×
Mada hii ni fatwa ambayo nimaswali aliyo yajibu Shaykh Muhammad ibn Saalih al-’Uthaymeen (Allah amrehemu) na swali nihili: Niweke wazi kuhusu aina za Tauhidi kwa urefu na mifano yake?.

    Aina za Tawhiid

    أنواع التوحيد

    < Swahili السواحليةسواحيلي >

    Shaykh Muhammad ibn Saalih al-'Uthaymeen (Allah amrehemu)

    سماحة الشيخ محمد بن صالح بن عثيمين (رحمه الله )

    —™

    Imetafsiriwa na:Shekh Yasini Twaha Hsaan

    ترجمة : ياسين طه حسن.

    Imepitiwa na:

    Yunus Kanuni Ngenda.

    المراجع:

    يونس كنون نغندا

    Aina za Tawhiid.

    Swali: Sheikh: Niweke wazi kuhusu aina za Tauhidi kwa urefu na mifano yake?

    JAWABU: Namna zote za Tauhidi kwa upande wa Mwenyezi Mungu Mtukufu zinaingia kwenye maana ya ujumla ya kwamba ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yale yanayo muhusu yeye, na imegawanyika katika namna tatu:

    1: Tauhidi Rububiyya: Ni Kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Kuumba na Ufalme na Uendeshaji.

    Mwenyezi Mungu pekeyake ndiye muumbaji hakuna muumbaji kinyume na yeye.

    Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Ati yupo muumba mwengine asiye kuwa Mwenyezi Mungu anaye kupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Hapana mungu ila Yeye tu). (Fatwir: 3).

    Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwa ni mwenye kubainisha na kubatilisha miungu ya makafiri, (Ati anaye umba ni kama asiye umba? Basi hebu, hamkumbuki?). ( Annahli: 17).

    Mwenyezi Mungu pekee ndie muumbaji, kaumba kilakitu na kukikadiria, na kuumba kwake kunakusanya vitendo vyake na vitendo vya waja wake pia, kwa sababu hiyo imekuwa miongoni mwa ukamilifu wa imani ni kuamini qadari, ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwenye kuumba vitendo vya waja, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya). ( Ass'afaat: 96).

    Ufafanuzi wake ni kwamba: vitendo vya mja ni miongoni mwa sifa zake, na mja kaumbwa na Mwenyezi Mungu, na muumbaji wa kitu ndio muumbaji wa sifa zake. Mfano mwengine: Hakika vitendo vya mja vinatokea kwa matakwa na uwezo ulio kamilika na matakwa na uwezo vimeumbwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na aliye umba sababu iliyo kamilika ndiyo aliye muumba mwenye kufanya sababu, utakapo sema: tutasemaje hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu kajipwekesha na kuumba, haliyakuwa kathibitisha uumbaji kwa asiyekuwa yeye, kama inavyo onyesha kauli yake tukufu: (Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji).

    (Al-Muminuna: 14).

    Na kauli yake Nabii Muhammad (s.a.w), kwa wapiga picha: (Wataambiwa vihuisheni mlivyo viumba). Kapokea hadithi hii Imam Bukhari na Muslim.

    Jibu lake ni kwamba: Hakika asiye kuwa Mwenyezi Mungu haumbi kama anavyo umba Mwenyezi Mungu, kwa sababu hawezi kuleta kisicho kuwepo, wala kuhuisha kilicho kufa, lakini kuumba kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu inakuwa katika kubadilisha kutoka kwenye sura Fulani kwenda kwenye sura nyingine, naye ni kiumbe wa Mwenyezi Mungu, ukiangalia mfano mpiga picha anapopiga picha hajafanya jambo jipya bali kachukua kivuli cha mtu kukiweka kwenye karatasi, kama vile udongo hubadilishwa ukawa kama ndege, au kama sura ya ngamia, au kutoa kwenye rangi Fulani kwende kwenye rangi nyingine, na wino wote ni katika viumbe vya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hii ndio tofauti kati ya kuthibitisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu na uumbaji wa viumbe, kwa maana hiyo jambo la uumbaji linamuhusu Mwenyezi Mungu Mtukufu pekeyake.

    2: Miongoni mwa maana za Tauhidi Rububiyya: Kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Ufalme, Mwenyezi Mungu Mtukufu pekeyake ndie mfalme, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (AMETUKUKA ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu). (Al-Mulku: 1).

