×
Makala hii inazungumzia hukumu za hija tangu alhaji kufika makkah mpaka anamaliza ibada ya hija.

    بسم الله الرحمن الرحيم

    MWENYE KUHIJI (TAMATUU) ANANUWIYA KWA KUSEMA: "LABAIKA ALLAHUMA UMRA MUTAMATIUN BIHA LILHAJI"

    MWENYE KUHIJI (QIIRAN) ANANUWIYA KWA KUSEMA: "LABAIKA ALLAHUMA HIJJA WA UMRA".

    MWENYE KUHIJI (IFRADI) ANANUWIYA KWA KUSEMA: "LABAIKA ALLAHUMA HIJJAH".

    SIKU

    -Inatakiwa mwenye kuhiji (TAMATUU) ahirimie afikapo (MIQAT) na anuwiye kufanya umra na kisha aanze kutowa Talbiya) (LABAIKA ALLAHUMA LABAIKA LABAIKA LA SHARIKA LAKA LABAIKA……NK).

    -Anatakiwa afanye twawafu ya umra kisha afanye saayi baina ya swafa na mar`wa ya umra, kisha aswali rakaa mbili nyuma ya Maqamu Iburahim ikiwa ataweza.

    -Ni sunna apunguze nywele zake badala ya kunyoa ili zibaki nywele atakazo nyoa pindi atakapo maliza hijja.

    (Inampasa kupunguza au kunyoa hata kama itakuwa ni kwa yule aliye chinja mnyama au akamuwakilisha mtu au bank imchinjie).

    Na pindi atakapo maliza kufanya Umra yote yaliokuwa haramu kwake yatakua ni halali kama kujipaka manukato au kufanya tendo landoa, nk.

    -Niwajibu kuhirimiya katika mipaka (MIQAT) anatakiwa anuwiye kuhiji kisha aanze kutoa Talbiya: (LABAKA ALLAHUMA LABAIKA LABAIKA LA SHARIKA LAKA LABAIKA……NK).

    -Ni sunna kwa mwenye kuhiji kufanya twawafu yakufika makkah.

    -Inajuzu kutanguliza saayi ya hijja baada ya kufanya twawafu ya kufika.

    -Anatakiwa mwenye kuhiji abaki amevaa ihram.

    SIKU YAKUFIKA MAKKAH.

    -Katika siku ya nane Mahujaji wanatakiwa kuelekea Mina, na yule alie hiji Tamatuu anapotoka Makkah au katika mipaka ya Haram niya yake inabakia isipokua atakapo rudi nyumbani kwake (yaani nchini kwake akawa hakumalizia hijja).

    - Na nisunna kwa mwenye kuhiji asichelewe kutia niya ya hijja katika siku hiyo.

    -Katika kutekeleza ibada ya swala kwa Alhaji atapunguza swala zenye rakaa nne nakuswali rakaa mbili na bora asikusanye ila atakapo hitaji kufanya hivyo.

    -Anatakiwa Alhaji azidishe kusema:

    (ALLAHU AKBAR ALLAHU AKBAR LAILAHA IL ALLAH ALLAHU AKBAR ALLAHU AKBAR WALILAHIL HAMDU).

    SIKU YA TARWIYA (8)

    Nisunna kwenda katika viwanja vya Arafa baada ya kuchomoza jua-

    -Alhaji akiwa katika viwanja vya arafa ataswali Adhuhuri na Alasiri kwa kuzikusanya na kuzipunguza katika wakati wa Adhuri, kwa adhana moja na Iqama mbili.

    -Alhaji anatakiwa azidishe matendo mema na azidishe dua, hiyo ndiyo ibada bora kwa atakae jaaliwa kufikishwa na Allah katika viwanja vya Arafa.

    -Alhajji anatakiwa akithirishe kuomba dua na ni sunna kuelekea kibla na kunyanyua mikono wakati wakuomba dua.

    -Alhajji anatakiwa kuja kua kuomba dua hali ya kua umeuelekea mlima (Jabal Rahma) ni bidaa, yaani ni uzushi uliokatazwa katika dini.

