×
KITABU HIKI NIMIONGON MWA VITABU MUHIMU KATIKA ZAMA HIZI, KINAZUNGUMZIA ITIKADI POTOVU YA USHIA KUPITIA VITABU VYAO VINAVYO TEGEMEWA.

SHIA ITHNA ASHARIA NI WATU GANI?

MTUNZI: ABDULLAHI BIN MUHAMMAD [AS-SALAFY]

MFASIRI: YASSINI TWAHA HASSANI [KONGOLO] KIMEREJEWA NA: ABUBAKARI SHABANI RUKONKWA

SHIA ITHNA ASHARIA

NI

WATU GANI?

MTUNZI

ABDULLAHI BIN MUHAMMAD [AS-SALAFY]

MFASIRI:

YASSINI TWAHA HASSANI [KONGOLO] KIMEREJEWA NA: ABUBAKARI SHABANI RUKONKWA

UTANGULIZI

Ninaanza kwa kumshukuru Allah kisha kumtakia rehma na amani Mtume wa Allah pamoja na Ahli zake na Maswahaba zake na wote waliyo ongoka kupitia Muongozo wa Mtume amma baad.

Kitabu hiki ni miongoni mwa mfululizo wa vitabu Ambavyo ni Muhtasari vyenye malengo ya kuwabainishia Waislamu na kuwawekea wazi Itikadi za Mapote [Makundi] yaliyo potea ili wawe na Tahadhari na Makundi hayo hasa ukizingatia kuwa baadhi ya Makundi hayo sasa yameanza kuwa na Sauti na yamekuwa na Harakati za waziwazi katika kueneza Upotovu wao na Tumeanza mfululizo huu kwa kundi la [SHIA ITHNA ASHARIA] Hasa miongoni mwa Makundi mengi ya Kishia kwa sababu Kundi hili ndilo lenye kudhihiri zaidi.

Pia sababu nyingine iliyo pelekea kuanza na kundi hili ni kwa kuwa kundi hili Mara nyingi hunadi kuwa Madhehebu yao hayatofautiani na Madhehebu ya Ahlus-sunnah na wanadai kuwa wamedhulumiwa tu na kuzuliwa mambo ambayo sii kweli pia kundi hili linafanya Juhudi kubwa sana katika kutetea Itikadi yake na kusambaza Vitabu na Risala mbali mbali ili kueneza Madai yao pia kundi hili limekuwa likifuatilia Vitabu mbalimbali vya Wanachuoni wa Ahlus-sunnah na Kuvirudi wakati Juhudi hizi hatuzioni katika Makundi Mengine, Na kwakuwa Vitabu vya Kishia sasa vime'enea Ueneaji ambao Hatukuuzoea huko Nyuma na wamekuwa wakivieneza kwa njia mbali mbali kila Mahala, kutokana na sababu hizi zimetupelekea kuona Ulazima kuviweka Bayana na kubainisha Itikadi Potovu zilizomo ndani yake, Ambazo walijitahidi sana kuzificha Lakini Tunasema kama Alivyosema Msemaji Mmoja: (Tutakusimamishieni Hoja kupitia Vinywa Vyenu)!

Tunamuomba Allah Ainyanyue Bendera ya Sunnah na watu wake na Aidhalilishe Batwili na watu wake Allah peke yake ndie anayajua makusudio na ndie Mwenye kuongoza njia iliyo sawa. NB: Kuna baadhi ya Maneno Ambayo nimeongeza yanaumuhimu kwa Msomaji.

Yameandikwa na: ABDULLAHI BIN MUHAMMADI AS-SALAFY

Yame Tafsiriwa na: YASSINI TWAHA HASSANI (KONGOLO)

ASILI YA MADHEHEBU YAO

Miongoni mwa itikadi za Shia ithna asharia: ni kwamba wanakiri na kukubali kwamba Ushia Asiliyake ni Uyahudi uliotokana na myahudi anaitwa Ibnu sabai pia wanakiri kwamba Aly bin abi Twalib -Radhi za Allah zimwendee- aliwachoma moto pindi walipomfanya kuwa Mungu na akatangaza wazi wazi kuwa yuko mbali nao kabisa na yuko mbali na itikadi hiyo. Rejea kitabu: (Firaqu shia). cha An-nubukhty. ukurasa. (22). pia rejea kitabu: (Ikhtiyaaru marifatir-rijaal). cha Atwuusy. ukurasa wa. (107).

Nao wanasema vilevile na kukiri bali kujifakharisha kwa kuitwa jina la Raafidhwa. Rejea kitabu: (Biharul- anwaar). cha almajlisy. (65/97).

ITIKADI YAO JUU YA ALLAH

Wanasema: Hakika sisi (Mashia) Hatuungani nao (yaani hawaungani na Ahlus-sunnah) katika itikadi ya Mungu wala Mtume wala Imamu kwa sababu wao wanasema kwamba: Mungu wao ni Yule ambaye Muhammadi alikuwa ndio Mtume wake na Khalifa wa Mtume wake alikuwa ni Abubakari. Na sisi (Mashia) Hatumuitakidi Mungu huyo wala Mtume huyo bali sisi Tunaitakidi kwamba Mungu ambaye khalifa wa Mtume wake alikuwa ni Abubakari huyo sio Mungu wetu na wala huyo sio Mtume wetu. Rejea kitabu: (Al-anwaarun-nuumaaniyya). cha Niimatullahi Aljazaairy. (2/278).

Na katika itikadi zao wanasema kuwa: Allah hataonekana siku ya Qiyama na kwamba Allah hasifiwi kwa mahala wala kwa zama wala haashiriwi na kwamba yeyote atakaye sema kuwa Allah hushuka katika Mbingu ya dunia na kwamba ataonekana kwa watu wa peponi wamuone wazi wazi kama wanavyo uona Mwezi basi Mtu huyo anakuwa ni sawa na Kafiri. Rejea kitabu: (Aqaaidul- Imaamiyyah). cha Muhammad Ridhwaa Midhfar. ukurasa (58).

Na wanasema vilevile: hakika Mwenyezi Mungu atakapo msemesha mja wake siku ya Qiyama atakuwa Amejishika Kiunoni na mja nae Atasimama mbele ya Mola wake hali kajishika nae kiunoni huku akitajiwa Madhambi yake. Pakaulizwa: nini makusudio ya kujishika kiunoni? Akasema mpokeaji wa habari hii: Yule msemaji akajishika kiunoni kisha akasema: yaani hivi kama vile Mtu anavyoongea na ndugu yake katika jambo la siri kati yao. Tazama kitabu: (Al-usuulus-sitata ashara). kilicho hakikiwa na: Dhwiyaud-diin alhamuudy. ukurasa (203).

Na wanasema vilevile: Hakika Allah huteremka siku ya Arafa pindi Jua linapo pinduka Akaja Ardhini akiwa juu ya Ngamia akiwa kawaenea Watu wa Arafa Kuliani na Kushotoni. Angalia kitabu: (Al-usuulus-sitata ashara). Kilicho Hakikiwa na: Dhwiyaud-diin Alhamuudy. ukurasa (204).

Na wanasema: Kulielekea Kaburi ni Jambo la Lazima hata kama litakuwa haliko upande wa Qibla pia kulielekea kaburi la Mtume kwa Mwenye kulizuru ni sawa na kuelekea Qibla na huo ndio (Muelekeo wa Mwenyezi Mungu) yaani alio waamrisha watu kuuelekea katika hali hiyo. Angalia kitabu: (Biharul- Anwaar). cha Almajlisy. (101/369).

Na wanasema kuwa: (Aaah) ni jina miongoni Mwa Majina ya Allah yaliyo mazuri hivyo Mwenye kusema neno hilo anakuwa kamwita Allah kwa namna ya kuomba msaada. Angalia kitabu: (Mustadrakul-wasaail). cha Annuury at-twabrasy. (2/148).

Pia wanasema kuwa: Mwenyezi Mungu huwa anamzuru (kumtembelea) Husein bin Ally na kupeana naye mkono na Anakaa naye juu ya Kiti. Rejea kitabu: (Swahiifatul-Abraar). cha Mirza Muhammad taqy. (2/140).

