Uzushi Wa Nusu Ya Sha’baan
Jamii ya vilivyomo
Vyanzo
Full Description
Zinduka (Tanabahi) Kuhusu Bid-ah (Uzushi) Ya Nusu Ya Sha’baan; Kufunga Swawm, Kumdhukuru Allaah Na Kuomba Du’aa.
Imeandaliwa na alhidaaya.com
Imepitiwa na Yunus Kanuni Ngenda
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi waa alihi wa sallam) ametahadharisha kuhusu bid’ah aliposema:
عليكم بسنتي وسنة الخلفاء الراشدين المهديين من بعدي، تمسكوا بها وعضوا عليها بالنواجذ، وإياكم ومحدثات الأمو، فإن كل محدثة بدعة ، وكل بدعة ضلالة و في رواية و كل ضلالة في النار
Kamateni Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa walioongoka baada yangu, zishikilieni na mzibane kwa magego (mzikamate kisawasawa). Na tahadharini na uzushi, hakika kila uzushi ni bid'ah na kila bid'ah ni upotevu. [Abu Daawuud na At-Tirmidhy] na katika riwaya nyingine: Kila upotevu ni kwenye Moto.
Shaykh Ahmad Baazmuwl alipoulizwa kuhusu: “Je, Bid’ah, hata bid’ah hiyo iwe ndogo vipi ni miongoni mwa madhambi makubwa? Au kuna ufafanuzi bayana wa hili?”. Alijibu:
Swali hilo jibu lake ni fupi! Swali hilo si sahihi (halikubaliki kuulizwa)! Na wala haliko katika manhaj ya Salaf. Kuweka vigawanyo, na kupiga mifano na mabishano ya kukubali bid’ah kwa kuhusisha na dhambi si katika manhaj ya Salaf!
Salaf walikuwa wakipinga bid’ah kikamilifu bila ya kuwekea mipaka kama walivyokuwa wakipinga dhambi, huku wakichukulia jambo la (bid’ah) kuwa ni dhambi. Lakini walolitilia nguvu kulikataza lilikuwa ni bid’ah na hivyo lilikuwa kwao ni jambo kuu!
Na vyovyote tutakavyotaka kuingia katika maudhui ya bid’ah na kutaka kuigawa katika bid’ah kubwa na ndogo, au aina za bid’ah (hoja inayotolewa kuunga mkono bid’ah kwamba ni: “bid’atun hasanah”), na mengineyo, basi mtu huyo hana isipokuwa analotaka ni kuwafanyiwa watu njia walichukulie jambo la bid’ah kuwa ni jambo jepesi. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikariri (katika khutba zake):
((..na kila bid’ah ni upotofu na kila upotofu ni Motoni))
Kwa hiyo tunamwambia muulizaji kwamba: “Baina yako na sisi ni Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((..na kila bid’ah ni upotofu na kila upotofu ni motoni))
Na huenda mmoja wenu akasema: “Vizuri! Lakini huenda ikawa ipo (bid’ah) ndogo”. Basi namjibu: “Njoo hapa! Njoo hapa usikilize Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na simulizi za Salaf.
Ama katika Hadiyth ni wale watu watu ambao mmoja wao alisema: “Mimi nitaswali usiku wote.” Mwengine akasema: “Mimi nitafunga Swawm mchana na wala sitofungua.” Na wa tatu akasema: “Mimi nitajiweka mbali na wanawake na sitaoa.”
Hao watu watatu walitaka kutekeleza vitendo hivyo wakidhania kwamba wanajikurubisha kwa Allaah (‘Azza wa Jalla). Lakini je, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia nini? Je aliwaambia: “Hayo ni mambo mepesi na sahali lakini yaachani na Allaah akujazeni kheri?”
Hapana! Bali aliwajibu:
((Ama mimi ninafunga na kufungua, ninaswali na kulala, ninaoa wanawake. Kwa hivyo yeyote atakaegeuka na kuwa kinyume na Sunnah (uongofu) yangu sio miongoni mwangu!))
Tazama aliwajibu nini! Aliwajibu:
((yeyote anayegeuka kinyume na Sunnah (uongofu) yangu sio miongoni mwangu!)
Huo ni mfano mmoja wa Hadiyth. Ama katika simulizi za Swahaabah, ni usimulizi wa ibn Mas-‘uwd (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuhusu watu walioketi kwa mzunguko wa duara Msikitini. Je walikuwa wakifanya nini?
