia imezungumzia muujiza wa Mtume (s.w.a) kwa Abuu Hurera (r.a).

Image

Miujiza Ya Mtume (s.a.w) 32 - (Kiswahili)

Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni muujiza wa kutemea mate katika kisima cha Anasi bin Maliki (r.a) maji yale yakawa matam kuliko visima vote vya Madina, pia imezungumzia muujiza wa Mtume (s.a.w) kwa Ukasha (r.a) wa kubadilisha mti kugeuka upanga vitani.