×
-

 Makasisi Waingia Uislamu

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MAKASISI WAINGIA UISLAMU

  

 1. KASISI YUSUFU ESTES ALIYEKUWA MFANYABIASHARA WA KIKRISTO & MUHUBIRI (USA[1])

Sasa hivi jina langu ni Yusufu Estes, lakini miaka iliyopita rafiki zangu walikuwa wakiniita Skip. Nimeshahubiri Ukristo na kufanya kazi za burudani na muziki tangu nilipokuwa mdogo katika miaka ya hamsini. Mimi na baba yangu tulianzisha duka la muziki, vipindi vya t.v, redio na burudani za nje ya nyumba kwa ajili ya kujifurahisha na (kujinufaisha). Nilikuwa mchungaji wa upande wa muziki, pia nilikuwa naendesha farasi na kuwaburudisha watoto nikiwa ni (Skippy the Clow).

Niliwahi kutoa huduma ya uwakilishi katika mazungumzo ya amani ya viongozi wa kidini wa Umoja wa Mataifa, kwa sasa mimi ni mstaafu wa taasisi ya kutunza taarifa za wafungwa nchini Marekani. Vilevile nafanyakazi pamoja na wanafunzi wa Kiislamu, jumuia za vijana na shule za watoto wa Kiislamu. Kwa hiyo, natembea ulimwengu mzima, nikitoa mihadhara na kushiriki katika kutoa ujumbe wa Kristo katika Quran kwenye Uislamu. Tumeshafanya mazungumzo na mijadala ya pamoja na watu wa imani zote na tumefurahia kufanya kazi ubavuni mwa marrabi[2] wa Kiyahudi, wachungaji, wahubiri na mapadri wa kila sehemu. Baadhi ya kazi zetu zinafanyika katika maeneo ya ustawi wa jamii, jeshi, vyuo vikuu na majela. Kimsingi lengo letu ni kuelimisha na kufikisha ujumbe sahihi wa Uislamu na kufahamisha ni nanihasa ndio Waislamu wa kweli. Ingawa kwa sasa Uislamu umeshakua na kuukaribia Ukristo ambao ni dini kubwa duniani. Tumeona wengi katika wale wanaodai kuwa ni Waislamu, hawafahamu vizuri hata kutangaza ujumbe wa “Amani, utiifu, na kusalimu amri kwa Mwenyezi Mungu. [Arabic = ‘Islam’]

Ilitokeaje: Inawezekana kuonekana ni ajabu sana, huku ikiwa huenda tukashirikiana baadhi ya taswira chache zilizotofauti tofauti pia itikadi juu ya Mungu, Yesu, Utume, dhambi na uwokovu. Lakini unajua tena, kipindi fulani nilikuwa katika boti moja na watu wengi walio katika boti hiyo sasa hivi. Kwa hakika nilikuwemo. Acha nieleze.

Nimezaliwa katika familia ya Kikristo madhubuti sana katika Midwest. Familia yetu na wazee wake sio tu wamejenga makanisa na shule katika ardhi hii ya Midwest, pia walikuwa ni miongoni mwa watu wa mwanzo kufika hapo. Nilipokuwa shule ya msingi, tulikuwa tunakaa Huston, Texas mwaka 1949 (nikiwa ni mtu mzima). Kila siku tulikuwa tunaenda kanisani na nilibatizwa Pasadena, Texas nikiwa na umri wa miaka 12. Nikiwa kijana wa umri wa miaka kumi na kitu, nilipendelea kutembelea makanisa mengine ili nijifunze zaidi mafundisho na imani zao. Kanisa la Kibatisti, Methodisti, Episcopalians, Charismatic movement, Full Gospel, Agepe, Katoliki, Presbyterians, na mengine mengi. Nilikuwa nimeshapevuka vizuri na kiu ya (Injili) au kama tuiitavyo; “Habari njema.” Uchunguzi wangu juu ya dini haukuishia Ukristo, hata kidogo. Ulishirikisha, dini ya Kihindu, Kiyahudi, Kibudha, Metaphizikia, imani za wamarekani asilia. Na ilikuwa ni dini moja tu ambayo sijaitazama kwa makini, nayo ilikuwa ni “Uislamu” Kwa nini? Swali zuri.

Mchungaji wa Muziki

Kwa vyovyote vile, nilikuwa navutiwa sana na aina mbali mbali za muziki, na hasa hasa muziki wa Injili na Klasikia. Kwa kuwa familia yangu yote ilikuwa ni ya kidini na muziki ilioufuata ndiyo huo huo nilioufuata na nikaanza masomo yangu katika maeneo hayo mawili. Mambo yote hayo yamenifanya niwe katika nafasi mwafaka ya uchungaji wa muziki katika makanisa mengi ambayo nilikuwa mshiriki wake kwa miaka mingi. Nilianza kufundisha ala ya Kibodi mnamo mwaka 1960 na hadi kufikia 1963 nilikuwa namiliki studio yangu mwenyewe eneo la Laurel, Maryland, iitwayo ‘Estes Music Studiy.’

Miradi ya Biashara mjini Texas, Oklahoma na Florida.

Miaka therathini iliyofuata, mimi na baba, tulifanya kazi pamoja katika miradi mingi ya kibiashara. Tulikuwa na vipindi vya burudani, kuonyesha shoo na vivutio. Tulifungua maduka ya piano na vinanda katika maeneo yote kuanzia Texas na Oklahoma hadi Florida. Tulichuma mamilioni ya dola katika miaka hiyo, lakini hatukupata utulivu wa moyo ambao unaweza kuja kwa kupitia kuufahamu ukweli na kuupata mpango sahihi wa uwokovu tu. Nina hakika kuwa umeshajiuliza swali hili “Kwa nini Mungu ameniumba?” au “Mungu ananitaka nifanye nini?” au “Nani ndiye Mungu wa kweli, kwa vyovyote vile?” “Kwa nini tunaamini dhambi ya asili?” na “Kwa nini wanadamu wamelazimishwa wakubali ‘dhambi’ za Adamu na kisha matokeo yake waadhibiwe milele?” Lakini kama utamuuliza mtu yeyote maswali hayo, watakujibu kuwa unalazimika uamini bila ya kuhoji, au kuwa hiyo ni “siri isiyoelezwa” na hutakiwi kuuliza “Kaka wewe amini tu.”

Maana ya Utatu

Jambo la kushangaza sana, neno ‘utatu’ halimo katika Biblia. Na limekuwa likihusishwa na wanazuoni wa kidini mapema mnamo miaka mia mbili baada ya kunyanyuliwa kwa Yesu kwenda kwa Mungu wake Muweza. Ningewaomba wahubiri na wachungaji wanipe japo fikra, vipi ‘moja’ itapigwa hesabu ili iwe ‘tatu’ au vipi Mungu mwenyewe awezaye kufanya kila kitu atakacho, hawezi kuwasamehe watu na dhambi zao, isipokuwa hadi ajifanye mwanadamu, aje chini duniani, awe mtu, na kisha achukuwe madhambi ya watu wote; huku tukiweka akilini kuwa pamoja na hayo yote yeye ni Mungu wa Ulimwengu wote na anafanya atakalo kulifanya, popote pale, ndani na nje ya ulimwengu kama tunavyojua. Hao wahubiri na wachungaji kamwe hawaonyeshi kuwa wataweza kuleta kitu kingine zaidi ya maoni yao au mlinganisho wa kiajabu ajabu.

Baba - Mchungaji Msimikwa Asiye Na Madhehebu

Baba yangu alikuwa mchangamfu sana katika kuunga mkono kazi za kanisa, na hasa hasa vipindi vya shule ya kanisa. Akasimikwa ukasisi katika miaka ya sabini. Yeye na mkewe (mama yangu wa kambo) walikuwa wanawajua wainjilisti na wahubiri wa kwenye tv wengi, vilevile wameshamtembelea Oral Roberts na wamesaidia kujenga ‘mnara wa sala’ katika Tulsa, pia walikuwa ni waungaji mkono imara wa Jimmy Swaggart, Jim na Tommy Fae Bakker, Jerry Fallwell, John Haggi na Pat Robertson.

Kukutana na Mtu Kutokea Misri

Ilikuwa ni mwanzoni mwa 1991 pale baba yangu alipoanza kufanyabiashara na mtu kutoka Misri na kuniambia kuwa anataka nikutane na mtu huyo. Wazo hilo lilinivutia kwani niliwaza juu ya wazo la kuwa na ladha ya kimataifa. Unajua tena, mapiramidi, Sphinx, mto Naili na mengineyo.

Alikuwa ni ‘Mwislamu’: Watekajinyara, Walipuaji mabomu, Magaidi, na ni nani ajuaye kingine ni nini?

Kisha baba yangu alieleza kuwa mtu huyo ni ‘Mwislamu.’ Awali, nilichukia wazo la kukutana na mtu asiye na imani, mtekajinyara, mlipuaji mabomu, gaidi, kafiri.’ Mtu yeyote wa kawaida angelikataa wazo hilo. Sikuamini masikio yangu. Mwislamu?’ Haiwezekani! Nilimkumbusha baba yangu mambo mbali mbali tuliyoyasikia juu ya watu hao ‘Waislamu.’

Uongo dhidi ya Waislamu na Uislamu – walitwambia, kuwa Waislamu:

  Hata hawaamini Mungu.

  Wanaabudu boksi jeusi liliopo jangwani.

  Na wanabusu ardhi mara tano kwa siku.

Haiwezekani! Sikutaka Kukutana Naye!

Sikutaka kukutana na Mwislamu huyo. Haiwezekani! Baba yangu alisisitiza nikutane naye na akanihakikishia kuwa mtu huyo ni mwema sana. Hilo lilikuwa ni kubwa mno kwangu. Na hasa hasa walokole tuliokuwa tunasafiri nao wote waliwachukia sana Waislamu na Uislamu. Hata walikuwa wakisema vitu visivyo vya kweli ili kuwatisha watu waougope Uislamu. Kwa hiyo, kwa nini mimi nihitaji kitu cha kufanya na watu hao?

Wazo: ‘Kumbadilisha Awe Mkristo.’

Kisha wazo fulani lilinijia, ‘Tunaweza kumbadili mtu huyo awe Mkristo.’ Kwa hiyo, nilikubali na kuafiki kukutana naye. Lakini kwa masharti yangu.

Nikutane naye nikiwa na Biblia, Msalaba na kofia ya chopeo (kepu) iliyoandikwa ‘Yesu ni Bwana.’ Nilikubali nikutane naye siku ya Jumapili baada ya kutoka kanisani. Kwa hiyo, sote tungesali na kusimama vizuri na Bwana. Ningechukua Biblia yangu chini ya kwapa kama desturi. Ningekuwa na msalaba wangu mkubwa ung`aao na kuning`inia pia ningevaa kofia yangu isemayo: ‘Yesu ni Bwana.’ Maandishi yaliyo kwa mkato upande wa mbele. Mke wangu na mabinti zangu wawili wadogo wangekuja na sote tungekuwa tayari kwa kukabiliana kwa mara ya kwanza na ‘Waislamu.’

Yupo wapi? Nilipoingia dukani na kumuuliza baba; “Huyo Mwislamu yupo wapi”, aliashiria na kusema: “Yule pale.” Nilichanganyikiwa. Huyo hawezi kuwa Mwislamu. Haiwezekani.

Kiremba na midevu? Nalitafuta jitu kubwa lenye majoho yanayoburura, mremba mkubwa kichwani mwake, midevu inayofikia nusu ya shati lake na minyusi ya machoni ambayo inakatiza paji la uso wake akiwa na upanga au bomu chini ya koti lake.

Hakuna Kiremba – Hakuna Midevu – [Hakuna Nywele Kabisa!]

Mtu huyo hakuwa na midevu. Kwa hakika, hakuwa na nywele kabisa kichwani mwake. Alikuwa nusu kipara. Zuri zaidi, alikuwa anapendeza sana pamoja na karibisho moto moto na kupeana mikono. Lakini jambo hilo halikuwa na taathira. Nilifikiria kuwa wao ni magaidi na walipua mabomu. Je, yote hayo ni kwa nini?

Mtu huyo anahitaji Yesu bila kujali. Nitamshughulikia mtu huyo. Anahitaji kuokolewa kwa ‘Jina la Yesu’ na mimi na Bwana tutafanya hivyo.

Kutambulishana na mahojiano

Baada ya kutambulishana kwa haraka haraka, nilimuuliza: “Je, unamwamini Mungu?”

Akasema: “Ndiyo (vizuri!)

Kisha nikasema: “Je, unaamini Adamu na Hawa?”

Akasema: “Ndiyo (vizuri sana!)

Nikasema: “Vipi kuhusu Ibrahimu? Je, unamwamini na namna alivyojaribu kumtoa muhanga mwanawe kwa ajili ya Mungu?”

Akasema: “Ndiyo (hata inawezekana ni vizuri zaidi!)

Kisha niliuliza: “Vipi kuhusu Musa?” “Amri kumi” “Kuvuka bahari nyekundu?”

Kwa mara nyingine akasema: “Ndiyo (bado ni vizuri zaidi!)

Kisha: Vipi kuhusu Mitume mingine, kama Daudi, Suleimani na Yahya (Yohana mbatizaji)?”

Akasema: “Ndiyo (bab kubwa!)

Nilimuuliza: “Je, unaiamini Biblia?”

Kwa mara nyingine, akasema: “Ndiyo (ok!)

Kwa hiyo, kwa hivi sasa ilikuwa ndio muda wa swali kubwa; Je, unamwamini Yesu? Aliyekuwa ndiye Messiah Kristo wa Mungu?

Kwa mara nyingine akasema: “Ndiyo (Safi sana!)

Sasa ni vizuri – “Huyu atakuwa ni mwepesi sana kuliko nilivyofikiria.” Alikuwa tayari kubatizwa ila alikuwa hatambui jambo hilo. Nami nilikuwa ndiye nitakayemfanya hivyo.

Elimu ya Kushtua – Waislamu wanaamini Biblia?

Siku moja katika majira ya michipuo mwaka 1991, nilijua kuwa Waislamu wanaamini Biblia. Nilishtushwa. Hilo litakuwaje? Lakini hilo si la mwisho, wanaamini Yesu kuwa ni:

  Mtume wa kweli wa Mungu.

  Nabii wa Mungu.

  Kazaliwa kimiujiza bila ya tendo la ndoa la wanadamu.

  Alikuwa ni “Kristo” au Messiah kama alivyobashiriwa na Biblia;

  Kwa sasa yupo pamoja na Mungu na la muhimu sana ni:

  Atarejea tena siku za mwishoni kuwaongoza waumini dhidi ya mpinga Kristo.

Baada ya “kushinda roho na kuipeleka kwa Bwana, kwa Yesu” siku baada ya siku, jambo hilo litakuwa ndiyo mafanikio yangu makubwa, kumnasa mmoja wa “Waislamu” hawa na ‘kumbadili’ awe Mkristo.”

Nilimuuliza kama anataka chai na akanijibu ndiyo. Kwa mbali, tulikiendea kibanda kidogo kilichopo katika jengo kubwa la biashara, kukaa na kuzungumzia mada yangu niipendayo ya Imani. Tulipokuwa tumekaa katika kiduka hicho cha chai kwa masaa huku tukizungumza (nilikuwa ndiye muongeaji sana) nikagundua kuwa alikuwa ni mtu mzuri sana, mtulivu na ni mwenye kuona haya kidogo. Alinisikiliza kwa umakini kila neno nililolazimika kulisema na hakunikatiza hata mara moja. Niliipenda njia ya mtu huyo na nilifikiria kuwa mtu huyo ana uwezekano wa wazi wa kuwa Mkristo mzuri. – Ni kidogo nilichokijua juu ya mtiririko wa matukio yanayojifungua mbele ya macho yangu.

Kwanza kabisa, niliafikiana na baba yangu kuwa tufanye biashara na mtu huyo na hata kupigia debe wazo la kusafiri naye katika misafara yangu ya kibiashara kuvuka eneo la Kaskazini mwa Texas. Siku baada siku tutaendesha na kujadili mambo mbali mbali yanayofungamana na imani za watu mbalil mbali. Tukiwa njiani, kwa hakika nilikuwa nahanikiza baadhi ya vipindi vya redio vya mambo ya kiibada nilivyokuwa navipenda sana na kuvitukuza ili vinisaidie kufikisha ujumbe kwa huyo masikini aliyepeke yake. Tulizungumza juu ya maana ya Mungu; maisha; lengo la kuumbwa; Mitume na kazi zao; na jinsi Mungu anvyofunua ufunuo wake kwa binadamu. Pia tulishiriki kujadili uzoefu na fikra za kila mtu binafsi.

Siku moja nilijua kuwa rafiki yangu, Mohammed alikuwa anataka kuhama kutoka katika nyumba aliyokuwa akiishi na rafiki yake na alikuwa anataka kukaa msikitini kwa muda fulani. Nilienda kwa baba na kumuomba tumwalike Mohammed aje kuishi nasi katika nyumba yetu kubwa iliyopo kijijini. Baada ya yote, anaweza kushirikiana nasi kazi na kulipia baadhi ya gharama na atakuwepo wakati tutakapokuwa tunaenda safari zetu. Baba alikubali na Mohammed akahamia.

Bila ya shaka nilikuwa bado ninapata nafasi ya kuwatembelea rafiki zangu wahubiri na wachungaji waishio Texas. Mmoja wao alikuwa anaishi Texas karibu na mpaka wa Mexico na mwingine aliishi karibu na mpaka wa Oklahoma. Muhubiri mmoja alipendelea salaba la mbao kubwa sana ambalo lilikuwa kubwa kuliko gari ndogo. Alikuwa anaubeba juu ya mabega yake na kuuburuza. Kitako chake ardhini na kupita nao mtaani au barabarani huku akihanikiza miale miwili iliyoundwa kwa umbo la msalaba. Watu walisimamisha magari yao na kumwendea na kumuuliza kulikoni; naye angewapa vijitabu na vijikaratasi juu ya Ukristo.

Siku moja rafiki yangu mwenye msalaba alipatwa na mshtuko wa moyo na kulazimika aende hospitali ya Veterans ambako alikaa kwa muda mrefu. Nilikuwa namtembelea hapo hospitalini kwa mara kadhaa kwa wiki na nilikuwa namchukuwa Mohammed pamoja nami, nikiwa na matarajio ya kuwa sote tutashiriki mada ya imani na dini. Rafiki yangu mwenye msalaba hakupandishwa mori, na ilikuwa ni wazi kuwa hakutaka kujua chochote kuhusu Uislamu. Kisha siku moja yule mtu ambaye alikuwa anashirikiana na rafiki yangu alikuja huku akiendesha kiti chake cha magurudumu na kuingia chumbani. Nilimwendea na kumuuliza jina lake na akasema kuwa hilo si muhimu na nilipomuuliza ametokea wapi alisema kuwa ametokea sayari ya Jupita. Nilifikiria kile alichokisema na kisha nilianza kustaajabu je, kama ningekuwa katika wodi ya mshtuko wa moyo au katika wodi ya wagonjwa wa akili ingekuwaje.

Nilijua kuwa yule mtu alikuwa ni mpweke na amefadhaika na anahitaji mtu katika maisha yake. Kwa hiyo, nilianza kumthibitishia kuhusu Bwana. Nilimsomea kwa sauti kitabu cha Jonah katika Agano la Kale. Na fikra ilikuwa ni kuwa kwa hakika hatuwezi kukimbia matatizo yetu kwa kuwa siku zote tunajua tulichokifanya na cha ziada, Mungu pia daima anajua ambacho tumekifanya.

Padri wa Kikatoliki

Baada ya kushiriki mazungumzo hayo na yule mtu aliye katika kiti cha magurudumu, mtu huyo alinitazama na kuniomba msamaha. Akaniambia kuwa amehuzunishwa na tabia yake ya ufedhuli na kuwa yeye amepatwa na matatizo makubwa hivi karibuni. Kisha akasema kuwa anataka kuungama kitu mbele yangu. Nikamwambia kuwa mimi si padri wa Kikatoliki na kwa hiyo, sitoi huduma ya kuungama dhambi. Akanijibu kuwa anajua hilo. Kwa hakika, alisema “Mimi ni padri wa Kikatoliki.”

Nilishtushwa. Hapa nilikuwa najaribu kumuhubiria Ukristo padri. Nini kilikuwa kinatokea hapa duniani?

Padri Wa Amerika Kusini

Yule padri akaanza kushiriki mazungumzo kwa kueleza kuwa, yeye alikuwa mmishionari[3] wa kanisa kwa zaidi ya miaka kumi na mbili katika maeneo ya kusini na kaskazini mwa Amerika na Mexico na hata New York Hell’s Kitchen.’ Alipotolewa hospitalini alihitaji sehemu ya kusubiria apone nami sikumwacha akakae na familia ya Kikatoliki, nilimueleza baba yangu kuwa tumwalike ahamie na kuishi na sisi kijijini pamoja na Mohammed. Jambo hilo lilikubaliwa na wote waliokuwepo, na kwa hiyo, mara moja akahamia.

Padri Lazima Ausome UISLAMU? – Ndiyo!

Katika msafara nje ya nyumba yetu, nilizungumza na padri kuhusu baadhi ya itikadi na imani za Kiislamu na kwa mshangao alikubali na kisha akashirikiana nami mazungumzo juu ya hilo kwa sana. Nilishtushwa aliponiambia kuwa mapdri wa Kikatoliki kwa hakika wanausoma Uislamu na baadhi yao wanafikia hata stashahada ya Udakitari katika somo hilo. Jambo hili lilinipa mwangaza sana. Lakini kulikuwa bado kuna mengi yatakayojiri.

Matoleo Ya Biblia Tofauti Tofauti

Baada ya kujipanga, sote tulianza kujikusanya kuizunguka meza ya jikoni baada ya chakula cha usiku kila usiku ili kujadili mambo ya kidini. Baba yangu ataleta toleo lake la Biblia ya King James Version of Bible, mimi nitaleta toleo langu la Biblia ya Revised Standard Version of the Bible, mke wangu alikuwa na toleo lingine la Biblia (huenda ni kitu kama vile Jimmy Swaggart’s “Good News For Modern Man.” Yule padri bila ya shaka, alikuwa na Biblia ya Kikatoliki ambayo ina vitabu saba vya ziada kuliko Biblia ya Kiprostanti. Kwa hiyo, tulitumia muda mwingi kuzungumzia Biblia ipi ndiyo ya haki, na sahihi zaidi, kuliko tulivyokuwa tukijaribu kumkinaisha Mohammed awe Mkristo.

Quran Ina Toleo Moja Tu – La Kiarabu – Na Bado Lipo.

Nukta moja ninayoikumbuka ni kumuuliza kuhusiana na Quran ina matoleo mangapi ambayo yamekuwepo katika kipindi cha miaka 1400. Akaniambia kuwa kulikuwa na Quran Moja tu. Na kuwa kamwe haijabadilishwa. Pia akawafahamisha kuwa Quran yote imehifadhiwa na mamia kwa maelfu ya watu, na imetawanywa duniani katika nchi mbali mbali. Baada ya karne nyingi tangu kuteremshwa kwa Quran, mamilioni wameshaihifadhi Quran yote kimoyo moyo na wameshawafundisha wengineo ambao nao wameshaihifadhi kikamilifu, kuanzia jalada hadi jalada, kila herufi bila ya kukosea. Leo hii, zaidi ya Waislamu milioni tisa wameshahifadhi Quran nzima kuanzia jalada hadi jalada.

Jambo lililoonekana kuwa haliwezekani kwa upande wangu. Baada ya yote, lugha zote za asili za Biblia zimekufa kabisa kabisa kwa karne nyingi na nyaraka zenyewe zimepotea katika uasili wake kwa mamia na maelfu ya miaka. Kwa hiyo, vipi itakuwa kitu kama hicho kiweze kulindwa kirahisi na kusomwa kuanzia jalada hadi jalada.

Hata hivyo, siku moja yule padri alimuomba Mohammed kama ataongozana naye na kuelekea msikitini ili aone kuna nini huko msikitini. Wakarudia kuongelea uzoefu wao kuhusu huko msikitini nasi hatukuwa na subira ya kungoja kumuuliza padri nini kilitokea huko msikitini na aina gani za taratibu za kidini walizokuwa wakizifanya. Naye akasema kuwa, Waislamu kwa hakika hawafanyi lolote. Wao huwa wanakwenda na kuswali na kuondoka. Nikasema: “Wanaondoka?” Bila ya mazungumzo yeyote au kuimba? Akasema hivyo ndivyo ilivyo.

Padri Aingia Uislamu!

Siku chache nyingine, zilipita na yule padri wa Kikatoliki alimuomba Mohammed kama atamkubalia ajiunge naye tena ili waende msikitini na jambo hilo wakalifanya. Lakini mara hii ilikuwa ni tofauti. Hawakurejea kwa muda mrefu. Hadi ikawa kiza na tukaogopa isije ikawa kuna kitu kilichowatokea. Mwishowe walifika na walipoingia mlangoni kwa haraka haraka nilimtambua Mohammed, lakini ni nani huyu aliye ubavuni mwake? Ni mtu anaevalia joho leupe na kofia nyeupe. Kwa kujiachia muda kidogo! Alikuwa ni yule padri. Nilimwambia: “Pete? – Je, umekuwa “Mwislamu?”

Akasema ameshaingia Uislamu siku hiyo hiyo. PADRI AMEKUWA MWISLAMU!! Nini kinafuata? (Utaona).

Mke wangu anatangaza Uislamu wake!

Kwa hiyo, nilienda upande wa juu kufikiria vitu vya juu kidogo na nikaanza kuongea na mke wangu kuhusiana na kadhia nzima. Kisha naye akaniambia kuwa yeye ataingia Uislamu, kwa kuwa ameshajua kuwa Uislamu ni dini ya kweli.

Kwa sasa nilikuwa nimeshtushwa barabara. Nilienda upande wa chini na kumwamsha Mohammed na kumtaka atoke nje pamoja nami ili tujadiliane. Tulitembea na tulizungumza usiku kucha.

Ukweli Umeshafika!

Wakati alipokuwa yupo tayari kuswali swala ya Alfajiri (swala ya Asubuhi kwa Waislamu) nilijua kuwa mwishowe ukweli umeshafika na sasa ilikuwa ni juu yangu kufanya sehemu yangu. Nilienda nje ya nyumba ya baba yangu na kukuta kipande cha tabaka za mbao cha zamani kikiwa chini ya Overhang na hapo hapo niliinamisha kichwa changu chini ya ardhi nikielekea upande wanaouelekea Waislamu katika sala zao tano za kila siku.

Niongoze! O Mungu! Niongoze!

Sasa, katika nafasi hiyo, nikiwa nimenyoosha mwili wangu katika zile tabaka za mbao na kichwa changu kikiwa juu ya ardhi, niliomba: “O Mola. Kama upo huko, niongoze, niongoze.”

Na kisha baada ya muda niliinua kichwa changu na nikagundua kitu. Sijaona ndege wala Malaika wanaotokeza kutoka mbinguni wala kusikia sauti au muziki, wala sijaona mwangaza na nuru, hapana. Ambacho nilikigundua ni mabadiliko ndani ya nafsi yangu. Kwa sasa nilikuwa nipo macho zaidi kuliko nilivyokuwa hapo kabla na huo ndiyo ulikuwa muda wangu wa kukomesha uongo wowote na kufanya chochote cha kisiri siri. Huu ndiyo muda madhubuti wa kutenda na kuwa mtu mwaminifu. Kwa sasa nimeshajua kitu nilicholazimika kukifanya.

Kwa hiyo, nilienda upande wa juu na kuoga kwa itikadi tofauti kabisa ya kuwa nilikuwa ninaosha madhambi ya mtu wa zamani mwenye dhambi tena aliyekuwa nazo kwa miaka mingi. Na kwa sasa nimeingia katika maisha mapya. Maisha yanayoegemea juu ya ukweli na uthibitisho.

Majira ya saa 11:00 asubuhi hiyo, nilisimama mbele ya mashahidi wawili, mmoja wao ni padri wa zamani, ambaye alikuwa akifahamika kama padri Peter Jacob`s na mwingine ni Mohammed Abdel Rahmani na kutangaza ‘shahada’ yangu (ushuhuda wa wazi juu ya Upweke wa Mungu na Mtume Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake).

“Nashuhudia kuwa hakuna Mola wa kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah Muweza, yeye peke yake hana mshirika na ninashuhudia kuwa Muhammad ni mjumbe wake na ni mtume wake.”