ITIKADI YAO KUHUSU KUBADILISHWA QUR-ANI

Wanasema: Qur-an imebadilishwa na kwamba ni Pungufu na Qur-an ambayo ni sahihi anayo Almahdi wao anayesubiriwa kuja kwake. Miongoni mwa Wanachuoni wa Kishia walio weka wazi Itikadi hii ni: Ally bin Ibrahim Alqummy Pamoja na Niimatullahi Aljazaairy na Alfaidhul Kaashaany na Ahmad Attwabrasy na Muhammad Baaqir Almajlisy na Muhammad bin Nuumaan wanaye muita Almufiid na Abulhasan al-Aamily na Adnaan Albahraany na Yusuf Albahraany na Annuury Attwabrasy na Wengineo wengi. Tazama kitabu: (Ash-shia al-ithnaa asharia wa tahriiful-quran). cha Muhammad Sayf. Na kitabu: (Mauqifur-raafidhwa Minal-Quran) cha Mamadoo kaaraambiiry.

Na wanasema kuwa tamko: (Aali Muhammadi na Aali Ally) liliondolewa katika Qur-an. Tazama kitabu: (Minhaajul-baraati sharhu nahjul-balaaghah). cha Habibullah alkhuui. (2/216).

Na wanasema kwamba: hakuna aliye ikusanya Qur-an yote ispokuwa Maimamu. (yaani maimamu wa shia ithna asharia) na kwamba wao ndio wanajuwa Elimu yake yote. Tazama kitabu: (Usuulul-kaafy). cha Alkulayny. (1/228).

Na wanasema: Qur-an haiwezi kuwa ni hoja mpaka atakapo kuja Alqayyim wao. (Mahdy). Angalia kitabu: (Usuulul-kaafy). cha Alkulainy. (1/169).

Na wanasema: katika Qur-an kuna sura inaitwa: Suuratul-wilaaya ambayo inaanza hivi: (Enyi mlio amini ziaminini nuru mbili…) kwamba Othman bin Afani aliifuta sura hii kama wanavyo dai. Angalia kitabu: (Faslul-khitwaab fiitahriif kitaab rabbul-arbaab). cha An-nuur attwabrasy. ukurasa (18).

Na wanasema kwamba: kuna Msahafu unaitwa Mus-haf Faatwimah na kwamba Msahafu huyo ukubwa wake ni mfano wa Qur-an yetu mara tatu. Angalia kitabu: (Usuulul-kaafy). cha Alkulainy. (1/239).

Na wanasema: kauli ya Mwenyezi Mungu iliyopo katika suratil-Maida aya ya (67) Isemayo: (Ewe Mtume yafikishe yale yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola wako na kama hukufanya hivyo basi hujafikisha Ujumbe wake). Mashia wanasema: aya hii ilikuwa hivi: (Ewe Mtume yafikishe yale yaliyo teremshwa kwako -Kuhusu Ally- na kama hukufanya hivyo basi hujafikisha ujumbe wake) wakaongeza katika aya neno: (kuhusu Ally). Yaani kwamba Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Aliliacha huenda kwa kuwaogopa Wanafiki kama walivyo eleza katika vitabu vyao vingi tu. Angalia kitabu: (Faslul-khitwaab fiitahriif kitaab rabbul-arbaab). cha An-Nuur attwabrasy. ukurasa (182).

Na wanasema: Hawamkemei mwenye kusema kuwa Qur-an imebadilishwa bali mtu kama huyo wanamzingatia ni miongoni mwa Wanachuoni ambao ni Mujtahid ama mwenye kukanusha (Wilaya -Utawala baada ya mtume-) ya ally kwa mashia huyo anazingatiwa ni Kafiri tena ukafiri usio na shaka ndani yake. Tazama kitabu: (Al-iitiqaadaat). cha Ibnu Baabawayhi Alqummy. ukurasa (103).

Na wanasema: kuwa wamewaamrisha wafuasi wao kuisoma Qur-an hii tuliyo nayo katika Swala zao na Sehemu nyingine pamoja na kuzifanyia kazi hukumu zake mpaka atakapo kuja: (Maulaana Swahibuz-zamaan) yaani Mahdi ndipo Qur-an hii itaondoshwa na kunyanyuliwa Mbinguni na hapo itakuja Quran aliyo itunga Amiril-muuminina iwe ndio yenye kusomwa na kufuatwa hukumu zake. Tazama kitabu: (Al-an war Annuumaaniyyah). cha Niimatullahi Aljazaairy (2/363).

Na wanasema kuwa: Msiwafundishe wanawake Surati Yusuf wala msiwasomeshe sura hiyo maana ndani yake kuna Fitna lakini wafundisheni Suratin-nuur maana ndani yake mna Mawaidha. Rejea kitabu: (Al-furuu minal kafy) cha Alkulayny (5/516).

AL-IMAAMAH (MRITHI) KWAO NI NGUZO NA ASIYE AMINI NGUZO HII NI KAFIRI

Wanasema: Hakika asiye amini Al-imaamah basi Imani yake haikamiliki ispokuwa kwa kuitakidi na kuamini hivyo. Angalia kitabu: (Aqaaidul-imaamiyyah). cha Muhammad Ridhwaa midhfar. ukurasa (78).

Na wanasema: Hakika al-imaamah ni muendelezo wa Utume na nidalili inayo wajibisha kutumwa Mitume na kuwatuma Manabii jambo hili pia linawajibisha kuwepo na Imamu baada ya Mtume. Angalia kitabu: (Aqaaidul-imaamiyyah). cha Muhammad Ridhwaa midhfar. ukurasa (88).

Na wanasema: Makusudio yao kuhusu swala la Al-imaama ni kuwa hiki ni cheo cha KiMungu Allah anamchagua atakaye mpa cheo hiki miongoni mwa waja wake kutokana na Elimu yake ya tangu kama vile anavyo Mteua Mtume wake kuufahamisha umati wake juu ya huyo Imamu na kuwaamuru wamfuate. Angalia kitabu: (Aslush-shia wa Usuulihaa). cha Muhammad Hussein kaashiful-ghitwaa. ukurasa (102).

Bali itikadi hii ni katika mambo ya msingi katika dini na Haitimii Imani ya Mtu ispokuwa kwa itikadi hii. Na kwa Ibara nyingine wanasema: Hakika Imama ni kuendelea kwa Utume.

Na wanasema: Hakika Mwenye kupinga Uimamu wa Amiril-muuminina Ally bin Abi Twaalib Radhi za Allah ziwe juu yake na Maimamu wengine baada yake ni kama Mtu aliye pinga Unabii wa Manabii wa Allah na kwamba Mwenye kukiri Uimamu wa Ally lakini akampinga hata Mmoja miongoni mwa Maimamu baada yake ni sawa na Mtu aliye wakubali Mitume wote lakini akakanusha Utume wa Muhammadi -rehma na amani za Allah ziwe juu yake-. pia wanasema: Mwenye kupinga Uimamu wa yeyote miongoni mwa Maimamu kumi na mbili ni sawa na Mwenye kuwapinga Mitume wote. Angalia kitabu: (Minhaajun-najaat). cha Alfaidhul-kaashy. ukurasa (48).

*Majina kumi na mbili ya maimamu wa kishia: 1/Ally bin Abi Twalib. (Al-mur-tadhwa) 2/Hassan bin Ally. (Azzakii – al-mujtabaa) 3/Hussein bin Ally. (Shahiid) 4/Ally bin Hussein. (Zainul-aabidiyna) 5/Muhammad bin Ally. (Al-baaqir) 6/Jaafar bin Muhammad. (Aswaadiq) 7/Mussa bin Jaafar.(Al-kaadhwim) 8/Ally bin Mussa. (Arridhwah) 9/Muhammad bin Ally. (Al-jawaadu) 10/Ally bin Muhammad. (Al-haady) 11/ Hassan bin Ally. (Al-askary) 12/Muhammad bin Hassan. (Al-mahdy)

Na wanasema: kwa Mujibu wa makubaliano ya Imaamiyyah wote ni kwamba yeyote Mwenye kupinga Uimamu wa yeyote miongoni mwa Maimamu wao na akakanusha kutekeleza Utiifu ambao Allah kawajibisha juu yao basi mtu huyo ni Kafiri na nimpotevu na anastahiki kudumu Motoni Milele. Angalia kitabu: (Haqqul-yaqiin Fii Maarifat Usuulid-diin) cha Abdallah bishri (2/189).

Na wanasema: Hakika tamko la Shirki au Kufru kwa kila asiye itakidi Uimamu wa Amiril-muuminina na Maimamu wengine miongoni mwa watoto wake na akawafadhilisha Wengine juu yao Matamko haya yanamaanisha kuwa watu hao ni wenye Kudumu Motoni milele. Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar). cha Almajlisy. (23/390).

