ZINGATIENI ENYI WATUMIAJI WA SIMU ZA MIKONONI NA INTERNET.
Jamii ya vilivyomo
Full Description
بسم الله الرحمن الرحيم
ZINGATIENI ENYI WATUMIAJI WA SIMU ZA MIKONONI NA INTERNET.
Imekusanywa na Abubakari Shabani
Imepitiwa na Yunus kanuni
Hizi ni miongoni mwa tabia zilizodumu kwa watumiaji wa simu za mkononi na internet, mambo haya yamekuwa kama ni kawaida kwenye nafsi za baadhi ya waumini.
Sasa tuangalie makosa haya pamoja na kukatazwa kwake, onyo lake au adhabu kwa mwenye kuyafanya.
1-KUSENGENYA.
Anasema Allah (subhanahu wataala):
(وَيْلٌ لِكُلِّ هُمَزَةٍ لُمَزَةٍ)
“Ole wake kila safihi, msengenyaji” (Suratul Humazah:1).
2-KUSEMA UONGO.
Amesema Mtume Muhammad(ﷺ) “Ni juu yenu kusema kweli! Na ole wenu na kusema uongo! kwani uongo unampeleka mtu motoni” Imepokelewa na Muslim.
3-KUFITINISHA.
Amesema Mtume wa Allah (ﷺ) : ”Haingii peponi mwenye kusengenya”. Bukhari na Muslim.
4-KUKARIBIA ZINAA.
Anasema Allah(subhanahu wataala):
(وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا)
“Wala msiikaribie zinaa (uzinzi) Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.”(Suratul Israa :32).
5-KUSAMBAZA UCHAFU MFANO VIDEO NA PICHA ZA HARAMU.
Anasema Allah (subhanahu wataala):
(إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَنْ تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ)
” Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera.Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.”
(Suratu Nnur:19).
6-KUSAMBAZA HABARI ZA UONGO BILA YA KUZITHIBITISHA.
Anasema Allah (subhanahu wataala):
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ)
”Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu (fasiq) na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.”(Suratul Hujurat: 6)
7-KUVUNJIANA HESHIMA BAINA WA WATU.
Anasema Allah (subhanahu wataala):
(وَلَا تَلْمِزُوا أَنْفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ ۖ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ ۚ وَمَنْ لَمْ يَتُبْ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ)
“Wala msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kuwa umekwisha amini, na wasio tubu, hao ndio wenye madhalimu (wenye kujidhulum nafsi zao) (Suratul Hujurat:11)
8-KUTUKANANA(KURUSHIANA MATUSI). Amesema Mtume wa Allah (ﷺ) “Kumtukana waislamu ni ufasiki, na kupigana ni ukafiri” Bukhari na Muslim.
TANBIHI (UZINDUO):
Ndugu katika imani hayo ni baadhi ya makosa na madhambi makubwa yanayofanywa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya internet na simu za mikononi, ni wajibu kwa muislamu kujiepusha na makosa hayo na mengine yanayofanana na hayo.
Tumuogope Allah katika kila jambo kwani kila mtu atailipwa kwa kadri ya matendo yake.
Allah (Subhanahu wataala) anasema:
(وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ)
“Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila mtu atalipwa alicho chuma, nao hawatadhulumiwa” (2:281)
Tunamuomba Allah atujaalie kuwa Miongoni mwa wenye kusikia maneno na kufuata yaliyo mezuri. Amee!!!!