×
Mada hii inazungumzia juu ya ubora wa ummat Muhammad s.a.w na kwamba ni umma wa mwisho duniani lakini akhera ndio umma utakaokua wa kwanza kuingia Peponi, pia mada hii inazungumizia namna walivyo tofautiana mayahudi na wakristo.

    بسم الله الرحمن الرحيم

    UMMATI MUHAMMAD UTAKUWA WA KWANZA KUINGIA PEPONI.

    Imeandaliwa na alhidaaya.com

    Imepitiwa na Yunus Kanuni Ngenda

    Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

    ((كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللّهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُواْ فِيهِ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلاَّ الَّذِينَ أُوتُوهُ مِن بَعْدِ مَا جَاءتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ فَهَدَى اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ لِمَا اخْتَلَفُواْ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ وَاللّهُ يَهْدِي مَن يَشَاء إِلَى صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ))

    ((Watu wote walikuwa ni Umma mmoja. Allaah Akapeleka Manabii wabashiri na waonyaji. Na pamoja nao Akateremsha Kitabu kwa Haki, ili kihukumu baina ya watu katika yale waliokhitalifiana. Na wala hawakukhitalifiana ila wale waliopewa Kitabu hicho baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi, kwa sababu ya uhasidi baina yao. Ndipo Allaah kwa idhini Yake Akawaongoa walioamini kuiendea haki katika mambo waliyokhitalifiana. Na Allaah Humwongoa Amtakaye kwenye Njia Iliyonyooka)) [Al-Baqarah: 213]

    Ibn 'Abbaas amesema kuhusu kauli hii: "Kulikuweko na vizazi (karne) kumi baina ya Aadam (‘AlayhisSalaam) na Nuuh (‘Alayhis Salaam), wote wakiwa katika dini ya haki. Kisha tena wakakhitilafiana, hivyo Allah Akatuma Mitume kama waonyaji na wabashiriaji" [Tafsiyr Ibn Kathiyr].

    Idadi ya Mitume ni 124,000 wakiwemo Wajumbe 313 kama ilivyo kauli ya wengi wa Maulamaa wa Ahlus-Sunnah wal Jama’ah. Mitume 25 wametajwa majina yao katika Qur-aan. [Aysarut-Tafaasiyr – Abu Bakr Al-Jazaairy 1:191]

    Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) alisema kuhusu kauli:

    ((فَهَدَى اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ لِمَا اخْتَلَفُواْ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ))

    ((Ndipo Allaah kwa idhini Yake Akawaongoa walioamini kuiendea haki katika mambo waliyokhitalifiana))

    Akasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

    ((نَحْنُ الْآخِرُونَ الْأَوَّلُونَ يَوْم الْقِيَامَة نَحْنُ أَوَّل النَّاس دُخُولًا الْجَنَّة بَيْدَ أَنَّهُمْ أُوتُوا الْكِتَاب مِنْ قَبْلنَا وَأُوتِينَاهُ مِنْ بَعْدهمْ فَهَدَانَا اللَّه لِمَا اِخْتَلَفُوا فِيهِ مِنْ الْحَقّ بِإِذْنِهِ فَهَذَا الْيَوْم الَّذِي اِخْتَلَفُوا فِيهِ فَهَدَانَا اللَّه لَهُ فَالنَّاس لَنَا فِيهِ تَبَع فَغَدًا لِلْيَهُودِ وَبَعْد غَد لِلنَّصَارَى)) البخاري, مسلم , مسند أحمد

    ((Sisi ni (Ummah) wa mwisho lakini ni wa kwanza siku ya Qiyaamah. Sisi ni wa kwanza kuingia Peponi ingawa wao (Mayahudi na Manaswara) walipewa Kitabu kabla yetu nasi tumepewa baada yao. Allaah Ametuongoza katika haki katika waliyokhitilafiana kwa idhini Yake. Hii ni siku (Ijumaa) waliyokhitilafiana, nasi Allah Ametuongoza nayo Hivyo watu wanatufuata kwani kesho (Jumamosi) ni siku ya Mayahudi na inayofuatia (Jumapili) ni ya Manaswara)) [Al-Bukhaariy, Muslim, Musnad Ahmad na wengineo]

    Ibn Wahb amesema kwamba 'Abdur-Rahmaan bin Zayd bin Aslam amesema kuwa baba yake amesema kuhusu Aayah hii:

    ((فَهَدَى اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ لِمَا اخْتَلَفُواْ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ))

    ((Ndipo Allaah kwa idhini Yake Akawaongoa walioamini kuiendea haki katika mambo waliyokhitalifiana))

    · Wamekhitilafiana kuhusu siku ya Jamaa (Ijumaa); Mayahudi wamesema ni Jumamosi, Manaswara wamesema ni Jumapili, Allaah Akaongoza Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kufuata Ijumaa.