KUMKOSEA KWAO ADABU MTUME MUHAMMADI-REHMA NA AMANI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE- NA MABINTI ZAKE NA WATU WA NYUMBANI KWAKE.

Wanadai kuwa: Pindi Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Alipo zaliwa alikaa Masiku kadhaa hana Maziwa ya kunyonya basi Abuu Twaalib Akamuweka katika Maziwa yake Allah akateremsha ndani yake maziwa hivyo Akanyonya kwa siku kadhaa mpaka Abuu Twalib Alipo mpata Halimatu Saadia na kumkabidhi ili Amnyonyeshe. Angalia kitabu: (Usuulul-kaafy). cha Alkulayny. (1/448).

Na wanasema kwamba: Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- Alikuwa ni Shujaa kuliko Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Bali Mtume hakupewa Ushujaa asilani. Angalia kitabu: (Al-an war annuumaaniyyah). cha Niimatullahi Aljazaairy. (1/17).

Na wanasema: Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Alikuwa hawezi kulala Mpaka Abusu Paji la Uso wa Faatwima (Binti yake) au kifua chake Kunyonya Maziwa!!!. Angalia kitabu: (Bihaarul-Anwaar). cha Al-majlisy. (42/43).

Na wanasema: Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Hakuwa na Mabinti ispokuwa Faatwima ama Ruqayyah na Ummu kulthum na Zainabu hawa ni watoto walio lelewa kwake tu. Angalia: (Daairatul-maariful-islaamiyyatu ash-shiiyyah) (1/27). *Mtume wetu Muhammad-rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Alikuwa na watoto saba wakiume wa tatu na wakike wa nne: 1/Qasim. 2/Abdullahi. 3/Ibrahim. 4/Zainabu. 5/Ruqayyah. 6/Ummu kulthum. 7/Faatwima.

Na wanasema kwamba: Hassan bin Ally-radhi za Allah ziwe juu yao- yeye ndie Aliwadhalilisha Waumini kwa sababu Alimbaayii (Alimpa kiapo cha utiifu) Muawiya-radhi za Allah ziwaendee. Angalia kitabu: (Rijaalul-kashy). cha Alkashy. ukurasa (103).

KUWAKUFURISHA KWAO MAMA WA WAUMINI: BI AISHA NA BI HAFSWA

Mashia wanasema: Hakika Mke wa Mtume anaweza akawa ni Kafiri kama alivyokuwa Mke wa Nabii Nuhu na Mke wa Nabii Lutwi. Wanamkusudia katika kusema hivyo Mke wa Mtume-rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Bibi Aisha Allah amuwie radhi. Angalia kitabu: (Hadiithul-ifki) cha Jaafar Murtadhwa. Ukurasa (17).

Na wanasema kwamba: Bibi Aisha Allah amuwie radhi Aliritadi Baada ya kufa Mtume-rehma na amani za Allah ziwe juu yake- kama walivyo ritadi wengi miongoni mwa Maswahaba. Angalia kitabu: (Ash-shihaabuthaaqib Fii bayaani maanan-naaswib). cha Yusuf al-bahraany ukurasa (236).

Na wanasema kwamba: Bibi Aisha-radhi za Allah ziwe juu yake- Alikusanya Dinari (40) kutokana na khiyana na Akazigawa kwa watu wenye kumchukia Ally -radhi za Allah ziwe juu yake-!. Angalia kitabu: (Mashaariqu anwaaril-yaqiin). cha Rajab Albisry. ukurasa (86).

Na wanasema kuwa: Bibi Aisha-radhi za Allah ziwe juu yake- Alifanya Faahisha (Zina) na kwamba kauli ya Allah katika suratin-nuur aya (26) Aliposema: {Hao ni wenye kutakaswa na hayo wayasemayo} wakasema: aya hii Imekuja kumtakasa Mtume-rehma na amani za Allah ziwe juu yake- kutokana na Zina na sio Bibi Aisha. Angalia kitabu: (Aswiraatul-mustaqiim). cha Zainud-diin An-nabatwi Albayaadhwi. (3/165).

Na wanasema kwamba: Bibi Hafsa-radhi za Allah ziwe juu yake- Alikufuru kwa kauli yake alipo Muuliza Mtume: {Nani kakupa habarihizi}?. Kama ilivyo kuja katika suratu Tahrim aya (3). Na ndipo Allah Akateremsha kuhusu yeye pamoja na Bibi Aisha kauli yake: {Ikiwa Mtatubia kwa Allah bila shaka nyoyo zenu zimekwisha elekea huko}. suratu Tahrim aya (4).

Wanasema: Neno: (Zaaghat) lina maana ya Ukafiri. Na wanadai kuwa Bibi Aisha pamoja na Hafsa walikubaliana kumnywesha Sumu Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- na pindi Allah alipo Mueleza Mtume wake njama zao akataka kuwauwa ndipo wakamuapia kuwa Hawakufanya hivyo na ndipo Allah akateremsha ayah ii: {Enyi mlio Kufuru Msitake Udhuru leo hii… } suratu Tahrim aya (7). Angalia kitabu: (Aswiraatul-mustaqiim). cha Zainud-diin An-nabatwi Albayaadhwi (3/168).

KUCHUPA KWAO MIPAKA KWA ALLY-RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE.

Wanasema: Hakika Allah Alimsemesha Mtume wake -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Usiku wa Miiraji kwa Lugha ya Ally bin Abi Twalib. Angalia kitabu: (kashful-yaqiin Fii Fadhwaaili Amiiril-muuminiin). cha Hasan bin Yusuf bin Al-mut-har Alhuly. ukurasa (229).

Na wanasema kuwa: Allah Alimsemesha Ally bin abi Twalib katika Mji wa Twaifu Akiwa pamoja na Jibril. Angalia kitabu: (Baswaairud-darajaat). cha Swaffaar. (8/230).

Na wanasema: Hakika Ally bin abi Twalib -radhi za Allah ziwe juu yake- Ndiye Mwenye kugawa Pepo na Moto!! Atawaingiza watu wa Peponi Peponi na watu wa Motoni Motoni!!!. Angalia kitabu: (Baswaairud-darajaat). cha Swaffaar). (8/235).

Na wanasema: Hakika Allah Atamuingiza Peponi Mwenye kumtii Ally hatakama atamuasi Allah! Na Allah atamuingiza Motoni Mwenye kumuasi Ally hatakama atamtii Allah!. Angalia kitabu: (Kashful-yaqiin Fii Fadhwaaili Amiiril-muuminina). Cha Hasan bin Yusuf Al-mut-har al-huly. Ukurasa (8).

Na wanasema: Hakika Ally bin Abi Twalib -radhi za Allah ziwe juu yake- Ndie siri ya Manabii na kwamba Allah Alimwambia Mtume wake: {Ewe Muhammadi hakika nilimtuma Ally pamoja na Mitume wengine kwa siri na nimemtuma pamoja Nawe kwa Dhahiri". Angalia kitabu: (Al-asraarul-alawiyya). Cha Muhammad Al-mas-uudy. Ukurasa (181).

Na wanasema kwamba: Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- ni Alama na Dalili ya Muhammadi na Muhammadi-rehma na amini za Allah ziwe juu yake- Alilingania juu ya Utawala wa Ally. Angalia kitabu: (Baswaairud-darajaat). cha Swaffaar. Ukurasa (91).

Na wanasema kwamba: Allah hakuwahi kumtuma Mtume yeyote Ispokuwa Alimtaka kuutambua Utawala wa Ally kwa kupenda au kwa kukarahishwa. Angalia kitabu: (Al-asraarul-alawiyya). Cha Muhammad Al-mas-uud. Ukurasa (190).

Na wanasema kuwa: Hakika Dini ya Mtu haikamiliki ispokuwa kwa kuutambua Utawala wa Amiril-muuminina Ally bin Abi Twalib. Angalia kitabu: (Al-ihtijaaj). Cha Attwabrasy. (1/57).

Na wanasema: Hakika Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Alisema: "Sikilizeni Jibril Alinijia akanambia: {Ewe Muhammadi Mola wako anakuamrisha Umpende Ally bin Abi Twalib na Anakuamrisha Kuutambua Utawala wake}. Angalia kitabu: (Baswaairud-darajaat). cha Swaffaar. Ukurasa (92).

Na wanasema: Ally bin Abi Twalib Ataingia Peponi kabla ya Muhammadi -rehma na amani za Allah ziwe juu yake-Angalia kitabu: (Ilalush-sharaai). Cha Ibnu Baabawayhi Alqummy. Ukurasa (205).

