×
Mada hii inazungumzia: Matendo mema katika siku kumi za Dhulhija imezungumzia ubora wa masiku kumi ya Dhulhija, na ubora wa matendo mema katika masiku hayo, pia imezungumzia sifa za takbira na aina zake.

    MATENDO MEMA KATIKA SIKU KUMI ZA DHUL HIJJA.

    [Swahili- Kiswahili سواحيلي -]

    Mwandishi:

    Abubakari Shabani Rukonkwa.

    —™

    Imerejewa na:

    Yasini Twaha Hassani.

    الأعمال الصالحة في عشر من ذي الحجة

    كتبه:

    أبوبكر شعبان ركونكوا

    مراجعة :

    ياسين طه حسن

    MATENDO MEMA KATIKA SIU KUMI ZA DHUL HIJJAH

    (MFUNGO TATU)

    Utangulizi:

    Sifa zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu ambaye amewaneemesha waja wake kwa kuwaletea misimu ya kheri ili iwe ni sababu ya kufutiwa madhambi yao na awalipe kutokana na mema yao, namshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumsifu kwa muwafikisha anayemtaka katika waja wake kwa kuyatumia masiku haya kwa kumtii na kumogopa, na akajaalia wengine katika waja wake ni wenye kuzipoteza siku hizo.

    Nakiri kwa moya na kutamka kwa ulimi ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokua Mwenyezi Mungu mmoja hana mshirika katika Uungu wake, na nina kiri kwa moya na kutamka kwa ulimi ya kwamba Muhammad ni mja wake na mjumbe wake, rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake pamoja na familia yake na Maswahaba wake na wote watakao mfuata kwa wema mpaka siku ya mwisho.

    Amma baad.

    Nisiku 10 bora kuliko masiku yote ya duniani Allah amebainisha ubora wake katika kitabu kitukufu pale alipo apia masiku haya kwakuusema:

    بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ((وَالْفَجْرِ)) ((وَلَيَالٍ عَشْرٍ))

    BisimiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym. ((Naapa kwa Alfajiri)) ((Na kwa masiku kumi)) (Al-Fajr: 1-2).

    Wanavyuoni wafasiri wa Qur-aan wamekubaliana kwamba zilokusudiwa hapo ni Siku kumi za Dhul-Hijjah.

    SIKU ZA MANUFAA NA KUMKUMBUKA ALLAH

    Inapasa kumdhukuru mno Allaah (Subhaanah wa Ta’ala) kwa kukumbuka Neema Zake zisizohesabika:

    ((لِيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ))

    ((Ili washuhudie manufaa yao na kulitaja Jina la Allaah katika siku zinazojulikana)) [Al-Hajj: 28[

    Ibn Abbaas kasema: “Hizo ni siku kumi za Dhul-Hijjah” . Na Amesema: “Manufaa ya dunia hii na ya Akhera” . Manufaa ya Akhera yanajumuisha kupata Radhi za Allaah. Manufaa ya vitu vya dunia inajumuisha wanyama wa kuchinjwa na biashara. [Tafsiyr Ibn Kathiyr[.

    AMALI ZAKE NI BORA KULIKO KWENDA KTK JIHAAD FIY SABILILLAH

    Kutokana na ilivyotajwa katika usimulizi wa Hadiyth ifuatayo, kwamba amali yoyote utendayo katika masiku kumi haya, ni bora kuliko kwenda kupigana jihadi vitani. Ukizingatia kwenda kupigana jihadi ni jambo zito mtu kuliitikia, kwani huko kuna mashaka mbali mbali, ikiwemo khofu ya kujeruhiwa na kupoteza viungo vya mwili, kufariki, kupoteza mali n.k. Ila hilo si zito kwa mwenye Imani ya hali ya juu kabisa kutaka kuyakabili mashaka hayo na kutamani kufa shahidi. Kwa hiyo usidharau Amali yoyote hata iwe ndogo vipi itekeleze kwani Allaah Subhaana wa Ta'ala ni Al-Jawwaad (Mwingi Wa Ukarimu), Al-Kariym (Karimu), Al-Wahhaab (Mwingi Wa Kutunuka, Mpaji Wa Yote), Al-Majiyd (Mwingi Mno Wa Vipawa Na Ukarimu).

    عن ابن عباس رضي الله عنهما، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:)) ما من أيام العمل الصالح فيها أحب إلى الله من هذه الأيام)) - يعني أيام العشر-. قالوا: يا رسول الله، ولا الجهاد في سبيل الله ؟ قال: ((ولا الجهاد في سبيل الله، إلا رجل خرج بنفسه وماله ثم لم يرجع من ذلك بشيء)) البخاري

    Imetoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kwamba Mjumbe wa Allaah Amesema: ((Hakuna siku ambazo vitendo vyake vyema Anavipenda Allaah kama siku kumi hizi)) (siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah) Akaulizwa, je, hata Jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu Aliyekwenda na nafsi yake na mali yake ikawa hakurudi na kimojawapo)) [Al-Bukhaariy].

