WIVU KWA MKE MWENZA
Jamii ya vilivyomo
Vyanzo
Full Description
بسم الله الرحمن الرحيم
WIVU KWA MKE MWENZA
Imeandikwa na Abdurahmani Muhina.
Imepitiwa na Yunus Kanuni Ngenda.
Itakapo tokea mumeo kaoa mke mwingine mkawa mko wawili au zaidi ya wawili nasaha zangu kwako ni hizi zifuatazo:
Soma kwa makini ewe mwanamke nasaha hizi
1-Unatakiwa ulazimiane na wajibu wako yaani ufanye wajibu wako kwa mumeo na wala usimpe shetani njia, atapata nafasi ya kukushawishi ukaanza kupunguza kutekeleza haki za mumeo kwa wivu wako.
2-Ukifanya hivyo utaukamata moyo wa mumeo na utapendwa na mumeo hata kama mumeo kaoa mke zaidi ya mmoja, na nilazima ujue kwamba mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja ni ruhsa aliyopewa na ALLAH.
3-Elewa Dada yangu kwamba miongoni mwa mambo muhimu ambayo atayachuma mwanamke ambae yupo katika ukewenza ni kumtendea wema mke mwenzie au wake wenzie na kuwasamehe makosa yao wanayo mfanyia kwani hakuna mkamilifu isipokuwa ALLAH.
Ili aonekane katika mtazamo wa mwanamke mwenye akili na heshima asiyekuwa na mambo ya kimaudhi, mwenye kushikamana na dini yake.
Mwanamke aliye faulu ni yule ambae anampa raha mumewe vyovyote iwavyo na mwanamke aliye feli na anaejiadhibu ni yule ambae anayajaza maisha ya mumewe tabu, malawama, ugomvi na malalamiko, mwanamke huyu atakosa dunia na akhera na hii ni hasara kubwa.
KUWA HIVI:
Mwanamke aliye swali sala ya alfajir kisha akakaa kwa ajili ya kumuandalia mumewe kahawa au mlo wa asubuhi wakati ameshatayarisha mavazi ya mumewe kwa utaratibu mzuri, mwanamke aliye wapanga vizuri watoto wake na kuwapatia kifungua kinywa kwa pamoja watoto wakatoka kwenda zao shuleni hali ya kuwa na furaha tele, na mumewe akaenda kazini akiwa na furaha, tabasamu, uchangamfu na nguvu, Mashallah!.
Hayo ni miongoni mwa mambo yanayoleta raha, furaha, utulivu na burudani katika ndoa.
USIWE HIVI:
Mwanamke aliye sali sala ya alfajir mwishoni mwa muda (kwa kuchelewa) kisha akarudi tena chumbani kwake kuendelea kulala ili akamilishe usingizi wake:
Mwanamke aliyechelewa kuamka na alipo amka akaanza kumpiga bint yake kisa hakuchana nywele huku kachelewa shule na mumewe amekwenda kazini amejaa mawazo ya ugomvi ulio tokea usiku na kukosa raha kisha akaandaliwa chai au kahawa na secretary huku akimuuliza vipi boss mbona umefunga vibaya vifungo na unaonekana hupo sawa! swali linakosa jibu la ukweli na mumewe anabakia katika mtihani.
Hayo ni miongoni mwa mambo yanayopelekea maisha ya ndoa kuwa ya tabu, dhiki, kero, ugomvi na hata kuvunjika kwa ndoa.
NENO LA MWISHO:
Ewe mwanamke wa kiislam elewa kuwa ndoa ni ibada, ndoa ni utulivu, ndoa ni raha, ndoa ni furaha, ndoa ni faraja, ndoa ni amani na upendo. Pia ndani ya ndoa kuna baraka na kheri nyingi kutoka kwa Allah.
Ni vema kuishi kwa kuzingatia hayo na huku ukijitahidi kumcha Allah subhanahu wa ta'ala.
Tunamuomba Allah ajaalie kheri barka na utulivu katika ndoa zetu, Ameen!!!!!