KUJITOA MUHANGA KUNAMUWEKA MTU MBALI NA ALLAH
Jamii ya vilivyomo
Full Description
Kujitoa Muhanga Kunamuweka Mtu Mbali Na Allaah
Mzungumzaji: Imaam Muhammad Swaalih bin bin ´Uthaymiyn
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com
Imepitiwa na: Yunus Kanuni Ngenda
بسم الله الرحمن الرحيم
Utangulizi
Kuhusu matendo [ambayo mtu humuonyesha Allaah hasira kwayo], ni pamoja na kuchana nguo, kupiga mashavu, kukokota nywele na mfano wa hayo. Baadhi ya watu wanafanya hivi. Hata hivyo lililo kubwa, chafu na baya zaidi ni kujiua. Kuna watu wanaojiua wakati wanapopatwa na misiba wasiyoweza kukabiliana nayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametueleza kuhusu mtu aliyejeruhiwa na hakuweza kuvumilia. Akafanya kitu ambacho hakijuzu na Allaah Akamuwajibishia Moto.
Mwenye kujitoa muhanga ili kuepukana na msiba huu - hivi kweli ataepukana nao? Jibu! Hapana. Hatouepuka. Anafikiria kuwa atapata kupumua baada ya kujiua. Pamoja na kwamba sivyo. Akifa ataadhibiwa Motoni kwa kile alichojiua nacho. Humo atadumishwa milele.
Kwa ajili hiyo tunawakataza ndugu zetu wanaoenda Palestina ili kujilipua kati ya mayahudi. Wanafikiri kwa kufanya hivo wanajikurubisha kwa Allaah. Uhakika wa mambo ni kwamba hili linawatia mbali na Allaah. Wanajiua wao wenyewe! Kujiua ni miongoni mwa madhambi makubwa. Mtu ataadhibiwa Motoni kwa kile alichojiua nacho. Pamoja na hivyo hatusemi kuwa hawa wanaingia katika kundi la watu hawa kwa kuwa wanafanya hivo kwa Ijtihaad. Wanafikiria kuwa kitendo hichi ni kizuri. Mtu mwenye kufanya kitu kwa kuelewa makosa pengine akasamehewa.
Hata hivyo kitendo hichi ni haramu Kishari´ah na sio katika Jihaad katika njia ya Allaah.
Kitendo hichi vilevile hakiingii akilini. Ni mayahudi wangapi anawaua pale anapojilipua? Ikiwa ni wengi ni watu 50-100. Matokeo yake mayahudi hufanya nini? Wataua mamia na wanazidi kuwa wenye kuchupa mipaka kuliko unavowaona sasa kwa kuteka mji.
Lakini watu wengi hawatazami matokeo. Hawafikirii mbali.
Talare: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com
Milipuko Inayofanywa Haijawapatia Waislamu Faida Yoyote Zaidi Ya Madhara Juu Ya Madhara
Kuhusiana na yale yanayofanywa na baadhi ya watu kujitoa muhanga kwa kujiweka mabomu na kuwaendea makafiri kisha wanajilipua pindi wanapokuwa kati yao, huku inachukuliwa ni kujiua - na tunaomba kinga kwa Allaah. Mwenye kuiua nafsi yake atadumishwa Motoni milele kama ilivyokuja katika Hadiyth yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Huyu aliyeiua nafsi yake hakuleta faida yoyote kwa Waislamu hata kwa wasiokuwa Waislamu. Kwa sababu akiua watu kumi, ishirini, mia au mia mbili, Uislamu haufaidiki chochote kwa hilo. Wala hilo haliwafanyi watu kuingia katika Uislamu. Tofauti na kile kisa cha yule kijana, yeye alisababisha watu wote wakaingia katika Uislamu. Hata hivyo haihitajiki kuua adui kumi, ishirini, mia au mia mbili kwa ajili watu waingie katika Uislamu. Kinyume chake huenda maudhi ya maadui ndiyo yakazidi kuwa mengi. Jambo hili ambalo Waislamu hawa wanafanya linapelekea makafiri kuzidisha maudhi yao dhidi ya Waislamu.
Mfano wa hili ni kama sasa jinsi mayahudi wanavofanya dhidi ya wapalestina. Mpalestina mmoja anapojilipua na kuua [mayahudi] sita mpaka saba, matokeo yake wanajilipiza kwa kuua wapalestina sitini, sabini au zaidi. Kwa hali hiyo kunakuwa hakuna faida yoyote kwa Waislamu wala hao waliojilipua. Ndio maana naona yeyote atakayefanya kitendo kama hicho atakuwa amejiua bila ya haki. Hili litasababisha yeye kuingia Motoni - na tunaomba kinga kwa Allaah. Aliyefanya hivo sio shahidi.
Lakini ikiwa mtu atafanya kitendo hiki kwa ujinga na huku akifikiria kuwa inajuzu, tunatumai kuwa hatopata madhambi. Hata hivyo hatofikia daraja ya aliyekufa shahidi kwa sababu
hakufanya kama anayekufa shahidi anavyopaswa kufanya. Lakini hatopama madhambi kwa kuwa amefanya hivo kwa kufahamu makosa. Yule mwenye kujitahidi na akakosea, anapata thawabu moja.