Na wanasema kuwa: Radi ni katika Amri ya kipenzi chenu alipo ulizwa Msemaji nani kipenzi chetu? Akasema: Amiril muuminina Ally bin abi Twalib. Angalia kitabu: (Al-ikhtiswaas). Cha Almufiid. Ukurasa (327).

Wanasema kuwa: Ally bin abi Twalib -radhi za Allah ziwe juu yake- Anauwezo wa Kufufua na Kuondoa Matatizo kwa wenye Matatizo. Angalia kitabu: (Uyuunul-muujizaati). Cha Husein Abdul-wahaab. Ukurasa (150). Na Risala (Halaalul-mashaakil).

Na wanasema: Hatoingia Peponi yeyote ispokuwa kwa Idhni ya Ally bin abi Twalib. Angalia kitabu: (Manaaqibu Amiril-muuminina). Cha ally bin Maghaazily. Ukurasa (93).

Na wanasema kuwa: kila Mwenye kum-khaalifu Ally basi huyo ni Kafiri na kila Mwenye kumfadhilisha Yeyote juu yake basi huyo anakuwa Karitadi. Angalia kitabu: (Bishaaratul- mustwafaa lishiiatil- murtadhwaa). (2/79).

Na wanasema kuwa: Mwenyezi Mungu Alijifakharisha Mbele ya Malaika wake kwa ajili ya Ally bin abi Twalib. Angalia kitabu: (Bishaaratul- mustwafaa lishiiatil- murtadhwaa). (1/66).

Wanasema: Manabii wote na Mitume walitumwa hali yakuwa wameamrishwa kukiri Utawala wa Ally bin abi Twalib. Angalia kitabu: (Al-maalimuz-zulfaa). Cha Shekh wao Haashimul-bahraany. Ukurasa (303).

Na wanasema: Ally bin abi Twaalib -radhi za Allah ziwe juu yake- Aliashiria kwa mkono wake Angani mara likatanda Wingu na Mawingu yakapandana kisha yakamtolea Salamu kisha Ally Akamwambia Ammar: Panda Pamoja nami na Useme: "Bismillahi Majreeha wamursaahaa". Kama ilivyo kuja katika suurat Huud aya (41). Ammar Akapanda kisha wakatoweka machoni kwetu. Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar). Cha Almajlisy.

Na wanasema kuwa: Mbwa Aliwang`ata Maswahaba wawili kwa ajili ya kumlipizia kisasi Ally bin abi Twaalib na kwamba Punda Alishuhudia kuwa Ally ni Walii wa Allah na ndie aliepewa wasia wa utawala baada ya Mtume - rehma na amani za Allah ziwe juu yake-. Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar). Cha Almajlisy. (41/247). Na (17/306).

KUCHUPA KWAO MIPAKA KWA FAATWIMA RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE

Wanasema kama: Fatwima na Hassan na Husein na wengine miongoni mwa kizazi cha Husein, ni maasuumin (Hawakosei). Angalia kitabu: (Aqaaidul-imaamiyya). Cha Muhammad ridhwaa. Ukurasa (89) na (98).

Na wanasema: Lau kama sio Ally basi Muhammad-rehma na amani za Allah ziwe juu yake- asingeumbwa, na lau kama sio Fatwima basi nisingelikuumbeni. Angalia kitabu: (Al-asraarul-faatwimiyya). Cha Muhammad almas-uudy. Ukurasa (98).

Na wanasema: Hakika Faatwima ni sehemu ya Uungu! Utukufu wangu nimeudhihirisha katika umbile la Mwanamke. Angalia kitabu: (Al-asraarul-faatwimiyya). Cha Muhammad Almas-uudy. Ukurasa (355).

Na wanasema kuwa: Faatwima alikuwa akiongea na Mama yake huku akiwa tumboni mwake. Angalia kitabu: (faatwimatu zahraa minal-mahdi ilal-lahdi). Cha Muhammad alqaz-wiiny. Ukurasa (38).

KUWAFADHILISHA KWAO MAIMAMU WAO JUU YA MANABII PAMOJA NA KUCHUPA KWAO MIPAKA

Mashia wanasemakuwa: Hakika Maimamu wa Shia ithna asharia ni bora kuliko Manabii na Mitume -rehma na amani za Allah ziwe juu yao-. Angalia kitabu: (Al-anwaarun-nuumaaniyya). Cha Niimatullahi aljazaairy. (3/308).

Na wanasema: Hakika Maimamu wa Shia wana Elimu ya yaliyo kuwepo na yatakayo kuwepo na kwamba hakifichikani kwao kitu chochote (yaani wanajua ghaibu) na kwamba wao hawafi ispokuwa kwa kutaka kwao. Angalia kitabu: (Usuulul-kaafy). Cha Alkulayny. (1/258-260).

Na wanasema: Hakika Imamu katika Maimamu wao anayo Daraja yenye kusifiwa mbele ya Allah na anao utawala ambao unanyenyekewa na kila kitu hapa Ulimwenguni. Angalia kitabu: (Tahrirul-wasiila). Cha Al-khumainiy. Ukurasa (52).

Na wanasema: Hakika Maimamu wao Kumi na mbili wanao Utawala usio kuwa kwa viumbe wote na kwamba utawala huo ni sawa na utawala wa Allah kwa viumbe wake. Angalia kitabu: (Misbaahul-fuqaaha). -Cha Abul-qaasim al-khuui. (5/33).

Na wanasema: Hakika sisi kwa Allah tunazo hali (yaani Maimamu wao kumi na mbili) hali ambazo hazipati yeyote si Malaika alie karibu wala Mtume alie tumwa. Angalia kitabu: (Tahrirul-wasiila). Cha Al-khumainiy. Ukurasa (94).

Na wanasema: Hakika Maimamu kumi na mbili Hakuna Pingamizi kabisa kuwa Mambo ya Ulimwengu yanaenda kwa Idhini yao na kuwa wanaipitisha lailatul-qadri na mengineyo na Hakuna Pingamizi kabisa kuwa jambo hili limethibiti. Angalia kitabu: (Al-burhaanul-qaatwii). Ambacho ni mkusanyiko wa majibu na mambo ya kiitikadi na sheria. cha shekh wao: Muhammad taqiyyul-bahjat. Ukurasa (41).

Na wanasema: Hakika mawaswii (Yaani Maimamu kumi na mbili wa kishia) Wanabebwa tumboni na wanatoka kwenye mapaja lakini hawaguswi na Uchafu (wakati wa kuzaliwa). Angalia kitabu: (Madiinatul-maajiz). cha Haashimul-bahrany. (8/22).

Na wanasema: Hakika Allah na Malaika wake na Mitume wake pamoja na Waumini huwa wana zuru kaburi la Ally bin Abi Twalib. Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy). Cha Alkulayny. (4/580).

Na wanasema: Imamu ni kama Nabii ni lazima awe kaepushwa na mambo yote machafu ya dhahiri na ya siri tangu utotoni mwake mpaka kufa kwake ya kufanya kwa kukusudia au hata kwa kusahau kwa kuwa Maimamu ndio wenye kuihifadhi sheria na wenye kuisimamia halizao katika hili ni kama hali ya Mitume. Angalia kitabu: (Aqaaidul-imaamiyya). Cha shekh wao: Ibrahim zanjaany. (3/179).

Na wanasema: Malaika wameumbwa ili kuwa watumishi wa Ahlul-baiti. Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar). Cha Almajlisy. (26/335).

KUWAKUFURISHA KWAO MASWAHABA WOTE ISPOKUWA WATATU TU MIONGONI MWAO

Mashia wanasema: Maswahaba wote watukufu Wamekufuru na Kuritadi kiongozi wa kuritadi alikuwa ni Abubakari na Omari na Othman na Khalid bin waliid na Muawiya bin Abi Sufyaan na Mughiirat bin Shuubah -radhi za Allah ziwe juu yao- Ispokuwa watatu tu katika Maswahaba. Angalia kitabu: (Ar-raudhwatu minal-kaafy). Cha Alkulayny. (8/245).