Dakika chache baadaye, mke wangu alifuatia na kutoa shahada hiyo hiyo. Lakini shahada yake ilikuwa mbele ya mashahidi watatu (mimi nikiwa ndiye wa tatu).

Baba yangu alichelewa kidogo katika suala hilo na alisubiri miezi michache kabla naye hajatoa shahada (ushuhuda wa mbele za watu). Lakini yeye naye, hatimaye aliingia katika Uislamu na akaanza kusali na mimi na Waislamu wengine katika msikiti wa mtaani.

Watoto walitolewa kutoka katika shule za Kikristo na kuingizwa shule za Kiislamu. Na kwa sasa ikiwa imepita miaka kumi, watoto hao wameshahifadhi sehemu kubwa ya Quran na mafundisho ya Kiislamu.

Mwishowe mke wa baba yangu alikubali, kabla hajafariki, kuwa Yesu haiwezekani awe mtoto wa Mungu na lazima atakuwa ni Mtume mkuba wa Mwenyezi Mungu, na siye Mungu. Naye alifariki ndani ya miezi michache baada ya maneno hayo akiwa na umri wa miaka 86. Allah mkubalie maneno yake ya kiimani, aamiin.

Sasa hebu simama na ufikiri. Familia zote za watu kutoka makundi, makabila na historia mbali mbali, wamejumuika pamoja katika ukweli ili wajifunze namna watakavyomjua na kumwabudu Muumba na Mpaji wa ulimwengu. Fikiria. Padri wa Kikatoliki; mchungaji wa muziki na muhubiri Injili; mchungaji msimikwa na mjenzi wa mashule ya Kikristo; na watoto; hata kibibi kikongwe – wote hao wameingia Uislamu!

Ni kwa rehema za Mungu tu ndiyo sisi sote tumeongoka na kuona ukweli halisi wa Uislamu, kwa kuondoshwa vizibo juu ya masikio yetu na upofu juu ya macho yetu, na hakuna tena vizibo juu ya mioyo yetu – Mungu anatuongoza hivi sasa.

Kisa cha kushangaza – famila na marafiki kuingia Uislamu – kutokana na mtu mmoja. Ingekuwa napaswa kusimama hapa, nina hakika kuwa ungekubali kuwa, kwa uchache, hiki ni kisa cha kushangaza sawa? Baada ya yote, viongozi watatu wa kidini wa madhehebu matatu tofauti tofauti wote wanaingia imani iliyokinyume kabisa na imani zao kwa wakati huo huo baadaye familia nzima.

Ziada? – Naam! Mwanafunzi wa seminari (shule ya kidini) ya Kibaptisti anasoma Quran – anaukubali Uislamu. Lakini hayo sio ndiyo ya mwisho. Kuna ya ziada! Mwaka huo huo nilipokuwa Grand Prairie, Texas (karibu na Dallas) nilikutana na mwanafunzi wa seminari ya Kibaptisti atokeaye Tennessee aitwaye Joe, ambaye naye aliingia Uislamu baada ya kusoma Quran Tukufu wakati alipokuwa katika CHUO CHA SEMINARI CHA KIBAPTISTI!

Ziada? – Naam! Padri wa Kikatoliki anaupenda Uislamu – lakini anahitaji kazi yake! – Kuna mengine vilevile. Ninakumbuka kadhia ya padri wa Kikatoliki katika chuo cha mjini ambaye alizungumzia mambo mazuri ya Uislamu kwa sana kiasi ambacho nikalazimika nimuulize kwa nini hajaingia Uislamu? Akajibu; “Nini?” Kisha nipoteze kazi yangu?” – Jina lake ni Baba John na tunaendelea kumuomba Allah amwongoze.

Padri mwingine wa Kikatoliki anatoa shahada

Mwaka uliofuata nilikutana na padri wa zamani Mkatoliki ambaye ameshawahi kuwa ni mmishionari kwa miaka minane barani Afrika. Amejifunza Uislamu wakati alipokuwa huko na akaingia Uislamu. Kisha akabadili jina lake na kuitwa Omar na akaenda Dallas Texas.

Lolote la ziada? Tena – naam! Askofu wa Kiothodoksi analiacha kanisa na kuingia Uislamu. Miaka miwili baadaye, nikiwa San Antonio, Texas nilielekezwa Askofu wa zamani wa kanisa la Kiothodoksi la Kirusi ambaye amejifunza Uislamu na kutupilia mbali kazi yake na kuingia Uislamu.

Binti wa kiongozi Bingwa wa Kihindu (Hindu Pundit) – anaukubali Uislamu na kusaidia Uislamu kwa maelfu ya mapesa.

Nilikutana na mwanamke mjini New York aliyetaka kutengeneza CDs zetu kuhusiana na “Uislamu ni nini?” Baada ya kupewa ruhusa yake miaka kadhaa iliyopita, nimesoma kuwa ameshatengeneza na kusambaza zaidi ya CDs laki sita kwa wasio Waislamu ndani ya Marekani. Allah amlipe thawabu na ampe nguvu katika juhudi zake, aamiin.

Mamia – Maelfu – Bado yanakuja

Tangu kuingia kwangu katika Uislamu na kuwa kasisi wa Waislamu ndani ya nchi na dunia nzima, nimeshakabiliana na watu wengi mmoja mmoja, ambao walikuwa ni viongozi, walimu na wanazuoni wa dini nyingine waliousoma Uislamu na wakauingia. Wamekuja kutoka katika dini za Kihindu, Kiyahudi, Kikatoliki, Kiprotestanti, Mashahidi wa Yehova, na Waothodoksi wa Kigiriki na Kirusi, wakibti kutokea Misri, makanisa yasiyo na madhehebu na hata wanasayansi ambao walikuwa wanamkana Mungu.

Mchanganyiko huo daima unaonekana ni ule ule; watu ambao kiuaminifu wanatafuta ukweli na wanataka kuweka kando tofauti za kihisia na upendeleo wao na kuanza kumuomba Mungu awaongoze katika maisha yao.

Kwa hiyo, hadi sasa umeshapata utangulizi wa kisa cha kuingia kwangu Uislamu na kuwa Mwislamu. Kuna mengi katika internet kuhusu kisa hiki na kuna picha nyingi vilevile. Tafadhali tenga muda na uniandikie email na uturuhusu tujumuike pamoja katika kweli tupu inayoegemea katika ushahidi ili tufahamu asili yetu, malengo yetu na makusudiyo katika maisha haya na ya baadaye.

Je, nitoe pendekezo kwa mtafutaji wa ukweli? Chukua hatua tisa zifuatazo ili utakase moyo.

1.  – Safisha – fikra zako, moyo wako, na nafsi – ondosha hisia zote za upendeleo.

2.  – Mshukuru Mungu – kwa kile ulichokuwa nacho – kila wakati kila siku.

3.  – Soma – tafsiri nzuri ya maana za Quran Tukufu katika lugha uifahamuyo vizuri. (www.islamtomorrow.com/downloads/noblequran.exe)

4.  – Tafakari juu ya maana yake na uzingatie ukarimu wa Mola wako.

5.  – Tafuta – kusamehewa dhambi kwa Mungu na jifunze kuwasamehe watu wengine.

6.  – Omba – kimoyo moyo uongozwe kutoka juu.

7.  – Funga – moyo wako na akili zako.

8.  – Endelea – kufanya haya kwa miezi michache. Na jizoeshe kufanya hayo kila siku.

9.  – Jiepushe – na sumu ya shetani wakati moyo wako utakapofunguliwa ili “kuzaliwa upya kwa moyo wako”.

Kumbuka – kujisafisha; kutoa shukrani; kusoma; kutafakari, kisha tafuta, “na nyinyi hakika mtapata. Omba, na utapewa. Bisha hodi utafunguliwa.”

Kisha endelea na Jiepushe:

Lililobaki ni kati yako na Mungu Muweza wa Ulimwengu. Kama kweli unampenda Mungu, Yeye tayari anajua hilo na atatushughulikia kila mmoja wetu kulingana na mioyo yetu.

Majibu ya Maswali:

Kwa sasa kama nilivyowaahidi kuna majibu ya maswali mengi niliyoulizwa yanayofungamana na chaguo langu la Uislamu:

1.  Vipi umebadilika kutoka katika mpango mkamilifu wa uwokovu wa Yesu Kristo msalabani kuokoa dhambi zako?

Jibu: Swali lako linaashiria bado hujazingatia mlingano uliopo kati ya mafundisho ya Biblia na Quran.

“Uislamu” maana yake ni kujisalimisha, kunyenyekea na kumtii Mola wako kwa uaminifu na amani.” Yeyote anayejaribu kufanya hayo, ni Mwislamu. “Kama mtu anaamini Mungu Muweza kuwa ni Mungu Mmoja na ni Mola Mmoja anayetaka kuyafanya maisha yao ili kumtumikia Yeye na kutii amri zake, mtu huyo atakuwa katika njia sahihi na watu hao watakuwa “wameokolewa.” Kulingana na Rehema za Mungu. Hakuna wa kuchukua dhambi za wengine na waovu lazima wasimame na kushitakiwa kwa vile walilivyovitenda. Itakuwa ni juu ya Mola Muweza kuwasamehe au kuwaadhibu kwa mujibu wa Hukumu yake katika siku hiyo.

Kwa mujibu wa mabaki ya tafsiri ya Biblia juu ya Yesu, Mungu amrehemu, hajahubiri habari za uwokovu kwa kumwabudu yeye. Jambo hili limeongezwa baada yake na Saul (ambaye baadaye akawa Paulo). Tunapata maelezo ya wazi kabisa yanayoashiria uwokovu utakaokuja kupitia kumkiri Mungu Muweza kuwa ni Mungu mmoja na kumwabudu kwa moyo wote, akili na nguvu zote tu! Yesu, Amani iwe juu yake, amefundisha wafuasi wake waabudu hivi “Mungu wangu Ndiye Mungu Wenu, Mola wangu Ndiye Mola wenu.”

Kwa mara nyingine, kwa mujibu wa tafsiri ya Biblia ya Kingereza iliyobaki, tunamuona mtu aangukwaye msalabani akilia kwa kusihi sana, “Eloi, Eloi, lama sabakhthani? (Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?) Sentensi hii juu ya msalaba kwa uwazi kabisa inaonyesha kuwa yule mtu aliye msalabani hajafurahishwa na hali hiyo na wala haichukulii hali hiyo kuwa ni haki au uadilifu. Kwa hiyo, mtu lazima ahitimishe jambo hilo kuwa lilikuwa ni kitu ambacho hakikutakiwa na Yesu wala kukubaliwa au vinginevyo ni mtu mwingine aliyekuwa msalabani katika nafasi yake. Kwa njia yeyote ile utakavyolitazama jambo hilo, mtu aliyekuwa msalabani hakukubali jambo hilo kuwa ni mpango wa uwokovu.

Quran kwa ukamilifu inapingana na mafundisho hayo, na Waislamu wanamwabudu Mungu na Bwana yule yule wa Yesu, Musa, Ibrahimu na Adamu, amani iwe juu yao. Quran katika sehemu nyingi inaeleza, hakuna mtu atakayebebeshwa kazi za dhambi za Mwingine, wala hakuna mtu atakaye beba mzigo wa mwingine. Sote tutakuwa na mambo yetu wenyewe siku hiyo. Na ninamuomba Allah awerehemu na awasamehe wote waliomwamini, aamiin.

Ninajiona kuwa sijaacha mafundisho ya Yesu Kristo, (amani iwe juu yake). Kinyume chake, nahisi kuwa nipo karibu na Yesu, amani iwe juu yake, na ninatarajia kurejea kwake hapa duniani kuliko nilivyokuwa zamani. Kwa sasa ninamwabudu Mungu yule yule anayemwabudu na ninamtumikia Bwana yule yule anayemtumikia, katika njia ile ile aifanyao. Yesu alimuomba Mungu Muweza, na alifundisha wafuasi wake wafanye hayo hayo. Mimi kwa wepesi kabisa ninafanya kile alichokiamrisha kwa uwezo wangu na ninamuomba Mungu Muweza anikubalie matendo yangu.

2.  “Je, unadhani kuwa ni kweli “umeokolewa” na kwa hakika umezaliwa upya?”

Jibu: Wabatisti wanamsemo usemao: “Aliyeokolewa, huokolewa daima” nilimuuliza mmoja wao kuhusu hilo na akakubali hilo kuwa ni kweli. Kisha nikataja kuwa kuna mara moja nilibatizwa (nikiwa na umri miaka kama kumi hivi) lakini kwa sasa nimeshakuwa Mwislamu. Pia niliokolewa na kubatizwa nikiwa na miaka kumi na mbili. Nilikubali maneno ya Yesu ya kuwa yeye ndiye njia, nuru na ukweli na hakuna mtu atakayekwenda kwa Baba ispokuwa kwa njia ya Yesu. Niliyafahamu maneno hayo kuwa yanamaanisha kuwa lazima nimfuate Yesu na mafundisho yake. Kwa hiyo, niliisoma Biblia mimi mwenyewe na sikuwaruhusu watu wengine waniambie jambo la kufikiria kuhusu nilichokuwa nakisoma.

Biblia inaeleza kuwa Yesu aliomba aokolewe nafsi yake katika bustani ya Gethsemane kwa njia hii. “Baba yangu ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke; walikini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.” Dua hili lilirudiwa na Yesu, amani iwe juu yake, mara nyingi na imeonyeshwa katika Injili nyingi. Ndiyo, kwa mujibu wa fikra za Kibiblia, Hilo Kombe halikumwepuka na dua zake hazikukubaliwa. Uislamu unafundisha kuwa dua zake zilikubaliwa naye hakukaa katika matendo ya ukatili na wala hajafa msalabani, lakini alichukuliwa akiwa hai na yupo pamoja na Mungu Muweza kwa hivi sasa na yupo tayari kurejea katika siku za Mwishoni ili kuleta ushindi kwa waumini.

Jambo la kuongezea, tunamkuta Yesu, amani iwe juu yake, anawafundisha wafuasi wake waombe kama hivi; “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.] Amin.” Kila Mwislamu niliyewahi kukutana naye anakubali kila neno la dua hii ila tamko la kumwita “Allah” “Baba yetu.” Waislamu wanchukulia kuwa ni vizuri kumwita Mungu Muweza kwa majina yake, ambayo tunayoyachukulia kuwa ni “matukufu.”

3- “Familia yako iliitikia vipi kusilimu kwako?”

Jibu: Jambo hilo daima ni gumu kwa familia kukaa sawa na mara nyingi linachukuwa muda mrefu. Familia yangu haikuwa na pingamizi. Ingawa mke wangu na watoto wangu waliingia Uislamu na hatimaye baba yangu akatangaza kuwa Uislamu ndiyo njia ya uwokovu kwake, mama yangu mzazi na watu wengine katika familia waliendelea kukasirishwa na kuingia kwetu katika Uislamu hapo mwanzoni. Mwishoni mambo yakawa ya kawaida na tuliishi kwa ukaribu, ingawa wao bado wanajihusisha na Ukristo.

Allah anaahidi kuwatia majaribuni wale wote wanaotangaza imani yao juu yake, kwa kuwapa aina nyingi za mambo magumu magumu, na familia ni moja ya mambo hayo yaliyotajwa kuwa ni jaribio ndani ya Quran. Nanawaombea Allah awaongoze wafuate kitu kilicho bora kabisa duniani na Ahera. Lakini juu ya Allah, kama anawataka wawe katika utiifu kwake (Uislamu maana yake ni, utiifu kwa Allah) au kama hataki kuwa hivyo.

4- “Vipi kuhusu usharika wako? Wamesema nini?

Jibu: Kamwe sijawahi kuwa na kanisa langu mwenyewe. Nilikuwa ni mchungaji wa muziki kanisa la Mungu (Anderson, Indiana branch) mjini Texas na nilikuwa natoa mahubiri yangu kwa wafanyabiashara na kwa makutano yasiyo ya kawaida. Wote wanaonijua kwa sehemu kubwa hawana kizuizi na baadhi yao wameshaingia katika Uislamu, lakini kuna wachache ambao walihisi kuchanganyikiwa sana na wakanitukana, kwa “kumkana Yesu, amani iwe juu yake.” Bila kujali kile nilichojaribu kukisema au kukitenda, hawa watu maalumu walio wachache hawasikilizi wala hawataki chochote kinachohusu Uislamu.

5- Je, umeshapata matatizo mengi kwa kubadili dini?

Jibu: Bila ya shaka, kila mtu atakaye kuuzingatia Uislamu siku hizi, kama ilivyokuwa mida iliyopita, lazima atambue kuwa kutakuwa na matatizo ya majaribio maalumu katika njia yake hiyo. Wafuasi wa Yesu, amani iwe juu yake, walikosolewa na kuteswa sana hadi walifikia kuuliwa (soma kile alichokisema Paulo kwamba alikuwa anakifanya kwa wanafunzi wa Yesu ndani ya Biblia; kitabu cha Matendo ya Mitume). Wote waliomfuata Muhammad, amani iwe juu yake, waliteswa mikononi mwa watu wa makabila yao wenyewe, ndiyo kuwa, walikuwa wameshaazimia kumwabudu Mungu Muweza peke yake, bila ya mshirika na kutii matakwa yake.

Tatizo kubwa kwa wasiokuwa Waislamu ni, ukosefu wao wa elimu na ufahamu juu ya nini ndiyo Uislamu wa kweli na akina nani wanaozingatiwa kuwa ndiyo Waislamu. Ninawaombea na kumuomba Allah awasamehe Waislamu kwa kutuonyesha picha nzuri kwa kila mtu.

6- “Nani ndiye muhusika mkuu katika kukubadilisha dini?”

Jibu: Nikiwa kama Waislamu wote, tunaamini kuwa ni Allah pekee aongozaye watu na yeyote amwongozaye hatopotoka na yeyote amwachaye apotee hakuna atakayeweza kumwongoza. Kwa hiyo, inamaanisha kuwa hatuamini kuwa kuna awezaye kumbadili dini mtu mwingine.

Pia, tunakubali kuwa watoto wote wanazaliwa wakiwa na maumbile ya kumtii Mungu Muweza na kwa hiyo, hilo linamaanisha kuwa wao ni Waislamu. Watoto wakifa wataingia Peponi kwa kuwa hawataulizwa kile wasichokifahamu.

7 – Je, hujawahi kufikiria juu ya kuwa Mkristo tena?

Jibu: “Mkristo” inaashiria mfuasi wa Kikristo. Wakati Yesu, amani iwe juu yake, atakaporudi duniani siku za Mwisho, Waislamu wote watalazimika kumfuata. Lakini hatojiita “Mkristo” kama atakavyokuwa. Yeye au wafuasi wake, kamwe, hawajajiita “Wakristo.” Biblia inatueleza kuwa wao kamwe hawajapatapo kuitwa “Wakristo” hadi pale Paulo alipohubiri ujumbe wake mjini Antokia.

8- “Je, jambo hilo halikukuudhi kwa kuacha njia ya amani, uadilifu na upendo na kuingia dini ya chuki, fujo na ukandamizaji dhidi ya wanawake na watu wengine?”

Jibu: Mitume wote, amani iwe juu yao, waliwaita watu waje wamwabudu Mungu Muweza ambaye ni Mungu Mmoja na ni Bwana Mmoja. Kwa hiyo, wote wasiotaka kumtii Mungu Muweza watawapinga hao Mitume na kuwatendea uadui, hadi kuwaua, kama alivyofanya Paulo alipokuwa Mfarisayo. Mitume, rehema na amani ziwe juu yao, waliwatia nguvu wafuasi wao waishi kwa amani na kuishi na watu kwa wema na mapenzi ya pekee kwa mtindo wa hali ya juu wa kihisia za kibinadamu zinazoweza kutendwa kwa watu wengine.

Naam, wakati huo huo waumini wanalazimika kujikinga nafsi zao, familia zao na dini yao, ili isije kuwa wale wasioamini wakaondosha imani kutoka katika kila eneo la ardhi. Uislamu, kama Ukristo unahubiri ujumbe wa amani na kuvumiliana – kwa kina. Lakini linapokuwa jambo hilo haliwezekani bila ya maafikiano ya moja kwa moja na mtu kupoteza njia ya maisha na mfumo wa imani, hapo ndipo kunapokuwa hakuna hiari ispokuwa kutumbukia katika mapigano ya kisilaha ya wazi dhidi ya wale wote wanaopigana dhidi ya waumini.

Yesu aliwaita wafuasi wake wauze makoti yao na wanunue mapanga. Naye akafafanua kuwa Yeye hakuja kwa amani bali kwa ncha ya upanga. Yeye na wafuasi wake walitumbukia katika pigano kuu na maadui zao, Wafarisayo wakati fulani pale mtumishi wa makasisi alipolazimika kukatwa sikio lake kwa upanga. Kisha Yesu akawaambia waweke chini mapanga yao. Jambo hili limetajwa katika Biblia.

Neno “upanga” limetajwa zaidi ya mara mia mbili katika Biblia- lakini hata hivyo, lugha ya Kiarabu ina zaidi ya dazeni moja ya maneno yenye maana ya upanga, lakini hakuna hata moja miongoni mwa maneno hayo liliopo katika sehemu yeyote ile ndani ya Quran.

Mapigano yameamrishwa na Quran, chini ya masharti maalumu na yenye kiwango maalumu tu, na hakuna lolote zaidi ya kile ambacho leo hii tunachoweza kukiita “vita vya ugaidi.” Kupambana dhidi ya matendo yote makundi ya uchokozi, ukandamizaji, utesaji na ugaidi ni jambo la lazima juu ya waumini wote. Lakini bila ya shaka yana mipaka maalumu na wanawake, watoto, wazee na yeyote asieshiriki hawauliwi au kuumizwa katika matukio hayo. Matendo ya kuwafanyia wafungwa wa kivita hayatakiwi yawe ya kuabisha au mateso ya aina yeyote ile. Hata maiti za maadui zinatakiwa zizikwe kwa heshima na wema.

Mungu akuongoze katika safari yako ya kuelekea ukweli kamili. Aamiin.

Na akufungue moyo wako na fikra zako katika uhakika wa ulimwengu huu na lengo la maisha haya. Aamiin.

Amani iwe juu yako, pia na uwongofu kutoka kwa Mungu Muweza, ambaye ni Mmoja Mwenye Nguvu, Muumba na Mpaji wa kila kitu kilichopo.

Rafiki yako,

Yusuf Estes

6317 Edsall Rd.

Alexandria, VA22312

United States of Amerca

SHEIKYUSUF@AOL.COM Tel: 001-703-354-5224

http://www.islamtomorrow.com/yusf.htm

http://thetruereligion.org/modules/xfsection/

 2 – ABDULLAH M. AL-FARUQUE ALIYEKUWA AKIIITWA KENETH L. JENKINS, MCHUNGAJI NA MZEE WA KANISA LA PENTECOSTAL. (USA)

Nikiwa ni mchungaji na ni mzee wa kanisa la Kristo, hapo zamani, ilikuwa ni wajibu wangu kuwaelimisha wale wote wanaoendelea kutembea kizani. Baada ya kuingia Uislamu nilihisi haja kubwa mno ya kuwasaidia wale wote wasiobarikiwa na kupata nuru ya Kiislamu.

Namshukuru Mungu Muweza, Allah, anihurumie, anijaalie niujue uzuri wa Uislamu kama ulivyofundishwa na Mtume Muhammad na maswahaba[4] zake waongofu. Ni kwa rehema za Allah tu, ya kwamba sisi tunapokea uongofu wa kweli kweli na uwezo wa kufuata njia iliyonyooka, inayoongoza katika mafanikio katika maisha haya na ya kesho ahera.

Mungu asifiwe kwa wema niliofanyiwa na sheikhi “Abdallah bin Abdul-Azeez bin Baz” wa Falme ya Saudi Arabia juu ya kuingia kwangu Uislamu. Naishi kwa matumaini na nitapitia juu ya elimu yote iliyopatikana kutokana na kila kikao nlichokaa naye. Kuna wengine wengi walionisaidia kwa kunipa nguvu na kunielimisha. Ni jambo la kutosha kusema kuwa namshukuru Mungu Muweza, Allah, kwa madada na makaka wote walioruhusiwa na Mungu kushiriki katika ukuaji na maendeleo yangu nikiwa Mwislamu.

Naiombea kazi hii fupi, iwe ni kwa faida ya wote. Natarajia Wakristo watagundua kuwa bado kuna matarajio licha ya masharti ya ukaidi yanayoshawishi makundi mengi ya Wakristo. Ufumbuzi wa matatizo ya Wakristo haupatikani kwa Wakristo wenyewe, kwani wao, kwa namna nyingi, ndiyo mzizi wa matatizo yao wenyewe. Kiasi ambacho, Uislamu umekuwa ndiyo suluhisho la matatizo yaliyosababishwa na ulimwengu wa Kikristo, pia kwa matatizo yanayoukabili ulimwengu wote wa kidini. Allah atuongoze na atulipe kwa mujibu wa matendo yetu mema na nia zetu.

Nikiwa kijana mdogo, nilimuogopa sana Mungu. Kwa kuwa kwa kiasi fulani nililelewa na bibi yangu aliyekuwa ni Mpentekoste mwenye msimamo mkali, na kanisa lilikuwa ni sehemu ya lazima katika maisha yangu tangu nikiwa mdogo. Nilipofikia miaka sita, nilijua vizuri kabisa faida inayoningojea huko Peponi kama nitakuwa kijana mwema, na adhabu ya Moto inayowangojea watoto watukutu. Nilifundishwa na bibi yangu kuwa uongo wa aina yeyote unaangamiza na unapeleka Motoni, sehemu ambayo waovu wataunguzwa milele na milele.

Mama yangu alikuwa anafanya kazi mara mbili na huku akiendelea kunikumbusha juu ya mafundisho aliyonipa kutokea kwa mama yake. Kila Jumapili tulienda kanisani huku tukivalia nguo nzuri nzuri kabisa. Babu yangu alikuwa ndiye tegemeo letu katika masuala ya usafiri. Muda wa kukaa kanisani ulidumu, kama nilivyokuwa nikiuona, kama kwa masaa machache tu. Tulikuwa tunafika mida ya saa tano asubuhi na wakati mwingine, tulikuwa hatuondoki hadi saa tisa jioni. Babu yetu hakuwa mwendaji wa kanisani, lakini alilitazama jambo hilo kuwa “familia yangu imelifanya liwe hivyo” kwa kila Jumapili. Mwishowe babu alipatwa na ugonjwa wa kupooza na kumfanya, kwa kiasi fulani, awe amepooza, na matokeo yake, tukawa hatuwezi kuhudhuria kanisani kama kawaida. Kipindi hicho ilikuwa ni moja ya hatua za maana sana katika maisha yangu.

Kujitolea kwa dhati.

Nilifarijika kiakili, kwa kule kutoweza tena kwenda kanisani, lakini nilihisi nasukumwa niende mwenyewe kwa muda huo na baadaye. Katika umri wa miaka 16 nilianza kuhudhuria kanisani kwa rafiki yangu ambaye baba yake alikuwa ni mchungaji. Kikanisa chenyewe, kilikuwa ni jengo dogo la stoo ya mbele ya nyumba, kikiwa na washiriki ambao ni, familia ya rafiki yangu, mimi, na wanafunzi wengine wachache tu. Jambo hili liliendelea kwa miezi michache tu kabla ya kufungwa kwa kanisa hilo. Baada ya kumaliza masomo ya sekondari na kuingia chuo kikuu nilifufua matendo yangu ya kidini na nikawa ni mwenye kujitumbukiza kikamilifu katika mafundisho ya Kipentekoste. “Nilibatizwa na kujazwa roho mtakatifu.” Ikiwa ni kama uzoefu niliouita. Nikiwa mwanafunzi wa chuo, kwa haraka haraka nikawa fahari ya kanisa. Kila mtu alikuwa na matarajio makubwa juu yangu, na nilikuwa ninafuraha kwa mara nyingine tena kuwa hivyo, “katika njia ya kuelekea uwokovu.”