    IBADA ZOTE ZIMEJUMUIKA KTK SIKU HIZI 10

    Ibada zote zimejumuika katika siku kumi hizi nazo ni Swalah, Swawm, Swadaqah, Hajj na Umra, wala hazijumuiki hizi wakati mwingine.

    KUFUNGA SIKU HIZI KHASWA SIKU YA 'ARAFA

    عن أبي سعيد الخضري رضي الله عنه قال: قال عليه الصلاة والسلام ((من صام يوما في سبيل الله باعد الله وجهه عن النار سبعين خريفا) رواه البخاري ومسلم

    Kutoka kwa Abu Sa'iydil-Khudhwriyy (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Mwenye kufunga siku kwa ajili ya Allaah, basi Allaah Atamuokoa uso wake kutokana na moto kwa umbali wa miaka sabini)) [Al-Bukhaariy na Muslim[.

    قال صلى الله عليه وسلم : (( كل عمل ابن آدم له الحسنة بعشر أمثالها إلى سبعمائة ضعف . يقول الله عز وجل : إلا الصيام فإنه لي وأنا أجزي به)) أخرجه البخاري ومسلم

    Amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Kila Amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah Anasema isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye nitakayemlipa)) [Al-Bukhaariy na Muslim).

    MATENDO MEMA YA KUTENDA KTK SIKU KUMI HIZI

    Kutekeleza Hajj na 'Umrah (kwa mwenye uwezo(

    عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال ((العمرة إلى العمرة كفارة لما بينهما . والحج المبرور ليس له جزاء إلا الجنة)) أخرجه البخاري و مسلم

    Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: (('Umrah hadi 'Umrah hufuta (madhambi) baina yake, na Hajjum-Mabruur haina jazaa ila Pepo)) [Al-Bukhaariy na Muslim(.

    عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: "سئل رسول الله صلى الله عليه وسلم: أي الأعمال أفضل؟ قال: ((إيمان بالله ورسـوله)). قيل: ثم مـاذا؟ قال: ((الجهاد في سبيل الله)) قيل: ثم ماذا؟ قال: ((حج مبـرور)) متفق عليه

    Imetoka kwa Abu Hurayrah(Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Aliulizwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amali gani ni bora kabisa?" Kasema: ((Kumuamini Allaah na Mtume Wake)), Akaulizwa:"Kisha nini?" Kasema: ((Jihaad katika njia ya Allaah)). Akaulizwa: "Kisha nini?" Kasema: ((Hajj Mabruur)) [Al-Bukhaariy na Muslim(.

    KUOMBA TAWBAH YA KWELI NA KUJIEPUSHA NA MAASI

    Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala:

    (( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا))

    ((Enyi mlioamini! Tubuni kwa Allaah toba iliyo ya kweli!))

    [At-Tahriym: 8).

    Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Ametupa matumaini makubwa ya kufutiwa madhambi na makosa yetu katika usimulizi ufuatao:

    عن أنس رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((قال الله: يا ابن آدم إنك ما دعوتني ورجوتني غفرت لك على ما كان منك ولا أبالي، يا ابن آدم لو بلغت ذنوبك عنان السماء، ثم استغفرتني غفرت لك ولا أبالي، يا ابن آدم إنك لو أتيتني بقراب الأرض خطايا، ثم لقيتني لا تشرك بي شيئاً لأتيتك بقرابها مغفرة)) أخرجه الترمذي وحسنه الألباني في الصحيحة

    Kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu 'anhu): "Nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Allaah Amesema: Ee Mwana Adam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakusamehe yale yote uliyonayo na wala Sijali, Ee Mwana Adam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfira, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee Mwana Adam, Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na msamaha unaolingana nao)) [Imetolewa na At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan[.

    KUMKUMBUKA SANA ALLAH (Subhaanahu wa Ta'ala)

    Kwa Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl, Takbiyr (kusema: Subhaana Allaah, AlhamduliLlaah,Laa Ilaaha Illa Allaah, Allaahu Akbar)

    عن ابْنِ عُمَرَ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال: (( مَا مِنْ أَيَّامٍ أَعْظَمُ عِنْدَ اللَّهِ وَلَا أَحَبُّ إِلَيْهِ مِنَ الْعَمَلِ فِيهِنَّ مِنْ هَذِهِ الْأَيَّامِ الْعَشْرِ فَأَكْثِرُوا فِيهِنَّ مِنَ التَّهْلِيلِ وَالتَّكْبِيرِ وَ التَّحْمِيدِ )) أخرجه أحمد

    Imetoka kwa ibn 'Umar kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Amesema: ((Hakuna siku zilizokuwa tukufu kwa Allaah na zilizokuwa vitendo vyake vipenzi kabisa Kwake kama siku hizi, basi zidisheni Tahliyl na Takbiyr na Tahmiyd)) [Ahmad[.