CHUKI ZAO JUU YA ABUBAKARI NA OMARI NA OTHMANI –RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAO

Mashia wanasema: Na imani yetu katika kuwatenga nikwamba tunajitenga mbali na Masanamu wanne: Abubakri na Omari na Othmani na Muawiya pamoja na wanawake wanne: Aisha na Hafswa na Hindu na Ummul-hakam (Dada yake na Muawiya) na tunajitenga mbali kabisa na wafuasi wao wote na tunaitakidi kuwa wao ni viumbe waovu kabisa miongoni mwa viumbe wa Allah juu yamgongo wa Ardhi na tunaamini kwamba haiwezi kutimia imani ya mtu kumuamini Allah na Mtume wake na Maimamu ispokuwa kwa kujiweka mbali kabisa na maadui zao. Angalia kitabu: (Haqqul-yaqiin). Cha Almajlisy. Ukurasa (519).

Na wanasema: Hakika Abubakari na Omari ni Makafiri, na kila Mwenye kuwapenda naye ni Kafiri. Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar). Cha Almajlisy. (69/137-138).

Na wanasema: Abubakari na Omari wamelaaniwa na wamekufa wakiwa ni makafiri, nani wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu mtukufu. Angalia kitabu: (Baswaairud-darajaat). Cha As-swaffaar. (8/245).

Na wanasema: Sababu iliyompelekea Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- kwenda na Abubakari Pangoni ilikuwa ni kuchelea asije kuwafahamisha Makafiri wa Kikuraishi Mahala alipo. Angalia kitabu: (Tafsiirul-burhaani). Cha Haashimul-bahraany. (2/127).

Na wanasema kwamba: Abubakari alikuwa akiswali nyuma ya Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- hali yakuwa Kaning'iniza Sanamu Shingoni mwake kisha analisujudia. Angalia kitabu: (Al-anwaarun-nuumaaniyyah). Cha Niimatullahil-jazaairy. (1/53).

Na wanasema: Omari alikuwa na Maradhi ambayo tiba yake ni Maji ya Wanamume (Yaani Mpaka Aingiliwe nyuma)! Na kwamba Bibi yake ni Motto wa zinaa. Angalia kitabu: (Al-anwaarun-nuumaaniyyah). Cha Niimatullahil-jazaairy). (1/63). Na kitabu: (Aswiraatul-mustaqiim). Cha Zainud-din annabatwy albayadhwy. (3/28).

Na wanasema: Tunaitukuza siku ya Tairuuz nisiku ambayo Majusi huitukuza (Baniani) na kuisheherekea siku aliyo uwawa Omari bin Khatwaab -radhi za Allah ziwe juu yake- na wana Mwita alie Muuwa Omari kuwa ni (Baba shujaa wa dini) na wanahimiza kulizuru kaburi lake kutokana na kazi kubwa aliyo ifanya ya kumuuwa Omari -radhi za Allah ziwe juu yake. Angalia kitabu: (Aqdu durar Fii Baqri Batnu Omar). Cha Yaasin As-swawaaf. Ukurasa (120).

Na wanasema: Kusoma dua ya kuwalaani Masanamu wawili wa Kiquraishi (Abubakari na Omari) ni katika Ibada tukufu za kujikurubisha nazo kwa Allah, na wamemwita abubakari na omari kuwa ni Aljibti na Twaaghuuti (Jibti ni Uchawi Twaaghuti ni Shetani). Angalia kitabu: (Ihqaaqul-haqq). Cha Al-mar-ashy. (1/337).

Na wanasema kwamba: Mahdi wao wauongo atamfufua Abubakari na Omari, Awasulubu na kisha kuwachoma Moto kisha Amfufue Bibi Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- na Amsimamishie Hadd. (Adhabu kwa Sababu ya zinaa). Angalia kitabu: (Ar-raj-a). cha Ahmad al-ahsaani. Ukurasa (1116) na (161).

Na wanasema: Hakika Othmani -radhi za Allah ziwe juu yake- Alikuwa ni Mzinifu na Khanithi na alikuwa ni Mpiga Dufu. Angalia kitabu: (As-siraatul-mustaqiim). Cha Zainud-diin annabtwy albyaadhwy. (3/30).

KUHUSU MAHDI WAO WA KUZUA NA KAULI ZAO JUU YA KUREJEA KWAKE

Na Wanasema kuwa: Jibril na Miikaail na Kursy na Lauhil-mahfuudh na Kalamu vyote hivi ni vyenye kudhalilika na kumnyenyekea Mahdi wa kishia, sababu sifayake ni Saffah (M-mwagaji damu). Angalia kitabu: (Aqaaidul-imaamiyya). Cha Muhammad ridhwaa midhfar. Ukurasa (102).

Na wanasema Kuwa: kiwiliwili cha Mahdi wa kishia ni kiwiliwili cha Israaili. (Chaguo la Mungu). Angalia kitabu: (Al-imaamul-mahdy minal wilaadati iladh-dhuhuur). Cha Muhammad qazwiiny. Ukurasa (53).

Na wanasema kuwa: Mahdi wa Mashia atakuja na Amri Mpya na Kitabu Kipya na Hukumu Mpya na Atakuwa ni Mkali sana kwa Waarabu hatokuwa na uamuzi juu yao zaidi ya Upanga tu Hatampa Nafasi yeyote ya kutubia wala hato'ogopa lawama ya mwenye kulaumu kwaajili ya Allah. Angalia kitabu: (Al-ghaibah). Cha Muhammad an-nuuman. Ukurasa (154).

Na wanasema: Pindi atakapo kuja Mahdi hakutakuwa kitu kati yake na Waarabu na Maquraishi, ispokuwa Upanga tu. Angalia kitabu: (Al-ghaibah). Cha Muhammad an-nuuman. Ukurasa (154).

Na wanasema: Haikubakia baina yetu na Waarabu ispokuwa Kuchinjana kisha msemaji akaashiria Shingoni mwake. Angalia kitabu: (Al-ghaibah). Cha Muhammad an-nuuman. Ukurasa (155).

Na wanasema kwamba: Mahdi wao atakapo kuja Atauvunja Muskiti wa Makkah na Muskiti wa Madina na Atahukumu kwa Sheria ya watu wa Daawud na Atamsemesha Allah kwa jina lake la Kiebrania sihivyo tu bali Atauwa Theluthi mbili ya watu wa Ardhini. Angalia kitabu: (Biharul-anwaar). Cha Al-majlisy.(52/338). Na kitabu: (Uswuulul-kaafy). Cha Al-kulainy. (1/397). Na kitabu: (Alghaibah). Cha Annuumaany. Ukurasa (326). Na kitabu: (Arraj'a). cha Ahmad al-ahsaai. Ukurasa (51).

Na wanasema: Jihadi haifai wala hairuhusiwi mpaka atakapo kuja Mahdi wao wakudai kutoka katika Pango lake. Angalia kitabu: (Wasaailush-shia). Cha Al-hurr al-aamily. (11/37).

KUCHUPA KWAO MIPAKA KULIKO KUBAYA KATIKA IBADA ZA MAKABURI

Mashia wanasema kuwa: Kulizuru kaburi la husein bin Ally ni bora kuliko kwenda Kuhiji Makkah si hivyo tu bali wanasema kuwa wanao kwenda kumzuru Husein ni watakasifu ama wanao kuwa katika Mauqifu (Arafa) katika Hijja ni Watoto wa Zinaa. Angalia kitabu: (Biharul-anwaar). Cha Al-majlisy. (98/85).

Na wanasema: Hakika kulizuru kaburi la Husein bin Ally-radhi za Allah ziwe juu yake- Nisawa na kufanya Hijja Milioni mbili (2,000,000) na Umra Milioni mbili (2,000,000) na kupigana Jihadi Milioni mbili (2,000,000) na Thawabu za kila Hijja na Umra na Jihadi ni sawa na Thawabu za Aliye Hijji na akafanya Umra na akapigana Jihadi Pamoja na Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Pamoja na Maimamu waongofu. Angalia kitabu: (Nuurul-ayni fil-mashyi ilaa ziyaarati qabril-husaini). Cha Muhammad al-istwihbaanaaty. Ukurasa (265).

Na wanasema kwamba: Karbalaa (Alipo zikwa Husaini) ni Ardhi takatifu katika Uislamu na ina Utukufu kushinda Makkah na Madina na kuliko hata Baitul-maqdis. (Muskiti wa palestina). Angalia kitabu: (Misbaahul-jinaani). Cha shekh wao Abbaas al-kaashaany. Ukurasa (360).

Na wanasema kuwa: Kula Udongo ulipo katika Kaburi la Husein -radhi za Allah ziwe juu yake- ni Shifaa (Dawa) ya kila Ugonjwa. Angalia kitabu: (Almizaar) cha Shekh wao Almufiid. Ukurasa (125).

