×
Makala hii inazunguzia: Faida ya kutoa sadaka, pia inazungumzia kwamba sada inapitia kwenye (mkono) wa Mwenyezi Mungu kabla ya kuingia mkononi mwa masikini

    بسم الله الرحمن الرحيم

    FAIDA YA KUTOA SADAKA

    Imeandaliwa na Yunus Kanuni Ngenda

    Imepitiwa na Yasin Twaha Hassani

    Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, na rehma na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na watu wake na Maswahaba wake wote. Amma baad:

    Hakika Mwenyezi Mungu anawalipa malipo makubwa wale wanaotoa sadaka kwa kutafuta radhi zake.

    Laiti mtoa sadaka angejua kwa yakini kwamba sadaka yake inapitia kwenye (mkono) wa Mwenyezi Mungu kabla ya kuingia mkononi mwa masikini, ingekuwa ladha ya mtoaji. ni kubwa kuliko ladha ya mpokeaji..
    Ibun Alqayyim.

    Je unajua faida ya kutoa sadaka?
    Sikilizeni enyi watoa sadaka, wenye kutoa na ambao wanasaidia kufikisha sadaka.

    1- Sadaka ni mlango miongoni mwa milango ya pepo

    2-Sadaka ni bora ya matendo mema, na sadaka bora ni kulisha chakula

    3- Sadaka inamfunika kivuli mtoaji na inamuondosha kwenye moto

    4-Sadaka inazima ghadhabu za Mola na joto la kaburi

    5- Sadaka ni jambo bora la kumzawadia maiti na inamfaa zaidi, na Mola anaitunza

    6-Sadaka ni usafisho, na utakaso wa nafsi na huongeza mema

    7- Sadaka ni sababu ya furaha kwa mtoa, na ni sababu ya kung'ara uso wake siku ya kiama

    8- Sadaka inaleta amani kutokana na hofu siku ya fazaa kubwa, na humfanya mtoa sadaka asipatwe na huzuni

    9- Sadaka ni sababu ya kughufiriwa dhambi na kusamehewa makosa

    10- Sadaka ni miongoni mwa bishara za mwisho mwema na sababu ya dua ya Malaika

    11- Mtoa sadaka ni mbora wa watu, na sadaka thawabu zake ni kwa kila aliyeshiriki

    12- Mwenye kutoa sadaka ameahidiwa kheri nyingi na ujira mkubwa

    13- Kutoa ni miongoni mwa sifa za wacha Mungu, na sadaka ni sababu ya mapenzi ya waja wa Mola kwa mtoa sadaka

    14- Sadaka ni ishara miongoni mwa ishara za ukarimu na alama miongoni mwa alama za ukarimu na wema

    15- Sadaka ni sababu ya kukubaliwa dua na kuondoshewa matatizo

    16- Sadaka inaondoa balaa na inaziba milango sabini ya mabaya ya dunia

    17- Sadaka inazidisha umri na mali, na ni sababu ya riziki na nusra

    18- Sadaka ni ponya, dawa, na shifaa

    19- Sadaka inazuia moto, gharika, wizi, na inazuia kifo kibaya

    20- Sadaka ujira wake ni ule ule japo ukitoa kwa wanyama au ndege.