Ubora wa hijja na faida zake
Jamii ya vilivyomo
Full Description
بسم الله الرحمن الرحيم
UBORA WA HIJA NA FAIDA ZAKE.
فضل الحج وفوائده
Imeandikwa na Dr.Jamali Almuraakibiy.
Imetafsiriwa na Abubakari Shabani Rukonkwa.
Imepitiwa na Yunus Kanuni Ngenda.
Utangulizi:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hija ninguzo kubwa miongoni mwa nguzo za uislam,ameifaradhisha Allah mtukufu kwa muislam mwenye uwezo kwakusema:
{ولله على الناس حج البيت من استطاع إليه سبيلا ومن كفر فإن الله غني عن العالمين }.
{آل عمران: 97}،
(Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu.) (Al 'Imran 97).
Nahawajaacha watu kutekeleza ibada ya hijja tangu alipo nyanyua na Ibrahim misingi ya ya nyumba tukufu ya Allah,na akawatangazia watu kutekeleza ibada ya Hijja kama alivyo muamrisha mola wake - Mshindi Mwenyenguvu- mpaka katika zama hizi,
Na haitamalizika ibada ya hijja kwamuda ambao kuna muislamu juu ya mgongo wa Ardhi,na pindi atakapo zitowa roho za waumini,nawakabakia juu ya mgongo wa Ardhi watu wenye kumuasi Allah(Watu washari katika viumbe) ambao watakao fikiwa na Qiyama wakiwa hai hapo ndipo utasiamama msafara wakwenda kuhijji kwenye nyumba ya Allah tukufu kama tutakavyo eleza.
FADHILA ZA HIJJA:
Fadhila zahija ninyingi na ziko tofautitofauti,miongoni mwa fadhila hizo:
1-Hijja nikatika ibada bora na nikatika ibada ambazo zinamkurubisha mja kwa molawake,katika hadithi alio ipokea Abuu hurayra –Radhi za allah ziwe juuyake-alisema :Aliulizwa mtume swala allahu alayhi wasalam:niipi ibada bora?akasema:Nikumuamini Allah na mtume wake,akaulizwa kisha nini?akasema mtume:"Nikupigana jihadi katika njia ya Allah" akaulizwa kisha nini? Akasema mtume :Nihijja ilio takasika.
(Imepokelewa na Bukharin a Muslim na Tirmithiy na Alnasaai na Ahmad)
2-Ibada ya hijja inalingana na Ibada ya kupigana jihadi katika njia ya Allah,na hija nibadala ya jihadi katika njia ya Allah kwayule ambae hakuweza kwenda kupigana jihadi.
Amepokea mama wa waumini bi Aisha –Radhi za Allah ziwe juu yake-alisema:Ewe Mtume wa Allah Tunaona jihadi ndio ibaada bora je kwanini nasisi tusipigane jihadi? Akasema mtume:"Hapana lakini Jihadi bora nihija ilio takasika".
Imepokelewa na Imamu Al-Bukhary katika kitabu cha hijja (No 1423).
-Nakatika upokezi mwingine:Nilimwambia mtume :"ewe mtume wa Allah unaonaje nasisi tutoke tukapigane vita nanyie?akasema:lakini vita vizuri na bora nikwenda kufanya ibada ya Hijja ilio takasika".
Akasema Aisha – Radhi za Allah ziwe juu yake - :Sinta acha kufanya hijja baada yakusikia maneno hayo ya mtume –rehma na amani ziwe juu yake-.
Al-Bukhary (1728).
Nakatika upokezi wa Imamu Annasaai:alisema Aisha:"ewe mtume wa Allah unaonaje na sisi tukatoka ili tupigane pamoja na wewe,hakika mimi sioni ibada ilio zungumziwa katika Quraan kwa ubora kuliko jihadi.
Akasema mtume-Rehma na amani ziwe juu yake-:Hapana,lakini jihadi nzuri na ilio bora nihija ilio takasika".