Pia wanasema kwa uongo na uzushi kuwa: Abu abdillahi (Jaafar As-swaadiq) -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Amesema: Wallahi laiti kama ninge kusimulieni juu ya Fadhila za kulizuru kaburi la Husein na juu ya ubora wa kaburi lake basi mgeliacha kufanya Hijja moja kwa moja na hakuna yeyote miongoni Mwenu ambaye ange fanya Hijja, olewako! Hivi hujuwi kama Allah kaifanya Ardhi ya Karbalaa (Aliko zikwa Husein) kuwa ni Haram (Sehemu takatifu) yenye amani na yenye kubarikiwa kabla ya kuifanya Makkah kuwa ni Haramu?!. Angalia kitabu: (Kaamiluz-ziyaaraat). Cha shekh wao Ibnu quuluwayhil-qummy. Ukurasa (449).

Na wanasema: Hakika kuswali katika Mashaahid zao (Makaburi) ni bora kuliko kuswali Miskitini bali wanasema: swala katika Msikiti wa Ally bin Abi Twalib malipo yake ni makubwa kuliko kuswali katika Msikiti Mtakatifu wa Makkah.!! Angalia kitabu: (Manhajus-swaalihiina). Cha Shekh wao Ally as-sistaany. (1/187).

Na wanasema kuwa: Hakika Sikukuu kubwa katika Uislamu sio Eidul-fitri wala Eidul-adhwhaa bali ni Eidi ya (Ghadiir) Eidi ya kizushi wala haina asili katika Uislamu. Angalia kitabu: (Eidul-ghadiir). Cha Shekh wao Muhammad ash-shiiraazy. Ukurasa (11). *Ghadiir: Ni sehemu Baina ya Makkah na Madina sehemu ambayo Mtume alimsifu Ally…

KUWAPENDA KWAO MAKAFIRI NA KHIYANA ZAO NA UDANGANYIFU WAO

Mashia wanasema: Na miongoli mwa makosa waliyo yafanya watu wa Kuufa, nikwamba wao walimchoma choma Visu Hassan bin Ally na wakamuuwa Husein -radhi za Allah ziwe juu yao- Baada ya kuwa walimwita. Angalia kitabu: (Taariikhul-kuufa). Ukurasa (113).

Na wanasema: Hakika Husein Alisema: Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba Uhukumu Baina yetu na baina ya watu walio Tuita ili watunusuru waka Tuuwa. Angalia kitabu: (Muntahal-aamaal). (1/535).

Na wanasema: Husein alisema: Hakika watu hawa wamenihofisha (Yaani mashia wa kuufa -iraqi) Nahizi hapa Barua za watu wa kuufa nao ni wenye Kuniuwa. Angalia kitabu: (Maqtalul-husaini). Cha Abdurrazzaaq almuqrim. Ukurasa (175).

Na wanasema kwamba: Ally bin Husein -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- Aliwaona watu wa Kuufa Wakiomboleza na Kulia, Akawaambia: Mnaomboleza na Kulia kwa Ajili Yetu! Ni nani Aliye Tuuwa??(Bila kua nyinyi).Angalia kitabu: (Nafsul-mahmuum). Cha Abasi al-qummy. Ukurasa (357).

Na wanasema: kisha wakampa Husein Baia (Utawala) katika watu wa Iraq, watu elfu ishirini (20,000) kisha wakamtelekeza na wakamtokea pamoja na viapo vyao, vya utiifu wakamuuwa. Angalia kitabu: Aa'yanush-shia). Cha Muhsinul-amiin. (1/32).)

Na wanasema: Niwaajibu kuwanusuru Maaduwi wanao Shambulia Dola (Nchi) ya Kiislamu nakuto waziwiya Makafiri wanao Washambulia Waislamu. Angalia: Fat'wa Aliyoitowa kiongozi wao Mkubwa: As-sistaany. Tarehe: (4/3/2003). Baada ya Marekani kuishambulia Iraq. Na kutilia Mkazo jambo hilo Anasema shekh wao Swaadiq Ash-shiirazy, Anaye ishi Irani: Nilazima kusaidiana Na Marekani katika kuangusha Utawala wa Iraq. Angalia: (Jariidatul-watwaniyya al-kuwaitiyya-al-jumua) (27/9/2002).

Na wanasema: Hakika Muislamu yeyote Mwenye kupigana Jihadi dhidi ya Makafiri basi Anahesabiwa ni Muuwaji Hapa Duniani na Akhera. Hakuna anaekufa Shahidi Ispokuwa Shia Imaamiyya, Hata akifia kitandani kwake. Angalia kitabu: (Tahdhiibul-ahkaam). Cha Atwuusy. (6/98).

KUICHUKIA KWAO MAKKAH NA MADINA

Mashia wanasema: Hakika watu wa Makkah wanamkufuru Mwenyezi Mungu wazi wazi, na watu wa Madina niwaovu kuliko watu wa Makkah, niwaovu zaidi yao mara sabini (70). Angalia kitabu: (Usuulul-kaafy). Cha Alkulainy. (2/410).

CHUKI ZAO KWA MISRI NA SHAM

Wanasema kuwa: Watu wa Misri wamelaaniwa kwa Ulimi wa Daaud, na miongoni mwao wamegeuzwa kuwa Manyani na Nguruwe. Na wanasema kuwa: Allah hakupata kuwakasirikia wana wa Izraail ispokuwa aliwaingiza (Misri) na pindi alipokuwa Radhi nao basi aliwatoa humo. Na wanasema kwamba: Abu Jaafar Imamu wao ambaye wanasema ni Maasuumu (Hafanyi dhambi) Alisema: Hakika Mimi nachukia kula kitu chochote kilicho pikwa katika vyungu vya Misri, wala sipendi kuosha kichwa changu kutokana na Udongo wake, usije kuniambukiza Udhalili na kuniondolea Ghera (wivu) wangu, Jitengeni na Misri wala msitamani kuishi humo. Pia nadhani alisema: kuishi katika nchi hiyo kunamrithisha mtu tabia ya Udayuthi (kuridhia maasi). Angalia kitabu: (Tafsiirul-qummy). Cha Alqummy. (2/241). Na kitabu: (Tafsiirul-bur-haan). Cha Hashimul-bahraany. (1/456). Na kitabu: (Furuu minal-kaafy). Cha Alkulainy. (6/501) Na kitabu: (Bihaarul-anwaar). Cha Almajlisy. (60/211).

Na wanasema: Bora ya Ardhi ni ardhi ya Sham, na watu wa baya ni watu wa Sham. na watu wa Roma walikufuru lakini hawakutufanyia Uaduwi, lakini watu wa Sham walikufuru na wakatufanyia Uaduwi, na wala msiseme: sisi niwatu wa Sham lakini semeni sisi niwatu wa sehemu mbaya. Angalia kitabu: (Tafsiirul-bur-haan). Cha Hashimul-bahraany. (1/456). Na kitabu: (Usuulul-kaafy). Cha Alkulainy. (2/410). Na kitabu: (Tafsiirul-qummy). Cha Alqummy. (2/241).

ULAJI WAO WA KHUMUS (MOJA YA TANO) KWA VIGOGO WAO WAVAAJI WA VIREMBA VIKUBWA

Mashia wanasema kuwa: Mali ya Khumus, (mali ikigawiwa mafungo matano fungo moja ndio linaitwa khumus) Ambayo ni maalumu kwa watu wa Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yao- wanapaswa kuichukuwa watu wa Viremba (vigogo wao) kwa hoja kwamba wao wanasimamia nafasi ya Imamu wao aliye jificha kwenye Pango. Angalia kitabu: (Wasaailush-shia). Cha Alhurrul-aamily. (6/383).

WANADAI KUJIPIGA MAKOFI NA KUJICHOMA VISU NI MIONGONI MWA MAMBO YA KUJIKURUBISHA

Mashia wanadai kuwa: Kujipiga piga Makofi na Kujichoma visu na kuvaa mavazi Meusi siku ya Ashura na kuomboleza ni miongoni mwa mambo Makubwa ya kujikurubisha kwa ajili ya Husain -radhi za Allah ziwe juu yake- na kwamba matendo hayo ni katika matendo mazuri. Angalia fataawa za Muhammad kaashif Alghitwaa, na Ar-rauhany, na At-tabrizy. na rejea nyingi miongoni mwa rejea za al-imaamiyyah.

