×
Makala hii inazunguzia: Ubora wa Tawhiyd na kwambaTawhiyd Ni Bora kuliko Mali Na Starehe Za Duniani Na Neno La Tawhiyd nizito katika mizani kuliko mbingu saba na ardhi saba.

    UBORA WA TAWHIYD

    [Swahili- Kiswahili سواحيلي -]

    IMEANDIKWA:

    SHEKH: YASINI TWAHA HASAN

    IMEPITIWA:

    ABUBAKARI SHABANI RUKONKWA.

    فضل التوحيد

    كتبه: فضيلة الشيخ ياسين طه حسن.

    راجعه: أبوبكر شعبان ركونكوا.

    بسم الله الرحمن الرحيم

    Utangulizi:

    Shukrani zote ni zake Mola wa ulimwengu wote, na mwisho mwema nikwawamchao Allah, na hapana uadui isipokuwa kwa madhalimu.

    Nashuhudia kuwa hapana anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah Peke yake Asiye na mshirika Mwenye Ufalme na haki iliyo wazi. Na nashuhudia kuwa Muhammad (s.a.w) ni mjumbe wake na Mtume wake nawa mwisho wa wajumbe wake na ni kiongozi wa wacha Mungu. Mola wetu mswalie na msalimie Mtume wako huyu pamoja na Masahaba wake na kila atakayemfuata kwa wema na uongofu mpaka Siku ya Qiyama.

    Tawhiyd Ni Bora kuliko Mali Na Starehe Za Duniani Na Neno La Tawhiyd litakuwa Zito Siku ya Qiyaamah

    Makafiri wa Kiquraysh wa Makkah walitaka kumpa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mali na starehe za dunia, walitaka kumpa cheo ili aache kulingania Tawhiyd lakini Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakufadhilisha hayo, bali alijikita katika da’wah yake kwa kuwa aliamini kulingania Tawhiyd ndio haki na ndio itakayomfaa bin Aadam Siku ya Qiyaamah, Siku ambayo mtu atatamani kufidia kwa mali yake yote aliyokuwa nayo duniani ili aepukane na adhabu ya Moto kwa kukanusha Tawhiyd.

    Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

    إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾

    Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitokubaliwa kutoka kwa mmoja wao (fidia ya) dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wakitaka kujikombolea nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru. [Aal-‘Imraan: 91]

    Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika Hadiyth iliyosimuliwa na Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu):

    ((يَقُولُ اللهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى لِأَهْوَنِ أَهْلِ النَّارِ عَذَابًا: لَوْ كَانَتْ لَكَ الدُّنْيَا وَمَا فِيهَا، أَكُنْتَ مُفْتَدِيًا بِهَا؟ فَيَقُولُ: نَعَمْ ، فَيَقُولُ: قَدْ أَرَدْتُ مِنْكَ أَهْوَنَ مِنْ هَذَا وَأَنْتَ فِي صُلْبِ آدَمَ: أَنْ لَا تُشْرِكَ -أَحْسِبُهُ قَالَ: وَلَا أُدْخِلَكَ النَّارَ - فَأَبَيْتَ إِلَّا الشِّرْك))

    ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Atamwambia mtu atakayekuwa na adhabu nyepesi kabisa Motoni “Je, ungekuwa una dunia nzima na yaliyomo ndani yake [mali n.k.] ungeitolea fidia?”)) Atajibu ((Ndio)) Atasema Allaah: ((Nilikutaka kwa jambo jepesi zaidi kuliko hayo, ulipokuwa katika uti wa mgongo wa Aadam kwamba usinishirikishe)) Nadhani Akasema: (na sitokuingiza motoni lakini umekataa isipokuwa kunishirikisha)). [Muslim]

    Ni dhahiri kwamba Tawhiyd ambalo ni jambo jepesi kabisa itakuwa na thamani zaidi kuliko dunia na yaliyomo duniani, bali neno la Tawhiyd; laa ilaa illa Allaah litakuwa zito kabisa katika Miyzaan ya ‘amali Siku ya Qiyaamah:

    عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرَيِّ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ الله (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((قَالَ مُوسَى عَلَيْهِ السَّلامُ يَا رَبِّ! عَلِّمْنِي شَيْئًا أَذْكُرُكَ وَأَدْعُوكَ بِهِ. قَالَ: قُلْ يَا مُوسَى: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ. قَالَيَا رَبِّ! كُلُّ عِبَادِكَ يَقُولُونَ هَذَا. قَالَ: يَا مُوسَى, لَوْ أَنَّ السَّمَوَاتِ السَّبْعَ وَعَامِرَهُنَّ غَيْرِي وَالأَرَضِينَ السَّبْعَ فِي كِفَّةٍ, ولاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ فِي كِفَّةٍ، مَالَتْ بِهِنَّ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ)) رَوَاهُ ابْنُ حِبَّانَ وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ.

    Imepokewa toka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudhriyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

    ((Muwsaa alisema: Ee Mola wangu! Nifundishe kitu ambacho kwacho nikudhukuru na nikuombe du’aa. Akasema [Allaah]: Ee Musa: Sema: “Laa ilaaha illa-Allaah”. Muwsaa akasema: Ee Mola wangu! Kila mja anasema hivi. Akasema [Allaah]: Ee Musa, lau kama mbingu saba na kila kilichokuwemo isipokuwa Mimi, na ardhi saba zikiwekwa katika kiganja cha mizani, na laa ilaaha illa-Allaah imewekwa katika kiganja kingine cha mizani, basi laa ilaaha illa-Allaah itazishinda hizo)).

    [Ibn Hibaan na Al-Haakim, na ameikiri kuwa ni Swahiyh].

    FAIDA ZA TAWHIID:

    Tawheed inafaida nyingi sana miongoni mwa faida hizo:

    1.Nisababu ya kuondoshewa matatizo ya kidunia na Akhera na kuziwiya adhabu zake.

    2.Inamziwiya mwanadamu kuishi milele motoni ikiwa katika moyo wake kuna kiasi cha imani kinacho lingana na tembe ndogo ya khaldali, na anapokua na imani kamili tawheed inamziwiya kuingia motoni.

    3.Mwenye tawheed anapata uongofu ulio kamilika na amani ilio timia katika dunia na akhera.

    4.Tawheed nisababu ya kupata radhi za Allah na thawabu zake, hakika atakae fanikiwa na uombezi wa mtume (s.a.w) siku ya qiyama niyule alie sema : (la ilaha ila Allah ) akitaraji malipo kwa Allah.

    5.hakika matendo ya mwanadamu ya dhahiri na yasiri hayawezi kukubaliwa pindi anapokuwa mtu hana Tawheed.

    6.Tawheed inamrahisishia mja kufanya kheri nakuacha mambo machafu, na inamlewaza pale penye misiba na masononeko.

    Tunamuomba Allah mtukufu atupe imani zilizo thabiti na atufutie madhambi yetu na atupe mwisho mwema.