    · Wamekhitilafiana kuhusu Qiblah; Manaswara wameelekea Mashariki na Mayahudi wameelekea Baytul-Maqdis (Palestina), Allaah Akaongoza Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Qiblah sahihi (Ka'bah iliyoko Makkah).

    · Wamekhitilafiana kuhusu Swalah; wengine wanarukuu lakini hawasujudu, wengine wanasujudu lakini hawarukuu, wengine wanaswali huku wakizungumza na wengine huku wanatembea. Allaah Amewaongoza Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika haki.

    · Wamekhitilafiana pia katika kufunga (Swawm); wengine wanafunga sehemu tu ya siku, wengine wanafunga kujizuia tu baadhi ya vyakula (vingine wanakula). Allaah Ameongoza Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika haki.

    · Wamekhitilafiana pia kuhusu Nabii Ibraahiym; Mayahudi wamesema "Alikuwa ni Myahudi" na Wakristo wakidai ni Mnaswara. Allaah Amemfanya ni Haniyfam-Musliman (Muongofu Muislamu) Allaah Ameongoza Ummah wa Muhammad katika haki.

    · Wamekhitilafiana pia kuhusu Nabii 'Iysaa; Mayahudi wamemkanusha na kumzulia mama yake kuwa kafanya madhambi makubwa (ya zinaa), Manaswara wamemfanya ni Mungu na mtoto wa mungu. Allaah Amemfanya kwa maneno Yake ni roho kutoka Kwake (Kwa Alivyoviumba) Allaah Ameongoza Ummah wa Muhammad katika haki"

    Kisha (muelezeaji) akamalizia maelezo hayo kwa kusema (Kwa idhini Yake [Allaah]) (kamailivyoendeleza Aayah hiyo tukufu kuwa sisi Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tumeongozwa na Allaah kwa Idhini Yake).

    ((فَهَدَى اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ لِمَا اخْتَلَفُواْ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ))

    ((Ndipo Allaah kwa idhini Yake Akawaongoa walioamini kuiendea haki katika mambo waliyokhitalifiana))

    Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anhaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapoamka usiku akisoma duaa ifuatayo:

    اللّهُـمَّ رَبَّ جِـبْرائيل ، وَميكـائيل ، وَإِسْـرافيل، فاطِـرَ السَّمواتِ وَالأَرْض ، عالـِمَ الغَيْـبِ وَالشَّهـادَةِ أَنْـتَ تَحْـكمُ بَيْـنَ عِبـادِكَ فيـما كانوا فيهِ يَخْتَلِفـون. اهدِنـي لِمـا اخْتُـلِفَ فيـهِ مِنَ الْحَـقِّ بِإِذْنِك ، إِنَّـكَ تَهْـدي مَنْ تَشـاءُ إِلى صِراطٍ مُسْتَقـيم

    Allaahuuma Rabbi Jibraaiyl wa Miykaaiyl, wa Israafiyl, Fatwiras-Samawaati wal-ardhw, 'Aalimal-Ghaybi wash-Shahaadah, Anta Tahkumu bayna 'Ibaadika fiymaa kaanu fiyhi yakhtalifuun. Ihdiniy lima-khtulifa fiyhi minal-Haqq Biidhnika, Innaka Tahdiy man Tashaau ilaa Swiraatwim Mustaqiym.

    Ee Allaah Mola wa Jibriyl na Mikaaiyl na Israafiyl, Muumba wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa mambo yaliyojificha na yaliyowazi, Wewe Unahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitofautiana, niongoze mimi kwenye haki katika yale waliotofautiana kwa ruhusa Yako. Hakika Wewe Unamuongoza Umtakae kwenye Njia Ilionyoka.

    Zaidi ya du'aa hiyo inatupasa pia tuombe du'aa ifuatayo daima ili tubakie katika haki,

    اللَّهُمَّ أَرِنَا الْحَقّ حَقًّا وَارْزُقْنَا اِتِّبَاعه وَأَرِنَا الْبَاطِل بَاطِلًا وَارْزُقْنَا اِجْتِنَابه وَلَا تَجْعَلهُ مُتَلَبِّسًا عَلَيْنَا فَنَضِلَّ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا

    Allaahumma Arinal-Haqqa Haqqan War-Zuqnat-tibaa'ah. Wa Arinal-Baatwila baatwilan War-Zuqnaj-tinaabah. Wa laa taj'alhu mutalabbisan 'alaynaa Fanadhwilla Waj-'alnaa Lil-Muttaqiyna Imaama.

    Ee Allaah, Tuonyeshe yale yaliyo haki, Uturuzuku tuweze kufuata (na kutekeleza).

    Na Tuonyeshe yaliyo batili (maovu) na Utuongoze tujiepushe nayo.

    Usituchanganye (usitufunike tusiiujue) hakika ya uovu ili tusipotee kuufuata, na Tujaaliye tuwe viongozi wa Wamumini))

    [Takhiryj Al-Ihyaaa 3: 1318].