KUHIMIZA KWAO MUT'A NA KUSTAREHE NA WANAWAKE MAKAHABA

Mashia wanasema: Mtu anaweza kuowa (kwa ndoa ya Mut'a) mpaka mara Elfu moja, (1000) kwa sababu Mwanamke wa Mut'a hapewi Talaka wala hana Mirathi, bali anahesabiwa ni Mwenye kukodiwa tu. Angalia kitabu: (Al-istibswaar). Cha Abii Jaafari atwuusy. (3/155).

Na wanasema: Hakika Mtoto aliye zaliwa katika Mut'a ni bora kuliko aliye zaliwa katika Ndoa ya kudumu. Angalia kitabu: (Manhajus-swaadiqiin). Cha Almulla fat-hullah al-kaashaany. Ukurasa (356).

Na wanasema kuwa: Inajuzu kufanya Mut'a na Wanawake wazinifu na ambao ni maarufu kwa (Uchangudoa-Ukahaba) bali wanadai kuwa kumepokelewa Mahimizo juu ya jambo hilo.! Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar). Cha Almajlisy. (100/319-320).

Na wanasema kwamba: Mwanamke wa kufanya nae Mut'a Haesabiwi katika Ile idadi ya Wanawake Wanne, kwa sababu yeye Haachwi kwa kupewa Talaka wala hana haki ya Mirathi, bali yeye ni Mwenye kukodiwa tu. Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy). Cha Alkulainy. (5/415).

Na wanasema: Inajuzu kufanya Mut'a na Wanawake Warembo hata kama watakuwa Wameolewa, au hatakama ni Wazinifu. Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy). Cha Alkulainy. (5/462).

Na wanasema kuwa: Uchache wa muda wa Mut'a ni kustarehe na Mwanamke mara moja tu. Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy). Cha Alkulainy. (5/460).

Na wanasema kwamba: Inajuzu kufanya Mut'a na Mwanamke Mzinifu hata kwa Kumlazimisha hasa akiwa ni miongoni mwa Wanawake Maarufu kwa Ukahaba. Angalia kitabu: (Tahriirul-wasiilah). Cha Khumainy. (2/256).

TAQIYYA NA KUSEMA UONGO NI KATIKA ASILI YA MADHEHEBU YAO

Mashia wanasema: Inajuzu kutumia Taqiyya na maana yake ni: (Mtu kudhihirisha mambo ambayo ni kinyume na vile anavyo itakidi moyoni) au kama alivyo eleza mmoja wa wanachuoni wao kwamba taqiyya nikusema au kufanya kinyume na unavyo itakidi kwa lengo la kujiondolea madhara au kulinda heshima yako. Angalia kitabu: (Ash-shiatu fil-miizaan). Cha Muhammad Jawaadu Maghniyah. Ukurasa (48).

Na wanasemakuwa: Sehemu kubwa ya Dini ni Taqiyya, wala hana Dini asie kuwa na Taqiyya. Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy). Cha Alkulainy. (2/217).

Na wanasema: Hakika Nyinyi mko katika Dini ambayo Mwenye kuificha basi atampa utukufu na Mwenye kuiweka wazi basi Mwenyezi Mungu Atamdhalilisha. Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy). Cha Alkulainy. (2/222).

Na wanasema: Hakika Husein Alikuwa akinyonya kidole cha Mtume -rehma na amani za Allah ziwe juu yake- kiasi cha kumtosha siku mbili mpaka tatu. Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy). Cha Alkulainy. (1/465).

KUWAKUFURISHA KWAO WAISLAMU PAMOJA NA CHUKI ZAO KUBWA JUU YA WAISLAMU

Mashia wanasema kuwa: Hakuna yeyote aliyopo katika Mila ya Kiislamu zaidi yetu (Yaani Maimamu wa Ithna Ashariyya Pamoja na Wafuasi wao miongoni mwa Shia Imaamiyya). Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy). Cha Alkulainy. (1/223-224).

Na wanasema kwamba: Mahdi wao Atarejea ili aje kuwalipizia kisasi Mashia kutoka kwa Maaduwi zao ambao ni Waislamu, ama Mayahudi na Wakristo wao Atafanya nao Suluhu na kuwasalimisha. Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar). Cha Almajlisy. (52/376).

Na wanasema kuwa: Mwenye kuturudi Sisi ni sawa na Mwenye kumrudi Allah, na anakuwa ni sawa na aliye mshirikisha Allah. Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy). Cha Alkulainy. (1/67).

Na wanasema kuwa: Watu wote ni Watoto wa Zinaa Ispokuwa Mashia tu. Angalia kitabu: (Arraudhwatu minal-kaafy). Cha Alkulainy. (8/285).

Na wanasema: Hakika Mtoto yeyote anapo zaliwa Ibilisi miongoni mwa Maibilisi huwa anahudhuria kuzaliwa kwake, Pindi anapojuwa kuwa Mwenye kuzaliwa ni Miongoni Mwetu, Basi huwa anamkinga kutokana na Shetani, na kama atakuwa mwenye kuzaliwa sio katika sisi basi Shetani humuingiza kidole Matakoni mwake akiwa ni kijana. na kwa ajili hiyo anakuwa ni Mwenye kuziniwa!!!, Na akiwa ni wakike basi hutia kidole chake katika Utupu wake (Sehemu ya siri ya mbele)!!! Na kwa ajili hiyo anakuwa ni Muovu. Angalia kitabu: (Tafsiirul-ayaashy). Cha Muhammad al-ayaashy. (2/218).

Na wanasema kwamba: Hakika yeyote ambaye sio katika Shia ithna asharia, au asiye muamini hata mmoja miongoni mwa Maimamu kumi na mbili, au akamkanusha hata mmoja wao, basi huyo ni Kafiri, na Akhera mafikio yake ni Motoni. Angalia kitabu: (Jaamiu ahaadiithi shia). Cha Alburuujirdy. (1/429).

Na wanasema: Hakika habari zinafidisha juu ya hukumu ya Ukafiri na Ushirikina huko Akhera kwa kila ambaye sio katika Shia ithna asharia. Angalia kitabu: (Tanqiihul-maqaal). Cha Abdallah Almaamaqany. (1/208).

CHUKI ZAO KWA AHLUS-SUNNA ZIMEPITA KIWANGO

Mashia wanasema: Hakika Naaswib (yaani Muislamu) damu yake ni halali, lakini mimi nakuepushia shari, ikiwa utaweza kumuangushia Ukuta, au Kumzamisha kwenye Maji, ili asije kukutolea ushahidi basi fanya hivyo, akauliza muulizaji: na vipi Mali yake? Akasema: Ichukuwe, ikiwa kama kuna uwezekano.! Angalia kitabu: (Wasaailu sh-shia). Cha Alhurrul-Aamaly. (18/463).

Na wanasema: Hakika Diya ya Sunni (yaani pindi Akiuliwa) ni sawa na Diya ya Beberu, na Beberu nibora kuliko Yeye. na Diya yao hailingani na Diya ya ndugu yao Mdogo ambaye ni Mbwa wa kuwinda, wala hailingani na ya ndugu yao Mkubwa ambaye ni Myahudi. Angalia kitabu: (Al-anwaarun-nuumaaniyyah). Cha Niimatullahi Aljazaairy. (3/308).

Na wanasema: Chukuwa mali ya Naaswib (Muislamu) Popote utakapo ipata na utupatie sisi Khumusi tu. (Moja ya tano). Angalia kitabu: (Wasaailu sh-shia). Cha Alhurrul-Aamaly. (6/340).

Na wanasema: Hakika siku ya Qiyama, mema waliyo yafanya Ahlus-sunnah watapewa Shia, na makosa waliyo yafanya Shia watapewa Ahlus-sunnah, kisha watupwe Motoni. Angalia kitabu: (Bihaarul-anwaar). Cha Almajlisy. (5/247-248).

Na wanasema: Ahlus-sunnah ni najsi (Wachafu) na Damu zao ni halali na Mali zao piya, na kwamba wao ni watu wa Motoni, na wala hawatatoka ndani ya Moto. Angalia kitabu: (Al-anwaarun-nuumaaniyyah). Cha Niimatullahi aljazaairy. (2/306). Na kitabu: (Haqqul-yaqiin Fii Maarifati Uswuulud-diin). Cha Abdallah Bishri. (2/188).

Na wanasema: Shia akimwita Mshia mwenzake (Ewe sunni) basi ana adhibiwa, na imethibiti juu yake kisheria kupewa adhabu itakayo mpa fundisho. Angalia kitabu: (hayaatul-muhaqiq alkarkry wa aatharuhu). (6/237).