Nilihudhuria kanisani kila mara ilipofunguliwa milango yake. Nilijifunza Biblia kwa masiku na mawiki, katika kipindi hicho. Nilihudhuria mihadhara iliyotolewa na wanazuoni wa Kikristo wa zama zangu, na nikajulikana na kualikwa katika uchungaji nikiwa na miaka ishirini. nilianza kuhubiri na kuwa mashuhuri sana, upesi upesi. Nilikuwa naamini na kung’ang’ania kikamilifu kuwa hakuna atakayepata uwokovu ila awe katika kundi la kanisa langu. Nami kwa waziwazi nilimlaumu kila mtu ambaye hakumjua Mungu kwa njia niliyomjua mimi. Nilifundishwa kuwa Yesu Kristo (amani iwe juu yake) na Mungu Muweza walikuwa ni kitu kimoja. Nilifundishwa kuwa kanisa letu haliamini utatu lakini Yesu (amani iwe juu yake) kwa hakika ndiye aliyekuwa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Mimi mwenyewe nilijaribu kutaka kuelewa jambo hilo, hivyo, nililazimika kukiri kuwa jambo hilo haliingii akilini mwangu (halifahamiki). Niliheshimu nguo takatifu za wanawake na tabia njema ya wanaume. Nilifurahia kuitekeleza imani, pale ambako wanawake walitakiwa wavae maguo yanayowafunika gubi gubi, wasitie rangi nyuso zao kwa vipodozi, na wawe mabalozi wa kweli wa Kristo. Nilikinaishwa nyuma ya pazia ya mashaka kuwa hatimaye nimepata njia ya kweli ya kuingia katika furaha ya kweli. Nilikuwa nabishana na yeyote wa kutoka kanisa lolote na imani yeyote na nilikuwa nawanyamazisha kabisa kabisa kwa elimu yangu ya Biblia. Nimehifadhi mamia ya vifungu vya Biblia, na hilo lilikuwa ndilo nembo ya mahubiri yangu. Naam, hata hivyo, nilihisi kuwa kwa hakika nipo katika njia iliyosahihi, na sehemu yangu nyingine ilikuwa bado inatafuta. Nilihisi kuwa kulikuwa na ukweli wa hali ya juu ambao unatakiwa ufikiwe.

Nilipokuwa peke yangu nilikuwa natafakari na kumuomba Mungu aniongoze katika dini sahihi na anisamehe ikiwa kile nilichokuwa nakitenda kilikuwa ni makosa. Kamwe nilikuwa sijawahi kuwa na mawasiliano na Waislamu. Watu pekee wanaodai kuwa Uislamu ndiyo dini yao walikuwa ni wafuasi wa Elijah Muhammad, ambao walikuwa wakizingatiwa na watu wengi kuwa ni “Waislamu Weusi” au “The Lost-Found Nation.” Na ilikuwa katika kipindi hiki mwishoni mwa miaka ya sabini pale mchungaji Louis Farrakhani kwa hakika, alikuwa vizuri katika kukijenga upya kile kilichojulikana kama ni “Taifa la Kiislamu” nilienda kumsikiliza mchungaji Farrakhani alipokuwa akizungumza katika mwaliko wa wafanyakazi wa ushirika na nikakata shauri kuwa jambo hilo limekuwa ni uzoefu unaoweza kubadili maisha yangu kwa mtindo wa kisanaa. Kamwe maishani mwangu sijapatapo kumsikia mtu mweusi akiongea kwa njia aliyoongea. Nami kwa haraka haraka nilitaka kuandaa nikutane naye ili nijaribu kumbadili na aingie dini yangu. Nilifurahia kuhubiri Injili, nikitaraji kuzipata nyoyo zilizopotea ili niziokoe ziepukane na Moto wa Jehannamu- bila kujali watu hao ni akina nani.

Baada ya kumaliza chuo kikuu nilianza kufanya kazi kamili. Nilifikia kilele cha uchungaji wangu, huku wafuasi wa Elijah Muhammad wakiwa wanaonekana sana, na niliziheshimu juhudi zao za kujaribu kuiondoa jamii ya watu weusi waepukane na maovu ambayo yalikuwa yakiwaharibu. Nilianza kuwaunga mkono, akilini, kwa kununua maandiko yao na hata kukutana nao kwa mazungumzo. Nilihudhuria mazungumzo na masomo yao ili nijue nini hasa walichokuwa wanakiamini. Kwa namna niliyokuwa nawajua, wengi wao walikuwa waaminifu, lakini sikuweza kununua (kukubali) wazo la kuwa Mungu, ni mtu mweusi. Nilipinga utuimiaji wao wa Biblia kuunga mkono upande wao katika mambo maalumu. Hiki kilikuwa ndicho kitabu nilichokijua vizuri sana, na nilisumbuka sana kwa kile nilichokifikiria kuwa ni kufahamu vibaya kwao, na upotoshaji wao wa kitabu hicho. Nilienda shule ya Biblia ya mtaani na nikawa na elimu kubwa katika nyanja mbali mbali za masomo ya Biblia.

Baada ya takriban miaka sita nilienda Texas na nikawa nashiriki katika makanisa mawili. La kwanza lilikuwa linaongozwa na mchungaji kijana ambaye alikuwa hana uzoefu wala elimu ya kutosha. Elimu yangu ya maandiko ya Kikristo kwa muda huo ilikuwa imeendelea kwa kitu kisicho cha kawaida. Nilijawa na mafundisho ya Kibiblia. Nikaanza kutazama kwa kina ndani ya maandiko na nikatambua kuwa nilikuwa ninajua zaidi kuliko kiongozi aliyekuwepo. Kwa kuonyesha heshima, nililiacha na kujiunga na kanisa lingine katika mji mwingine ambako nilihisi kuwa nitajifunza zaidi. Mchungaji wa kanisa hili la kipekee alikuwa ni mwanazuoni sana. Alikuwa ni mwalimu wa daraja la juu lakini alikuwa na baadhi ya ya fikra ambazo hazikuwa za kawaida kwa umoja wa kanisani kwetu. Yeye alikuwa na mitazamo ya kiliberali lakini bado nilikuwa nafurahia mafundisho yake. Punde tu nikajifunza somo la thamani sana juu ya maisha yangu ya Ukristo, ambalo lilikuwa ni “Kila king’acho si dhahabu” kinyume na umbile lake la nje, kulikuwa na uovu uliochukua nafasi ambao kamwe sijaufikiria kuwa unawezekana kuwepo kanisani. Uovu huo ulinisababishia nitafakari kwa kina, na kuanza kusaili mafundisho ambayo nilijizatiti nayo kwa sana.

Karibu Katika Ulimwengu Wa Kweli Wa Kanisa.

Punde tu niligundua kuwa kulikuwa na wivu mkubwa ulioenea katika makasisi watumishi wa Bwana. Vitu vimebadilika kutoka vile nilivyovizoea. Wanawake walikuwa wanavaa nguo ambazo nilidhani kuwa ni za kuaibisha. Watu walivaa ili kuvutia, na mara nyingi watu wa jinsia nyingine. Nimegundua kuwa pesa na uchoyo vinacheza pati kubwa katika huduma za kazi za kanisani. Kulikuwa na makanisa madogo madogo mengi yakisuasua, na wao walituita tuitishe mikutano na kuwasaidia kuwachangia pesa.

Niliambiwa kuwa kama kanisa halina idadi maalumu ya wanachama, nisipoteze muda wangu kuhubiri katika kanisa hilo kwa sababu sitopata faida ya mali ya kutosha. Kisha nami nilieleza kuwa mimi sipo katika kanisa hilo kwa ajili ya pesa na kwa hiyo, ningehubiri hata kama kungekuwa na mtu mmoja tu… na ningefanya hivyo bure! Jambo hilo lilisababisha mkanganyiko. Nilianza kuwahoji wale wote niliowadhania kuwa ni wenye busara, ili nijue kama wameingia katika ulaghai. Nikagundua kuwa pesa, nguvu na madaraka vilikuwa ni vitu muhimu sana kwao kuliko kufundisha ukweli juu ya Biblia. Nikiwa mwanafunzi wa Biblia nilijua kwa ukamilifu kuwa kulikuwa na makosa, kupingana na uzushi. Nilidhani kuwa lazima watu wawekwe wazi kuelekea ukweli kuhusu Biblia. Wazo hili la kuwawekea watu wazi mtazamo huo wa Kibiblia lilikuwa ni wazo ninalolidhania kuwa ndilo linaloungwa mkono na shetani. Lakini kwa uwazi, nilianza kuwauliza walimu zangu maswali mengi wakati wa darasa za Biblia, maswali ambayo hakuna hata mmoja wao aliyeweza kuyajibu. Hakuna hata mmoja aliyeweza kufafanua vipi Yesu anafanywa kuwa ni Mungu, Mwana na Roho Mtakatifu aliyefinyangwa pamoja na kuwa mmoja na bado si sehemu ya utatu. Mwishowe, wahubiri kadhaa walilazimika kukiri kuwa wao pia hawajafahamu jambo hilo lakini tulitakiwa kuamini tu kirahisi rahisi.

Kesi za uzinzi na uasherati zilipita bila ya kutolewa adhabu. Baadhi ya wahubiri walitawaliwa na madawa ya kulevya na wameshaharibu maisha yao na ya familia zao. Viongozi wa baadhi ya makanisa waligundulika kuwa ni mashoga. Kulikuwa na wachungaji waovu watendao uzinzi na mabinti wadogo wadogo wa makanisa mengine. Yote hayo yalihusishwa na kushindwa kupata majibu ya kile nilichokifikiria kuwa ni maswali magumu yaliyotosha kunifanya nitafute mabadiliko. Mabadiliko hayo yalikuja wakati nilipokubali kufanya kazi nchini Saudi Arabia.

Mwanzo Mpya

Haikuchukua muda mrefu baada ya kuwasili Saudi Arabia nikaona mabadiliko ya haraka katika mfumo wa maisha ya Waislamu. Walikuwa wanatofautiana na wafuasi wa Elijah Muhammad na mchungaji Louios Farrakhan kwa upande wa kuwa wote walikuwa ni wazalendo, rangi moja na lugha moja. Nami, kwa haraka haraka nilieleza shauku yangu ya kusoma zaidi kuhusu dini hii ya kipekee yenye kushangaza. Nilishangazwa na maisha ya Mtume Muhammad na nilitaka kuyafahamu zaidi. Niliazima vitabu kutoka kwa mmoja wa jamaa aliyekuwa mchangamfu katika kuwalingania watu waingie Uislamu. Nilipewa vitabu vyote nilivyokuwa navitaka. Nilikisoma kila kitabu. Kisha nikapewa Quran Tukufu na nikaisoma yote yote kwa mara kadhaa katika kipindi cha miezi minne. Kilichonivutia zaidi ni kuwa, wale jamaa hawakuwa ni wenye kunigandamiza kwa elimu zao. Kama ndugu yeyote hakujua jibu la swali aliloulizwa, aliniambia kwa wepesi kabisa, kuwa hawezi kulijibu na ataliangalia kwa mtu anayeliweza. Na siku inayofuata daima ataniletea jibu. Nikaona jinsi ya unyenyekevu ulivyofanya kazi kubwa katika maisha ya watu hao wa ajabu wa mashariki ya kati.

Nilishangazwa kuwaona wanawake wakijifunika kuanzia nyuso zao hadi miguuni. Sijaona dini yeyote ya makasisi ikiwa hivyo. Hakuna mtu aliyeshindana kwa ajili ya kupata cheo cha kidini. Yote hayo yalikuwa ni mazuri ajabu, lakini vipi nitaziendesha fikra za kuacha mafundisho ambayo nimeshayafuata tangu nikiwa mdogo? Je, kuna nini kuhusiana na Biblia? Nilijuwa kuwa kuna baadhi ya ukweli ndani yake hata hivyo, imeshabadilishwa na kurejewa kwa mara nyingi. Kisha nilipewa mkanda wa video wa mahojiano kati ya sheikh Ahmadi Deedat na Reverend Jimmy Swaggart. Baada ya kutazama mjadala huo kwa haraka haraka nikawa Mwislamu.

Unaweza kusikiliza majadiliano hayo katika website

sitehtt:// www.islam.org/audiyo/ra622_4.ram

Unaweza kuvishusha vitabu vya

Shaykh Ahmadi Deedat

Kupitia website hizi:

www.ahmed-deedat.co.za

au www.aljame3.com

Nami kirasmi nilitangaza kuukubali Uislamu. Na ilikuwa hapo ndipo nilipopewa ushauri wa mdomo juu ya namna ya kujiandaa kwa safari ndefu huko mbele. Ilikuwa ni mazazi ya kweli kutoka kizani na kuingia katika nuru. Nilistaajabu, kivipi, wenzangu wa kutoka kanisani wangenifikiria watakaposikia kuwa nimeingia Uislamu. Haikuchukuwa muda mrefu kabla sijagundua. Nilirudi USA kwa ajili ya likizo na nilikosolewa vikali mno kwa “ukosefu wangu wa imani.” Nilibandikwa majina mengi – kuanzia muhaini hadi mpotovu. Watu waliambiwa na viongozi wa kanisa hata wasinikumbuke wakati wa sala. Hiyo ilikuwa ni kama ugeni, inavyoonekana kwani mwishoni sikuudhika. Nilikuwa na furaha sana kwa kuwa Mungu Muweza, Allah, amenichagua na kuniongoza katika haki ambayo hakuna kitu kingine cha kukijali.

Kitu pekee, ninachohitaji kwa sasa ni kuwa Mwislamu niliyejitolea kwa dhati kama nilivyokuwa Mkristo. Hili, bila ya shaka, linamaanisha kusoma. Nilitambua kuwa mtu anaweza kukua kielimu kama atakavyo ndani ya Uislamu. Hakuna ukiritimba wa elimu – na elimu ni bure kwa kila atakaye kujinufaisha kwa nafasi ya kusoma. Nilipewa seti ya Saheeh Muslim kama zawadi kutoka kwa mwalimu wangu wa Quran. Na ilikuwa ni hapo ndipo nilipogundua kuwa kuna haja ya kujifunza kuhusu maisha, maneno na matendo ya Mtume Muhammad. Nilisoma na kijifunza hadithi nyingi zilizokuwepo katika Kingereza kwa kadiri ilivyowezekana. Nilitambua kuwa elimu yangu ya Biblia ilikuwa ni rasilimali ambayo inafaa zaidi kwa sasa katika kushughulika na wale wenye historia ya kuwa Wakristo. Kwangu maisha yalikuwa na maana mpya kabisa. Moja ya mabadiliko ya kimtazamo ya maana sana ni matokeo ya kujua kuwa maisha haya kwa hakika yatumiwe kwa kujiandaa na Ahera. Pia, ilikuwa ni uzoefu mpya kujua kuwa tunalipwa hata kwa nia zetu. Kama umenuia kutenda jema, utalipwa. Hiyo ilikuwa ni tofauti kabisa na kanisani. Mtazamo ulikuwa ni “njia ya Motoni imepambiwa nia nzuri nzuri.” Kulikuwa hakuna njia ya kushinda. Kama umefanya dhambi, ulitakiwa uungame kwa mchungaji, na hasa hasa kama dhambi yenyewe ni kubwa, kama vile uzinzi. Ulihukumiwa moja kwa moja kwa matendo yako.

Wakati Uliopo na Mustakabala

Baada ya kufanya mahojiano na gazeti la Madinah niliulizwa kuhusu kazi zangu za sasa na mipango yangu ya baadaye. Kwa sasa, lengo langu ni kusoma Kiarabu, na kuendelea kujifunza ili kupata elimu kubwa kuhusu Uislamu. Kwa sasa nimejizatiti katika nyanja ya da’wah na ninawaita, kwa mahubiri wasiokuwa Waislamu ambao wamekuja kutokea Ukristo. Kama Allah Muweza, ataniacha hai, natarajia kuandika zaidi kuhusu somo la mlinganisho wa dini.

Ni wajibu wa Mwislamu ulimwenguni kote afanye kazi ya kusambaza elimu ya Kiislamu. Kama vile nilivyotumia muda mwingi nikiwa kama mwalimu wa Biblia, nahisi hisia za pekee za wajibu wa kuwaelimisha watu kuhusu makosa, mikanganyiko na visa vya kughushi vya kitabu kinachoaminiwa na mamilioni ya watu. Moja ya furaha kuu ni kujua kuwa silazimiki kujidhatiti katika mabishano na Wakristo, kwa sababu nilikuwa ni mwalimu ambaye amefundisha mbinu nyingi za mabishano wanazozitumia. Pia nimejifunza namna ya kubishana kwa kutumia Biblia ili kuulinda Ukristo. Na wakati huo huo ninajua jibu la mabishano ambayo sisi, kama wachungaji, tulikatazwa na wakuu wetu tusiyajadili au tusiyaweke wazi.

Namuomba Allah anisamehe uzembe wangu wote na atuongoze njia ya Peponi. Sifa zote ni za Allah. Rehema na Amani ziwe juu ya Mjumbe wake wa mwisho, Mtume Muhammad na familia yake, na wafuasi wa kweli wote.

Abdullah Muhammad al-Faruque (Kenneth L. Jenkins)

At-Ta’if, Kingdon of Saudi Arabia

  

 3- DR. JERALD F. DIRKS (ABU YAHYA) ALIYEKUWA MCHUNGAJI (SHEMASI) WA KANISA LA MUUNGANO WA WAMETHODISTI. ANA STASHAHADA YA UZAMILI YA THEOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA HARVARD NA STASHAHADA YA UDAKITARI WA FALSAFA KATIKA MAMBO YA KISAIKOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA DENVER. (USA)

Moja ya kumbukumbu zangu za utotoni kabisa ni kusikia mlio wa kengele ya kanisani kwa ajili ya ibada ya Jumapili katika kitongoji nilichokulia. Kanisa hilo la Methodisti, lilikuwa kongwe, la miti, na lina mnara wa kengele, shule ya kila Jumapili yenye madarasa madogo madogo ya watoto wawili iliyokuwepo nyuma ya zizi, milango ya mbao inayotenganisha madarasa hayo na eneo la kanisa, kulikuwa na roshani ya kwaya inayotoa makazi kwa madarasa ya shule ya Jumapili kwa vijana walio wakubwa. Kanisa hilo lilikuwepo umbali si zaidi ya magorofa mawili kutokea nyumbani kwangu. Kengele inapogonga, sote tulikuwa tunaenda kwa pamoja kama familia, na kufanya hija yetu ya kila wiki kulitembelea kanisa hilo.

Katika kijiji kilichoanza tangu miaka ya 1950, makanisa matatu yaliyokuwepo katika mji huo yenye takriban watu mia tano ndiyo yaliyokuwa makao makuu ya maisha ya usharika. kanisa la Methodisti la mtaani, ambalo lilikuwa linamilikiwa na familia yangu, lilikuwa linatoa askrimu za kijiti, askrimu zilizotengenezwa nyumbani, chakula cha usiku cha (chicken potpie), na losti ya vikopo. Mimi na familia yangu daima tulikuwa tukishiriki katika makanisa yote matatu, lakini kila moja tuliliendea mara moja kwa mwaka. Kwa kuongezea, kulikuwa na shule ya usharika wa Biblia ya wiki mbili kila mwezi wa Juni, kila siku, nilikuwa nahudhuria shule yangu ya hatua nne kwa mwaka. Hata hivyo, ibada ya Jumapili asubuhi na shule ya Jumapili yakiwa ni matukio ya kila wiki, na nilijitahidi kuulinda mjumuisho wangu na kuhudhuria sehemu hizo kikamilifu, nilijifunga kibwebwe na kupata zawadi ya kuhifadhi Biblia.

Katika siku za shule za hatua ya kwanza ya sekondari. Lile kanisa la Methodisti la mtaani lilifungwa, na tulikuwa tunahudhuria kanisa la Methodisti lilokuwepo katika mji wa karibu, ambalo ni kubwa kidogo kuliko lile la kitongoji alimokuwa akiishi. Hapo kwanza fikra zangu zilianza kutazama uchungaji kama unavyoitwa. Nikiwa mchangamfu katika ufuasi wa umoja wa vijana wa Methodisti, na hatimaye nikahudumia pande mbili, jimbo na uofisa wa mazungumzo. Pia nikawa muhubiri wa kawaida katika kipindi cha huduma kwa vijana siku za Jumapili kila mwaka. Mahubiri yangu yalianza kuongeza idadi ya washirika, na kabla ya muda kurefuka mara kwa mara nilikuwa najaza nafasi za membari za padri katika makanisa mengine, katika nyumba za uuguzi, katika usharika wa vijana wa makanisa mbali mbali na makundi ya akina mama, sehemu ambazo kwa aina yake, niliweka rekodi za mahudhurio.

Nilipotimiza miaka miaka kumi na saba nilianza masomo ya mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Harvard, uamuzi wangu wa kuingia uchungaji ulikuwa wa nguvu. Katika kipindi cha mwaka wangu wa kwanza chuoni hapo, nilijiandikisha katika kozi ya mihula miwili ya mlinganisho wa dini ambayo ilikuwa inafundishwa na Wilfred Cantwell Smith, aliyekuwa mtaalamu bingwa wa dini ya Kiislamu. Katika kozi hiyo, nilitoa mazingatio madogo kiasi kwa Uislamu kuliko dini nyinginezo, kama vile Uhindu na Ubudha, kwani hizo mbili za mwishoni zilionekana ni za faragha sana na ni ngeni sana kwangu. Ikiwa ni kinyume na Uislamu, ulionekana kuwa, kwa kiasi kidogo ni sawa sawa na dini yangu ya Ukristo. Kwa hiyo, sikutoa umakini mkali juu ya Uislamu kama inavyotakiwa, ingawa ninaweza kukumbuka kuandika waraka wa istilahi za hiyo kozi juu ya maana ya ufunuo katika Quran. Hata hivyo, kwa kuwa kozi hiyo ilikuwa ni moja ya kozi ngumu kabisa, kwa viwango vya kitaalamu, nilihitaji maktaba ndogo ya nusu dazeni ya vitabu vya Kiislamu, hivyo vyote viliandikwa na wasiokuwa Waislamu, na vyote vilikuwa ni vya kunihudumia kwa umadhubuti, miaka ishirini na tano baadaye. Pia nilihitaji tafsiri tofauti tofauti za maana ya Quran kwa Kingereza, ambazo nilizisoma kwa muda huo.

Katika majira ya michipuo chuo cha Harvad kilinitangaza kuwa ni mwanazuoni mkali, akimaanisha kuwa, nilikuwa ni mmoja wa wanafunzi wa hali ya juu katika maandalizi ya theolojia chuoni hapo. Katika majira ya kiangazi ya mwaka wangu wa kwanza chuoni Harvard na mwaka wa pili, nilifanya kazi ya uchungaji kwa vijana walio katika kanisa kubwa kabisa la umoja wa Wamethodosti. Kiangazi kilichofuata, nilipata leseni ya kuhubiri kutoka kanisa la muungano wa Wamethodosti. Baada ya kumaliza chuo cha Havard mwaka 1971, nilijiandikisha shule ya Utakatifu ya Havard, na hapo nilipata stashahada ya uzamili juu ya theolojia mwaka 1974, baada ya kusimikwa kikamilifu katika ushemasi wa muungano wa makanisa ya Methodisti mwaka 1972, na kwa kuwa, hapo kabla nilipata udhamini wa masomo wa Stewart Scholarship kutoka muungano wa makanisa ya Methodisti ikiwa ni kama nyongeza ya udhamini wangu wa Havard Divinity School. Nikiwa katika elimu ya seminari, pia nilimaliza masomo ya nje ya vipindi vya miaka miwili ya ukasisi wa mahospitalini katika hospitali ya Peter Bent Brigham mjini Boston. Baada ya kumaliza masomo katika shule ya utakatifu ya Havard, niliutumia wakati wa kiangazi nikiwa ni mchungaji wa makanisa mawili ya Methodisti katika viunga vya Kansas, ambako mahudhurio yalipanda juu kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana katika makanisa yote hayo kwa miaka kadhaa.

Kwa nje ilionyesha kuwa, nilikuwa mchungaji kijana mwenye kutunza ahadi sana ambaye amepokea elimu bora zaidi, kuvutia kundi kubwa la watu katika ibada ya Jumapili asubuhi, na kulikuwa na mafanikio katika kila kituo kwenye njia ya utumishi. Hata hivyo, kwa ndani ilionyesha, nilikuwa napambana vita vya daima kudumisha msimamo wangu binafsi katika uso wa majukumu ya utumishi. Vita hivi vilikuwa mbali sana na vile vinavyotazamiwa vya kupambana na baadhi ya wainjilisti wa hivi karibuni katika majaribio yasiofanikiwa ya kuendeleza utu wa kiroho na kingono. Hivyo, ilikuwa ni vita tofauti sana na vile nilivyopambana na mapadri Pedophilic waliotamba katika vichwa vya habari vya zama za sasa. Hata hivyo, mihangaiko yangu ya kudumisha uadilifu wa utu wangu huenda ikawa ni jambo la kawaida kukabiliwa na wanachama wa utumishi wenye elimu bora sana.

Kuna aina fulani ya kejeli katika ukweli kwamba wale wanaodhaniwa kuwa ni watumishi bora kabisa wanaochaguliwa kwa elimu bora kabisa ya seminari, kwa mfano: wale wanaopewa ofa katika muda ule wa shule ya Theolojia ya Harvard. Kejeli ni kuwa, kwa kupewa elimu hiyo, wanaseminari wanawekewa wazi historia nyingi ya ukweli kama inavyojulikana: 1)- maelezo ya kanisa la mwanzo, na vipi lilijengwa kwa siasa ya nchi kama inavyoathiriwa na mambo ya kijografia. 2)- masomo “asilia” ya maandiko mbali mbali ya Kibiblia, mengi yao yakiwa katika makindano makali na yale yanayosomwa na Wakristo wengi wanapobeba Biblia zao, ingawa kidogo, baadhi ya maelezo hayo hayajaharibiwa na kutiwa katika tafsiri mpya na bora zaidi; 3)- mabadiliko ya itikadi hizo kama ya nafsi tatu kwa moja ya Mungu na uwana wa Yesu, amani iwe juu yake; 4)- mambo ya wasiokuwa na dini yapo katika kanuni za imani na mafundisho ya Wakristo wengi; 5)- kuwepo kwa makanisa yote hayo ya mwanzo na harakati za Kikristo ambazo hazikubali itikadi ya utatu wa Mungu, na ambazo kamwe hazikubali itikadi ya uungu wa Yesu, amani iwe juu yake; 6)- mengineyo (baadhi ya matunda haya ya elimu yangu ya seminari yanasimulia habari nyingi zaidi katika kitabu changu kipya, Msalaba na Mwezi; mazungumzo ya imani mchanganyiko kati ya Ukristo na Uislamu, yaliyochapishwa na Amana Publications 2001.)

Kwa hiyo, si ajabu kabisa kuwa wanaomaliza masomo ya seminari wengi wao wanatoka kutoka katika seminari si kwenda “kujaza majukwaa,” sehemu ambayo wataombwa wahubiri kile wanachokijua kuwa si cha kweli, lakini kinyume chake wanajiingiza katika kazi mbali mbali za ushauri. Hali hiyo ndiyo iliyonikumba, kwani nilijiendeleza ili nipate stashahada ya uzamili na udaktari ya matibabu ya kisaikolojia. Niliendelea kujiita Mkristo, kwa sababu hilo lilikuwa linahitajika kwa ajili ya kujitambulisha, na kwa kuwa nilikuwa Mkristo, baada ya yote, ni mchungaji msimikwa, hata hivyo, kazi yangu ni kazi ya kutibu magonjwa ya kiakili. Hata hivyo, elimu yangu ya seminari ilikuwa ni kinga dhidi ya imani ya kuamini utatu wa Mungu, au uungu wa Yesu, amani iwe juu yake. (Kura za maoni mara kwa mara zinabainisha kuwa wachungaji wanaimani ndogo katika kuamini mambo hayo na imani nyinginezo za kanisa kuliko walei (waumini wa kawaida) wanaowahudumia, kwa sitiari, huku wakazi wa parokia wakifahamu jambo hilo kimaneno tu.) Mimi nilikuwa Mkristo wa Krismasi na Pasaka.” Naenda kanisani mara moja moja sana, kisha nikakerekeza meno yangu na kuuma ulimi wangu nilipokuwa nasikiliza mahubiri yaliotetea kile nilichokijua kuwa hakikuwa kadhia husika.

Hakuna hata moja katika hayo yaliyopita liwezalo kuchukuliwa ili lionyeshe kuwa mimi nilikuwa nina upeo wa dini mdogo au uelewa wa kiroho mdogo kuliko vile nilivyokuwa zamani. Nilikuwa ninasali kila siku, imani yangu kwa Mungu Mkuu ilibaki imara na salama, na niliendesha maisha yangu binafsi katika mstari pamoja na maadili niliyofundishwa kanisani na katika shule ya Jumapili. Kiwepesi, nilikuwa ninajua lilobora zaidi kuliko kununua imani zilizotengenezwa na mtu na mamlaka za kiimani za usharika wa kanisa, ambazo zilikuwa zimeshehenezwa mambo mazito mazito ya kipagani, fikra za kishirikina (kuabudu miungu mingi), na athari za kijografia za miongo iliyopita.