Walikuwa wakimsabbih Allaah (wakisema: Subhaanah Allaah), wakimsifu Allaah (wakisema: AlhamduliLLaah), wakimpwekesha Allaah (wakisema: Laa ilaaha illa Allaah), wakimtukuza Allaah (wakisema: Allaahu Akbar). [Usimulizi kamili upo chini]
Je, walikuwa wako wapi watu hao? Je walikuwa disco? Au katika kiwanja cha michezo? Au katika baa? Hapana! Walikuwa wako Msikitini! Je, ibn Mas-‘uwd (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliwaambia nini? Aliwaambia:
“Naapa kwa Yule Ambaye roho yangu ipo mikononi Mwake! Aidha mupo kwenye njia (Dini) iliyoongoka zaidi kuliko njia ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ama munafungua milango ya upotofu!”
Hakuwaambia: “Naapa kwa Allaah, vitendo vyenu si sahihi lakini ni bid’ah ndogo Allaah awahidi! Na bid’a ndogo dhambi yake ni ndogo kuliko bid’ah kubwa, kwa hiyo acheni jambo hili Allaah Awabariki! Na watu watendo bid’ah kubwa dhambi zao ni kubwa kuliko nyinyi manofanya bid’ah ndogo!”
Hapana! Hapana! Hapana!
Bali aliwaambia: “Aidha mpo kwenye dini iliyoongoka zaidi kuliko Dini ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ama mnafungua milango ya upotofu!”
Hakuna kuyumbayumba wala kulifunika jambo, bali ni kudhihirisha haki au ubatilifu. Inapohusu Sunnah na bid’ah, basi ima ni haki au ubatilifu! Ndio maana maneno haya yatiliwe manani kama nilivyotaja awali.
[Usimulizi uliotimia wa kadhia hiyo ya watu waliokuwa wamekusanyika kumdhukuru Allaah Msikitini]:
عن عمرو بن سلمة (رضي الله عنه): كُنَّا نَجْلِسُ عَلَى بَابِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ قَبْلَ صَلاَةِ الْغَدَاةِ فَإِذَا خَرَجَ مَشَيْنَا مَعَهُ إِلَى الْمَسْجِدِ, فَجَاءَنَا أَبُو مُوسَى الأَشْعَرِيُّ فَقَالَ: َخَرَجَ إِلَيْكُمْ أَبُو عَبْدِ الرَّحْمَنِ بَعْدُ؟ قُلْنَا لاَ: فَجَلَسَ مَعَنَا حَتَّى خَرَجَ, فَلَمَّا خَرَجَ قُمْنَاإِلَيْهِ جَمِيعًا فَقَالَ لَهُ أَبُو مُوسَى: يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ إِنِّي رَأَيْتُ فِي الْمَسْجِدِ آنِفًا أَمْرًا أَنْكَرْتُهُ وَلَمْ أَرَ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ إلاَّ خَيْرًا. قَالَ: فَمَا هُوَ؟ فَقَالَ: إِنْ عِشْتَ فَسَتَرَاهُ. قَالَ: رَأَيْتُ فِي الْمَسْجِدِ قَوْمًا حِلَقًا جُلُوسًا يَنْتَظِرُونَ الصَّلاَةَ, فِي كُلِّ حَلْقَةٍ رَجُلٌ وَفِي أَيْدِيهِمْ حَصًى. فَيَقُولُ, كَبِّرُوا مِائَةً ,فَيُكَبِّرُونَ مِائَةً, فَيَقُولُ هَلِّلُوا مِائَةً, فَيُهَلِّلُونَ مِائَةً, وَيَقُولُ سَبِّحُوا مِائَةً, فَيُسَبِّحُونَ مِائَةً, قَالَ: فَمَاذَا قُلْتَ لَهُمْ ؟ قَالَ: مَا قُلْتُ لَهُمْ شَيْئًا انْتِظَارَ رَأْيِكَ وَانْتِظَارَ أَمْرِكَ. قَالَ أَفَلاَ أَمَرْتَهُمْ أَنْ يَعُدُّوا سَيِّئَاتِهِمْ وَضَمِنْتَ لَهُمْ أَنْ لاَ يَضِيعَ مِنْ حَسَنَاتِهِمْ؟ ثُمَّ مَضَى وَمَضَيْنَا مَعَهُ حَتَّى أَتَى حَلْقَةً مِنْ تِلْكَ الْحِلَقِ فَوَقَفَ عَلَيْهِمْ فَقَالَ. مَا هَذَا الَّذِي أَرَاكُمْ تَصْنَعُونَ؟ قَالُوا: يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ حَصًى نَعُدُّ بِهِ التَّكْبِيرَ وَالتَّهْلِيلَ وَالتَّسْبِيحَ. قَالَ: فَعُدُّوا سَيِّئَاتِكُمْ فَأَنَا ضَامِنٌ أَنْ لاَ يَضِيعَ مِنْ حَسَنَاتِكُمْ شَيْءٌ وَيْحَكُمْ يَا أُمَّةَ مُحَمَّدٍ, مَا أَسْرَعَ هَلَكَتَكُمْ هَؤُلاَءِ صَحَابَةُ نَبِيِّكُمْ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) مُتَوَافِرُونَ وَهَذِهِ ثِيَابُهُ لَمْ تَبْلَ وَآنِيَتُهُ لَمْ تُكْسَرْ. وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إِنَّكُمْ لَعَلَى مِلَّةٍ هِيَ أَهْدَى مِنْ مِلَّةِ مُحَمَّدٍ أَوْ مُفْتَتِحُو بَابِ ضَلاَلَةٍ. قَالُوا: وَاللَّهِ يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ مَا أَرَدْنَا إِلاَّ الْخَيْرَ. قَالَ وَكَمْ مِنْ مُرِيدٍ لِلْخَيْرِ لَنْ يُصِيبَهُ. إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) حَدَّثَنَا أَنَّ قَوْمًا يَقْرَءُونَ الْقُرْآنَ لاَ يُجَاوِزُ تَرَاقِيَهُمْ وَايْمُ اللَّهِ مَا أَدْرِي لَعَلَّ أَكْثَرَهُمْ مِنْكُمْ. ثُمَّ تَوَلَّى عَنْهُمْ فَقَالَ عَمْرُو بْنُ سَلَمَةَ: رَأَيْنَا عَامَّةَ أُولَئِكَ الْحِلَقِ يُطَاعِنُونَا يَوْمَ النَّهْرَوَانِ مَعَ الْخَوَارِجِ.