    Na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Sema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu, naye ndiye anaye linda, wala hakilindwi asicho taka). (Al-Muuminun: 88).

    Mfalme wa wafalme wote ni Mwenyezi Mungu pekeyake, kunasibisha ufalme kwa asiyekuwa Allah ni kunasibisha kwa ziyada tu, kwa hakika amenasibisha Mwenyezi Mungu Mtukufu utawala kwa mwengine, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (au za mlio washikia funguo zao). (An-Nuur: 61).

    Na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia). (Al-Muuminun: 6).

    Na dalili nyingine tofauti na hizo zinazo onyesha ya kwamba asiyekuwa Mwenyezi Mungu anao ufalme, lakini ufalme huo sio kama ufalme wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni ufalme ulio na mipaka usio enea, nyumba ya Zaidi hawezi kuimiliki Amru, na nyumba ya Amru hawezi kuimiliki Zaidi, kisha ufalme huo wenye vikwazo hawezi binadamu kuutumia kinyume na alivyo amrisha Mwenyezi Mungu, kwa sababu hiyo amekataza Nabii Muhammad (s.a.w), kuharibu mali. Katika hadithi aliyo ipokea Imam Bukhari na Muslim.

    Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Wala msiwape wasio na akili mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameyajaalia yawe ni kiamu yenu). (An-Nisaai: 5).

    Na hii nidalili ya kuonyesha ya kwamba utawala wa binadamu ni mdogo, na wenye mipaka maalum tofauti na ufalme waMwenyezi Mungu Mtukufu niwa moja kwa moja wenye kuenea, anafanya Mwenyezi Mungu Mtukufu atakavyo, na wala haulizwi kwa anayo yafanya lakini viumbe huulizwa.

    Nguzo ya tatu katika nguzo za Tauhidi Rrububiyya: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ni pekeyake katika uendeshaji, yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye ambaye anaendesha viumbe, anaendesha mambo ya mbinguni na aridhini kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote). (Al-A'araaf: 54).

    Na uendeshaji huu niwa jumla, hakuna pingamizi wala kizuizi kati kati, na uendeshaji unao patikana kwa baadhi ya viumbe kama vile binadamu kuendesha mali zake na watoto wake na wafanya kazi wake namfano wa hayo, ni uendeshaji mfinyu wenye mipaka maalum, kwa maana hiyo ikawa ni sahihi kauli yetu tuliposema ya kwamba: hakika Tauhidi Rrububiyya ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuumba na ufalme na uendeshaji, hii ndio Tauhidi Rrububiyya.

    2: Tauhidi Ulu'hiyya: nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Ibada, kwa maana binadamu asifanye chochote pamoja na Mwenyezi Mungu katika Ibada inayo mkurubisha mbele ya Mwenyezi Mungu, kama anavyo muabudu Allah na kujikurubisha kwake, na namna hii ya Tauhidi ndiyo waliyo potea washirikina ndani yake, ambao wamepigwa vita na Mtume Muhammad (s.a.w), na ikawa ni halali wake zao na watoto wao na mali zao na ardhi yao na nyumba zao, na Tauhidi hiyo kwa sababu yake wametumwa Mitume na vikateremshwa vitabu, pamoja na Tauhidi ya kuamini majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake, lakini Mitume walikuwa wakiwatibu watu wao kutokana na Tauhidi hii ya Ulu'hiyya, kwa maana binadamu asifanye jambo lolote la Ibada kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu, isiwe ni kwaajili ya Malaika aliye karibu wala Nabii aliye tumwa, au walii, au kwa sababu ya kiumbe yeyote, kwa sababu Ibada haikubaliwi isipokuwa iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na yeyote atakae kwenda kinyume na Tauhidi hii huyo ni mshirikina tena kafiri, japo akikubali na kukiri Tauhidi ya Ulezi na Tauhidi ya majina na sifa, mfano mtu akiamini ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye muumbaji mfalme muendeshaji wa mambo yote, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndie mwenye kustahiki kwa yale anayo stahiki kutokana na majina yake na sifa zake, lakini anaabudu pamoja na Mwenyezi Mungu kitu kingine, haito mnufaisha imani yake ya kuamini Tauhidi ya Uungu na Tauhidi ya majina na sifa, lakini anakwenda makaburini na kuabudu alie zikwa, au akaweka nadhiri au kichinjo kwa alie kufa anajikurubisha kwavyo, kwa hakika huyu ni mshirikina tena kafiri, mwenye kuishi milele motoni, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

    (Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru). (Al-Maida: 72).