Baada ya kupita miaka kadhaa, nimekuwa najihusisha zaidi na kupotea kwa dini katika jamii ya Kimarekani. Dini ni uhai/roho inayopumua na wema kwa kila mtu, na haitakiwi ichanganywe na ubabaishaji wa kidini, ambao unajihusisha na ada za kidini, ibada, na kutunga sheria za baadhi ya vyama vilivyopo, kama ilivyo kwa kanisa. Utamaduni wa Marekani unadhihirisha kuwa unaendelea kupoteza utu na dira ya kidini. Ndoa mbili katika kila ndoa tatu zinaisha kwa talaka; vurugu zimekuwa ni sehemu ya urithi uongezekao mashuleni kwetu na mabarabarani; majukumu binafsi yamepungua; heshima binafsi imedidimizwa na moyo wa “Kama unahisi ni kizuri, kifanye;” viongozi na taasisi mbali mbali wa Kikristo zimesombwa na kashfa za ngono na mali; na fikra za kujihalalishia tabia zao, vyovyote zitakavyochukiza.

Utamaduni wa Kimarekani umekuwa ni taasisi inayofilisika kiutu, nami binafsi nilikuwa ninayahisi mambo hayo katika mikesha yangu ya kidini.

Ilikuwa ni hali hiyo iliyonifanya nianze mawasiliano na jamii za Kiislamu za mtaani. Kwa miaka michache kabla ya, mimi na mke wangu kujishughulisha kikweli kweli katika uchunguzi juu ya historia ya farasi wa Uarabuni. Hatimaye, ili kupata tafsiri salama za nyaraka mbali mbali za Kiarabu, uchunguzi huu umetupelekea tukaingia katika mawasiliano na Wamarekani wa Kiarabu ambao walikuwa ni Waislamu, mawasiliano yetu ya kwanza yalikuwa na Jamal wakati wa kiangazi cha mwaka 1991.

Baada ya mazungumzo ya awali kwa kutumia simu, Jamal alitembelea nyumba yetu, na akajitolea kutufanyia tafsiri, na kusaidia kutuongoza katika historia ya farasi wa Kiarabu katika mashariki ya kati. Kabla Jamal hajatuacha mchana huo, alituomba kutumia, bafu yetu ili ajioshe kabla ya kutamka sala zake za ratiba ya kila siku; na alituazima kipande cha gazeti ili akitumie kama zulia la kuswalia, kwa hiyo, alitamka sala zake kabla hajaondoka na kuiacha nyumba yetu. Na sisi, bila ya shaka, tulilazimika, lakini tulistaajabu kama kungekuwa na kitu kizuri zaidi cha kutoa ambacho tungempa akitumie kuliko gazeti. Sisi bila ya kutambua kitu kwa muda huo, Jamal alikuwa anafanya aina nzuri sana ya Dawa (kuhubiri au kushawishi). Hakutoa maelezo yeyote juu ya ukweli kwamba sisi hatukuwa Waislamu, naye hajatuhubiria chochote kuhusiana na imani yake ya kidini. Yeye alitufikishia mifano ya imani yake tu; mfano uliosema sauti kubwa, kama mtu alihitaji kuwa msikivu wa somo.

Baada ya miezi kumi na sita, kukutana na Jamal kuliongezeka kidogo kidogo na kuwa mara kwa mara, hadi ikawa mara moja kila wiki mbili na kufikia kila wiki. Katika safari hizo, Jamal kamwe hajanihubiria kuhusu Uislamu, kamwe hajaniuliza kuhusu imani ya dini yangu au ninachokikinai, na kamwe hajapendekeza kwa mdomo kuwa niwe Mwislamu. Hata hivyo, nilianza kujifunza mengi. Kwanza kabisa, kulikuwa na mfano wa matendo ya daima kutoka kwa Jamal wa kunionyesha vipindi vya sala zake za kila siku. Pili kulikuwa na mfano wa kimwenendo wa namna Jamal alivyokuwa akiyaendesha maisha yake ya kila siku kwa unyofu wa hali ya juu na tabia ya maadili, anafanya yote mawili hayo katika ulimwengu wake wa kibiashara na katika ulimwengu wake wa kijamii. Tatu, kulikuwa na mfano wa kimwenendo juu ya namna Jmal anavyohusiana na watoto wake wawili. Kwa mke wangu, mke wa Jamal alitoa mifano hiyo hiyo. Nne, daima kulikuwa na wigo wa kunisaidia nifahamu historia ya farasi wa Uarabuni wa Mashariki ya Kati, Jamal alianza kushirikiana nami: 1) visa vya Warabu na historia ya Uislamu; 2) hadithi za Mtume Muhammad, rehema ziwe juu yake; na 3) aya za Quran na mijadala yake inayozingatia muktadha na ifanyayo kituo juu ya baadhi ya mitazamo ya Kiislamu, lakini daima alikuwa anaiwasilisha kwa istilahi za kunisaidia kifikra ili nifahamu muktadha wa Uislamu katika historia ya farasi wa Uarabuni. Kamwe sijaambiwa kuwa “hivi ndivyo vitu vilivyo”, nilikuwa naambiwa “hivi ndivyo Waislamu wanavyoamini” tu. Kwa kuwa sikuwa “nahubiriwa,” na kwa kuwa Jamal kamwe hajataka imani yangu, sikuhitaji kujisumbua na kujaribu kutetea upande wangu. Mambo yote yalifanyika kiakili, na si kama mbadilishaji dini.

Kidogo kidogo, Jamal alianza, kututambulisha kwa familia za Waarabu wengine katika jamii ya Waislamu wa mtaani. Kulikuwa na Wa’eli na familia yake, Khalidi na familia yake, na wengine wachache kwa unyofu, niliona mtu mmoja na familia ambazo zilikuwa zinaishi maisha yao kwa maadili ya hali ya juu, yaliyo sawa sawa kuliko jamii ya Kimarekani ambayo kwayo sisi sote tulikuwa ndani yake. Huenda kulikuwa na jambo katika matendo ya Uislamu niliyokuwa nayakosa wakati nilipokuwa mwanachuo na katika siku za seminari.

Hadi Desemba, 1992, nilianza kujiuliza baadhi ya maswali makali juu ya wapi nilipokuwepo na nilikuwa ninafanya nini. Maswali hayo yalichochewa na nadhari zifuatazo. 1) Baada ya kozi ya awali ya miezi kumi na sita, maisha yetu ya kijamii yalianza kukua katika kutilia maanani wigo wa Waarabu wa jamii ya Kiislamu ya Mtaani. Kufikia Desemba, karibia 75% ya maisha yetu ya kijamii yalikuwa yanajumuisha na kupitishwa na Waislamu wa Kiarabu. 2) Kwa maadili ya mafunzo na elimu yangu ya seminari, nilijua kuwa kuna kuharibiwa vibaya kwa Biblia (mara nyingine nilijua kwa hakika kabisa lini, wapi, na kwa nini), sikuwa na imani yeyote juu ya utatu wa Mungu, na sikuwa na imani ya chochote zaidi ya sitiari tu “Uwana” wa Yesu, amani iwe kwake. Kwa ufupi, huku nikiwa namwamini Mungu kikamilifu, nilikuwa nina imani kali juu ya Mungu Mmoja kama rafiki zangu wa Kiislamu. 3) Thamani yangu binafsi na akili yangu ya maadili iliyokuwa inaegemea sana kukaa na marafiki Waislamu kuliko na jamii ya “Wakristo” iliyonizunguka. Baada ya yote, nilikuwa na mifano isiyopingana ya Jamal, Khalid, na Wa’el ikiwa ni vielelezo kwangu. Kwa ufupi, kiu yangu ya miaka mingi ya kupata aina ya jamii ambayo nimekulia ilipatikana na kupendeza kutika jamii ya Kiislamu. Jamii ya Kimarekani, imemomonyoka kimaadili, lakini ni jambo hilo halikuwa tatizo kwa sababu ya ile ya jamii ya Waislamu ambayo nimeshawasiliana nayo. Ndoa zilikuwa ni imara, wanandoa walikuwa wanawajibika wao kwa wao, wema, uadilifu, msimamo, kubeba majukumu na thamani ya familia ilitiliwa mkazo. Mke wangu alijaribu tuishi maisha yetu kwa njia hiyo hiyo, lakini kwa miaka mingi nimehisi kuwa tulikuwa tunafanya hivyo katika muktadha ombwe (tupu, wazi) wa kimaadili ya kiroho. Jamii ya Kiislamu ilionekana kuwa ni tofauti. Nyuzi mbali mbali, zilifumwa pamoja na kuwa kamba moja.

Farasi wa Kiarabu, malezi yangu ya utotoni, uvamizi wangu wa kuingia uchungaji wa Kikristo na kuwasiliana kwangu na jamii ya Waislamu yalikuwa ni mambo tata yanayosokotana. Kujiuliza kulifikia kichwani pale, hatimaye nilipofikia kujiuliza kuna nini hasa kinachonitenganisha na imani ya rafiki zangu Waislamu. Nikapendekeza kuwa niibue swali hilo kwa Jamal au Khalid, lakini sikuwa tayari kuchukua hatua hiyo. Kamwe sijawahi kujadiliana nao juu ya imani ya dini yangu mwenyewe, na sikufikiria kuwa nilitaka kuitoa mada hiyo katika urafiki wetu. Kwa hiyo, nilianza kuegesha pembeni rafu yote ya vitabu juu ya Uislamu ambavyo nilivipata nilipokuwa chuoni na seminarini. Hata hivyo, kwa mbali imani yangu ilikua kutokana na nafasi asilia ya kanisa, na ingawa nilienda kanisani mara chache lakini kwa hakika nilihudhuria kanisani, na bado nilikuwa najitambulisha kuwa mimi ni Mkristo, na kwa hiyo, niligeukia kazi ya uanazuoni wa Kimagharibi. Mwezi huo wa Desemba, nilisoma nusu dazeni au zaidi ya vitabu juu ya Uislamu vilivyoandikwa na wanazuoni wa Kimagharibi, kikiwemo kimoja cha historia ya Mtume Muhammad, amani iwe juu yake. Zaidi, nilianza kusoma tafsiri mbili za Kingereza zilizotofauti tofauti za maana ya Quran. Kamwe sikuongea na rafiki zangu wa Kiislamu kuhusu huo uchunguzi wangu binafsi wa kugundua mwenyewe. Kamwe sikutaja ni aina gani ya vitabu nilivyokuwa navisoma, wala kuzungumzia kwa nini nilikuwa navisoma vitabu hivyo. Hata hivyo, mara kwa mara nilikuwa nawapelekea maswali yenye mipaka maalumu.

Huku nikiwa siwaambii rafiki zungu wa Kiislamu kuhusu vitabu hivyo, lakini mimi na mke wangu tulikuwa na mijadala mbali mbali juu ya kile nilichokuwa nakisoma. Kufikia wiki ya mwisho ya Desemba 1992, nililazimika kukiri, kuwa sijapata upenyo wowote wa kukataa kimsingi kati ya imani yangu ya kidini na mafundisho ya Kiislamu. Nilipokuwa tayari kufahamu kuwa Muhammad, amani iwe juu yake, alikuwa ni Mtume (mmojawapo aliyeongea kwa, au chini ya msukumo) wa Mungu, na nilipokuwa sina uzito wowote wa kuthibisha kuwa hakuna Mungu kinyume na Allah, Mtukufu aliyetukuka, nilikuwa bado ninasitasita kuchukua uamuzi wowote. Tayari nilikuwa nimekiri katika nafsi yangu kuwa nilikuwa pamoja sana na imani ya Kiislamu kama baadaye nilivyoifahamu, kuliko nilivyofanya na mila ya Kikristo ya kuweka umoja wa kanisa. Nilijua vizuri sana kuwa kiwepesi kabisa ningeweza kuthibitisha kutokana na mafunzo na elimu yangu ya seminari, mambo mengi ambayo Quran ililazimika kuusema Ukristo, Biblia, na Yesu, amani iwe juu yake. Hata hivyo, nilisita. Zaidi, nilitazama kimantiki usitaji wangu kwa kujiendesha mimi mwenyewe kuwa kweli sikijui kiini na suala la msingi na maelezo kamili juu ya Uislamu, na kwa hiyo, maeneo yangu ya kuafiki yaliwekewa mipaka kwa dhana nzima. Kwa hiyo, niliendelea kusoma, na kurudia kusoma.

Wazo moja la kujitambulisha, mimi ni nani, ni uthibitisho wenye nguvu zaidi juu ya nafasi ya mtu binafsi ulimwenguni. Katika kazi zangu nizifanyazo, mara kwa mara niliitwa kutibia tabia mbaya, zinazojipanga kuanzia, kuvuta sigara, hadi ulevi, utumiaji wa madawa ya kulevya. Nikiwa ni tabibu, nilijua kuwa msingi wa tabia mbaya za kiwili wili lazima utibiwe ili kuunda kinga ya awali. Na hilo lilikuwa ni sehemu rahisi sana ya matibabu. Mark Twain alisema: “Kuacha sigara ni kwepesi; nimeshaacha mara mia kadhaa.” Hata hivyo, pia nilijua kuwa funguo ya kudumisha uzuiaji wa wigo wa muda ilikuwa ni kumtibu mgonjwa tabia mbaya za kisaikolojia, ambazo kwa kiasi kikubwa zilizunguka mzizi wa fikra za mgonjwa za kujitambulisha, yaani, mgonjwa anajitambulisha kuwa yeye alikuwa ni “mvuta sigara,” au “mlevi” na kuendelea. Tabia mbaya imeshakuwa ni sehemu na ni mfuko wa fikra hii ya kujitambulisha, ilikuwa ni muhimu sana katika kurekebisha matibabu ya kisaikolojia. Na hii ndiyo iliyokuwa sehemu ngumu sana kimatibabu. Kubadilisha msingi wa fikra za mtu za kujitambulisha ni kazi ngumu sana. Akili ya mtu inang`ang`ania mambo ya zamani na yaliyozoeleka, ambayo yanaonekana ni yenye kutia raha sana kisaikolojia na ni yenye usalama sana kuliko mambo mapya na yasiyozoeleka.

Kwa msingi wa kazi, nilikuwa na elimu hiyo, na niliitumia kila siku. Hata hivyo, kwa dhihaka ya kutosha, sikuwa tayari kuutumia msingi huo kwa nafsi yangu mwenyewe, na katika kadhia yangu ya kusitasita iliyozunguka utambulisho wangu wa kidini. Kwa miaka 43, utambulisho wangu wa kidini kimaridadi ulikuwa ni jina la “Ukristo” hata hivyo, sifa nyingi niliweza kuziongeza katika jambo hilo kwa miaka mingi. Kuacha jina hilo la kujitambulishia dhati binafsi, lilikuwa si rahisi. Lilikuwa ni sehemu na fuko la namna nilivyofahamu kuwepo kwangu. Kupewa faida ya kung’amua, ni wazi kuwa kusita kwangu kulihudumia lengo la kuhakikisha kuwa nitunze utambulisho wangu wa kidini niliouzoea wa kuwa mimi ni Mkristo, ingawa ni Mkristo ambaye anaamini kama wanavyoamini Waislamu.

Na ilikuwa mwishoni kabisa mwa Desemba, mimi na mke wangu tulipokuwa tukijaza fomu za maombi ya pasipoti za US, kwa hiyo, safari iliyopendekezwa ya kwenda mashariki ya kati imekuwa ni ya uhakika. Moja ya swali lilikuwa ni kuhusu ushiriki wa kidini. Hata sikufikiria jambo hilo, na bila kufikiri nikaangukia kule kule kwa zamani na mazoea, nilifungwa katika “Ukristo.” Ulikuwa ni mwepesi na ulikuwa uliozoeleka, na wenye kutia raha.

Hata hivyo, raha hivyo ilikuwa ni ya muda tu na ilivurugika pale mke wangu aliponiuliza vipi nilijibu swali la utambulisho wa dini katika fomu ya maombi. Nami haraka haraka nilijibu “Mkristo”, na kuchekelea chini chini kunakosikika. Sasa, moja ya nadharia ya udadisi ya Kifreudi inayosaidia kufahamu nafasi ya mwanadamu ilikuwa ni kutambua kuwa kicheko mara nyingine ni tiba ya mfadhahiko wa kisaikolojia. Hata hivyo, nadharia ya udadisi ya Kifreudi inaweza ikawa katika mitazamo mingi ya nadharia yake ya mwendelezo wa saikolojia ya ngono, utambuzi wake katika kicheko ulikuwa katika lengo kabisa. Nilicheka! Nini kilikuwa mfadhaiko wa kisaikolojia ambao nililazimika kuutuliza kupitia kicheko cha wastani?

Kisha haraka haraka niliendelea kumpa mke wangu maelezo mafupi yanayothibitisha kuwa nilikuwa Mkristo na sio Mwislamu. Katika kujibu hayo, naye kiungwana alinifahamisha kuwa alikuwa anauliza tu kama mimi nimeandika “Ukristo”, au “Uprotestanti”, au “Umethodisti”. Kwa mujibu wa kanuni za kazi, nilijua kuwa mtu hajitetei kwa lawama ya kitu asichokifanya. (kama itakuwa katika mwendo wa baraza ya tiba za kisaikolojia, na mgonjwa wangu akaropoka, na kusema “sijakikasirikia” na sijaanzisha habari za hasira, ilikuwa ni wazi kuwa mteja wangu alikuwa na hisia za kujitetea dhidi ya mashtaka ambayo bila ya kujijua alikuwa anayafanya. Kwa ufupi, huyo mteja kwa hakika alikuwa na hasira, lakini hakuwa tayari kukiri kitu hicho au kukishughulikia.) Kama mke wangu asingefanya tukio hilo, yaani “wewe ni Mwislamu,” tukio hilo lingenitoka bila ya kujijua, kwa vile ndiye mtu pekee aliyekuwepo. Nilikuwa macho na hilo, lakini niliendelea kusita sita. Jina la dini ambayo imekita katika fikra zangu za kujitambulisha kwa miaka 43 ilikuwa haiwezekani kuondoka kirahisi rahisi.

Takriban mwezi umeshapita tangu mke wangu kuniuliza lile swali. Na ilikuwa mwishoni mwa Januari ya 1993. nilipoweka pembeni vitabu vyote juu ya Uislamu vya wanazuoni wa Kimagharibi, kwa kuwa nimevisoma kikamilifu. Zile tafsiri mbili za Kingereza za maana ya Quran zilirejea tena katika rafu, na nilikuwa nina kazi ya kusoma tafsiri ya tatu ya maana za Quran. Uhenda katika tafsiri hii nitapata uthibitisho wa ghafla kwa….

Nilikuwa nautumia muda wangu wa chakula cha mchana kwa kutoka katika kazi zangu binafsi na kuutumia katika mgahawa wa Kiarabu wa mtaani ambao nimeanza kufululiza kuutembelea. Niliingia kama kawaida, nikakaa katika meza ndogo, na nilifungua tafsiri yangu ya tatu ya Kiingereza ya maana ya Quran kuanzia pale nilipoishia kupasoma. Nilifikiria kupata kusoma kidogo wakati wa chakula cha mchana. Kwa kitambo baadaye, nilikuwa macho kuwa Muhammad alikuwa mabegani mwangu, na anangojea kuchukua oda yangu. Naye akakitupia jicho kile nilichokuwa nakisoma, lakini hakusema lolote kuhusiana na hilo. Oda yangu ilichukuliwa, nami nikarejea katika kisomo changu cha faragha.

Dakika chache baadaye, mkewe, Imani, Mwislamu wa Kimarekani, aliyevalia hijabu na nguo za heshima ambazo nilizizoea kwa wanawake wa Kiislamu, aliniletea oda yangu. Naye aliona kuwa nilikuwa ninasoma Quran, na kwa adabu akaniuliza kama nilikuwa Mwislamu. Neno lilinitoka mdomoni kabla halijarekebishwa na adabu za kijamii au kiungwana: “Hapana” Neno hilo lilitamkwa kwa nguvu, na lilikuwa ni zaidi ya vidokezo vya kukasirika upesi. Kwa ajili hiyo, Iman kwa adabu alijiondoa kutoka pale mezani kwangu.

kimenitokea nini? Nimefanya tabia mbaya na uchokozi. Mwanamke amefanya nini cha kustahiki apate ufedhuli ule kutoka kwangu? Hili halikuwa linalonistahiki. Kwa kupewa malezi ya utotoni, naendelea kutumia “bwana” na “ma’am” nilipokuwa natambulisha makarani na makeshia ambao walikuwa wananingojea madukani. Nilijifanya kudharau kicheko changu mwenyewe kuwa ni kitulizo cha mfadhaiko, lakini sikuweza kuanza kudharau aina hii ya tabia ya kutojitambua niliyoianza. Nikaweka pembeni kule kusoma, na kiakili nililewa na aina hii ya matukio kupitia chakula changu, kila nikiongezeka kuchukuliwa na kile chakula ndiyo nikiongezeka kuhisi uovu juu ya tabia yangu. Nilijua kuwa wakati Imani atakaponiletea cheki baada ya kumaliza chakula, nitahitajika kufanya marekebisho. Kama si kwa ajili nyingine, ila kiwepesi kwa ajili ya uungwana ukiwa unanifanya nifanye hivyo. Zaidi, nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa juu ya kiwango cha uadui nilichomfanyia kwa swali lake lisilo na madhara. Kilichokuwa kinaendelea upande wangu ni kuwa nimejibu kwa hasira sana lile swali lepesi na la wazi lisilo na mitego? Kwa nini lile swali moja, swali lepesi limepelekea aina ile ya tabia mbaya upande wangu?

Baadaye, Imani alipokuja na cheki yangu, nilijaribu kumuomba msamaha kwa kusema: “nasikitika kidogo nilipagawa na kukujibu vibaya swali lako pale mwanzo. Kama ungeniuliza iwapo ninaamini kuwa kuna Mungu Mmoja tu, jibu langu lingekuwa ndiyo. Kama ungeniuliza iwapo ninaamini kuwa Muhammad alikuwa ni mmoja wa Mitume ya Mungu, jibu langu lingekuwa ndiyo.” Naye kwa uzuri kabisa na uvumilivu kabisa alisema: “Sawa; jambo hilo linachukua muda mrefu kidogo kwa watu wengine.”

Huenda msomaji wa habari hii atakuwa mwadilifu vya kutosha kunukuu mchezo wa kisaikolojia nilioucheza na nafsi yangu bila ya kujichekelesha chini chini kwa sana katika mazoezi yangu ya kiakili na kitabia. Mimi naelewa vizuri kuwa kwa njia yangu mwenyewe, ya kutumia maneno yangu mwenyewe, nimeshatamka shahada, ushuhuda wa imani wa Kiislamu, yaani “Ninashuhudia kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah, na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah.” Hata hivyo, baada ya kusema hivyo, na kutambua kile nilichokisema, bado niliendelea kung`ang`ania mambo yangu ya zamani na niliyoyazowea ya jina la utambulisho wa dini yangu, baada ya yote, sikusema kuwa nilikuwa Mwislamu. Kwa wepesi kabisa nilikuwa Mkristo, ijapokuwa ni Mkristo wa aina yake ambaye alikuwa anataka kusema kuwa kuna Mungu Mmoja tu, na si utatu, na aliyekuwa anataka kusema kuwa Muhammad alikuwa ni mmoja wa Mitume iliyopewa ufunuo na Mungu huyo huyo Mmoja. Kama Mwislamu angetaka kunikubali kuwa mimi nimekuwa Mwislamu hilo lingekuwa ni juu yake na ni jina lake la kunitambulisha mimi kidini. Hata hivyo, si kuwa mimi. Nilifikiria kuwa nimeshapata njia ya kunitoa katika tatizo la utambulisho wa kidini. Nilikuwa Mkristo niliyefafanua kwa uangalifu kuwa ninaafiki na nilikuwa ninataka kushuhudia shahada ya imani ya Kiislamu. Baada ya kutengeneza ufafanuzi wa mateso yangu, na baada ya kuianisha lugha ya Kingereza karibu na kila nchi ya maisha yake, wenginewe wanaweza kunibandika jina lolote watakalo. Na jina hilo ni lao wao, na si langu.

Sasa ilikuwa ni mwezi machi 1993, mimi na mke wangu tulikuwa tunafurahia likizo ya wiki tano katika mashariki ya kati. Pia ulikuwa ni mwezi wa Ramadhani wa Kiislamu, wakati ambapo Waislamu wanafunga kuanzia alfajiri hadi kuzama kwa jua. Kwa kuwa mara nyingi tulikuwa tukikaa au kusindikizwa na wanafamilia wa marafiki zetu wa Kiislamu nyumbani Marekani, mimi na mke wangu tuliamua tufunge si kwa lengo lingine zaidi ya adabu ya kikawaida. Katika kipindi hiki, vilevile nilianza kutekeleza swala tano za Kiislamu za kila siku na marafiki zangu wa mashariki ya kati niliowapata hivi karibuni, baada ya yote, kulikuwa hakuna kitu katika swala hizo ambacho nilikipinga.

Nilikuwa ni Mkristo au hivyo ndivyo nilivyosema. Ingawaje baada ya yote, nimezaliwa katika familia ya Kikristo, nimelelewa Kikristo, nimeshahudhuria kanisani na shule za Jumapili kila Jumapili nikiwa mtoto, nimehitimu masomo kutoka katika seminari yenye kuheshimika sana, na nilikuwa mchungaji msimikwa katika madhehebu makubwa ya Kiprotestanti. Hata hivyo, pia nilikuwa ni Mkristo: nisiyeamini utatu au uungu wa Yesu, amani iwe juu yake, nilikuwa ni mtu anayefahamu vizuri jinsi ilivyoharibiwa Biblia; na ni mtu niliyetamka shahada ya Kiislamu kwa maneno ya upambanuzi wangu mwenyewe yenye uangalifu mkubwa; niliyefunga Mwezi wa Ramadhani; niliyeswali swala za Kiislamu mara tano kwa siku; na ambaye alishinikizwa sana na mifano ya mienendo niliyoishuhudia katika jamii za Kiislamu, sehemu zote Marekani na Mashariki ya kati. (Muda na nafasi haviniruhusu kutoa maelezo mapana juu ya mifano ya utu na mfumo wa maadili niliyoyakabiliana nao mashariki ya kati.) kama ningeulizwa kama nilikuwa Mwislamu ilinichukua dakika tano kutoa maneno binafsi marefu na kuliacha swali halijajibiwa. Nilikuwa ninacheza mchezo wa maneno wa kiakili, na nilifanikiwa kwa jamaa hao vizuri kabisa.

Na ilikuwa ni mwishoni mwa safari yetu ya Mashariki ya kati. Pale rafiki mmoja mzee aliyekuwa hajui Kingereza, na nikiwa natembea katika njia iliyopindapinda, njia ndogo, katika moja ya maeneo yaisioendelea kiuchumi katika mji mkongwe wa ‘Amani, Jordan.’ Tulipokuwa tunatembea, kikongwe kimoja kilitusogelea kutokea upande unaokabiliana nasi, na kusema, “Salam Alaykum”, yaani “Amani iwe juu yenu”, na akatupa mikono. Tulikuwa watu watatu tu sehemu hiyo. Sijui Kiarabu, pia rafiki yangu naye hajui, wala yule mgeni haongei Kingereza. Yule mgeni, akanitazama, na akaniniuliza, Mwislamu?

Katika kipindi hiki barabara, nilikuwa nimenaswa kikamilifu. Kulikuwa hakuna mchezo wa maneno ya kiakili utakaochezwa, kwa kuwa nilikuwa ninaweza kuwasiliana kwa Kingereza tu, na wao walikuwa wanaweza kuwasiliana kwa Kiarabu tu. Kulikuwa hakuna mkalimani wa kunidhamini na kunitoa katika hali hiyo, na kuniruhusu nijifiche nyuma ya mazungumzo yangu ya Kingereza yaliyoandaliwa kwa uangalifu mkubwa. Sikuweza kujidai kuwa eti sijaelewa swali, kwa kuwa lilikuwa wazi kabisa. Uchaguzi wangu ulikuwa ni wa ghafla, usiotabirika, na usioelezeka na umepunguzwa na kubakia mambo mawili tu: nisema “Naam” yaani “Ndiyo” au niseme “La” yaani “Hapana”. Chaguo ni langu, na nilikuwa sina chaguo jengine. Kwa sasa nililoazimika kuchagua; ilikuwa ni lepesi kabisa. Allah atukuzwe, Nilijibu “Naam”.