Kutoka kwa ‘Amru ibn Salamah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tulikuwa tumeketi mlangoni mwa ‘Abdullaahi bin Mas’ud kabla ya Swalaah ya Alfajiri, akatoka nje. Tukaenda naye Msikitini. Kisha Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy (Radhiya Allaahu ‘anhu) akatujia na kusema: “Je, Abu ‘Abdir-Rahmaan ameshakuja kwenu?” Tukasema: “Hapana!” Akaketi hadi akatoka nje na alipotoka nje tukasimama. Abu Muwsaa akamwambia: “Ee Abaa ‘Abdir-Rahmaan! Sasa hivi nimeona jambo Msikitini sijapatapo kuliona kabla, lakini sidhanii baya ila ni jambo jema”. Akasema: “Jambo gani?” Akasema. “Ukiendelea kuishi utaliona”. Akasema: “Nimeona Msikitini watu wameketi kwa mkusanyiko wa duara wakisubiri Swalaah. Katika kila duara alikuweko mtu na mikononi mwao mna changarawe. Mmoja wao akisema: “Semeni Allaahu Akbar mara mia!” nao wakisema “Allaahu Akbar!” mara mia. Kisha husema: “Semeni laa ilaaha illa-Allaah mara mia”! Nao husema “laa ilaaha illa-Allaah!” mara mia. Kisha husema: “Semeni Subhaana-Allaah mara mia!” Nao husema “Subhaana-Allaah!” mara mia. Akasema: “Je umewaambia nini?” Nikasema: “Sikusema lolote, nilikuwa nasubiri nione utaonaje na nikisubiri amri yako”. Akasema: “Kwa nini usiwaambie wahesabu vitendo vyao viovu na kuwahakikishia kwamba vitendo vyao vyema havitapotezwa?”
Kisha akasogea nasi tukaenda hadi alipofikia moja kati ya maduara hayo akasimama na kusema: “Mnafanya nini?” Wakasema. “Ee Abaa ‘Abdir-Rahmaan, hivi ni vijiwe tunavyohesabia takbiyr, tahliyl na tasbiyh”.Akasema: “Hesabuni vitendo vyenu viovu, kwani nakuhakikisheni kwamba vitendo vyenu vyema havitapotea hata kimoja! Ole wenu Ee Umma wa Muhammad! Ni kwa haraka gani munakimbilia kwenye uharibifu! Hawa ni Maswahaabah wa Mtume wenu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao wameenea. Hizi ndizo nguo zake ambazo bado hazijachakaa, na bakuli lake ambalo halijavunjika! Naapa kwa Yule Ambaye roho yangu ipo mikononi Mwake! Aidha mupo kwenye dini iliyoongoka zaidi kuliko Dini ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ama munafungua milango ya upotofu!”
Wakasema: “Ee Abaa ‘Abdir-Rahmaan, hatukukusudia lolote ila kheri tu”. Akasema: “Wangapi waliokusudia kheri hawakuzipata?” Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia: ((Watu wataisoma Qur-aan, lakini haitovuka zaidi ya koo zao)) “Naapa kwa Allaah! Mimi sijui, lakini pengine mengi kati ya hayo yanatoka kwenu!” Baadaye akaondoka. ‘Amr bin Salamah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tumewaona wengi kati ya watu hao wakipigana dhidi yetu katika siku ya Nahrawaan, wakiwa pamoja na Khawaarij
Sunan Ad-Darimy 206