3-Hijja ilio takasika haina malipo yoyote ila pepo.
Kutoka kwa Abuu hurayra –Radhi za Allah ziwe juu yake-,utoka kwa mtume wa Allah - Rehma na amani ziwe juu yake-alisema:"Umra mpaka umra nyingine nikafara ya madhambi yaliopo baina yake,na hijji ilio takasika haina malipo ila nipepo".
{Imepokelewa na Imamu Al-Bukhary (1650)na Muslim (2403)}
4-Hijja ilio takasika nisababu yakufutiwa madhambi.
Kutoka kwa Abuu hurayra- Radhi za Allah ziwe juu yake-alisema:nilimsikia mjumbe wa Allah- Rehma na amani ziwe juu yake –akisema:"Atakae hijji kwaajili ya Allah na hakusema maneno ya upuuzi na hakufanya vitendo vya uovu,atarejea nyumbani baada yakumaliza hijja kama siku alio zaliwa na mamake".
Imepokelewa na Imamu Al-Bukhary (1424).
Nakutoka kwa Imamu Al-Tirmidhiy: "Atakae hijji kwaajili ya Allah na hakusema maneno ya upuuzi na hakufanya vitendo vya uovu atasamehewa madhambi yalio tangulia".(739).
5-Kukithirisha kufanya ibada ya Hijja na Umra vinafuta Umasikini.
قال رسول اللَّه صلى الله عليه وسلم : "تابعوا بين الحج والعمرة، فإن المتابعة بينهما تنفي الفقر والذنوب كما ينفي الكير خبث الحديد".
{الترمذي ح738 عن ابن مسعود، وابن ماجه ح2887 عن عمر، والصحيحة ح1200}.
Alisema mtume–rehma na amani ziwe juu yake-:"Fatisheni baina ya Hijja na Umra,hakika ufatisha hijja kwa kufanya umra kunaondoa umasikini na kufuta madhambi kama Kama mvukuto unavyo ondoa uchafu kutoka wenye chuma chenye kutu ".
Imepokelewa na tirmidhiy No (738).
kutoka kwa ibn Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake,na Ibn Maajah No(2887)kutoka kwa ibn Omar.
6-Mwenye kuhiji anakuwa mgeni wa Allah- tabaaraka wataala-,na mwenye kuwa mgeni wa Allah basi Allah atamkirim.
عن عمر رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: "الغازي في سبيل الله، والحاج، والمعتمر، وفد الله، دعاهم فأجابوه، وسألوه فأعطاهم". {ابن ماجه ح2893، الصحيحة 1820}.
وفي رواية: "الحجاج والعمار وفد الله، إن دعوه أجابهم، وإن استغفروه غفر لهم". {ابن ماجه ح2883}.
Kutoka kwa Omar-Radhi za Allah ziwe juu yake-kutoka kwa mtume - rehma na amani ziwe juu yake-alisema:"Mwenye kupigana jihadi katika njia ya Allah,na mwenye kuhiji,namwenye kufanya Umra,niwageni wa Allah,amewaita Allah wakamuitikaa,na wakamuomba Allah, akawapa yoote walio muomba"
Imepokelewa na ibn majah No(2893).
Nakatika upokezi mwingine:"mahujaji na wafanya Umra niwageni wa Allah,ikiwa wakimuomba atawapa,na wakimuomba msamaha atawasamehe".
Imepokelewa na ibn majah No(2883).
Faradhi ya hijja niyenye kudumu na kuendelea,mpaka baada ya kudhihiri fitna kubwa katika zama zamwisho,ili waweze kutekeleza ibada ya hija kwenye nyumba tukufu,na wafanye Umra baada ya kutoka Yajuja na Maajuja"
Imepokelewa katika (swahihu Aljaamiy No 5361).