Kwa kusema neno hilo moja, michezo ya maneno ya kiakili yote ilikuwa nyuma yangu. Ikiwa michezo ya maneno ya kiakili ipo nyuma yangu, mchezo wa kisaikolojia wa kuzingatia utambulisho wangu wa kidini nao ulikuwa nyuma yangu. Sikuwa mmoja wa Wakristo wa ajabu nisiye wa kawaida. Nilikuwa Mwislamu. Allah atukuzwe, mke wangu mwenye miaka therathini na tatu akawa Mwislamu katika muda huo.

Na si miezi mingi baada ya kurejea Marekani kutokea mashariki ya kati, jirani mmoja alitualika twende nyumbani kwake, na kusema kuwa anataka kuongea nasi juu ya kubadili kwetu dini na kuwa Waislamu. Alikuwa ni mchungaji mstaafu wa Kimethodisti, ambaye nilikuwa na mijadala naye mingi hapo kabla. Ingawa mara kwa mara tulikuwa tukizungumza kijuu juu kuhusiana na mambo kama uundwaji wa kibandia wa Biblia kutokana na vyanzo mbali mbali vya mwanzo vilivyotengana, kamwe hatukuwa na maongezi ya kina juu ya dini. Nilichojua ni kuwa amepata elimu madhubuti ya seminari, na alikuwa anaimba katika kwaya ya kanisa la mtaani kila Jumapili.

Mwitikio wangu wa awali ulikuwa ni “Oh, oh, hilo linakuja”. Hata hivyo, ni wajibu wa Mwislamu awe jirani mwema, na ni wajibu wa Mwislamu kutaka kujadili Uislamu na watu wengine. Kwa hiyo, nilikubali ule mwaliko wa jioni ifuatayo na nilitumia muda mwingi niliokuwa ni macho wa saa 24 zilizofuatia katika kutafakari nanma nzuri ya kumwendea muungwana huyu katika mada ya maombi yake. Muda tuliokubaliana ukafika, na tukaendesha gari yetu hadi tukafika kwa jirani yetu. Baada ya muda mchache wa maongezi madogo, yeye, mwishowe, aliuliza kwa nini nimeamua kuwa Mwislamu. Nilikuwa ninalingojea swali hilo, na nilikuwa nimeshaandaa vizuri jibu langu. “Kama ujuavyo ukiwa na elimu ya seminari, kuna mambo mengi yasio ya kidini ambayo yametayarishwa na kuunda maamuzi ya Baraza la Nicaea.” Naye kwa haraka haraka akanikatiza kwa sentensi nyepesi: “Wewe hatimaye hukupendezwa na imani ya kuabudu miungu mingi, au siyo?” alijibu kikamilifu kwa nini nilikuwa Mwislamu, naye hakupinga maamuzi yangu! Yeye mwenyewe, kwa umri wake na nafasi yake maishani, alichagua awe “Mkristo wa aina yake”. Allah anamtaka, na hadi kufikia sasa ameshamaliza safari yake kutoka msalabani hadi mwezini.

Kuna muhanga unaotakiwa kutolewa kwa kuwa Mwislamu nchini Marekani. Katika jambo hilo, kuna muhanga unaotakiwa kutolewa kwa kuwa Mwislamu sehemu yeyote ile. Hata hivyo, inawezekana kuwa ni mikali sana Marekani na hasa hasa miongoni mwa waliobadili dini katika Wamarekani. Baadhi ya mihanga hiyo ni yenye kutabirika ikiwemo kubadili mavazi na kujizuia na pombe, nguruwe, na kuvutiwa na pesa za mtu mwingine. Baadhi ya mihanga hiyo haitabiriki kwa mfano, familia moja ya Kikristo, ambayo ilikuwa ni mrafiki zetu wa karibu, ilitufahamisha kuwa hawatoshirikiana nasi tena, kwa kuwa wao hawashirikiani na mtu yeyote “ambaye hamfanyi Yesu Kristo kuwa ndiye mwokozi wake.” Kwa kuongezea, baadhi ya wafanyakazi wenzangu wachache wamebadili tabia zao za kufungamana nami. Ima jambo hilo lilikuwa la upatanifu au la pato langu la kazi, nalo lilipungua na kulikuwa na takriban 30% inashuka katika pato langu kama matokeo ya hayo. Baadhi ya mihanga hiyo isiyotabirika ilikuwa ni mikali mno kuikubali, ingawa mihanga ilikuwa ni thamani ndogo sana kuilipa kwa kile kilichopatikana kama malipo mbadala.

Kwa tafakuri zote hizo kuukubali Uislamu na kujisalimisha kwa Allah – Mtukufu na Mpaji, kutakuwa na kujitoa muhanga tu katika njia yake. Mingi ya mihanga hiyo kiwepesi ni yenye kutabirika, huku mingine huenda ikawa ni ya kushangaza na isiyotabirika. Hakuna kukataa kuwepo kwa mihanga hiyo. Uchambuzi wa mwisho kabisa, mihanga hiyo si muhimu sana kuliko fikra zako za sasa. Allah anakutaka, upate mihanga hiyo ambayo ni sarafu rahisi sana kuilipa ili kupata heri nyingi” utakazozinunua.

  

 4 - SISTA KHADIJA “SUE” WATSON ALIYEKUWA MCHUNGAJI, MMISHIONARI, NA PROFESA ANA STASHAHADA YA UZAMILI YA MASWALA YA THEOLOJIA (NI MMAREKANI MWENYE ASILI YA KIFILIPINO)

“Nini kimekutokea?” Kila siku hicho ndicho kitendo rejeshi cha kwanza, ambacho nilikabiliana nacho. Wakati wanafunzi wenzangu wa zamani, marafiki na wachungaji wenzangu waliponiona baada ya kuingia Uislamu. Nadhani sikuweza kuwalaumu kwa kuwa mimi mwenyewe nilikuwa sipendi kabisa mtu abadili dini. Zamani, nilikuwa Profesa, mchungaji, mwasisi wa kanisa na mmishionari. Kama kuna mtu yeyote aliyekuwa na msimamo mkali kabisa, basi nilikuwa ni mimi.

Baada ya kuhitimu stashahada ya uzamili ya theolojia kutoka katika seminari ya watu wenye vipaji na uwezo maalumu miezi mitano hapo kabla. Ilikuwa ni baada ya wakati huo nilipokutana na bibi mmoja ambaye aliwahi kufanya kazi nchini Saudi Arabia na ameshasilimu. Bila ya shaka nilimuuliza juu ya namna wanavyotendewa wanawake katika Uislamu. Nilishutushwa na jibu lake, kwani halikuwa ni lile niliolitarajia kwa hiyo, niliendelea kuuliza maswali mengine yanayohusiana na Allah na Muhammad amani iwe juu yake (S.A.W)[5]. Naye akanifahamisha kuwa atanipeleka katika kituo cha Kiislamu sehemu ambayo wataweza kujibu maswali yangu.

Baada ya kusali- yaani kumuomba Yesu anikinge dhidi ya Shetani na pepo wabaya, ikionyesha kuwa kile tulichofundishwa kuhusu Uislamu kuwa ni dini ya mapepo na mashetani. Kwa kuwa nimeshafundishwa uinjilisti nilikuwa nimeshtushwa kabisa kabisa na ujaji wa Waislamu, kwani ulikuwa ni wa moja kwa moja na usio na mizengwe. Hakuna vitisho, hakuna bughudha, hakuna kutawaliwa kisaikolojia, hakuna kuvutwa bila ya kujihisi! Hakuna lolote katika hayo, “Acha tukupatie mafunzo ya Quran nyumbani mwako”, iwe ni kama mwenzi wa mafunzo ya Biblia. Sikuweza kuamini jambo hilo! Walinipa baadhi ya vitabu na wakaniambia kama nitakuwa na maswali wao wapo ofisini, tayari kuyajibu maswali hayo. Usiku huo nilisoma vitabu vyote walivyonipatia. Na hiyo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kusoma kitabu juu ya Uislamu kilichoandikwa na Mwislamu, tumeshajifunza na kusoma vitabu juu ya Uislamu vilivyoandikwa na Wakristo tu! Siku iliyofuata nilitumia masaa matatu pale ofisini kwao nikiuliza maswali. Tukio hilo liliendelea kila siku kwa wiki moja, kwa muda huo tayari nilikuwa nimeshasoma vitabu 12 na kujua kwa nini Waislamu ni watu wagumu zaidi duniani kubadili dini na kuwa Wakristo. Kwa nini? Kwa sababu hakuna kitu cha kuwapa!! (Katika Uislamu) kuna kufungamana na Allah, kusamehewa dhambi, uwokovu na kuahidiwa maisha ya milele.

Kikawaida, swali langu la kwanza lilitilia umuhimu suala la Uungu wa Allah. Ni nani huyu Allah ambaye Waislamu wanamwabudu? Sisi kama Wakristo tumeshafundishwa kuwa huyo ni Mungu mwingine, Mungu wa uongo. Wakati, kwa hakika yeye ndiye Mjuzi, Mwenye nguvu, na Aliye hai. Mmoja asiye na mshirika wala aliye sawa naye. Ni jambo la kuvutia kujua kuwa kulikuwa na maaskofu katika kipindi cha miaka mia tatu ya mwanzoni ya kanisa ambao walikuwa wanafundisha kama wanavyofundisha Waislamu kuwa Yesu (A.S)[6] alikuwa ni Mtume na si Mwana wa Mungu!! Na ilikuwa ni baada ya mageuzi ya utawala ya mfalme Constantine kuwa yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kutangaza na kujulisha imani ya utatu. Yeye alikuwa ni mtu aliyebadili dini na kuwa Mkristo ambaye hajui lolote la kidini na aliitambulisha itikadi ya kipagani ambayo historia yake inarejea zama za Mababyloni. Kwa sababu nafasi hainiruhusu kuingia katika maelezo kwa upana juu ya somo hilo insha-Allah, nitazungumza hayo mara nyingine. Kitu pekee ambacho ni lazima nikizungumze ni neno utatu kuwa halimo katika Biblia, katika tafsiri nyingi za Biblia wala halipatikani katika Biblia ya Kigiriki au ya Kiyahudi!

Swali langu muhimu jengine lilitilia umuhimu juu ya Muhammad (S.A.W). Ni nani huyu Muhammad? Nimegundua kuwa Waislamu hawamwabudu kama vile Wakristo wanavyomwabudu Yesu. Yeye si mpatanishi na kwa hakika ni haramu kumwabudu. Tunamuombea abarikiwe mwishoni mwa sala zetu lakini vilevile Tunamuombea Abrahamu naye abarikiwe. Yeye ni Mtume na ni mjumbe, Mtume wa mwisho. Kwa hakika, hadi sasa, ni miaka elfu moja mia nne na kumi na nane imeshapita hakuna Mtume yeyote baada yake. Ujumbe wake ni kwa watu wote ikiwa ni kinyume na ujumbe wa Yesu au Musa (rehema ziwe juu yao) ambao walitumwa kwa Wayahudi. “Sikia ee Israeli” lakini ujumbe wenyewe ni ule ule ujumbe wa Allah. “Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;” (Marko 12:29)

Kwa kuwa sala ilikuwa ni sehemu muhimu sana ya maisha yangu ya Kikristo nilikuwa navutiwa na nina udadisi wa kutaka kujua Waislamu walikuwa wanakiswali nini? Tukiwa kama Wakristo tulikuwa tunapuuzia mtazamo huo wa imani ya Kiislamu kama vile katika mitazamo mengine. Tulifikiria na tulifundishwa kuwa, Waislamu walikuwa wanainamia Kaaba (iliyopo Maka), na hiyo Kaaba ndiyo ilikuwa Mungu wao na ndiyo kiini cha huyo Mungu wa uongo. Kwa mara nyingine, nililishtushwa kujua kuwa namna ya sala imelezwa na Mungu Mwenyewe. Dua za sala, na yale ya kumtukuza na kumsifu. Mwelekeo wa kuielekea sala (udhu au kuoga) kwa usafi upo chini ya maelezo ya Allah. Yeye ni Mungu Mtakatifu na haifai kwetu sisi kumwendea kwa hali ya kiholela holela lakini jambo la kiakili pekee ni kuwa Yeye mwenyewe atwambie tumwendeeje.

Mwishoni mwa wiki hiyo baada ya kutumia miaka minane ya masomo ya kitauhidi[7] ya kawaida nilijuwa kiutambuzi kabisa (head knowledje) kuwa Uislamu ulikuwa ni ukweli. Lakini sikuuingia Uislamu kwa wakati huo kwa kuwa sikuuamini moyoni mwangu, niliendelea kusali, kusoma Biblia, kuhudhuria mihadhara katika kituo cha Uislamu. Nilikuwa ni mwenye ari na bidii ya kuuliza na kutafuta mwongozo wa Mungu. Si rahisi kubadili dini yako. Sikutaka kupoteza uwokovu wangu kama kulikuwa na uwokovu wa kuupoteza. Niliendelea kushtushwa na kushangazwa kwa kile nilichokuwa najifunza kwa sababu kilikuwa si kile nilichofundishwa kuwa Uislamu unakiamini. Katika kiwango changu cha stashahada ya uzamili, profesa niliyekuwa naye alikuwa ni mwenye kuheshimika kama ni mwenye mamalaka ya juu ya Uislamu, mafundisho yake na Ukristo wake kiujumla umejaa upotoshaji. Yeye na Wakristo wengi kama yeye ni waaminifu lakini wao ni waaminifu wa kitu cha makosa.

Miezi miwili baadaye baada ya kuswali tena ili kutafuta maelekezo ya Mungu, nilihisi kuna kitu kinanidondokea na kuniingia! Nilikaa kitako, na hiyo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kutumia jina Allah, na nilisema “Allah, ninakuamini wewe kuwa ni Mmoja na ndiye Mungu wa pekee wa kweli.” Kulikuwa na amani iliyonishukia na tangu siku hiyo ni miaka mine imepita hadi kufikia sasa Kamwe sijajuta kuingia kwangu katika Uislamu. Uamuzi huu haukuja bila ya majaribio. Nilifukuzwa kazi kwani nilikuwa nafundisha katika shule mbili za Biblia kwa wakati huo, nilitenganishwa na wanafunzi wenzangu wa zamani, maprofesa na wachungaji, nilikanwa na familia ya mume wangu, nilifahamika vibaya na watoto wangu wakubwa, na nilikuwa napelelezwa na serikali yangu mwenyewe. Bila ya kuwa na imani ambayo inamuwezesha mtu kusimama kidete dhidi ya nguvu za shetani nisingeweza kuhimili mambo yote hayo. Mimi ninamshukuru sana Allah kwa kuwa mimi ni Mwislamu na naomba niishi na kufa nikiwa ni Mwislamu.

“Sema: “hakika Sala yangu, na ibada zangu (zote nyingine) na uzima wangu, na kufa kwangu; (zote) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Muumba wa walimwengu wote. (Likinisibu jambo limenisibu kwa kutaka Mwenyezi Mungu si kwa kutaka viumbe vyake. Na yote ninayoyafanya nayafanya kwa ajili Yake). Hana mshirika. Na hayo ndiyo niliyoamrishwa, na mimi ni wa kwanza wa waliojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu).” Quran[8] 6:162-163

Sista Khadija Watson anafanyakazi ya ualimu wa wanawake katika moja ya vituo vya Da`wah (kuwaita watu waingie Uislamu) kilichopo Jeddah, Falme ya Kiarabu ya Saudia - Arabia.

 5 IBRAHIM KHALIL AHMED (IBRAHIM KHALIL PHILOBUS) PADRI WA COPTIC NA NI MMISHIONARI (MISRI).

Al-haji Ibrahimu Ahmad, zamani akiitwa Ibrahim Khalil Philobus, alikuwa ni padri wa Coptic mwenye asili ya Kimisri aliyejifunza mambo ya itikadi na kupata digrii ya juu katika chuo kikuu cha Princeton. Alijifunza Uislamu ili apate mianya ya kuushambulia; kinyume chake akaingia Uislamu akiwa pamoja na watoto wake wanne, mmoja wao kwa sasa ni profesa mwenye kung’ara katika chuo kikuu cha Sorbonne, Paris Ufaransa. Kwa njia ya kuvutia, anatumilia mitindo yake mwenyewe kwa kusema; “nimezaliwa Alexandria 13/1/1919 na niliingizwa shule ya misheni ya Kimarekani hadi nilipopata cheti cha elimu ya sekondari hapo hapo. Mnamo mwaka 1942 nikapata diploma katika chuo kikuu cha Asiyut na kisha nikajikita katika masomo ya dini kama utangulizi wa kujiunga na kitengo cha itikadi. Ilikuwa si kazi nyepesi kujiunga na kitengo hicho, kwani hakukuwa na mtu atakaye kujiunga na akakubaliwa ispokuwa awe amepata kupendekezwa kwa pendekezo maalumu kutoka umoja wa kanisani na vilevile, baada ya kupasi idadi ya mitihani migumu. Nilipata pendekezo kutoka katika kanisa la Al-Attareen la Alexandria na pendekezo lingine kutoka mkusanyo wa kanisa wa Misri ya chini (maeneo ya kaskazini) baada ya kufaulu mitihani mingi ili kujua uwezo wangu wa kuja kuwa mtu wa dini kisha nikapata pendekezo la tatu kutoka mkusanyiko wa kanisa la Snodus ambalo linajumuisha makasisi wa Sudani na Misri.

Kanisa la Snodus liliidhinisha niingie kitengo cha itikadi mwaka 1944 nikiwa ni mwanafunzi wa bweni. Huko nilijifunza mikononi mwa walimu wa Kimarekani na Kimisri hadi nilipohitimu mwaka 1948.

Nilipendekezwa, aliendelea, niajiriwe Jerusalemu kama kusingekuwa na vita vilivyolipuka nchini Palestina mwaka huo huo, kwa hiyo. Nilipelekwa Esna Misri ya juu (maeneo ya kusini). Mwaka huo huo nilijiandikisha kwa ajili ya kusomea hoja katika chuo kikuu cha Marekani kilichopo Cairo. Jambo hilo lilikuwa linahusiana na kazi za Kimishionari kwa Waislamu. Ujuzi na uzoefu wangu juu ya Uislamu ulianzia katika kitengo cha itikadi nilpojifunza Uislamu na mifumo yote ambayo kwayo tungeweza kuyumbisha imani ya Waislamu na kuibua upotoshaji wa ufahamu wao wa dini yao wenyewe.

Mwaka 1952 nilipata stashahada yangu ya M.A. katika chuo kikuu cha Priceton USA na niliajiriwa kama mwalimu katika kitengo cha itikadi huko Asiyuti. Nilikuwa nafundisha Uislamu katika kitengo hicho hicho vilevile hatia ya kueneza upotoshaji Uislamu kutoka kwa maadui zake na wamishionari waliodhidi yake. Katika kipindi hicho niliamua kuongeza masomo yangu juu ya Uislamu, kwa hiyo, sikusoma vitabu vya wamishionari peke yake. Nilikuwa najiamini sana kiasi ambacho nikajidhatiti kusoma mtazamo wa upande mwingine. Kwa hiyo, nilianza kusoma vitabu vilivyoandikwa na waandishi wa Kiislamu. Vilevile niliamua kusoma Quran na kuifahamu maana yake. Hili lilitokana na kuvutiwa na mapenzi yangu juu ya elimu na kusukumwa na shauku ya kuongeza ushahidi zaidi dhidi ya Uislamu. Matokeo yakawa, hata hivyo, ni kinyume kabisa. Nafsi yangu ilianza kuyumba na nilianza kuhisi migongano mikali ya ndani kwa ndani katika nafsi yangu na niligundua Uongo wa kila kitu nilichojifunza na kukihubiri kwa watu. Lakini sikuweza kujikabili mimi mwenyewe kishujaa na badala yake nilijaribu kuyashinda mambo hayo ya migogoro ya ndani kwa ndani na niliendelea na kazi yangu.

Mnamo mwaka 1954, aliongeza bwana Khalil, nilipelekwa Aswan nikiwa ni katibu mkuu wa misheni ya Ujerumani na Uswizi. Kazi hiyo ilikuwa ni nafasi yangu ya dhahri lakini kazi yangu hasa ilikuwa ni kuhubiri dhidi ya Uislamu katika Misri ya juu na hasa hasa kwa Waislamu. Mkutano wa wamishionari ulifanyika muda huo huko Cataract Hotel mjini Aswani na nilipewa uwanja wa kuongea. Siku hiyo niliongea kupita kiasi, nikirudia rudia upotoshaji wote dhidi ya Uislamu; na mwisho wa maneno yangu, ule mgogoro wa ndani kwa ndani ulinijia tena na nilianza kuipitia upya nafasi yangu.

Akiendelea na mazungumzo yake juu ya kile akisemacho migogoro, bwana Khalil amesema: “Nilianza kujiuliza kwa nini nilisema na kutenda mambo yote hayo ambayo nayajua kwa uhakika kabisa kuwa mimi ni mwongo, na kuwa huo si ukweli? Nikachukua likizo kabla ya kuisha kwa mkutano na kutoka nje hadi nyumbani kwangu. Nilikuwa ninayumba kikamilifu. Nilipokuwa natembea kupitia bustani ya umma ya Firiyal, nilisikia aya ya Quran redioni. Ilikuwa inasema: “Sema: imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikia (Qurani) likasema: ‘Hakika tumesikia Qurani ya ajabu. ‘Inaongoza katika uongofu; kwa hivyo tumeiamini, hatutamshiriki yeyote tena na Mola wetu.” (Qurani 72:1-2)

“Nasi tulipousikia uwongofu tuliuamini; basi anayemwamini Mola wake hataogopa kupunjwa wala kutwikwa (kubebeshwa) dhambi (za mtu mwengine).” (Qurani 72:13)

Nilihisi faraja ya kina usiku huo na niliporudi nyumbani niliupitisha usiku wote nikiwa peke yangu katika maktaba yangu nikisoma Qurani. Mke wangu alitaka nimjulishe lengo la kukesha kwangu usiku kucha na nilimweleza aniache peke yangu. Nilisimama kusoma kwa muda mrefu nikifikiria na kutafakari juu ya aya; “Lau kama Tungaliiteremsha hii Quran juu ya mlima, ungaliuona ukinyenyekea (na) kupasuka kwa sababu ya hofu ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mifano Tunawapigia (Tunawaeleza) watu ili wafikiri.” (Qurani 59:21) na “Hakika utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu (wengine) kwa Waislamu ni Mayahudi na wale mushirikina (wasiokuwa na Kitabu), na utawaona walio karibu kwa urafiki na Waislamu ni wale wanaosema: “Sisi ni Wakristo.” (Hayo) ni kwa sababu wako miongoni mwao wanavyuoni na wamchao Mungu, na kwa sababu wao (Wakristo) hawatakabari; (wakijua haki huifuata). Na wanaposikia yaliyoteremshwa kwa Mtume (na yakawatulilikia kuwa ni kweli), utaona macho yao yanamiminika machozi kwa sababu ya haki waliyoitambua; wanasema: “Mola wetu! Tumeamini, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (ukweli huu).” (Na wakilaumiwa kwa kusilimu kwao husema): “Na kwa nini tusimwamini Mwenyezi Mungu na haki iliyotufikia, na hali tunatumai Mola wetu atuingize (Peponi) pamoja na watu wema?” (Qurani 5:82-84).

Bwana Khalil kisha alinukuu nukuu ya tatu kutoka katika Quran Tukufu isemayo; “Ambao wanamfuata Mtume, Nabii aliye Ummy (asiyejua kusoma wala kuandika, na juu ya hivi atafundisha mafundisho hayo ya ajabu ya Uislamu), ambaye wanamuona ameandikwa kwao katika Taurati na Injili ambaye anawaamrisha mema na anawakataza yaliyo mabaya, na kuwahalalishia vizuri na kuwaharamishia vibaya, na kuwaondolea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao (yaani sharia ngumu za zamani na mila za kikafiri). Basi wale waliomwamini yeye na kumuhishimu na kumsaidia na kuifuata Nuru iliyoteremshwa pamoja naye (yaani Qurani) hao ndiyo wenye kufaulu. Sema (Ewe Nabii Muhammad): “Enyi watu; Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote; (Mungu) ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi, hapana aabudiwaye (kwa haki) ila Yeye; Yeye ndiye Ahuishaye na ndiye Afishaye. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, aliye Nabii Ummy (asiyejua kusoma na wala kuandika) ambaye humuamini Mwenyezi Mungu na maneno Yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka.” (Qurani 7:157-158).

Kwa sasa yaani usiku ule ule, Bwana Khalil kama mchezo wa kuigiza alihitimisha: “Nilichukua uamuzi wangu wa mwisho. Wakati wa asubuhi nilizungumza na mke wangu ambaye nilizaa naye watoto wa kiume watatu na wa kike mmoja. Lakini haukupita muda mrefu hadi akadadisi kuwa mimi naelekea kuingia Uislamu naye akalia na kuomba msaada kwa mkuu wa misheni. Jina lake lilikuwa ni Monsieur Shavits kutoka Uswizi. Bwana huyo alikuwa ni mtu mjanja sana. Aliponiuliza kuhusu mtazamo wangu wa kweli, nilimwambia kinaganaga kile nilichokuwa nakitaka na kisha akasema: Hebu jifanye kuwa upo nje ya kazi hadi tutakapojua nini kimekutokea. Kisha nilisema: hii ndiyo barua yangu ya kuacha kazi. Alijaribu kunikinaisha niahirishe jambo hilo, lakini mimi niling`ang`ania. Kwa hiyo, yeye akatengeneza uvumi kwa watu kuwa nimekuwa chizi. Kwa hiyo, niliteseka vikali kwa mtihani huo mkali na ukandamizwaji hadi nilipoondoka na kuuacha mji wa Aswan kwa wema na kurudi Cairo.”

Alipoulizwa juu ya hali ya kubadili kwake dini alijibu: “Mjini Cairo nilitambulishwa kwa profesa mmoja anaheshimika sana ambaye alinisaidia kuyashinda majaribu yangu yaliyokuwa makali mno na alifanya hivyo bila ya kujua chochote juu ya mkasa wangu. Alinitendea kama Mwislamu kwani nilijitambulisha kwake hivyo ingawa hadi wakati huo nilikuwa sijaingia Uislamu kirasmi. Huyo bwana alikuwa ni: Dr. Muhammad Abdul Moneim Al Jamal ambaye ni mtunza hazina mkuu. Naye alikuwa anajishughulisha na masomo ya Kiislamu na alitaka kutafsiri Quran Tukufu ikachapishwe Marekani. Aliniomba nimsaidie kwa sababu nilikuwa nafahamu vizuri Kingereza kwa kuwa nilipata stashahada yangu ya M.A katika chuo kikuu cha Marekani. Pia alijua kuwa nilikuwa najiandaa kufanya uchunguzi wa mlinganisho wa Quran, Taurati na Biblia. Tukashirikiana katika uchunguzi huo wa mlinganisho na katika kutafsiri Quran. Wakati: Dr. Jamal alipojuwa kuwa nimeacha kazi huko Aswan na kwa hiyo, sina kazi, alinisaidia kwa kunipatia kazi katika shirika la Standard Stationary mjini Cairo. Kwa hiyo, nilijiunda vizuri baada ya muda mfupi. Sikumwambia mke wangu nia yangu ya kuingia Uislamu kwa hiyo, alifikiria kuwa nimeshasahau mambo yote na sikuwa na lolote ila ni mgogoro wa mpito ambao haupo tena. Lakini, nilijua vizuri kabisa kuwa kusilimu kwangu kirasmi na kuingia Uislamu kunahitaji majaribio ya kutatanisha marefu na kwa hakika ilikuwa ni vita ambavyo nilipendelea kuviahirisha kwa muda hadi pale nitakapoimarika na baada ya kukamilisha uchunguzi wangu wa mlinganisho.”