    Alisema mtume –swala allah alaihi wasalam-:"Dua bora nidua ya siku ya Arafa na maneno bora ambayo niliyo yasema mimi na mitume waliopita kabla yangu :

    ....(لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ ،لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ).

    "Laa Illaha ila LLah wahdahu la sharika lahu lahul mulku walahul hamdu wahuwa ala kuli shay in qadiir".

    -Ni kuelekea muzdalifa baada ya kutoka Arafa baada ya kuzama jua, mwenye kuhiji ataswali akiwa muzdalifa, Maghribi na Ishaa kwa kukusanya na kupunguza swala za rakaa nne, kwa adhana moja na iqama mbili, na sio sunna kuswali swala ya suna baada ya swala hizo ila ikiwa nisunna ya witri.

    -Ni kulala Muzdalifa na kuswali alfajiri katika mwanzo wa wakati wake, atakaa hapo muzdalifa mpaka kupambazuke, kisha ataelekea Mina kabla ya juwa kuchomoza, na kwa wale wenye ulemavu wasioweza kutembea au wagonjwa inajuzu kwao kwenda mina katikati ya usiku.

    SIKU YA ARAFA (9)SIO SHERIYA KWA ALHAJI KUFUNGA SIKU YA ARAFA.

    -Nikuelekeya mina.

    -Ni kukusanya vijiwe njiyani au kuvichukua ukiwa mina, na hayafai mawe yaliyo tengenezwa kama cement na chokaa nk….

    Ukubwa wa vijiwe hivyo nikama tembe ya (Himswi).-

    -Inafaa kuchukuwa vijiwe karibu na jamarati, na si kuchukua vijiwe katika Haudhwi (yaani sehem yanapodondokea mawe baada ya kutupwa kwenye kiguzo)m.

    -Ni kutupa vijiwe saba katika kiguzo kikubwa (Jamaratul Aqaba Alkubraa) na niwajibu vijiwe viangukie katika Haudhwi (yaani sehem yanapodondokea mawe baada ya kutupwa kwenye kiguzo).

    -Ni kunyoa au kupunguza nywele, na kunyoa nibora kuliko kupunguza kwa wanaume, na mwanamke atapunguza kiasi (UNMULA).

    -Kuhalalika kwa kuvua ihramu ni kuhalalika kwa mwanzo.

    -Kutufu Alkaaba (TWAWAFUL IFADHWA) ni nguzo katika Hijja, na kufanya (SAAYI) baina ya swafaa na marwa ni nguzo kwa yule anaehiji (TAMATUU), na kufanya hiyo saayi ni ya hijja na sio ile aliyoifanya kwa ajili ya Umra.

    -Ama yule aliyehiji (IFRADI) au (QIRAAN) yeye hatofanya saayi ikiwa alifanya SAAYI baada ya kufanya twawafu (kutufu) pindi alipoingia makkah (TWAAFUL QUDUUM), kwa huyu mwenye kuhiji Qiiraan au Ifraad na alitanguliza Saayi alipofika makkah akinyoa siku ya kumi huwa amehalalika kuhalalika kwa mara yapili.

    -Atakae tanguliza Ibada kabla ya nyingine katika matendo ya hijja inaswihi na hakuna tatizo lolote.

    -Baada ya kuhalalika kwa mara ya kwanza niharamu kufanya tendo landoa, na baada ya kuhalalika kwapili inajuzu kufanya tendo la ndoa kwa mume na mke.

    SIKU YAKUCHINJA (10)

    NIKATIKA MASIKU BORA KWA MWENYEZI MUNGU MTUKUFU,NISIKU YAKUCHINJA ALIE HIJI (TAMATUU),NA (QIRAAN),WANYAMA WAO,NAYOYOTE ALIE PELEKA WANYAMA MAKKAH ATA HALALIKA MPAKA ATAKAPO CHINJA WANYAMA WAKE.

    Kulala Mina zaidi ya siku moja ni wajibu.-

    -Ni kutupa vijiwe katika viguzo vitatu (JAMARATI) kila kiguzo kimoja atatupa vijiwe saba, atatoa takbiir (ALLAHU AKBAR) kwa kila kijiwe, na ataanza kutupa vijiwe kwenye kiguzo kidogo, nisunna kumuomba Allah baada ya kutupa vijiwe haliyakuwa ameelekea kibla, na nimwenye kunyanyua mikono yake, kisha atatupa kiguzo cha kati, na ataomba dua akiwa ameelekea kibla na kunyanyua mikono yake, kisha atatupia kijiwe kikubwa vijiwe saba na ataondoka bila kuomba dua.