Allah Atakapo chukuwa roho za waumini katika zama za mwisho,na ikawa hakubakiya aridhini ispokua viumbe vyenye shari,ambavyo vitakavyo fikiwa na Qiyama vikiwa hai,ndipo ibada yahijja itakapo simamishwa.
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : "لا تقوم الساعة حتى لا يحج البيت".
{صحيح الجامع 7419}.
Alisema mjumbe wa Allah- rehma na amani ziwe juu yake-:"Hakita simama Qiyama mpaka wakapo kua watu hawahiji"
Imepokelewa katika (swahihu Aljaamiy No 7419).
Kwasababu hii ndio ikawa wajibu kwa kila muislam mwenye kuweza afanye haraka kutekeleza ibada ya hijja,inaweza kuja siku akawa muislam anauwezo wakwenda kuhiji kisha ssiweze.
"من أراد الحج فليتعجل، فإنه قد يمرض المريض، وتضل الضالة، وتعرض الحاجة".
{صحيح الجامع}.
Alisema mtume wa Allah- rehma na amani ziwe juu yake-:"Atakae taka kuhiji basi afanye haraka,kwahakika anaweza kupatwa na maradhi,au kupotelewa na mali,au akapatwa na shida akashindwa kwenda kutekeleza ibada ya hija ".
Imepokelewa katika (swahihu Aljaamiy).
HABARI NJEMA KWA ATAKAE SHINDWA KUHIJI.
Nijuu ya muislam kujichumia malipo na ujira kama anao upata mtu alie kwenda kuhiji.
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : "من صلى الفجر في جماعة، ثم قعد يذكر الله حتى تطلع الشمس، ثم صلى ركعتين كانت له كأجر حجة وعمرة تامة، تامة، تامة".
{الترمذي عن أنس، صحيح الجامع 7346}.
Alisema mtume wa Allah- rehma na amani ziwe juu yake-:"Mwenye kuswali swala ya alfajiri kwa jamaa,kisha akabaki msikitini au sehemu alio swalia,akawa anamtaja Allah mpaka juwa likachomoza,kisha akaswali rakaa mbili za kuchomoza jua-(Shuruuq)-atapata malipo ya hijja na umra,zilizo timia,zilizo timia,zilizo timia ,".
Imepokelewa na Imamu Al-Tirmithiy kutoka kwa Anasi swahihu Aljaamiy No7346).)
MAMBO MEMA YANAYO ANGALIWA KATIKA IBADA YA HIJA:
1-Nikuitukuza Alkaaba kwasababu nikatika ibada za Allah na kufanya hivyo nikumtukza Allah mtukufu.
قال تعالى: إن أول بيت وضع للناس للذي ببكة مباركا وهدى للعالمين (96) فيه آيات بينات مقام إبراهيم ومن دخله كان آمنا ولله على الناس حج البيت من استطاع إليه سبيلاً {آل عمران: 96، 97}
Alisema Allah mtukufu:" Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote.(96) Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu.
(Al 'Imran 96-97).
وقال تعالى: ومن يعظم شعائر الله فإنها من تقوى القلوب {الحج: 32}.
Na alisema Allah mtukufu:" Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo".
(Hajj- 32).
2- NIKUFIKA URAFIKI NA UMOJA.
Wanakusanyika waislam kwa rangi tofauti na lugha tofauti na miji yao katika pahala pamoja,kwalengo la kumuomba Allah pekeyake,wakielekea kwenye nyumba moja,nalengo lao linakua moja,malengo na makusudio yao yanakua kitu kimoja,na Umma unakua nikama roho ya mtu mmoja.
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : "مثل المؤمنين في توادهم وتعاطفهم كمثل الجسد، إذا اشتكى منه عضو، تداعى له سائر الأعضاء بالحمى والسهر". {مسلم: 20/8}.