Kisha Bwana Khalil aliendelea; “Mnamo mwaka 1955 nilikamilisha uchunguzi wangu na mambo yangu ya kiuchumi na kimaisha yakaanza kuwa mazuri. Nikaacha kazi kutoka katika lile shirika na nikaanzisha ofisi ya kufundisha uagizaji wa vifaa vya kuandikia na vyombo vya mashuleni. Ilikuwa ni biashara iliyofanikiwa sana kutokana na biashara hiyo nilichuma pesa nyingi zaidi kuliko vile nilivyohitaji. Kwa hiyo, nikaamua kutangaza rasmi kusilimu kwangu nakuwa Mwislamu rasmi. Mnamo 25/12/1959, nilimtumia telegramu Dr. Thompson, kiongozi wa misheni ya Marekani nchini Misri nikimjulisha kuwa nimeingia Uislamu. Nilipomweleza: Dr. Jamal mkasa wangu wa kweli alishangazwa sana. Nilipotangaza kusilimu kwangu na kuingia Uislamu, matatizo mapya yalianza. Watu saba miongoni mwa jamaa zangu wa zamani katika misheni walijaribu kwa kila hali kunishawishi niondoe tangazo langu, lakini nilikataa. Wakatishia kunitenga na mke wangu na nikawaambia: yupo huru kufanya atakavyo. Wakatishia kuniua. Lakini waliponikuta nipo imara waliniacha peke yangu na wakaniletea rafiki yangu wa zamani ambaye naye pia alikuwa ni mwenzangu katika misheni. Naye akalia sana mbele yangu. Kwa hiyo, nilimsomea mbele yake aya zifuatazo kutoka katika Quran:(Hayo) ni kwa sababu wako miongoni mwao wanavyuoni na wamchao Mungu, na kwa sababu wao (Wakristo) hawatakabari; (wakijua haki huifuata). Na wanaposikia yaliyoteremshwa kwa Mtume (na yakawatulilikia kuwa ni kweli), utaona macho yao yanamiminika machozi kwa sababu ya haki waliyoitambua; wanasema: “Mola wetu! Tumeamini, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (ukweli huu).” (Na wakilaumiwa kwa kusilimu kwao husema): “Na kwa nini tusimwamini Mwenyezi Mungu na haki iliyotufikia, na hali tunatumai Mola wetu atuingize (Peponi) pamoja na watu wema?” (Qurani 5:84).

Nikamwambia, “ulitakiwa ulie kwa unyenyekevu mbele ya Mungu kwa kusikia Quran na kuamini ukweli ambao unaujua lakini unaukataa. Alisimama na kuondoka na kuniacha kwa vile alivyoona kuwa hakuna njia. Kusilimu kwangu kirasmi na kuingia Uislamu kulikuwa Januari 1960.”

Kisha bwana Khalil aliulizwa kuhusiana na mtazamo wa mkewe na watoto wake, naye akasema: “Mke wangu aliniacha kwa muda huo na akachukua vyombo vya nyumbani vyote akaondoka navyo; lakini watoto wangu wote waliungana nami na kuingia Uislamu. Na aliyekuwa na shauku sana miongoni mwao alikuwa ni mtoto wangu mkubwa Isaac ambaye alibadili jina lake na kuwa Osmani, kisha mtoto wangu wa pili Joseph (Yusufu) na mwanangu Samuel ambaye jina lake lilikuwa Jamal na binti yangu Majida ambaye kwa sasa anaitwa Najwa. Osmani kwa sasa ni Dakitari wa falsafa anaefanyakazi ya uhadhiri katika chuo kikuu cha Sorbonne mjini Parisi akifundisha masomo ya utamaduni wa kimashariki na saikolojia. Pia ni mwandishi katika jarida la “Le monde.” Kwa kumtazama mke wangu, aliiacha nyumba kwa miaka sita na akakubali kurudi mnamo mwaka 1966 huku akisisitiza kuwa ataendelea na dini yake. Nilimwambia: sitaki uwe Mwislamu kwa ajili yangu lakini ni baada ya kukinai tu. Naye kwa sasa alihisi kuwa anaamini Uislamu lakini hawezi kutangaza jambo hilo kwa kuiogapa familia yake lakini sisi tulimtendea kama ni mwanamke wa Kiislamu na alikuwa akifunga Ramadhani kwa sababu watoto wangu wanaswali na kufunga. Binti yangu Najwa ni mwanafunzi katika kitengo cha biashara, Joseph ni Dakitari mtaalamu wa madawa na Jamal ni injinia.

Katika kipindi hiki, ambacho ni tangu 1961 hadi muda huu nimeshachapisha idadi kubwa ya vitabu juu ya Uislamu na mifumo ya kimishionari na utaalamu wa mambo ya mashariki dhidi ya jambo hilo. Kwa sasa najiaandaa na uchunguzi wa mlinganisho juu ya wanawake katika dini tatu huku nikitilia umuhimu nafasi ya mwanamke katika Uislamu. Mwaka 1973 nilifanya hija na ninafanya kazi za kuhubiri Uislamu. Ninafanya semina mbali mbali katika vyuo vikuu na jumuia za wahisani. Nimepokea mwaliko kutoka Sudani mwaka 1974 ambako nilifanya semina nyingi. “Muda wangu wote unatumiwa kwa kuuhudumia Uislamu na shukrani ni za Allah kwa sababu kwa juhudi zangu mapadri wengi na watu wengi wamesilimu na kuwa Waislamu.”

Mwisho kabisa Bwana Khalil aliulizwa juu ya vitu vilivyomvutia sana katika Uislamu. Na kujibu: “Imani yangu katika Uislamu imeletwa kupitia kusoma Quran Tukufu na historia ya Mtume Muhammad, amani iwe juu yake. Kwa sasa siamini upotoshaji dhidi ya Uislamu na hasa hasa nimevutiwa na itikadi ya Upweke wa Mwenyezi Mungu, kwani hiyo ndiyo picha muhimu sana ya Uislamu. Mungu ni mmoja tu. Hakuna kitu kinachofanana naye. Imani hii inanifanya niwe mja wa Mungu peke yake na si kwa mwingine. Upweke wa Mungu unamkomboa mtu kutoka katika utumwa kwa mtu yeyote na huo ndiyo uhuru wa kweli.

Pia ninapenda sana sheria ya kusamehe katika Uislamu na mafungamano ya moja kwa moja kati ya Mungu na mja wake.

“Sema, “Enyi waja wangu mliojidhulumu nafsi zenu! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu; bila shaka Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu. “Na rejeeni kwa Mola wenu na mnyenyekee Kwake kabla ya kukujieni adhabu kisha hamtanusuriwa.” (Quran 39:53-54)

Chanzo: Habari za Kiislamu, San Francisco, (A 94141 – 0186)

 6- MARTIN JOHN MWAIPOPO ALIYEKUWA KASISI MKUU WA KILUTHERANI (TANZANIA).

Ilikuwa ni Desemba 23, 1986, siku mbili kabla ya Krismasi, wakati Askofu mkuu Martin John Mwaipopo, alipotangaza kwa makutano yake kuwa anauacha Ukristo na kuingia Uislamu.

Yale makutano yalipooza kwa mshtuko wa kusikia habari hiyo walishtushwa sana kabisa kiasi ambacho msimamizi wake alisimama kutoka kitini kwake, akafunga milango na madirisha na kutangaza kwa wanakanisa kuwa akili ya Askofu imeganda, yaani amechizika. Vipi ashindwe kufikiria na kusema hivyo, wakati katika kipindi cha dakika chache tu zilizopita, mtu huyo huyo alichukua kifaa chake cha muziki na kuimba kwa kucheza cheza sana na kuliimbia kanisa? Ni kidogo mno walichokijua cha ndani ya moyo wa Askofu kama kulikuwa na uamuzi ambao utawapasua akili zao, na burudani ile ilikuwa ni sherehe ya kuagana tu. Lakini hisia za makutano zilifadhaishwa sana, naam! Wakawaita polisi waje wamwondoshe mwendawazimu” Akawekwa kolokoloni hadi mida ya usiku wa saa sita ndipo Sheikh Ahmed Sheikh, mtu aliyemwingiza katika Uislamu alipoenda kumtoa. Tukio hilo lilikuwa ni mwanzo mdogo mdogo wa mshtuko uliojificha dhidi yake. Magazeti yote ya habari za Qalam, Simphiwe Sesanti, yalizungumzia juu ya mtu aliyezaliwa Tanzania na aliyekuwa Askofu mkuu wa Kilutherani Bwana Martin John Mwaipopo, aliyeingia Uislamu amekuja na kujulikana kuwa ni Al-Haji Abu Bakar Mwaipopo.)

Sifa lazima ziende kwa ndugu wa Kizimbabwe, Sufiyan Sabelo, kwa kusababisha huu udadasi wa maandishi, baada ya kusikiliza maneno ya Mwaipopo katika kituo cha Kiislamu cha Wyebank mjini Durban. Sufyan si mpiga debe, lakini usiku huo lazima atakuwa amesikia kitu naye hakusimama kuongelea kuhusu mtu huyo! Ambaye hataathiriwa baada ya kusikia hayo naye ni Askofu mkuu, ambaye hakuwa na stashahada ya BA na Uzamili peke yake, lakini pia alikuwa na stashahada ya udakitari wa falsafa, ya mambo ya kiitikadi, mwishowe amebadilika na kuwa Mwislamu? Na kwa kuwa vigezo vya kigeni ni muhimu sana kwake, basi huyo mtu alipata diploma ya uongozi wa kanisa nchini Uingereza na baadaye digrii, mjini Berlin, Ujerumani! Mtu ambaye, kabla hajakuwa Mwislamu, alikuwa ni katibu wa Baraza la makinisa ulimwenguni kwa nchi za Afrika mashariki – zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, na sehemu za Ethiopia na Somalia. Katika baraza la makanisa, alikuwa anagusana mabega na mwenyekiti wa sasa wa kamishna ya Haki za Binadamu ya Afrika Kusini. Bw. Barney Pityana na mwenyekiti wa tume ya ukweli na maridiano, Askofu Dasmound Tutu.

Hiki ni kisa cha mtu aliyezaliwa miaka 61 iliyopita, mwezi februari tarehe 22 huko Bukoba, eneo linalopakana na Uganda. Miaka miwili, baada ya kuzaliwa kwake, familia yake ilimbatiza, na miaka mitano baadaye, walimtazama kwa jicho la fahari na wakitarajia kuwa atakuwa kijana wa mageuzi. Kwa kumuona anamsaidia mchungaji wa kanisa, kuandaa “mwili na damu” ya Kristo, walimjaza Mwaipopo fahari, na walimjaza Mwaipopo mkubwa, wazo zuri juu ya mustakabali wa mwanawe.

“Nilipokuwa katika shule ya bweni, hapo baadaye, baba yangu aliniandikia”, akieleza kuwa ananitaka niwe padri. Aliandika hivyo, katika kila barua aliyoiandika” Anakumbuka bwana Abuu Bakri. Lakini Mwaipopo alikuwa na mawazo binafsi juu ya maisha, ambayo ni kujiunga na jeshi la polisi. Lakini alipofikia umri wa miaka 25, aliacha mawazo yake na akasalimu amri kwa matakwa ya baba yake. Na hii ni kinyume na huko Ulaya ambako watoto wanaweza kufanya watakavyo baada ya kufikia umri wa miaka 21, lakini Afrika, watoto wamefunzwa kuheshimu matakwa ya wazazi wao kinyume na matakwa yao binafsi.

“Mwanangu kabla sijafumba macho (sijafa), nitafurahi sana kama utakuwa padri.” Hivyo ndivyo baba ya alivyomweleza mwana, na hivyo ndivyo mtoto alivyoenenda, mwendo ambao ulimshuhudia akielekea Uingereza mnamo mwaka 1964, kusomea diploma ya Uongozi wa kanisa na mwaka mmoja baadaye alienda Ujerumani kusomea BA. Alipokuwa anarudi mwaka mmoja baadaye, alisimikwa na kuwa Askofu anayetoa huduma.

Baadaye alienda tena kuchukua Stashahada ya Uzamili. “Muda wote huo, nilikuwa nafanya vitu bila ya kuuliza.” Na ilikuwa pale alipoanza kufanya ‘uzamili wake’ ndipo alipoanza kuuliza vitu. “Nilianza kushangazwa … kuna Ukristo, Uislamu, Uyahudi, Ubudha na kila dini inadai kuwa yeye ndiyo ya kweli. Ukweli ni upi? Nilitaka ukweli”, anasema Mwaipopo. Kwa hiyo, akaanza uchunguzi wake, hadi alipopunguza dini hizo na kubakisha dini kuu “nne.” Akajipatia nakala ya Quran, na kutabiri nini kitatokea?

“Nilipoifungua Quran, Aya za kwanza kabisa nilizozisogelea zilikuwa ni za “surati Ikhlasi” “Sema: Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja (tu). Mwenyezi Mungu (tu) ndiye anayestahiki kukusudiwa (na viumbe Vyake vyote kwa kumwabudu na kumuomba na kumtegemea). Hakuzaa wala Hakuzaliwa. Wala hana anaefanana Naye hata mmoja.” Anakumbuka jambo hilo. Na hiyo ilikuwa pale mbegu za Uislamu, hazijulikani kwake na zilikuwa ni mara ya kwanza kuonekana. Na ilikuwa ni hapo alipogundua kuwa Qurani ndicho Kitabu cha pekee kisichovurugwa na wanadamu tangu kilipoteremshwa. “Na katika kuhitimisha uchunguzi wangu wa uzamili nilisema hivyo. Sikujua kama watanipa stashahada yangu ya uzamili au hawanipi – huo ndiyo uliokuwa ukweli, na nilikuwa nautaka ukweli.”

Alipokuwa katika hali hiyo ya kiakili alimwita profesa wake ampendaye sana: bwana Van Burger. “Nilifunga mlango, na kumwangalia machoni na kumuuliza “katika dini zote duniani ni ipi ya ukweli?” Akajibu ni Uislamu. “Kwa nini wewe si Mwislamu? Niliuliza tena. Akaniambia: “Mosi, nawachukui Waarabu, pili, Je, unaviona vitu vya anasa vyote hivi niliovyonavyo? Je, unadhani itakuwaje kama nitavitupa vitu vyote hivi kwa ajili ya Uislamu?” Nilipofikiri kuhusu majibu yake, pia nilifikiria nafsi yangu mwenyewe.” Anakumbuka Mwaipopo. Kazi yake, gari zake, vyote hivyo katika taswira yake. Hapana, hatoingia Uislamu, na kwa mwaka mmoja madhubuti, aliliweka jambo hilo nje ya akili yake. Lakini baadaye ndoto zilikuwa zikimjia kwa kumsumbua, Aya za Quran ziliendelea kumtokea, watu waliovalia nguo nyeupe waliendelea kumjia. “Hasa hasa siku za Ijumaa; hadi alipofikiria kuwa hawezi kuvumilia tena jambo hilo.

Kwa hiyo, mnamo tarehe 22 Desemba, aliingia Uislamu kirasmi. Ndoto hizo zilizomwongoza - Je, hazikuwa za “kishirikina” kama ilivyo kwa tabia za Kiafrika? “Hapana, siamini kuwa ndoto zote ni mbaya. Kwani kuna zile ambazo zinakuongoza katika mwelekeo sahihi, na kuna nyingine hazifanyi hivyo, na za kwangu, kwa upekee kabisa zimeniongoza katika mwelekeo sahihi, kuufikia Uislamu,” ametueleza.

Kwa hiyo, kanisa lilimnyang`anya nyumba na gari. Mkewe hakuweza kuvumilia hayo, akafungasha virago vyake, akachukua watoto wake na kuondoka, licha ya Mwaipopo kumuhakikishia kuwa halazimishwi awe Mwislamu. Mwaipopo alipoenda kwa wazazi wake nao pia, walikuwa wameshasikia habari zake. “Baba yangu aliniambia niukane Uislamu na mama yangu, yeye alisema: “Hataki kusikia upuuzi wowote kutoka kwangu;” alikumbushia Mwaipopo. Naye alikuwa kivyake vyake! Aliulizwa vipi anajihisi hivi sasa kwa upande wa wazazi wake, anasema kuwa nimeshawasamehe, kwa hakika alipata muda wa kusuluhishwa na baba yake kabla hajaiaga dunia.

“Hao wazazi walikuwa ni wazee wasiojiweza. Walikuwa hawajui hata kuisoma Biblia… Chote walichokijuwa ilikuwa ni kile walichokisikia kikisomwa na mapadri” anaelezea. Baada ya kuomba akae kwa usiku mmoja tu, mchana uliofuatia, alianza safari yake ya kuelekea kule kwenye asili ya wazazi wake, Kyela, karibu na mpaka kati ya Tanzania na Malawi. Wazazi wake walifanya makazi mjini Kilosa, Morogoro. Katika safari yake hiyo, alikwamia Basale, kwa familia moja ambayo ilikuwa inauza pombe zilizosindikwa nyumbani. Na ilikuwa ni hapo ndipo alipokutana na mkewe wa baadaye, ambaye ni mtawa wa Kikatoliki, jina lake ni Sista Gertrude Kibweya, kwa sasa anajulikana kwa jina la Sister Zainabu. Na ilikuwa ni pamoja naye ndipo Mwaipopo aliposafiri hadi Kyela, ambako yule mzee, aliyempa hifadhi kwa usiku uliopita alipomwambia kuwa hiyo ndiyo namna Mwaipopo atavyowapata Waislamu wengine. Lakini kabla ya hivyo, wakati wa asubuhi ya siku hiyo alipopiga adhana, kitu kilichowafanya wanakijiji watoke, huku wakimuuliza mwenyeji wake kwa nini alikuwa anamuhifadhi “mwendawazimu.” Alikuwa ni yule mtawa ndiye aliyeeleza kuwa mimi sikuwa mwendawazimu, ispokuwa ni Mwislamu” anasema Mwaipopo. Na alikuwa ni mtawa huyo huyo aliyemsaidia Mwaipopo hapo baadaye kulipia ada ya matibabu katika hospitali ya Misheni ya Kianglikana, alipokuwa mgonjwa sana, shukrani kwa mazungumzo aliyoyafanya na mtawa huyo.

Kisa chenyewe kinaenda hivi, Mwaipopo alipomuuliza mtawa huyo kwa nini alikuwa anavaa shanga ya Rozali, naye akajibu kuwa ni kwa sababu Yesu Kristo alisulubiwa msalabani. “Lakini, hebu sema, kama mtu amemuua baba yako na bunduki, Je, utatembea huku umebeba bunduki kifuani kwako?” Mmmhhh. Hilo lililmfanya yule mtawa afikirie, akili zake zikapata “changamoto”, na Askofu wa zamani alimuomba amuoe hapo baadaye, jawabu lilikuwa “sawa”. Walioana kwa siri, na wiki nne baadaye, huyo mtawa aliandika barua kwa viongozi wake, akiwajulisha kuwa anaondoka. Wakati yule mzee aliyempa hifadhi Mwaipopo, (mjomba wa mtawa) aliposikia juu ya ndoa hiyo, na Mwaipopo na mkewe walipofika nyumbani kwa mzee huyo, walishauriwa wahame nyumba hiyo, kwa sababu “yule mzee alikuwa anashindilia bunduki yake”, na Baba wa yule mtawa alikasirika sana, “alikuwa mkali kama simba”.

Kutoka katika kasri la Askofu, Mwaipopo alienda kuishi katika nyumba aliyoijenga mwenyewe nyumba ya udongo. Kutoka alipokuwa akijipatia matumizi ya maisha yake kwa kazi ya ukatibu mkuu wa baraza la makanisa Duniani kwa nchi za Afrika mashariki, akaanza kujipatia pato la maisha yake kwa kuuza kuni na kulimia mashamba ya watu wengine. Na wakati alipokuwa hafanyi kazi hizo (anapomaliza) alikuwa anahubiri Uislamu wazi wazi. Hilo lilimpelekea, kwa muda mfupi atiwe kolokoloni kwa kuhubiri kwa kuukashifu Ukristo.

Alipokuwa Hija 1988, ulimpata msiba mkubwa, nyumba yake ililipuliwa kwa bomu, na matokeo yake, vitoto vyake vitatu vilivyokuwa mapacha viliuwawa. “Askofu, ambaye mama yake na mama yangu walikuwa ni watoto wa baba mmoja, alishiriki katika njama hizo” anakumbushia Mwaipopo. Anasema badala ya kumvunja moyo, tukio hilo lilifanya kinyume chake, kwani idadi ya watu walioingia Uislamu, iliongezeka, na idadi hiyo ikijumuisha baba mkwe wake.

Anasema kuwa kila siku anayoachwa huru, basi polisi walienda kumkamata tena. Hebu tabiri ni kitu gani? “Wanawake wakasema: haiwezekani! Watatumia nguvu dhidi ya polisi kuzuia asikamatwe. Pia, walikuwa ni wanawake waliomsaidia kuvuka mpaka bila ya kujulikana. Walimvalisha nguo za kike! Kwa mujibu wa kauli ya Mwaipopo. Na hilo ni moja ya sababu inayomfanya awaheshimu sana wanawake.

“Wanawake lazima wapewe nafasi kubwa, lazima wapewe elimu bora katika Uislamu. Vinginevyo, vipi mwanamke atafahamu kwa nini mwanamume anaoa zaidi ya mke mmoja… Alikuwa ni mke wangu, Zainabu, aliyetoa ushauri wa kuoa mke wa pili, Shela (rafikiye), wakati mke wangu alipolazimika kwenda ng`ambo kusomea Uislamu.” Ni Askofu asemayo hayo. Ndiyo?

Kwa Waislamu, Al-Haji Abuu Bakri Mwaipopo ana ujumbe huu: “Kuna vita dhidi ya Uislamu… Epukeni dunia ya maneno matupu. Sasa hivi, Waislamu tumefanywa tuone aibu kwa kuwa tunahesabiwa ni siasa kali. Waislamu lazima tuache mifarakano. Waislamu lazima tuungane.

Chanzo: hhttp://mandla.co.za/al-qalam/sept97/bishop.htm

 7- RAPHAEL NARBAEZ ALIYEKUWA MCHUNGAJI WA MASHAHIDI WA YEHOVA (USA)

Latino, Raphael mwenye miaka arobaini na mbili ni mchekeshaji mwenye kufanya maskani yake Los Angeles na ni muhadhiri wa chuo kikuu. Alizaliwa Texas, sehemu ambayo ndiyo aliyohudhuria ushahidi wake na miaka minne baadaye aliyaelekea makutano yake mwenyewe akiwa na miaka ishirini, na alipewa nafasi ya uongozi kwa Mashahidi wa Yehova 904,000 laki tisa na elfu nne nchini (USA). Aliiuza Biblia yake kwa Quran baada ya kupata ushujaa wa kutembelea msikiti wa mtaani.

Novemba 1, 1991, aliingia Uislamu, huku akiiletea jamii ya Waislamu ujuzi wa kuunda usharika na kuuzungumzia alioupata miongoni mwa Mashahidi wa Yehova. Yeye huongea na Waislamu wapya kwa haraka haraka, lakini yeye ni mmoja wa wale wanaoweza kuwafanya wanaohamia Uislamu wajichekee.

Alisimulia kisa chake kwa mtindo wa kuigiza, nakumbuka wazi wazi nilikuwa katika mjadala ambao sote tulikuwa tumekaa katika sebule ya wazazi wangu na kulikuwa na baadhi ya Mashahidi wa Yehova wengine. Walikuwa wanaongelea juu ya: “Vita kati ya wema na uovu; muda wa Mwisho! Na Kristo anakuja! Na wajua tena, mvua ya mawe itakuwa na matone makubwa kama gari ndogo! Mungu atatumia vitu aina zote vya kuungamiza mfumo huu mbaya na kuondosha serikali! Na Biblia inayozungumzia dunia itafunguka! Itameza magorofa ya mji mzima”

Naogopa sana kifo! Kwa hiyo, mama yangu alinigeukia: “Tazama kitakachotokea kama hutobatizwa, na hutofanya matakwa ya Mungu? Dunia itatumeza, au moja ya mawe hayo makubwa mno litakupiga juu ya kichwa na litakuangusha, na hautoishi tena. Nami nitalazimika kutengeneza mtoto mwingine.”

Sikutaka kuchukua nafasi ya kugongwa na moja ya mawe hayo ya mvua yaliyo makubwa. Kwa hiyo, nikabatizwa. Bila shaka mashahidi wa Yehova hawaamini kunyunyiza maji. Wao wanakuzamisha kabisa kabisa, wanakuacha ndani ya maji hayo kwa sekunde moja, kisha wanakutoa.

Nilifanya hivyo nikiwa na miaka 13, Septemba 7, 1963 mjini Pasadena, Calfornia, katika birika la Rose Bowl. Ilikuwa ni mkutano wa kimataifa mkubwa sana. Tulikuwa watu 100,000 laki moja. tuliendesha magari kutokea Lubbock, Texas.

Hatimaye nilianza kutoa maneno makubwa – dakika kumi mbele ya mkutano. Na kundi la wahudumu wa sinema walinipendekeza nitoe muhadhara wa saa moja ambao ulifanyika Jumapili walialikwa watu wengi. Wao kikawaida huwa wanayahifadhi mahubiri hayo kwa ajili ya wazee wa makutano.

[Kwa sauti ya mamlaka:] “Kwa hakika ni ndogo, Lakini anaweza kukamata jambo hilo. Yeye ni kijana wa Kikristo mzuri. Hana maovu, na ni mtiifu kwa wazazi wake na anaonekana ana elimu bora na kubwa sana ya Biblia.”

Kwa hiyo, nikiwa na miaka kumi na sita nilianza kutoa muhadhara wa saa moja mbele ya makutano yote. Kwanza kabisa niliandikwa katika kikundi kilichopo Sweetwater, Texas, na Kaosha, hatimaye, mjini Brownfield, Texas, nilipopata makutano yangu ya kwanza. Katika umri wa miaka ishirini, nilikuwa ni kile wakiitacho mchungaji chipukizi (mtangulizi).

Mashahidi wa Yehova wana mpango wa mafunzo wa kisasa sana, wana aina mfumo wa haki. Unalazimika kutenga masaa kumi hadi kumi na mbili kwa mwezi ya kuhubiri nyumba kwa nyumba. Ni kama muuza biashara. IBM haifai chochote kwa vijana hao.

Kwa hiyo, nilipokuwa mchungaji mtangazaji, nilitenga muda wangu mwingi kufanya utumishi wa nyumba kwa nyumba. Nilikuwa nalazimika kufanya hivyo kiasi cha masaa mia moja kwa mwezi, na nililazimika kuwa na masomo saba ya Biblia. Nilianza kuwahubiria makutano mengine. Nilikubaliwa katika shule ya Brooklyn, New York, ni shule ya tabaka bora sana waimilikayo Mashahidi wa Yehova “the Crème de la crème, ni ya kwanza kwa kuwa na asilimia kubwa. Lakini sikuenda.

Vitu vichache ambavyo kwa sasa haviniingii akilini. Kwa mfano, mfumo wa sehemu ya haki. Jambo hilo linaonekana kama vile kila mara nilipotaka kupinda kona nakujikuta katika nafasi nyingine ya majukumu, nililazimika vitu hivyo vya kisekyula ili kuuthibitisha uungu wangu. Hiyo ni kwa kuwa kama utafikia malengo ya sehemu yako ya haki ya mwezi huu, Mungu anakupenda. Na kama hutafikia sehemu yako ya haki katika mwezi unaofuata Mungu hakupendi. Jambo hilo halikuniingia akilini kabisa kabisa. Mwezi mmoja ananipenda na mwezi mwengine hanipendi?

Kitu kingine nilichoanza kukiona ni mtazamo wa njia ya chini. Mashahidi wa Yehova ni watu pekee watakaookolewa katika mpango mpya wa Mungu, hakuna mtu mwingine atakayeokoka, kwa sababu, watu hao wanatekeleza dini ya uongo. Sawa, nilifikiria: mama Tereza wa Kikatoliki. Huyo ni adui yetu wa kutisha. Kwa hiyo, nilisema ngoja kidogo mama Tereza ametoa maisha yake yote akifanya vitu alivyosema Yesu: kuwalea masikini, wagonjwa na mayatima. Lakini hatopata huruma za Mungu kwa sababu ni Mkatoliki?

Tulikuwa tunalikosoa kanisa la Kikatoliki kwa sababu Wakatoliki wana mtu ambaye ni padri, wanamwendea na kuungama dhambi zao kwake. Na tuna msemo “Usiende kwa mtu kuungama dhambi zako! Dhambi zako ni dhidi ya Mungu!” Ndiyo sisi tulienda kwa baraza la wazee. Unaungama dhambi zako kwao, na wao wanakuwekea mkono, na walisema [mzee ni kama oporeta wa simu:] “Jizuie kwa dakika moja hivi … unafikiri nini, bwana? Hapana? … sawa, samahani tumejaribu vya kutosha lakini wewe bado hujatibika vya kutosha. Dhambi zako ni kubwa mno, kwa hiyo, ima upoteze ufuasi wako kanisani au upelekwe majaribuni.”

Ikiwa dhambi ni dhidi ya Mungu, Je, sikupaswa nimwelekee Mungu moja kwa moja na kumuomba msamaha?