UZUSHI WA MASHIA

Mashia wanadai kuwa: Eti kundi miongoni mwa Malaika walizozana kuhusu jambo Fulani, kisha wakamtaka mwanaadamu awe muamuzi baina yao, Allah akawateremshia wahyi, kuwa chaguweni kati ya Wanaadamu, wakamchaguwa Ally bin Abiitwalib. Angalia kitabu: (Musnad faatwima). Cha Husein Attuwaisir kaany. Ukurasa (296).

Na wanasema kwamba: Punda aitwae (Ghufair) alimsemesha Mtume -rehma na amani za Allah ziwe zuu yake- Akamwambia: Namtowa Fidia Baba yangu na Mama yangu, hakika Baba yangu Alinisimulia kutoka kwa Baba yake, kutoka kwa Babu yake, kutoka kwa Baba wa Babu yake, kwamba: Alikuwa na Nabii Nuhu katika Safina (Jahazi) Nabii Nuhu akasimama kisha Akampakusa katika Matako yake, kisha Akasema: Atatoka katika Mgongo wa Punda huyu, Punda ambaye atapandwa na Bwana wa Mitume wote na wa Mwisho wao, hivyo namshukuru Allah aliye nijaalia kuwa Mimi ndiye Yule Punda.!!! Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy) Cha Alkulainy. (2/237).

Na wanasema kuwa: Imamu wao Albaaqir Alitengeneza Tembo wa Udongo kisha Akampanda Yule Tembo, akaruka naye mpaka Makkah.!!! Angalia kitabu: (Madiinatul-maajiz). Cha Haashimul-bahraany. (5/10).

Na wanasema: Mikojo na Mavi ya Maimamu wao hamna Uchafu wowote wala Harufu mbaya, bali ni kama Miski (Mafuta uzuri namba moja) na Mwenye Kunywa Mikojo ya Maimamu wao na Mavi yao na Damu zao Allah Atamziwiya kuingia Motoni, na ata Muingiza Peponi. Angalia kitabu: (Anwaarul-wilaaya). Cha A'ayatullah Al-aakhundi Mulaa zainul-Aabidiina alkalbaaikaany. Ukurasa (440).

Na wanasema: Hakika Ushuzi na Mavi ya Maimamu zao vina harufu kama ya Miski.!!! Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy). Cha Alkulainy. (1/319).

Na wanasema: Kuvaa Viatu vyeusi kunasababisha mambo matatu, Nikasema: Nimambo gani hayo? Akasema: kunasababisha: Kudhoofika kwa nuru ya Macho, na kurefusha dhakari (Sehemu ya siri inakuwa ndefu) na kunamjengea Mtu kuwa na Huzuni. Angalia kitabu: (Uswuulul-kaafy). Cha Alkulainy. (6/465).

Na wanasema: Kuvaa Viatu vya njano kunasababisha mambo matatu: kunaleta nuru ya Macho, na kuikomaza Dhakari, na kuondowa Huzuni. Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy). Cha Alkulainy. (6/465).

Na wanasema: Kula Karoti kunachemsha Bandama, na kusimamisha Dhakari (sehemu ya siri) na kunaongeza Nguvu za tendo la ndoa. Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy). Cha Alkulainy. (6/372).

Na wanasema: Hakika Sheitwani huwa anakuja na kumkalia Mwanamke kama vile Mwanamume anavyo mkalia, na yanatokea kama yale yanayo tokea kwa Mwanamume. Nikasema: yanajulikana vipi hayo? Akasema: Yanajulikana kwa kutupenda sisi na kutuchukia, Mwenye kutupenda anakuwa ni Tone la Mja, na Mwenye kutuchukia anakuwa ni Tone la Shaitwani. Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy). Cha Alkulainy. (5/502).

Na wanasema: Uchi upo aina mbili (Wa mbele na wa nyuma) ama Uchi wa nyuma huo umekingwa na matako, hivyo ukimsitiri Bwana Mkubwa (Dhakar) na Mapumbu mawili, Tayari unakuwa Umekwisha stiri Uchi. Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy). Cha Alkulainy. (6/501).

Na wanasema: Ama aina nyingine za kujifurahisha kama vile Kumshika shika Mwanamke, Kumkumbatia, kuchezea Mapaja yake, sio Vibaya Hatakama ni Mtoto Mchanga. Angalia kitabu: (Tahriirul-wasiilah). Cha Khumainy. (2/221).

Na wanasema: Inaruhusiwa Kumuingilia Mwanamke wakati wa Hedhi (Akiwa kwenye siku zake) Kabla Hajaoga (Yaani kabla Haja Jitwaharisha). Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy). Cha Alkulainy. (5/395).

Na wanasema: Inasuhusiwa Kumuingilia Mwanamke Kinyume na Maumbile (Sehemu ya Nyuma). Angalia kitabu: (Alfuruu minal-kaafy). Cha Alkulainy. (5/540).

Na wanasema: Mwanamke akiwa katika Hedhi Anaruhusiwa Kuswalia Jeneza, Lakini hakai pamoja nao katika safu. Angalia kitabu: (Manlaa yahdhuruhul-faqiih). Cha Ibnu Baabawaihi Alqummy. (1/179).

Mwisho kabisa Tunasema: Rehma na amani za Allah zimuendee Mbora wa Viumbe Mtume wetu Muhammadi Pamoja na watu wa Nyumbani kwake na Maswahaba zake na Woote watakao fuata Mwenendo wake mpaka siku ya Malipo. Haya ndiyo ambayo tume jaaliwa na Allah kuyaandika katika Kitabu hiki, kuhusiana na Habari za Mashia (Ithna asharia) Ambao wameeneya kwa kasi katika Nchi zetu za Africa ikiwemo: Tanzania, Kenya, Uganda, Congo, na Burundi, … Bila kuusahau Mkoa wa Kigoma! Umevamiwa na Mashia!!! Juhudi za Daawa zina Hitajika.

TOVUTI MUHIMU ZINAZO WARUDI RAFIDHWA (SHIA) ITHNA ASHARIA

http://www.dd-sunnah.net

http://www.fnoor.com http://www.albrhan.com

http://www.wylsh.com

http://www.khomaiy.com

http://www.dhr12.com

http://www.albainah.net

http://www.ansar.org

http://www.almanhaj.com

http://www.isl.org.uk

http://www.almhdi.com

VITABU MUHIMU VYA KUWARUDI RAAFIDHWA (SHIA) NAKUNASIHI KUWA NAVYO

1- Fataawa Sheikhul-islam ibnu Taimiyyah. 2- Minhaajus-sunnah Sheikh ibnu Taimiyyah. 3- Almilalu wannihalu Cha Shahristaany. 4- Alfarqu bainal-firaq Cha Al-baghdaady. 5- Maqaalaatul-islaamiyyiin Cha Al-ash-ary.

VITABU VYA WANACHUONI WA ZAMA HIZI 1- Vitabu vyote vya Sheikh Ihsaan ilahi dhwahiir. 2- Mas-alatu ttaqriib. Sheikh dr: Naswir alqifaary. 3- Uswulu madh-habi shia al-ithnaa ashariyyah. Sheikh dr: Naswir alqifaary. 4- Vitabu vyote vya Sheikh Muhammadi maalullah. 5- Badhlul-majhuud fii mushaabahatir-raafidhwa lil-yahuud. Cha Abdallah al-jumaily. 6- Hattaa laa nankhadia. Cha Abdallah almuuswily. 7- Ashiatul-ithnaa ashariyyatu watakfiiruhum liumuumil-muslimiin. Cha Abdallah assalafy. 8- Man qatalal-husain. Cha Abdalla bin Abdul-aziiz. 9- Alburhaan fii tabriati abi hurairata minal-buhtaan. Cha Abdallah An-naaswir. 10- Al-intiswaaru lis-swahabi wal-aali. Cha dr: Ibrahimu Ar-ruhaily. 11- Kashful-jaanii muhammadut-tiijaany. Cha Sheikh Othman Khamis. 12- Bai dhwalalta fii raddi abaatwiilit-tiijaany. Sheikh Khalid Al-asqalaany.

13- Ma'al-ithnai ashariyyah fil-uswuli wal-furui. Cha dr: ally As-saaluus. 14- Tabdiidudh-dhwalaami watanbiihun-niyaami alaa khatwarit-tashayyui alal-muslimiina wal-islaami. Cha Sheikh Sulaiman Aljabhaan. Navingine vingi hivi nilivyo vitaja ni kwa muhtasari tu.