Alisema mtume wa Allah-rehma na amani ziwe juu yake-:"Mfano wa waumini katika kupendana na kuoneyana huruma nikama mwili wa binadamu,kinapo uguwa kiungo kimoja,viungo vingine vinaumwa kwa homa "
Imepokelewa na imamu Muslim( 8/20).
Hija inaonyesha nguvu kwa umoja wa kislam na musanyiko wa ulinzi wao,na kuinyoshe sheria yao.
قال تعالى: {وإذ جعلنا البيت مثابة للناس وأمنا...}البقرة 125
Alisema allah mtukufu:(Na kumbukeni tulipo ifanya ile Nyumba (ya Alkaaba) iwe pahala pa kukusanyikia watu na pahala pa amani) Al-Baqara125.
3-Nikuafikiyana baina ya mambo ambayo walio rithi watu kutoka kwa nabii Ibrahimu na mwanae Ismaili,na akayalingania Mtume Muhammad-rehma na amani ziwe juu yake-,Nakumbuka sehemu hizo na kuafikiyana huko pale alipo sema Allah mtukufu:
وإذ يرفع إبراهيم القواعد من البيت وإسماعيل ربنا تقبل منا إنك أنت السميع العليم (127) ربنا واجعلنا مسلمين لك ومن ذريتنا أمة مسلمة لك وأرنا مناسكنا وتب علينا إنك أنت التواب الرحيم (128) ربنا وابعث فيهم رسولا منهم يتلو عليهم آياتك ويعلمهم الكتاب والحكمة ويزكيهم إنك أنت العزيز الحكيم {البقرة: 127- 129}.
Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi(127).
Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.( 128)
Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
(Al-Baqara 127-128-129)
Na alikuwa mtume - rehma na amani ziwe juu yake- anawambia watu,katika hija yake ya kuaga:"simameni atika sehemu zenu tukufu hakika ninyi mko katika miradhi katika miradhi ya babaenu Ibrahim"
Sahihi Abii Daudi No1702).)
Na mtume- rehma na amani ziwe juu yake- alikua akisema:"chukueni kutoka kwangu ibada yenu ya hijja huenda sintakutana nanyinyi baada ya hija ya mwaka huu".
Imepokelewa na imamu Muslim.
4.Nikutangaza Tauheed ambayo ndio sababu ya kutumwa mitume,na kuidhihirisha katika maneno na vitendo.
Katika kusema Tlbiya,anasema mwenye kuhiji:
"لبيك اللهم لبيك، لبيك لا شريك لك لبيك، إن الحمد والنعمة لك والملك، لا شريك لك".
Labaika Allahuma labaika,labaika la sharika laka labaika,innalhamda waniimata,laka walmulku la shariika laka.
Maana yake:(Nimeitika ewe Allah nimekuitikia,Nimekuitikia ewe allah hauna mshirika nimekuitikia,Hakika sifa kamilifu na neema zote nizako hauna mshirika).
Nawalikuwa watu wakati wa ujahiliya wanaitika Talbiya ya ushirikina,wakisema:
(لبيك لا شريك لك ، إلا شريكا هو لك ، تملكه وما ملك)
Maana yake:(Nimeitika huna mshirika,ispokua mshirika ambae yeye niwako,unae mmiliki na vyote alivyo miliki).
Na baki ya sehemu na ibada ambazo anakua mja nimtumwa katika kumpwekesha Allah na kumtii Allah mshindi mtukufu,na kuchukua ahadi ya utii na mtume- rehma na amani ziwe juu yake-,basi anapita na kusimama pale alipo muamrisha Allah mtukufu,na Ananyoa nywele,na anachinja mnyama kwakufuata vile alivyo muamrisha Allah mtukufu,na anafuata vile alivyo fundisha mtume- rehma na amani ziwe juu-. yake-.
Ewe Allah mtukufu turuzuku uwezo wa kufanya Hija,na utupe taufiiqi ya kuyafanya yale unayo yapenda na kuyaridhia.Amiin.