    -Haijuzu kufunga katika masiku ya kukaa mina kwa mahujaji ispokua aliye hiji TAMATUU au QIIRAAN, na hakupata wanyama wa kuchinja.

    SIKU YA (11)

    Ni kulala Mina.-

    Ni kutupa viguzo vitatu (JAMARATI) baada ya kukengeuka kwa jua-

    -Kwa yule mwenye haraka yakuondoka mina anatakiwa aondoke kabla ya swala ya Maghribi, na atakaeanza kwene basi hata magharibi ikimkuta njiani hukumu yake ni hukumu ya mwenye kuondoka.

    -Kutufu kwa ajili ya kuiaga nyumba ya Allah (TWAWAFUL WADAA) Ni wajibu ila kwa mwanamke mwenye Hedhi au mgonjwa.

    SIKU YA (12)

    Ni kutupa viguzo vitatu (JAMARATI) baada ya kukengeuka kwa jua.-

    Ni kuondoka mina.-

    Ni kutufu twawafu ya kuaga (TWAWAFUL WADAA)-

    SIKU YA (13)

    أحكام الحج

    [email protected]

    Imeandikwa na Shekh:Abdurahmani bin Muhamad Al-Harfy

    Imetafsiriwa na Abubakari S. Rukonkwa

    Imepitiwa na Yunus Kanuni ngenda

    NGUZO ZA UMRA

    1.Nikuhirimiya,Nako nikuweka niya yakuingia katika ibada,nania pekee inatoshelezea ,na kuitamka nisunnah.(Nasuna hii nisunna kuitamka katika nia ya Umra ao Hijja).

    2.Nikutufu kwenye alkaaba.

    3.nikufanya Saayi baina ya swafa na marwa.

    NGUZO ZA HIJJA:

    1.Ni kuhirimiya, nako ni kutia niya ya kuingia katika ibada, na niya pekee inatoshelezea, na kuitamka ni sunnah. (Na sunna hii ya kutamka ni katika niya ya Umra au Hijja).

    Akitaka kuhirimiya hijja kwamtu anae ishi ndani ya mipaka ya makkah basi atahirimiya nyumbani kwake.

    2.Ni kusimama katika viwanja vya Arafa.

    TNB: (HII NDIYO NGUZO KUBWA YA HIJA INAANZA TANGU KUTOKA KWA ALFAJIRI YA SIKU YA ARAFA MPAKA KUTOKA KWA ALFAJRI YA SIKU YA IDDI)

    Wakati wowote utakapo simama katika muda huo itaswihi sawa iwe usiku au mchana.

    3.Ni kufanya twawafu ya hijja (TWAWAFUL IFADHWA).

    4. Ni kufanya saayi baina ya swafa na marwa.

    UZINDUO KWA MWENYE KUTAKA KUHIJI:

    a. Mwenye kuacha kuweka niya ya kuingia katika ibada ya Hijja au Umra basi hana Hijja wala Umra.

    b. Atakaepitwa na kusimama katika viwanja vya Arafa hatakuwa na hijja na kama aliharibikiwa na gari au usafiri au foleni au maradhi ikiwa aliweka niya kwamba ikishindikana kufika Arafa ahalalike pale atakapoishia njiani basi atafanya Umra.

    Nakama hakuweka niya hiyo kisha akashindwa kufika Arafa atahalalika kwa kufanya umra kisha atachinja mnyama kisha atalipa hijja mwaka utakaofata Allah akimfikisha.

    c. Mwenye kuacha kufanya twawafu au akaacha kufanya saayi niwajibu kwake arudi makka afanye twawafu au saayi hatakama amesha toka nje ya mipaka ya Makkah na hana fidiya yoyote.