    INAVYOPASA KUFANYA TAKBIIR:

    Katika ibada ambazo zinazo takiwa kufanywa katika masiku kumi ya Dhul Hijja nikukithirisha kutowa Takbira, kutoka kwa Muhamad bin Abubakari AL Thaqafy kwamba alimuuliza Anasi bin maliki (ﷺ‬.a) wakiwa wanatembea kutoka mina kwenda Arafa, mlikuwa mnafanya nini katika masiku haya kumi wakati mlipokuwa na mtume (s.a.w) akasema :alikuwa miongoni mwetu mtu anatowa Tahlil (Laiha haila Allah), na mtume hamkatazi, na miongoni mwetu kuna wanao towa takbira, na mtume hawakatazi.

    Imepokelewa na imamu Bukharin a Muslim.

    AINA ZA TAKBIRA KATIKA SIKU KUMI ZA DHUL HIJA.

    Takbira zinazo takiwa kusemwa na muislam zimegawanyika katika sehemu mbili:

    1.Takbira ambayo ni Mutlaq:

    Nayo nitakbira ambayo haina muda maalumu,bali inatajwa na muislam wakati wowote na sehemu yoyote, asubuhi na jiuni, kabla ya swala na baada ya swala.

    Nisuna kupiga takbira katika masiku kumi ya mwanzo katika mwezi wa dhul hijja, na baki ya masiku ya Tashriiq.

    Na takbira hiyo inaanza kwa kuingia mwezi wa dhul hijja tangu kuzama kwa juwa siku ya mwisho ya mwezi wa dhul hijja (mfungo tatu), mpaka mwisho wa siu za tashriiq, yaani tarehe (11-13) katika mwezi wa dhul hija.

    2.Takbira ambayo ni Muqayad:

    Nayo nitakbari inayo semwa baada ya swala zote za faradhi, nazo zinaanza alfajiri ya siku ya Arafa mpaka kuzama juwa katiku siku za Tashriiq, ni juu ya kila muislam kila anapo toa salam katika kila swala kisha akasema Adhkari za baada ya swala basi anatakiwa atowe takbira, nah ii nikwa asiekuwa Hji, ama alhaji anaanza siku ya kumi baada ya kutupa mawe katika kiguzo kikubwa mpaka siku ta kumi na tatu katika masiku ya Tashriiq.

    SIFA YA KUTOWA TAKBIRA:

    Amesema Imamu Ibn Othaymin (Allah amrehemu) katika kitabu sha Sharhu Al mumty.:

    Sifa za Takbira katika masiku kumi ya Dhul hijja yana Qaulii tatu katika qauli za wana wa chuoni:

    1.Nimuislam kusema: Allah akbar, Allah akbar, Laa ilaha ila Allah Allah akbar Allah akbar walilahil hamdu

    الله أكبر، الله أكبر، لا إله إلا الله، والله أكبر، الله أكبر، ولله الحمد).)

    2.Nimuislam kusema: Allah akbar, Allah akbar, Allah akbar, Laa ilaha ila Allah Allah akbar, Allah akbar, Allah akbar, walilahil hamdu.

    .(الله أكبر، الله أكبر، الله أكبر، لا إله إلا الله، والله أكبر، الله أكبر، الله أكبر، ولله الحمد)

    3. Nimuislam kusema: Allah akbar, Allah akbar, Allah akbar, Laa ilaha ila Allah waAllah akbar, Allah akbar walilahil hamdu.

    "الله أكبر، الله أكبر، الله أكبر، لا إله إلا الله، والله أكبر، الله أكبر، ولله الحمد

    Katika maswala haya ya sifa za takbira hakuna dalili ambazo zimekuja kusema kuwa moja katika hizi aina tatu nibora kuliko zingine, inabaki nijuu ya muislam atowe takbira kulingana na anavyo taka mwenyewe.

    KUZIDISHA VITENDO VYEMA MBALI MBALI

    Mbali ya kutekeleza fardhi ya Swalah kwa kuswali kwa wakati wake, kuswali Sunnah zaidi, kusoma Qur-aan, Swadaqah, Du'aa, kutii wazazi na kuwafanyia wema, kuwasiliana na jamaa (kuunga undugu), kuwafanyia wema jirani, kuamrishana mema na kukatazana maovu, kufanyiana wema na ihsani na kadhalika.

    Allah tujalie na utupe tawfiiq ya kutenda mema atika masiku haya matukufu, na katika masiku mengine, wasamehe wazazi wetu na waislam wote, Allah tunakuomba mwisho mwema.