Uhenda msumari uliogongelewa jeneza ulikuwa ni ule ule niliouna kuwa wao waliianza kuisoma Biblia kidogo tu. Mashahidi wa Yehova wana vitabu vya kila kitu ambavyo vimetayarishwa na mnara wa wachunguzi wa Biblia na jumuia ya vitabu vya dini watu pekee katika sayari nzima ya dunia wanaoweza kujua namna ya kutafsiri maandiko ya Biblia kisawa sawa ni kundi la wanaume wa tume ya Brooklyn, ambao wanawaambia Mashahidi wa Yehova ulimwengu mzima wavae vipi, waseme nini, watumie vipi maandiko matakatifu, na wakati ujao utakuwaje. Mungu amewaambia wao, kwa hiyo, wao nao wanaweza kutwambia sisi. Niliviheshimu vitabu hivyo. Lakini kama Biblia ndicho kitabu cha elimu na ikiwa Biblia ni mafundisho ya Mungu, vizuri, Je, hatupaswi kupata majibu yetu kutoka katika Biblia? Paulo mwenyewe alisema jitafutie mwenyewe kile cha kweli na maneno ya Mungu yanayokubalika. Usiruhusu watu kuyazuga masikio yako.

Nilianza kusema: “Usihofu sana juu ya kile kinachosemwa na mnara wa wachunguzi – soma Biblia wewe mwenyewe.” Masikio yalianza kusimama na kusikiliza kwa makini.

[Old Southerner`s drawl:] “Nadhani tumejipatia uasi hapa, hoji,. Yup. Nadhani kijana huyu wa zamani ni {one taco short} la kitu fulani.”

Hata baba yangu alisema: “Bora uchunguze, wewe kijana, huo ni usemi wa pepo wabaya huo. Hayo ni majaribio ya pepo wabaya kutaka kuingia na kusababisha mgawanyiko.”

Nilisema: “Baba, hayo si mambo ya pepo wabaya. Watu hawahitaji kusoma sana haya machapisho mengine. Wanaweza kupata majibu yao kwa kusali na ndani ya Biblia.”

Kiroho sikuwa tena, nahisi wepesi. Kwa hiyo mnamo mwaka 1979, nikijua kwamba sikuweza kuendelea, niliacha, sikuridhika na nikiwa nasikia ladha mbaya mdomoni, kwa sababu nimeshayaweka maisha yangu yote, roho yangu, moyo, na akili kanisani. Hilo lilikuwa tatizo. Sikuliweka kwa Mungu. Nimeliweka katika mipango iliyosukwa na watu.

Siwezi kwenda katika dini nyingine. Nikiwa ni Shahidi wa Yehova, nimeshafundishwa, kupitia maandiko, kuonyesha kuwa dini nyingine zote ni za makosa. Yale masanamu ni kitu kibaya. Utatu wa Mungu haupo.

Mimi ni sawa sawa na mtu asiye na dini. Lakini sikuwa mtu asiye na Mungu. Lakini wapi nitakapoweza kupaendea?

Mnamo mwaka 1985 nilamua kwenda Los Angeles na kujiunga na shoo ya Johnny Carson na kufanya utambulisho wangu kuwa ni mwana maigizo mkuu na ni mcheza sinema. Daima nilikuwa nahisi kuwa, kama vile nimezaliwa kwa ajili ya kitu fulani. Sikujua kama kitapatikana, dawa ya kutibu kansa au nitakuwa mcheza sinema. Niliendelea kusali na jambo hilo lilizuiwa kwa muda mchache.

Kwa hiyo, nilienda katika kanisa Katoliki lilokaribu na nyumba yangu, na nilijaribu kufanya jambo hilo. Nakumbuka siku ya Jumatano ya majivu hayo ya msalaba katika paji la uso wangu. Nilikuwa najaribu kitu chochote nilichokiweza. Nilienda kwa miezi miwili au mitatu, na sikuweza kufanya hayo tena, awe mtu. Ilikuwa ni: Simama. Kaa.

Sawa, toa ulimi wako

Ungepata mazoezi mengi. Nadhani nilipoteza uzito kiasi cha paundi tano. Lakini hilo lilikuwa ni juu ya jambo hilo. Kwa hiyo, kwa sasa nimepotea zaidi kuliko nilivyokuwa.

Lakini jambo hilo halikupita akilini mwangu kuwa hakuna Muumba. Nina namba ya simu yako lakini siku zote namba hiyo inatumiwa na watu wengine. Nilipiga picha za sinema. Filamu iitwayo Azimio Baya. Tangazo la biashara ya simu mjini Chicago. Tangazo la biashara la Exxon. Matangazo mawili ya benki. Wakati huo huo ninafanya kazi za ujenzi sehemu nyingine.

Tumefanyakazi katika duka kubwa. Na huu ni msimu wa mapunziko, na wao wameweka hivi vibanda vya ziada njia za ukumbini. Katika kibanda kimojawapo kulikuwa na msichana mmoja, nasi tulilazimika kupita mbele yake. Nilimwambia: “Habari za asubuhi, vipi hali yako?” Kama dada huyo alisema kitu, kitu hicho kilikuwa ni “mambo.” Ni hilo hilo tu alilolisema.

Mwishowe nilimwambia: “Bibie, husemi lolote. Nilitaka kukuomba radhi kama nimesema mabaya.” Naye akaniambia: “Hapana, unajua, mimi ni Mwislamu.” “Wewe ni nani?” Mimi ni Mwislamu, na wanawake wa Kiislamu, hatuongei na wanaume ispokuwa tuwe na kitu maalumu cha kuongelea; vinginevyo hatuna kitu cha kufanya na wanaume.” Ohhhh yeye akasema, “Ndiyo, tunatekeleza dini ya Kiislamu.”

Uislamu – vipi uanatamka herufi zake?”

“I-s-l-a-m.”

Kwa muda huo, nilichokijua ni kuwa Waislamu wote ni magaidi. Lakini dada huyo hata hakuwa na ndevu. Vipi dada huyo anaweza kuwa Mwislamu?

Dini hii ilianza vipi?”

“Vizuri, kulikuwa na Mtume.”

“Mtume?” “Muhammad.”

Nilianza uchunguzi fulani. Lakini mimi nimetokea dini moja. Sina nia ya kuwa Mwislamu.

 Likizo ikaisha. Vibanda vikaondolewa. Naye akatoweka.

Niliendelea kuomba dua na kusali, na kuuliza kwa nini dua zangu hazijibiwi? Mnamo Novemba 1991, nilikuwa nampeleka mjomba wangu Richie nyumbani kutoka hospitalini. Nilianza kutoa vitu kutoka katika droo yake ili nipakie vitu vyake na kulikuwa na Biblia ya Gideon. Nilisema, Mungu ameshajibu dua zangu. Biblia hii ya Gideon. (Bila ya shaka, wameiweka katika kila chumba cha hotel hii.) Hii ni alama kutoka kwa Mola kuwa yupo tayari kunifundisha. Kwa hiyo, nikaiiba Biblia hiyo.

Nilienda nyumbani na kuanza kuomba: “Ee Mungu nisomeshe niwe Mkristo. Usinisomeshe njia ya Mashahidi wa Yehova. Usinifundishe njia ya Wakatoliki. Nifundishe nji yako! Wewe hujaifanya Biblia hii iwe ngumu sana kasi cha watu wa kawaida waliowaaminifu katika sala washindwe kuifahamu”.

Nilipita njia zote katika Agano Jipya. Nilianza Agano la Kale. Vizuri, hatimaye kulikuwa na sehemu katika Biblia juu ya Mitume. Bing!

Nilisema, subiri dakika moja (kidogo) yule bibie wa Kiislamu alisema kuwa wao wana Mtume. Vipi hiyo, na Mtume huyo hayupo humu?

Nilianza kufikiria, Waislamu – wapo bilioni moja ulimwenguni – hiyo maana yake ni mtu mmoja kwa kila watu watano mtaani, kinadharia ni Mwislamu. Na nilifikiria: watu bilioni moja! Jumuika , njoo, shetani ni mzuri. Lakini yeye si mzuri hivyo.

Kwa hiyo, baadaye nilisema, nitasoma kitabu chao, ambacho ni Quran, na nitaona aina ya uongo iliyopo ndani yake. Huenda kina mafundisho ju ya kuficha bunduki aina ya AK – 47. Kwa hiyo, nilienda duka la vitabu vya Kiarabu.

Wakaniuliza, “Tukusaidie nini?”

“Nataka Quran.”

“Sawa, hapa tunazo nakala za Quran.”

Walikuwa na nakala nzuri sana – kwa dola therathini, dola arobaini.”

“Tazama, nataka kusoma tu, sitaki kuwa mmoja wao, sawa?”

“Sawa, tuna huo hapo mdogo dogo kwa dola tano wenye jarada la karatasi.”

Nilirudi nyumbani, na kuanza kusoma Quran yangu kuanzia mwanzo, wa Suratul Fatihah. Na sikuweza kuyatoa macho yangu kutoka katika Quran.

Oyaa, tazama hii. Inazungumzia juu ya Nuhu humu. Tunaye Nuhu katika Biblia yetu pia. Oyaa, Inazungumzia Lutwi na Ibrahimu. Siamini. Kamwe sijalijua jina la shetani kuwa ni Ibilisi. Oyaa, vipi kuhusu hayo?

Unapopata picha hiyo katika T.V yako na ikiwa na maelezo kidogo nawe unabonyeza swichi ya kusafisha picha. Hilo ni jambo la hakika linalotoke na Quran.

Nilipitia kila kitu. Kwa hiyo, nilisema: sawa; nimeshafanya haya, sasa kitu gani utakachofanya baadaye? Vizuri, uende katika eneo lao la kukutania. Nilitazama kitabu cha kurasa za manjano (kitabu cha kuelezea mambo mbali mbali yanapopatikana) na mwishowe nilikipata kituo cha Kiislamu cha Calfornia kusini, katika Vermont. Niliwapigia simu nao wakasema, “Njoo Ijumaa.”

Sasa tayari nilianza kuchanganyikiwa, kwa sababu, sasa ninajua nitaanza kukabiliwa na Habibu na bunduki yake ya AK-47.

Nataka watu wafahamu, Wakristo wa Marekani wapoje katika ujio wa Uislamu. Nafanya mambo ya kitoto kuhusiana na AK- 47, lakini sijui kama watu hao wana masime chini ya makoti yao, unajua? Kwa hiyo, nilienda hadi mbele, na nina hakika vya kutosha, kuwa kulikuwa na huyu ndugu mwenye (six-foot-three, 240-paundi) ndevu na kila kitu, na nilikuwa ni mwenye heshima.

Nilitembea na kusema: “Samahani bwana.”

[Lahaja ya Kiarabu] “Rudi nyuma!”

Alidhani kuwa mimi tayari ni mwenziwao.

Nikasema; “Ndiyo bwana” [kinyenyekevu].

Sikujua kwa nini nilirejeshwa nyuma, lakini hata hivyo, nilirudi nyuma. Walikuwa na hema na mazuria yaliyokuwa nje. Nilisimama hapo, kwa aina fulani ya kuona haya, na walikuwa wamekaa chini na kusikiliza mahubiri. Na watu wengine wakasema, nenda mbele, ndugu, kaa chini. Nami ninaenda, hapana, shukrani, hapana, shukrani, ninawatembelea tu.

Kwa hiyo, mwishowe mahubiri yakaisha. Wote walipamga mstari ili waswali na wakasujudu. Kwa hakika nilirejeshwa nyuma yaani nilikumbushwa kujua mambo ya nyuma.

Nilianza kutia akilini, katika mishipa yangu, mifupa yangu, moyoni mwangu na roho yangu. Kwani sala imeisha. Nasema, oyaa, nani atakayenitambua? Kwa hiyo, nilianza kujichanganya kama vile mimi ni mmoja wao, na nilikuwa natembea msikitini na ndugu mmoja anasema, “Assalaamu alaykum.” Nami nafikiria, Je amesema: “Chumvi na nyama.”

“Assalaamu alaykum.”

Kuna mtu mwingine aliyeniambia “Chumvi na nyama.”

Sikujua kitu gani katika dunia hii wanachokisema, lakini wote walitabasamu.

Kabla ya mmoja wao kugundua kuwa mimi si mtu wa kuwa hapo na akanichukua hadi chumba cha mateso, au cha kunikata kichwa, nilitaka kuona mambo mengi niwezayo kuyaona. Kwa hiyo, hatimaye, nilienda maktaba na huko kulikuwa na ndugu wa Kimisri; jina lake lilikuwa ni Omar Mungu ameniletea mtu huyo.

Omar alinijia, na akasema, “samahani. Je, hii ndiyo mara yako ya kwanza kuja hapa? Kwa hakika alikuwa na lahaja nzito.

Nikasema; eenhe, ndiyo.

“Oh, vizuri sana. Je, wewe ni Mwislamu?”

“Hapana, nasoma kidogo tu.”

“Oh, wewe unajifunza? Hii ndiyo mara yako ya kwanza kutembelea msikitini?”

“Ndiyo.”

“Njoo, acha nikuonyeshe sehemu hii.” Na akaninyanyua kwa mkono, nikawa natembea kwa nguvu ya mtu mwingine – tulikamatana mikono. Nilisema, Waislamu hawa ni marafiki. Kwa hiyo, akanionyesha maeneo hayo.

“Kwanza kabisa, huu ndiyo ukumbi wetu wa kuswalia, vua viatu vyako katika eneo hili.”

“Hivi ni vitu gani?”

“Hiki ni chumba kidogo, Hapa ndiyo sehemu ya kuweka viatu vyako.”

“Kwa nini?”

“Vizuri, kwa sababu wewe unasogelea eneo la kuswalia, na eneo hilo ni takatifu sana. Huruhusiwi kuliingia na viatu vyako; sehemu hiyo inakuwa safi kabisa muda wote.”

Kwa hiyo, alinichukua na kunipeleka eneo la wanaume.

“Na hapa, ndiyo sehemu tunayotilia wudhu.”

“Voodoo! Sijasoma chochote juu ya voodoo!”

“Hapana, sio voodoo. Ni wudhu!”

“Sawa, kwa sababu nilimuona mfanyakazi huyo akiwa na mwanasesere na pini, nami sipo tayari kufanya ahadi ya aina hiyo.”

Yeye anasema; “Hapana, wudhu, hapo ni pale tulipojisafisha.”

“Kwa nini unafanya hivyo?”

“Vizuri, wakati unaswali mbele ya Mungu, lazima uwe msafi, kwa hiyo, tunaosha mikono yetu na miguu yetu.”

Kwa hiyo, nikajifunza vitu vyote hivyo. Naye akaniruhusu niondoke, na alisema, njoo tena. Nilienda tena na nikamuomba yule mtunza maktaba vitabu vya swala, na nilirudi nyumbani na kuvifanyia mazoezi. Nilihisi kuwa ninajaribu kutenda hiyo swala vizuri, Mungu ataikubali. Niliendelea kusoma na kusoma na kuutembelea msikiti ule.

Nilikuwa na ahadi ya kutembelea Midwest katika umoja wa wanamaigizo. Vizuri, nilichukua kizuria cha kusalia. Nilijua kuwa nilitakiwa niswali kwa wakati maalumu, lakini kulikuwa na maeneo maalumu ambayo huruhusiwi kusali, na mojawapo ni chooni. Nilienda chumbani kwa wanaume katika kituo cha watalii na nikatandika zulia langu na nikaanza kusali sala zangu.

Nikarudi, na Ramadhani ilipofika, nilianza kupokea simu kutoka sehemu mbali mbali za hapa nchini niende nikatoe muhadhara nikiwa ni mchungaji wa Mashahidi wa Yehova aliyeingia Uislamu. Watu waliniona ni mgeni na ni mpya. [Wahamiaji wawili waliongea:]

Kijana huyu ni kama epple pie na anaendesha (a Chevy truck). Yeye ni Mmarekani Mwekundu Alikuwa ni Shahidi wa Yehova.”

“Watu hao walikuja asubuhi hiyo?”

“Ndiyo, hao hao.”

“Hilo, lilitufanya tusilale siku za Jumapili?”

“Ndiyo, kijana huyu alikuwa mmoja wao. Na sasa ni mmoja wetu.”

Hatimaye mtu mmoja alinijia na kusema [kwa lahaja za Kipakistani] “Oh ndugu, mazungumzo yako yalikuwa mazuri sana. Lakini unajua wewe, katika madhehebu ya Kishafii…”

Kisha kitu pekee nilichoweza kukifanya ni kuwageukia na kusema, “Ahaa, wandugu, Samahanini sana, natumai ningejua hayo, lakini sijui chochote juu ya Uislamu ispokuwa kile kilichopo katika Quran na Sunnah.[9]

Mmoja wao aliduwaa na kusema; “Ha –ha! Maskini ndugu, hajui lolote. Anajua Quran peke yake.”

Vizuri, hayo ndiyo yale ninayoyajua. Na hilo limekuwa ni kinga niipendayo sana. Nadhani yote hayo yapo mikononi mwa Allah.”

http://www.newmuslims.tk

chanzo ni: habari za Kiislamu, San Francisco, CA 94141-0186

 8- GEORGE ANTHONY – ALIYEKUWA PADRI WA KIKATOLIKI (SRI LANKA)

Fr. Anthony alikuwa ni padri wa Kikatoliki nchini Sri-lanka. Masimulizi yake ya kuwa muumini wa kweli na kuchagua jina la Abdulrahmani ni jambo la kuvutia sana. Kwani kwa kuwa padri wa Kikatoliki kwa hakika alikuwa na ujuzi sana wa mafundisho ya Biblia. Alikuwa ananukuu Biblia mara kwa mara pale alipokaa na kutusimulia safari yake ya kuingia Uislamu. Alipokuwa anasoma Biblia aligundua migongano mingi ndani yake. Anaendelea kunukuu Aya za Biblia kwa lugha ya Kisri-lanka na kuonyesha utata.

Ananukuu Esaih 29:12 isemayo: “Kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi.” Aya hii ni utabiri wa Mtume Muhammad (S.A.W), kwa sababu Muhammad (S.A.W), ndiye aliyekuwa Mtume asiyejua kusoma na kwa kuwa yeye ndiye Mtume asiyejua kusoma na alipotakiwa na malaika Jibrilu asome ufunuo mtakatifu wa kwanza mbele yake alisema; “Mimi si msomi” na hii ni kinyume na imani ya Kikristo kuwa Yesu ni Mungu, huku Matendo ya Mitume 2:22 ya Biblia Takatifu inayomchukulia Yesu kuwa ni mtu. Inasema; “Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;”

Ukristo na dini nyinginezo, haziuelezei utume kwa uwazi kwa mujibu wa kauli yake. Wala Ubudha na ukimya wake juu ya Mitume wengine. Kinyume na hayo, kwani katika Uislamu ni lazima kuamini Mitume yote iliyotangulia na kuwaheshimu. Kwa mujibu wa Abdulrahmani imani hii ni ya kukinaisha kabisa na ni ya kupendeza kwa kila mtu. Abdulrahmani anasema kuwa hakuna sababu ya kuwazuia mapadri wa Kikatoliki wasioe, wakati mapadri wa madhehebu mengine ya Kikristo wnaoa. Abdulrahmani alikuwa anatafakari juu ya mkorogeko wa imani ya Kikristo wakati huo huo alipata mkanda wa kaseti wa padri wa Kikristo wa Kisir-lanka aliyesilimu Shareef D. Alwis. Mkanda wa Ahmad Deedat pia ulimvutia. Juhudi zake za kuendelea kuupata ukweli mwishowe zilitoa matokeo ya kumbadili dini na kuwa Mwislamu. Fr. Goerge Anthony.

Abdulrahmani, anatokea kijiji cha Rathnapura Sri-lanka. Alikuwa anafanya huduma zake kama padri katika kanisa la Katumayaka. Ana salio la miaka kumi katika kufundisha upadri. Aliandika barua kwenda kwa mama yake akimfahamisha Uislamu. Baada ya kusoma kwa miezi kadhaa naye alifuata njia ya mwanawe na kuingia Uislamu. Dada pekee wa Abdulrahmani anafanyakazi Ugiriki. Baba yake na dada yake bado ni Wakristo. Abdulrahmani aliacha kazi yake inayoheshimika sana ya upadri kwa ajili ya ukweli. Naye kwa furaha kabisa ametoa muhanga mapato yake ya mali kwa furaha ya kiroho. Kwa sasa anafanyakazi ya ukufunzi katika tume ya kutangaza Uislamu nchini Kuwaiti.

 9- DR. GARY MILLER (ABDUL-AHAD OMAR) MWANAHISABATI NA MMISHIONARI WA KIKRISTO (CANADA)

Gary Miller (Abdul-Ahad Omar) anaonyesha jinsi tunavyoweza kuanzisha imani ya kweli kwa kuweka viwango vya ukweli. Yeye anafafanua jambo lepesi, lakini ni njia yenye kufanya kazi sana katika kuupata mwelekeo sahihi katika uchunguzi wetu wa kusaka ukweli.

G.R. Miller ni mwanahisabati na ni mtaalamu wa mambo ya kitikadi. Alikuwa ni mchapakazi katika umishionari wa Kikristo akifanyakazi katika maeneo maalumu maishani mwake lakini punde tu alianza kugundua mambo yasiyowiana katika Biblia. Mwaka 1978, ilimtokea kuisoma Quran akitarajia kuwa nayo vilevile itakuwa na mchanganyiko wa ukweli na uongo.

Kwa mshangao, aligundua kuwa ujumbe wa Quran kwa usahihi kabisa ulikuwa ni ule ule kama ilivyo asili ya ukweli alioutiririsha kutoka katika Biblia. Akawa Mwislamu na tangu hapo amekuwa ni mchapakazi mchangamfu katika kutoa mafunzo ya Uislamu kwa watu wengine ikiwemo njia ya kutokea redioni na katika Tv. Pia, yeye ni mtunzi wa makala nyingi na machapisho kadhaa juu ya Uislamu.

Mmishionari muhimu sana wa Kikristo ameingia Uislamu na amekuwa mpiga debe mkubwa wa Uislamu, alikuwa ni Mmishionari mchapakazi sana na alikuwa na elimu nyingi ya Biblia. Mtu huyo anapenda sana hisabati, na hiyo ndiyo sababu kuwa anapenda mantiki. Siku moja, aliamua kusoma Quran ili kujaribu kupata Kosa lolote ambalo atafaidika nalo wakati wa kuwaita Waislamu waingie Ukristo… Alitarajia Quran itakuwa ni kitabu cha zamani kilichoandikwa karne kumi na nne zilizopita, kitabu kinachozungumzia jangwa na kadhalika… Alishangazwa na kile alichokikuta. Aligundua kuwa kitabu hiki kina vitu ambavyo, vitabu vyengine ulimwenguni havina… Alitarajia atakuta baadhi ya visa juu ya wakati mgumu aliokuwa nao Mtume Muhammad (S.A.W), kama vile kifo cha mkewe Khadija (Allah amrehemu) au kifo cha mwanawe na mabinti zake … Hata hivyo, hakukuta chochote kama hivyo … na kile kilichomfanya achanganyikiwe zaidi ni kuwa alikuta “sura” kamili katika Quran inaitwa “Mariamu/Maria” ambayo imeshamiri heshima nyingi kwa Mariamu (amani iwe juu yake) jambo ambalo halipo katika vitabu vilivyoandikwa na Wakristo na hata Biblia yao haina. Hakukuta sura yeyote iliyoitwa “Fatuma” (binti ya Mtume) wala “Aisha” (mkewe), Mungu awarehemu wote wawili. Pia alilikuta jina la Yesu (amani iwe juu yake) limetajwa ndani ya Quran mara ishirini na tano, wakati jina la Muhammad (S.A.W), limetajwa mara nne tu, kwa hiyo, akawa amechanganyikiwa zaidi. Akaanza kuisoma Quran kwa uangalifu zaidi akitarajia kugundua kosa, lakini alishtushwa pale aliposoma aya kubwa kabisa ambayo ni aya namba 82 ya surat Al-Nisaa (Wanawake) isemayo: “Hawaizingatii nini, hii Qurani? Na kama ingelitoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu bila shaka wangalikuta ndani yake khitilafu nyingi.”

Dr. Miller anazungumzia aya hii: “Moja ya misingi ya kisayansi ni msingi wa kugundua kasoro au kutafuta kasoro katika nadharia hadi itakapothibitishwa kuwa ni sahihi (jaribio la kugundua uongo wake)… kile kilichomshangaza ni kuwa Quran Tukufu inawaambia Waislamu na wasiokuwa Waislamu wajaribu kugundua makosa katika kitabu hiki na kinawaambia watu hao kuwa hawatagundua kosa lolote.” Pia anasema juu ya aya hii, hakuna mwandishi yeyote ulimwenguni mwenye ushujaa wa kuandika kitabu na kusema kuwa kitabu chake hakina makosa, lakini Quran, kinyume kabisa, inakueleza kuwa haina kosa na inakutaka ujaribu kugundua hata kosa moja na kamwe hutoligundua.

Aya nyingine ambayo Dr. Miller ameihakisi kwa muda mrefu ni aya namba 30 ya Surat “Al-Anbiya’a” (Mitume): “Je! Hawakuona wale waliokufuru ya kwamba mbingu na ardhi vilikuwa vimeambatana, kisha Tukaviambua, (Tukavipambanua). Na Tukafanya kwa maji kila kitu kilicho hai. Basi je, hawaamini?”

Anasema: aya hii kwa hakika ni mada ya uchunguzi wa kisayansi ambayo imeshinda zawadi ya nobel mwaka 1973 na ilikuwa ni juu ya nadharia ya “Mlipuko mkuu.” Kwa mujibu wa nadharia yake, ulimwengu ulikuwa ni matokeo ya mlipuko mkuu ambao umepelekea kuundika kwa ulimwengu ukiwa na mbingu zake na sayari.

Dr. Miller anasema: “Sasa tumekifikia kile kinachoshangaza juu ya Mtume Muhammad (S.A.W) ni kile kinachodaiwa kuwa ni msaada wa shetani juu yake, Mungu anasema: “Wala mashetani hawakuteremka nayo (hii Qurani kama wanavyodai kusema hao makafiri katika kuitukana). Wala haiwi kwao (kuiteremsha Qurani inayovunja hayo mambo yao), na hawawezi. Bila shaka wao wamezuiliwa kusikia (yanayosemwa na Malaika huko mbinguni).” (Quran 26:210 – 212) na aya: “Na Tunapoibadili Aya kwa Aya (nyingine), na hali ya kuwa Mwenyezi Mungu (Akulinde) na shetani aliyefukuzwa (katika rehema yake Mwenyezi Mungu. Anza kwa kusoma Audhu).

Unaona? Je, hii inaweza kuwa ni njia ya shetani ya kuandika kitabu? Vipi aandike kitabu kisha akwambie umuombe Mola akupe ulinzi dhidi ya shetani kabla ya kukisoma kitabu hicho? Hizo ni aya za miujiza katika kitabu hiki cha miujiza! Na kina jibu la kimantiki kwa wale wote wanaodai kuwa kitabu hicho ni cha Shetani.” Na miongoni mwa visa vilivyomshangaza Dr. Miller ni kisa cha Mtume (S.A.W) na Abu-Lahabi… Dr. Miller anasema: “Mtu huyo alikuwa anauchukia sana Uislamu kiasi ambacho alikuwa anamfuatilia Mtume popote aendapo ili amwaibishe. Kama atamuona Mtume anazungumza na wageni, alikuwa anasubiri hadi anapomaliza kisha anawauliza: “Muhammad amekwambieni nini?” Na kama alisema cheupe basi yeye atasema kwa hakika ni cheusi na kama amesema ni usiku yeye atasema ni mchana. Yeye anakusudia kumwambia Muhammad ni mwongo kwa yote asemayo na kuwafanya watu wawe na mashaka juu ya kitu hicho. Na miaka kumi kabla ya kifo cha Abu Lahabi, iliteremshwa Sura kwa Mtume, iitwayo “Al-Masadi.” Sura hiyo inasema kwamba Abu Lahabi hatoingia Uislamu. Katika kipindi cha miaka kumi, Abu Lahabi aliweza kusema: “Muhammad anasema kuwa mimi sitokuwa Mwislamu na kwa hiyo, nitaingia Motoni, lakini sasa ninawaambia nataka kuingia Uislamu na niwe Mwislamu. Je, sasa mnaonaje juu ya Muhammad? Je, anasema ukweli au sio? Je, ufunuo wake umetoka kwa Mungu? Lakini Abu Lahabi hakufanya jambo hilo, kabisa, ingawa alikuwa ni mpinzani wa Muhammad (S.A.W) katika kila jambo, lakini si katika jambo hili. Kwa maneno mengine, ilikuwa ni kama vile Mtume (S.A.W) alikuwa anampa Abu Lahabi nafasi ya kuhakikisha makosa yake! Lakini hakuthibitisha kwa miaka kumi yote! Hakuingia Uislamu na hata hajajifanya eti ni Mwislamu!! Katika miaka kumi, alikuwa na nafasi ya kuuharibu Uislamu kwa dakika moja tu! Lakini hilo halikutokea kwa sababu hiyo Quran si maneno ya Muhammad (S.A.W) lakini ni maneno ya Mwenyezi Mungu ambaye ni Mjuzi wa kilichofichikana na Anajua kuwa Abu Lahabi hatokuwa Mwislamu.