    MAMBO YA WAJIBU KATIKA HIJJA:

    1. Nikuhirimiya katika mipaka yoyote ya kuingia makkah. (Akipita mipaka bila kuweka nia anatakiwa kurejea na hakuna fidiya yoyote, na ikiwa atahirimiya baada ya kuivuka mipaka hiyo atalazimika kutowa fidiya ya Damu).

    2. Nilazima kukaa Mina zaidi ya siku moja katika masiku ya kuanika nyama.

    3. Kutupa vijiwe (na vinakuwa vijiwe saba kwa kila nguzo akiacha jiwe moja atatowa fidiya ya Damu).

    4. Nikunyoa au kupunguza.

    5. Nikutufu twawafu ya kuaga.

    TNB: MWENYE KUACHA CHOCHOTE KATIKA HAYO YALIO ELEZWA HAPO JUU NIJUU YAKE KUTOA FIDIYA YA KUCHINJA MBUZI AU KONDOO AKIWA MAKKAH NA AWAGAWIE MASIKINI WA MAKKAH NA KAMA HAWEZI KWA UMASIKINI WAKE BASI ALLAH ANAMUONA KWAHIYO HATA TOA CHOCHOTE.

    MAMBO YA TAHADHARI KWA ALIE HIRIMIYA HIJJA.

    1. MAMBO AMBAYO AKIYAFANYA ALIE HIRIMIYA HIJJA HATAKIWI KUTOWA FIDIA.

    -Ni kufunga ndoa, na hukumu ya ndoa hiyo nibatili pindi atakapo kuwa walii au mmoja kati ya mume au mke amehirimiya Hijjah.

    2. MAMBO AMBAYO AKIYAFANYA ALIE HIRIMIYA HIJA ANATOA FIDIA MFANO WAKE.

    -Ni kuwinda, kiwindwa kitakadiriwa na wataalamu na wenye uzoefu, kinapo kuwa hakikukadiriwa na maswahaba na mataabii –Radhi za allah ziwe juu yao-.

    3. MAMBO AMBAYO AKIYAFANYA ALHAJI ANATAKIWA KUCHINJA MNYAMA.

    - Ni kufanya tendo landoa,

    mwenye kufanya tendo hilo akiwa katika ibada ya hijja anahali mbili:

    1. Ikiwa amefanya tendo la ndoa kabla ya kuhalalika ya kwanza, (yaani kabla haja tupa mawe siku ya kumi au kuchinja na kunyoa mawili katika ya hayo matatu) Hija yake inakuwa imeharibika, na niwajibu arudie tena mwaka mwingine, na anapaswa achinje mnyama, na atubie kwa Allah.

    2. ikiwa amesha fanya tahalulu ya kwanza anatakiwa akahirimie katika mpaka wa (TANIIIM) kisha amalizie ibada zilizo bakiya na itamlazimu achinje Mbuzi au Kondoo ,kisha atubie kwa Allah tauba ya kweli.

    4. MAMBO AMBAYO YANATAKIWA KUTOA DAMU KWA KUKHIYARISHWA.

    -Ni mwanaume kufunika kichwa kwa kitu ambacho kinacho shika kichwa kama vile kofia au kilemba nk……

    -Kujipaka manukato (Inajuzu kutumia shampoo na sabuni na mafuta yenye harufu ya kemikali).

    -Ni kuvaa nguo ilioshonwa kwa mtindo wa viungo kama shati au flana au suruwali nk… na hii nikwa mwanaume.

    -Ni kukata kucha na (Inajuzu kukata kucha iliyokatika yenyewe kwakua inaudhi na kuleta maumivu makali).

    -Ni kuchezeana mke na mume ikiwa atatokwa na maji ya uzazi atatoa fidiya.

    -Ni kupunguza nywele (inajuzu kuchana nywele hata kama zitadondoka baadhi).

    Mwenye kufanya chochote katika hayo tuliyoyaeleza hapo juu atakhiyarishwa baina ya mambo yafuatayo:

    1. kuchinja mbuzi au kondoo akiwa makkah na kugawa nyama yake, na hatakiwi kula chochote katika nyama hiyo.

    2. Au kuwapa chakula masikini sita (6) atawapa akiwa Makkah.

    3. Atafunga siku tatu sehemu yoyote sawa akiwa makkah au akisharudi.