KINGA YA KILA SIKU DHIDI YA SHETANI, UCHAWI, HUSDA NA KILA UBAYA
Jamii ya vilivyomo
Full Description
بسم الله الرحمن الرحيم
KINGA YA KILA SIKU DHIDI YA SHETANI, UCHAWI, HUSDA NA KILA UBAYA.
Imeandaliwa na :Yunus Kanuni Ngenda.
Imepitiwa na :Abubakari Shabani Rukonkwa.
Uislam ni dini iliyokamilika katika kila idara miongoni mwa mambo ambayo pia yanapatikana ndani ya uislam ni kinga ya kisheria dhidi ya kila shari kama vile shetani,uchawi, husda, kijicho n.k.
Kinga hii ndiyo mujarrab na hupaswi kujikinga kwa hirizi wala chale kama wafanyiwavyo wengi miongoni mwa jamii ya wanaadamu na la kusikitisha zaidi katika kundi la wanaoamini na kufanya ushirikina huu ni waislam!
Ndugu zangu shirki ni jambo baya sana na ni miongoni mwa dhambi kubwa ambayo ALLAH amemuambia mtume wake kuwa
وَلَقَدۡ أُوحِىَ إِلَيۡكَ وَإِلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكَ لَٮِٕنۡ أَشۡرَكۡتَ لَيَحۡبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَـٰسِرِينَ
Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa walio kuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a'mali zako zitaanguka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kukhasiri
Surat Zumar: 65
Huyo ni mtume wa allaah vipi mimi na wewe?
Kwa kuzingatia hilo nimeona ni kheri leo nikawaletea taratibu sahihi za kujikinga ambazo unatakiwa udumu nazo kila siku asubuhi na jioni.
Ni matarajio yangu kwamba tutaendelea kuwa pamoja ili tuweze kufaidika na elimu hii ya bure kabisa kwa ajili ya kutafuta radhi za ALLAH.
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Laa Ilaaha Illa llaahu wahdahuu laa shariika lahu lahulmulku walahul hamdu wahuwa alaa kulli shai-in qadiir
mara 100 asubuhi na jioni
ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَىُّ ٱلۡقَيُّومُۚ لَا تَأۡخُذُهُ ۥ سِنَةٌ۬ وَلَا نَوۡمٌ۬ۚ لَّهُ ۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَمَا فِى ٱلۡأَرۡضِۗ مَن ذَا ٱلَّذِى يَشۡفَعُ عِندَهُ ۥۤ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَىۡءٍ۬ مِّنۡ عِلۡمِهِۦۤ إِلَّا بِمَا شَآءَۚ وَسِعَ كُرۡسِيُّهُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَۖ وَلَا يَـُٔودُهُ ۥ حِفۡظُهُمَاۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِىُّ ٱلۡعَظِيمُ
Allaahu laa ilaaha illaa huwalhayyul qayyuum laa ta-akhudhuhuu sinatun walaa nauum lahuu maa fis samaawaati wamaafil-ardhwi yashfa'u 'in-dahuu illaa bi-idhnihii ya'alamu maa baina aidiihim wamaa khalfahum walaa yhiitwuuna bishai-in min 'ilmihii illaa bimaa shaa-a wasi'a kursiyyuhus samaawaati wal-ardhwa walaa ya-uuduhuu hifdhuhumaa wahuwal'aliyyul'adhwiim.
mara 1 kila baada ya swala ya fardhi.
بِسۡمِ ٱللهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ (١) ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ (٢) لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ (٣) وَلَمۡ يَكُن لَّهُ ۥ ڪُفُوًا أَحَدٌ (٤(
Qul huwa llaahu ahadu.1) Allaahus Swamadu. 2) Lam yalid wa lam yuulad. 3) Wa lam yakunlahuu kufuwan ahad. 4)
Mara 3 kila baada ya swala ya fardhi.
بِسۡمِ ٱللهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ (١( مِن شَرِّ مَا خَلَقَ (٢( وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ (٣( وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّـٰثَـٰتِ فِى ٱلۡعُقَدِ (٤( وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ (٥(
Qul a'uudhu birabbil falaq. 1) Minsharri maa khalaq. 2) Wa minsharri ghaasiqin idhaa waqaba. 3) Wa minsharrin n affaathaati fil'uqad. 4) Wa minsharri haasidin idhaa hasada.5)
بِسۡمِ ٱللهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾ مَلِكِ النَّاسِ ﴿٢﴾ إِلَـٰهِ النَّاسِ ﴿٣﴾ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ ﴿٤﴾ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ ﴿٥﴾ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ ﴿٦﴾
Qul-a'uudhu birabbin naas.1) Malikin naas. 2) ILaahin naas.3) Minsharril was-waasil khannaas. 4) Alladhii yuwas’wisu fii swuduurin naas. 5) Minaljinnati wan naas.6)
Sura hizo tatu za unatakiwa kuzisoma kila baada ya swala ya fardhi mara 3, na wakati wa kulala.
Isipokua wakati wa kulala ukishazisoma hizo sura mara 3 unapulizia kwenye viganja vyako vya mikono kisha unajifuta mwili mzima.
أعوذ بكلمات الله التامات من شر ما خلق
A'uudhu bikalimaati LLaahi taammaati minsharri maa khalaqa. mara 3 baada ya Maghribi
بسم الله الذي لا يضر مع اسمه شيء في الأرض ولا في السماء وهو السميع العليم،
Bismi llaahi lladhiy laa yadhurru ma'asmihi shay-un fil-ardhwi walaa fis samaa-i wahuwas samii'ul-'aliim. mara 3 asubuhi na jioni.
Hizo ni baadhi ya nyiradi za Asubuhi, Mchana, Jioni na Usiku ambazo kwa nwenye kudum nazo basi mtu huyo atakua na kinga ya Allah! Kutokana na mambo tuliyozungumza hapo juu.
Tunamuomba Allah atulinde na kila shari, na atujaalie mwisho mwema. Ameen!!