Vipi Mtume (S.A.W) ajue kuwa Abu Lahabi atathibitisha kile kilichosemwa ndani ya sura hiyo ikiwa huo haukuwa ufunuo wa Allah? Vipi Mtume atakuwa na uhakika katika kipindi cha miaka kumi kuwa kile kilichomo (ndani ya Quran) ni sahihi kama hajajua kuwa huo ni ufunuo kutoka kwa Allah? Kwa mtu ajitiaye katika changamoto hatari kama hiyo, jambo hilo lina maana moja tu: nayo ni kuwa huo ni ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

“Pana kuangamia mikono miwili ya Abu Lahab! Naye amekwisha angamia. Hayatamfaa mali yake wala alivyovichuma. (Atakapokufa) atauingia Moto wenye mwako (mkubwa kabisa). Na mkewe, mchukuzi wa kuni (za fitina), (fattani, anayefitinisha watu wasiingie katika Dini; atauingia Moto huo). (Kama kwamba) shingoni mwake iko kamba iliyosokotwa (anayochukulia kuni za fitina hizo). (Quran 111:1-5).

Dr. Miller anasema kuhusu aya iliyomshangaza: moja ya miujiza ndani ya Quran ni changamoto ya wakati ujao kwa vitu vile ambavyo mtu hawezi kuvitabiri na kwa vitu hivyo “jaribio la kuona uongo wa kitu” inatumika, jaribio hili linakusanya kutafuta makosa hadi pale kile kitu kinachojaribiwa kinapothibitishwa kuwa ni sahihi. Kwa mfano, hebu tutazame Quran imesemaje juu ya mafungamano kati ya Waislamu na Mayahudi. Quran inasema kuwa Wayahudi ni maadui wakuu wa Waislamu na jambo hilo ni kweli hadi hivi sasa kwani maadui wakuu wa Waislamu ni Wayahudi.

Dr. Miller anaendelea: hili linazingatiwa kuwa ni changamoto kubwa sana kwani Wayahudi wana nafasi ya kuuangamiza Uislamu kirahisi kwa kuwatendea wema Waislamu kwa miaka michache na baadaye waseme: Sisi tunakutendeeni kama marafiki zetu na Quran inasema kuwa sisi ni maadui zenu, Quran lazima iwe na makosa! Lakini hili halijatokea kwa miaka 1400!! Na kamwe halitatokea kwa sababu hayo ni maneno ya Mmoja ambaye anajua kisichoonekana naye ni Mwenyezi Mungu na si maneno ya wanadamu.

Dr. Miller anaendelea: Je, waweza kuona namna aya ambazo zinazungumzia juu ya uadui kati ya Waislamu na Wayahudi zinaanzisha changamoto kwa akili ya mwanadamu? “Hakika utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu (wengine) kwa Waislamu ni Mayahudi na wale mushirikina (wasiokuwa na Kitabu), na utawaona walio karibu kwa urafiki na Waislamu ni wale wanaosema: “Sisi ni Wakristo.” (Hayo) ni kwa sababu wako miongoni mwao wanavyuoni na wamchao Mungu, na kwa sababu wao (Wakristo) hawatakabari; (wakijua haki huifuata). Na wanaposikia yaliyoteremshwa kwa Mtume (na yakawatulilikia kuwa ni kweli), utaona macho yao yanamiminika machozi kwa sababu ya haki waliyoitambua; wanasema: “Mola wetu! Tumeamini, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (ukweli huu).” (Na wakilaumiwa kwa kusilimu kwao husema): “Na kwa nini tusimwamini Mwenyezi Mungu na haki iliyotufikia, na hali tunatumai Mola wetu atuingize (Peponi) pamoja na watu wema?” (Qurani 5:82-84).

Aya hizi zilitumiwa na: Dr. Miller pia alipokuwa Mkristo lakini alipoujua ukweli, aliamini na kuingia Uislamu na akawa ni muhubiri wa Kiislamu. Mungu alitie nguvu.

Dr. Miller anasema juu ya mtindo wa kipekee wa Quran kuwa yeye anauona ni wa kupendeza sana: hakuna shaka kuwa kuna kitu cha pekee na cha kushangaza katika Qurani ambacho hakijatajwa sehemu yeyote ile, kwani Quran inakupa maelezo maalumu na inakuambia kuwa ulikuwa huyajui hapo kabla. Kwa mfano: Hizi ni habari za ghaibu Tunazokufunulia; nawe hukuwa nao walipokuwa wakitupa kalamu zao ndani ya maji (kwa kura, wajue) nani wao atamlea Maryamu, na hakuwa nao walipokuwa wakishindana. (Quran 3:44)

Hizi ni katika khabari za siri Tunazokufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala watu wako, kabla ya hii (Qurani kuteremshwa). Basi subiri; hakika mwisho (mwema) utawathubutikia wanaomcha Mungu.” (Quran 11:49).

Hizi ni katika khabari za siri Tulizokufunulia. na hukuwa pamoja nao walipoazimia shauri lao, hali wakifanya vitimbi vibaya. (Quran 12:102).

Dr. Miller anaendelea: “Vitabu vitakatifu vingine havitumii mtindo huu, vitabu vingine vyote vina maelezo ambayo yanakwambia maelezo hayo yametokea wapi. Kwa mfano, wakati Biblia Takatifu iliyopotoshwa inazungumzia juu ya kisa cha mataifa ya kale, inakusimulia kuwa mfalme huyu aliishi katika eneo hili na kiongozi yule alipigana katika vita vile, na mtu yule maalumu ana idadi kubwa ya watoto na majina yao ni … lakini kitabu hiki (Biblia iliyopotoshwa) daima inakusimulia kuwa kama unataka kujua zaidi, soma kitabu maalumu kwani maelezo hayo yamekuja kutoka katika kitabu hicho.”

Dr. Miller anaendelea: “Hii ni kinyume na Quran ambayo inakupatia maelezo na inakwambia kuwa ni mapya!! Na kile kinachoshangaza ni kuwa watu wa Maka wa wakati huo-wakati wa ufunuo wa aya hizo walikuwa wanazisikia aya hizo na changamoto iliyokuwemo katika aya hizo ambayo ni mpya na ilikuwa haijulikani na Muhammad (S.A.W) wala watu wake wa wakati huo, lakini licha ya hivyo, kamwe hawajasema: tunayajua hayo na hayo si mapya, na hawajasema: tunapajua pale Muhammad alipozitoa aya hizo. Hilo halikutokea, lakini kilichotokea ni kuwa hakuna mtu aliyethubutu kusema kuwa Muhammad (S.A.W) alikuwa anawaongopea kwa sababu maelezo hayo yalikuwa ni maelezo mapya kabisa, hayajakuja kutoka katika akili za wanadamu lakini yamekuja kutoka kwa Allah ambaye anajua kisichoonekana hapo zamani, na sasa na wakati ujao.”

 10- REV. DAVID BENJAMIN KELDANI (ABDUL’L-AHAD DAWUD) (IRAN).

Profesa Abdu ‘l-Ahad Dawud, B.d., mwandishi wa mtiririko wa makala kwa sasa, zamani alikuwa ni Padri wa Roman Katoliki kwa jina la Reverend David Benjamin Keldani, B.D., wa Uniate-Caldean sect. Alipoulizwa vipi aliingia Uislamu aliandika:

“Kuingia kwangu Uislamu hakukuweza kumpa sifa mtu yeyote aliyesababisha zaidi ya maelekezo ya Mwingi wa rehema. Bila ya mwongozo huu mtakatifu juhudi zote za masomo na uchunguzi wa kutafuta ukweli huenda zingepelekea mtu kupotea. Kipindi ambacho niliamini Umoja kamilifu wa Mungu na Mtume wake Mtukufu, Muhammad amekuwa ni sehemu ya mwenendo na tabia yangu.”

“Abdu ‘l-Ahad Dawud ni padri wa Roman Katoliki wa zamani kwa jina la Rev. David Benjamin, B.D., wa Uniate – Caldean Sect. Alizaliwa 1867 mjini Umia Persia alisoma shule ya watoto mjini mwake. Toka 1886-89 (kwa miaka mitatu) alikuwa katika walimu wa Uaskofu wa Canterbury`s Mission to the Assyrian (Nestorian) Wakristo wa Urmia. Mwaka 1892 alipelekwa na Cardinal Vaughan hadi Rome, sehemu ambayo alipitia kozi ya masomo ya falsafa na nadharia katika chuo cha Propandanda cha Fide, na mnamo mwaka 1895 alikuwa ni padri msimikwa. Katika kipindi hicho alitawanya mlolongo wa makala katika vibao juu ya “Assyria, Rome na Canterbury”; pia Aryland Akirekodi juu ya uthibitisho wa Torati.” Ana tafsiri nyingi za Eva, Maria katika lugha tofauti tofauti, zimechapishwa kwa vielelezo vya Misheni ya Kikatoliki. Alipokuwa njiani Constantinople kuelekea Pershia mwaka 1895, alitawanya mlolongo mrefu wa makala za Kingereza na Kifaransa katika magazeti ya kila siku, yaliyochapishwa sehemu hiyo chini ya jina la The Levant Herald, kwa Makanisa ya mashariki mwaka 1895 alijiunga na misheni ya Lazarist ya Kifaransa katika eneo la Urmia, na kwa mara ya kwanza alichapisha katika historia ya misheni ndani ya jarida la muda maalumu kwa lugha ya wenyeji Syriac iitwayo Qala-la Shara, yaani “Sauti ya Ukweli.” Mwaka 1897 alikuwa ni mwakilishi kwa taasisi mbili. Uniate-Caldean Archbishops ya Urmia na Salmas to espresent-le-Monial nchin Ufaransa chini ya uongozi wa Cardunal Perrand. Jambo hili bila ya shaka lilikuwa, kwa mwaliko rasmi. Nyaraka ziliosomwa mbele ya baraza la wazee na “Baba Benjamin” zilichapishwa katika kumbukumbu za kihistoria za Baraza la wazee la kalamu ya Bwana, liitwalo “Le Pelirin” kwa mwaka huo. Katka waraka huo padri wa Cadean (hiyo ilikuwa ni amani yake rasmi) akisikitikia mfumo wa elimu wa Kikatoliki miongoni mwa Nestorians, na alitabiri kukaribia kutokea kwa mapadri wa Kirusi katika mji wa Urmia.

Mnamo mwaka 1898 baba Benjamin alirudi tena Pershia, katika kijiji chake asilia, Digala, kiasi cha maili moja kutokea mjini, alifungua shule ya bure. Mwaka uliofuatia alipelekwa na mamlaka ya makasisi kuchukua uongozi wa dayosisi ya Salmas, pale migogoro mikali na kashfa kati ya Unitiate wa Askofu, Khudabash, na mapadri wa Lazzarist ilipozidi kwa muda mrefu amekuwa anaogopea mfarakano. Katika siku ya mwaka mpya 1900, padri Benjamin alihubiri mahubiri yake ya mwisho na ya kukumbukwa sana kwa makutano, wakiwemo, Waaramenia wengi wasio Wakatoliki na watu wengine kutoka kanisa kuu la Mt.George. Khorovabad, Salmas. Maudhui ya mahubiri yalikuwa ni “Karne mpya na watu wapya.” Alikumbushia ukweli kwamba Wamishieni Wanestorian, kabla ya kudhihiri kwa Uislamu, wamehubiri Injili katika Asia yote; wanazo taasisi mbali mbali nchini India (hasa hasa) katika mji wa Malbar Coast). Tartary, China na Mongolia; na kuwa wametafsiri Injili kwa Kituruki, Kiughurs na lugha nyinginezo; Wakatoliki, Wamarekani na misheni za Kianglikana, ingawa wamefanya vizuri kidogo kwa taifa Waassyro (Haldean) katika Elimu ya utangulizi, wameligawa taifa hilo dogo na kuwa Pershia, Kurdistani na Mesopotamia, na kulitumbukiza katika uadui wa aina mbali mbali na madhehebu; na kwa hiyo, juhudi zao zilikuwa ni zenye kujaaliwa kuleta mporomoko wa mwisho kabisa. Kwa hiyo, aliwashauri watu asilia wajitoe muhanga ili wasimame kidete juu ya miguu yao wenyewe kama wanaume, na wasitegemee misheni za kigeni na kadhalika.

Misheni kubwa tano za kujivunia – za Kimarekani, Kifaransa, Kijerumani, na Kirusi – wakiwa na wenziwao, Magazeti yanayoungwa mkono na jamii za dini tajiri, Mabalozi wadogo na Mabalozi. Walikuwa wanajitahidi kuwabadilisha zaidi ya Waassyro – Chaldean laki moja wotoke kutoka katika uasi wa kidini wa Nestorian na wawe katika kundi mojawapo miongoni mwa makundi matano hayo ya uasi. Lakini misheni ya Kirusi punde ilizishinda misheni nyingine, na ilikuwa misheni hiyo ambayo mnamo mwaka 1915 iliwasukuma au iliwalazimisha Waassyrian pia, makabila ya milimani ya Kurdistani, ambao baadaye walihamia uwanda wa Salmas na Urmia, kusaidia kuinua silaha dhidi ya Serikali yao inayoheshimika. Matokeo yalikuwa ni kuwa nusu ya watu hao waliangamia vitani na waliobakia walifukuzwa kutoka katika ardhi zao za asili.

 Swali kuu ni: Je, Ukristo, ukiwa na uma wake wote, maumbile na rangi zake zote, na huku ukiwa na mambo ya bandia yaliyo madhubuti na maandiko yaliyoharibiwa, Je, hiyo ilikuwa ni dini ya kweli ya Mungu? Wakati wa kiangazi mwaka 1900 alistaafu na kuelekea katika nyumba yake ndogo iliyopo katikati ya shamba la mizabibu karibu na chemchem ya sherehe ya Chali-Boulaqhi mjini Digala, na hapo kwa kipindi cha mwezi mmoja alitumia muda wake kwa kusali na kutafakari, akisoma na kumaliza maandiko matakatifu katika maandiko yake asilia. Mgogoro uliishia kwa kustaafu kikawaida kulikopelekwa hadi kwa Maaskofu wa Unite wa Urmia, na hapo kwa uwazi alimweleza Mar (Mgr.) Touma Audu sababu ya kujitoa katika kazi zake za kikasisi. Majaribio yote yaliyofanywa na mamlaka ya makasisi ili aondoe uamuzi wake yalikuwa bila ya faida. Kulikuwa hakuna uadui wa kibinafsi au mabishano kati ya Fther Benjamini na vigogo wake; yote hiyo ilikuwa ni swala la dhamiri.

Aliajiriwa Tarbiz kwa kazi ya ukaguzi katika shirika la huduma za posta na forodha la Pershia chini ya utaalamu wa Belgian. Kisha alichukuliwa katika huduma ya Mtukufu mwana wa mfalme Alihammad Ali Mirsa kwa kazi ya ualimu na ukalimani. Na ilikuwa ni mwaka 1903 ambapo kwa mara nyingine alitembelea Uingereza na huko alijiunga na jamii ya Wakristo wasioamini utatu. Na mwaka 1904 alipelekwa na Uingereza ikishirikiana na Umoja wa Wakristo wageni wasioamini utatu, kuendeleza kazi za elimu na kuelimisha miongoni mwa watu wa nchi yake. Akiwa njiani kuelekea Pershia alitembelea (constantinople, na baada ya mahojiano kadhaa na Sheikh l-Islamu Jemalu d-Din Effendi na Maulamaa wengine (wanazuoni wa Kiislamu), alisilimu na kuingia Uislamu.

 11- MUHAMMAD AMAN HOBHM MWANADIPLOMASIA, MMISHIONARI NA MFANYAKAZI WA KAZI ZA JAMII (UJERUMANI).

Kwa nini watu wa magharibi wanaingia Uislamu?

Kuna sababu nyingi juu ya hilo. Inayoshika nafasi ya kwanza, ni kuwa ukweli daima una nguvu zake. Msingi wa imani ya Kiislamu ni ya uwiano sana, ni ya kimaumbile sana na ni ya kuvutia sana kiasi ambacho mtafuta ukweli aliye mwema hawezi kutovutiwa na hayo. Tuchukulie kwa mfano; imani ya kuwa kuna Mungu mmoja. Namna inavyoinua heshima ya mtu na namna inavyotuweka huru na ung`ang`aniaji wa mambo ya kichawi na ya hovyo hovyo! Namna inavyoongoza kimaumbile kueleke katika usawa wa kibinadamu, kwa kuwa binadamu wote wameumbwa na Mungu Mmoja na wote ni watumishi wa Mola huyo huyo! Kwa Wajerumani, kwa sifa ya kipekee, imani ya kumwamini Mungu ni chanzo cha ufunuo, chanzo cha ushujaa wa kutokuwa na woga na ni chanzo cha kuhisi usalama. Kisha dhana ya maisha baada ya kifo inapindua meza. Maisha katika dunia hii yanabakia kuwa si lengo kuu tena, na sehemu kubwa ya nguvu ya mwanadamu itolewayo kwa ubora wa ahera. Imani ya kuamini siku ya Kiama yenyewe inampa mtu heshima ya kuacha matendo mabaya, na kufanya matendo mazuri pekee ambayo yanaweza kuhakikisha uwokovu wa milele, ingawa matendo mabaya yanaweza kustawi hapa duniani kwa kipindi chenye mipaka maalumu tu. Imani ya kuamini kuwa hakuna mtu awezaye kukimbia matokeo ya hukumu ya haki, na Mungu Mjuzi afanyaye mambo mawili kabla ya mtu kufanya chochote kile kilichokibaya na kwa hakika huu ukaguzi wa milele ni wenye kutenda kazi zaidi kuliko polisi wenye kufaa sana duniani.

Kitu kingine ambacho kinawavutia wageni wengi kuingia Uislamu ni msisitizo wake juu ya kuvumiliana. Kisha sala za kila siku zinamfundisha mtu awe anapanga wakati na mwezi mmoja wa kufunga unamuwezesha mtu kufanya mazoezi ya kujimiliki juu ya nafsi yake na bila ya shaka kupanga wakati na kuwa na nidhamu binafsi ni vitu viwili vya fikra muhimu sana ya mtu mwema na mtu mbora.

Sawa, yanakuja mafanikio halisi ya Uislamu. Uislamu ni itikadi pekee ambayo imefanikiwa kuingiza, kidogo kidogo, kwa wafuasi wake roho ya kuona mfumo wa maadili na mipaka ya utu bila kulazimishwa na vitu vya nje. Kwani Mwislamu anajua kwamba, popote alipo, anatazamwa na Mungu. Imani hii inamwepusha na dhambi. Kwa kuwa binadamu kwa kawaida anamili kwa Mwenyezi Mungu, Uislamu pia, unatoa amani ya moyo na akili – na jambo hili limesahauliwa kabisa na jamii za Kimagharibi za hivi sasa.

Nimeshaishi chini ya mifumo ya maisha mbali mbali na nimeshapata nafasi ya kujifunza itikadi mbali mbali, lakini nimehitimisha kuwa hakuna imani yeyote iliyokamilika kama Uislamu.

Ujamaa una vivutio vyake, na hivyo hivyo kwa mfumo Kidemokrasia wa Kisekyula na mfumo wa Kinazi. Lakini hakuna mfumo wowote katika hiyo wenye kanuni kamilifu kwa maisha mema. Ni Uislamu pekee wenye ukamilifu huo, na kwa hiyo, ndiyo sababu watu wazuri wanauingia Uislamu.

Uislamu si nadharia bali ni wa vitendo. Uislamu si jambo la kupita, Uislamu unamaanisha utiifu mkamilifu kwa matakwa ya Mungu.

Kutoka “Islam, Our Choice = “Uislamu ndio Chaguo Letu”

 12- PADRI MKUU VIACHESLAV POLOSIN (URUSI).

Viacheslay Sergeevich Polosin alizaliwa mwaka 1956. Mwaka 1979 alihitimu kitengo cha falsafa cha MGU na mnamo 1984 alihitimu Seminari ya makasisi Moscow. Alikuwa ni padri msimikwa na alihudumia parokia katika dayosisi ya Asia ya kati na Kaluga ya RPTS. Mwaka 1990 alinyanyuliwa daraja ya upadri mkuu. Mwaka huo huo alichaguliwa kaimu wa watu wa RSFSR kutoka jimbo la Kaluga na aliongoza tume ya mamlaka kuu kabisa ya Soviet, alihitimu katika shule ya kidiplomasia ya wizara ya mambo ya nje na kutetea makala zake juu ya madai ya: “Kanisa la Kiothodoksi la Kirusi na hali ya USSR, 1971-1991.” Kuanzia 1993 amekuwa ni mwajiriwa wa kazi za serikali ya Duma katika Baraza la harakati za kidemokrasia ya Kikristo ya Kirusi na ni mwanachama wa baraza la umoja wa Kikristo. Mwaka 1991, alienda likizo kutokea dayosisi ya Kaluga na tangu mwaka 1995 hajasalisha katika Liturujia (kawaida ya ibada ya usharika mtakatifu). Katika mahojiano yake na jarida la Musulmane yeye, kirasmi alijiita Mwislamu: “Ninazingatia kuwa Quran ni ufunuo wa mwisho duniani, ulioteremshwa kwa Mtume Muhammad. Hakuna Mola ispokuwa ni Mungu Mmoja, Allah, na Muhammad ni Mtume wake.” Viacheslav Polosin ni mtunzi wa kazi nyingi za kisomi juu ya mambo ya kihistoria, kisiasa, kidini, na mada za kifalsafa. Mwezi Februari wa mwaka huo alitetea makala nyingine juu ya mada: “Lahaja ya visa vya kubuniwa na waundaji wa visa vya kubuni vya kisiasa.” Mawazo yake ya msingi ya kifalsafa ni kukiwasilisha kitabu chake “visa vya kubuni, Dini, na hali.” (Moscow, 1999).

Katika mahojiano na jarida “Musulmane;” VIACHESLAV POLOSIN alisema kuwa Uislamu haujaanza kutokana na Ukristo lakini ni mapinduzi ya pili na makuu ya imani ya Mungu Mmoja imani ya Ibrahimu. Ibrahimu alikuwa anaamini Mungu Mmoja na alikuwa ni mtu wa kwanza kueleza jambo hili wazi wazi. Alitangaza jambo hilo na alilithibitisha kwa mafanikio, akawa “baba” wa waumini wote. Baadaye utamaduni huo ukakatizwa na mkengeuko. Hilo linajulikana kwa kuwa Mitume yote na wengi wao vilevile wanaitwa “waokozi”… wakiwakosoa watu kwa mkengeuko wao na kutumbukia katika upagani na ukafiri. Na Mtume mkuu ambaye ni Yesu, vilevile alikosoa watu kwa kukengeuka na kuingia ukafiri. Zaidi ya hayo, Yesu yeye mwenyewe alijizungumzia nafsi yake kwa mafumbo kuwa ametumwa na Mungu kufanya kazi maalumu. Kabla watu hawa kusema: “Mitume ni watu kama sisi.” Lakini Mungu amempeleka Malaika wa Mungu asiye na dhambi – katika Biblia malaika wanaitwa “watoto wa Mungu” (Job 38:7) – ambaye alikuwa ni Mtume mtakatifu kabisa lakini alikuwa hatiiwi. Wao walifikiria hamu ya kumwangamiza. Naye alikosoa utawala ulioshindwa kufikia malengo ya wakati huo na kusambaza habari njema za Mungu bila ya mipaka ya mtu hata mmoja, kwa watu wote; hayo yalikuwa ni mapinduzi makubwa ya Uyahudi. Uislamu ni mapinduzi ya pili, yaliyosafisha sana Ukristo wa karne ya sita na saba kutokana na ukuaji wa upagani ambao umeundika katika kipindi chake na kujipatia madaraka rasmi na kukubaliwa kwa wingi mkubwa.

Kinachovutia katika Uislamu ni jambo lepesi tu Tauhidi (imani ya kuamini Mungu Mmoja) kwa mfumo wake maridadi ili tusimfikiri Mungu katika tabia isiyofaa. Napenda jambo hilo kwani hakuna kupingana na kuna hali ile ile ya kimantiki. Quran Tukufu inasema papo hapo kuwa ukweli hauna kupingana. Kuna mafundisho ya dini, Mungu mwenye miujiza, Muumba, Mwenye nguvu, Mwenye Rehema na yote yaliyobaki lazima yawe yanaafikiana na hayo. Kama kuna kitu kinapingana na haya, hilo linamaanisha kuwa jambo hilo lazima liwe limefutwa.

Nevasisimaia gazeta..religii, 2 June 1999

chanzo:http://www.edu/~psteeves/relnews/9906a.html#03

MAKASISI WAINGIA UISLAMU

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

 “Hakika utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu (wengine) kwa Waislamu ni Mayahudi na wale mushirikina (wasiokuwa na Kitabu), na utawaona walio karibu kwa urafiki na Waislamu ni wale wanaosema: “Sisi ni Wakristo.” (Hayo) ni kwa sababu wako miongoni mwao wanavyuoni na wamchao Mungu, na kwa sababu wao (Wakristo) hawatakabari; (wakijua haki huifuata). Na wanaposikia yaliyoteremshwa kwa Mtume (na yakawatulilikia kuwa ni kweli), utaona macho yao yanamiminika machozi kwa sababu ya haki waliyoitambua; wanasema: “Mola wetu! Tumeamini, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (ukweli huu).” (Na wakilaumiwa kwa kusilimu kwao husema): “Na kwa nini tusimwamini Mwenyezi Mungu na haki iliyotufikia, na hali tunatumai Mola wetu atuingize (Peponi) pamoja na watu wema?”

[QURANI TAKATIFU, Surah Al-Maidah 5:82-84]

KWA MAELEZO ZAIDI JUU YA MAPADRI, MAKASISI NA WAHUBIRI WANAOINGIA UISLAMU, TAFADHALI TEMBELEA TOVOTI HIZI:

HTTP://WWW.ISLAMTOMORROW.COM

HTTP://WWW.NEWMUSLIMS.TK

HTTP://WWW.THETRUELIGION.ORG

HTTP://WWW.WADEE3.5U.COM

 HTTP://WWW.ISLAMWAY.COM

S.A.W: REHEMA NA AMANI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE.

Makasisi Waingia Uislamu

 Vyombo vya habari vya kuupinga Uislamu vinawagawa Waislamu katika makundi yafuatayo:

“Magaidi” “Walipua Mabomu” Waporaji” na “Wateka Nyara”

Kwa hiyo, mtu atautazama vipi Uislamu?

Kwa nini mapadri na wahubiri wengi wanaingia Uislamu?

Haya ni maswali mazuri ambayo tutayatolea majibu.

“Salam Alaykum” yaani “Amani iwe juu yenu”

Hili kava limetengenezwa na

www.harunyahia.com

kwa ajili ya kitabu

(Yesu Atarejea)



[1] USA ni kifupi cha United States of Amerca yaani Marekani.

[2] Marrabi ni Wanazuoni au wakuu wa dini ya Kiyahudi.

[3] Mjumbe maalum wa kutangaza Ukristo katika maeneo yaisiyo ya Kikristo.

[4] Swahaba ni mfuasi wa Mtume Muhammad (S.A.W) aliyekuwepo zama za Mtume.

[5] Ni kifupi cha maneno ya Kiarabu na maana yake ni rehema na amani ziwe juu yake.

[6]  Ni kifupi cha maneno ya Kiarabu yenye maana Iwe juu yake amani.

[7] Tauhidi ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu, yaani kumfanya Mwenyezi Mungu Mpweke- yupo mmoja tu au ni somo la kumpwekesha Mwenyezi Mungu

[8] Tafsiri za aya za Quran kwa kiswahili zimenukuliwa kutoka QURANI TAKATIFU ya marehemu Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy

[9] Sunna ni maelezo yanayohusishwa na Mtume Muhammad (S.A.W), sawa yale aliyoyatenda, kuyasema au kuyakubali.