    Kama inavyo julikana kwa kila anaesoma kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, ya kwamba washirikina ambao Nabii Muhammad (s.a.w), aliwapiga vita na kuhalalisha damu zao na mali zao na kuwateka wake zao na watoto wao na kutekwa ardhi yao, walikuwa niwenye kukiri ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu pekeyake ndiye muumbaji, hawana shaka kwa hilo, lakini walipokuwa wakiabudu pamoja na Mwenyezi Mungu kitu kingine wakawa ni washirikina kwa hilo, ikawa ni halali damu yao na mali zao.

    3: Miongoni mwa namna za Tauhidi, ni Tauhidi ya majina na sifa.

    KumpwekeshaMwenyezi Mungu Mtukufu kwa majina aliyo jiita na kujisifu mwenyewe katika kitabu chake au kupitia Mtume wake Muhammad (s.a.w), kwa kuthibitisha aliyo yathibitisha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika nafsi yake, bila ya kupindisha wala kubadilisha wala kupunguza wala kuongeza chochote katika majina yake na sifa zake na bila ya kumpigia mfano katika majina yake na sifa zake, hapana budi ya kuamini kama alivyo jiita Mwenyewe na kujisifu Mwenyewe kwa ukweli kabisa bila ya kufananisha.

    Mfano: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu kajiita nafsi yake ya kwamba yeye ni "Hayyu Qayyum" ni wajibu kwetu kuamini ya kwamba " Hayyu" ni jina miongoni mwa majina yake, na nilazima tuamini yanayo fungamana na jina hilo kutokana na sifa, nayo ni Uhai ulio kamilika haukutanguliwa na kutokuwepo, wala haukutani na kutoweka, na akajiita Mwenyezi Mungu Mtukufu nafsi yake kama ni "Mwenye kusikia Mwenye elimu" niwajibu juu yetu kuamini ya kwamba "Assamiu" ni jina miongoni mwa majinaya Allah, na kusikia ni sifa miongoni mwa sifa zake, na kwamba yeye husikia, na ndio hukumu inayo fungamana na jina hilo na sifa hiyo, lakini ukisema ya kwamba anasikia bila ya kuelewa vinavyo ongelewa jambo hilo ni muhali, kwa haya tulio zungumza kisia majina yote ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa zake.

    Mfano mwingine: kauli yakeMwenyezi Mungu Mtukufu:

    (Na Mayahudi walisema: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndiyo iliyo fumba, na wamelaaniwa kwa sababu ya waliyo yasema. Bali mikono yake iwazi. Hutoa apendavyo).

    (Al-Maida: 64).

    Hapa amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Bali mikono yake iwazi) Akathibitisha katika nafsi yake Mikono kwa sifa ya ukunjufu, nako ni kutoa kwa wingi, niwajibu juu yetu kuamini ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anayo Mikono miwili mikunjufu kwa kutoa neema, pia haifai juu yetu kusema kwa nyoyo zetu wala kufanya tass'wira wala kwa ndimi zetu namna ilivyo mikono hiyo, wala kuifananisha na mikono ya viumbe, kwasababu Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Hapana kitu kama mfano wake,Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona). (Ash-shura: 11).

    Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya dhaahiri na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asicho kiletea uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua).

    (Al-A'araaf: 33).

    Na anasemaMwenyezi Mungu Mtukufu: (Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa). (Al-Israai: 36).

    Yeyote atakae fananisha mikono hiyo miwili kwa mikono ya viumbe kwa hakika kakadhibisha kauli yaMwenyezi Mungu Mtukufu: (Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona). (Ash-shura:11).

    Na atakua kapinga kauli yaMwenyezi Mungu Mtukufu pale alipo sema:(Basi msimpigie Mwenyezi Mungu mifano). (An-Nah'li: 74).

    Na atakae ifananisha na akasema ipo namna fulani atakua kamsemea Mwenyezi Mungu asio yasema, na bila ya elimu.