×
Kitabu hiki kinazungumzia: Umuhimu na ubora na uzito wa funga ya mwezi wa Ramadhan kwa mujibu wa Aya na Hadithi za Mtume wetu Muhammad (s.a.w) pia kimezungumzia juu ya mambo yanayo tengua swaumu.

    UKUMBUSHO KWA WAFUNGAJI.

    Kiswahili

    Kimeandikwa na :

    Yasini Twaha Hassani

    Kimepitiwa:

    Yunus Kanuni Ngenda.

    تذكير الصائمين

    السواحلية

    تأليف: شيخ ياسين طــه

    راجعه: شيخ يونس كنوني

    ----------------------------------------------

    بسم الله الرحمن الرحيم

    UTANGULIZI

    Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake Nyingi ambazo hazina Idadi na Mwenyezi Mungu ambae katujaalia kuufikia mwezi mtukufu wa ramadhani mwezi wenye neema mbali mbali, mwezi ulio faradhishwa ndani yake funga, Rehma na Amani zimuendee kiongozi wetu muombezi wetu Mtume Muhammad (s.a.w), pamoja na Familia yake na Maswahaba zake na Waislamu wote watakao fuata Mwenendo wake mpaka siku ya Mwisho Mungu atujaalie nasi tuwe Miongoni Mwahao AMIN.

    Ndugu zangu katika iman katika kurasa hizi chache tutakumbushana badhi ya mambo yanayo husiana na funga ya mwezi mtukufu wa ramadhani ili Muislamu aijuwe funga na yepi yasiofaa ili aichunge funga yake na vinavyo funguza.

    Tunaanza kutaja dalili ndani ya Qur-ani inayo wataka waislamu kufunga.

    Kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu (Enyi mlio amini! Mmelazimishwa kufunga, kama walivyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu* Siku maalum za kuhisabika. Na atakaekuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha maskini. Na atakae fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua* Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Quran kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi.

    Basi atakae kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru). Al-Baqara: (183-187).

    Hadithi zilizo pokelewa kuhusu funga na fadhila zake ni nyingi mno tutakumbushana badhi yake tu.

    1: Kutoka kwa Bibi Aisha (ﷺ‬.a), amesema: (Ilikuwa swaumu inayo pendezwa zaidi kwa Mtume Muhammad (s.a.w), kuifunga Shabani kisha anafuatanisha Ramadhani). Kapokea hadithi hii Imam Abuu Daudi (2431), na Annasai (4/199), na kaisahihisha Sheikh Albani, swahihi Nnasai (2214), na Al-Baihaqy katika sunani (4/483).

    Anatukumbusha mama yetu mke wa Nabii Muhammad (s.a.w), ya kwamba ilikuwa desturi ya Mtume Muhammad (s.a.w), kufunga katika mwezi wa shabani siku kadha, kama ilivyo pokelewa katika upokezi mbali mbali ima kufunga siku (15), au zaidi ya (15), au chini ya (15), njia zote zimethibiti kutoka kwa nabii Muhammad (s.a.w), kisha anafunga mwezi wenye Baraka wa Ramadhani. Yatupasa na sisi wafuasi wake utapo fikia mwezi wa shabani tuwe tunafunga sunna kwa wingi ili tupate radhi za Allah.

    2: Kutoka kwa Abahuraira (ﷺ‬.a), amesema: amesema Mtume Muhammad (s.a.w), (Funga ilio bora bada ya Ramadhani ni funga katika mwezi mtukufu wa Muharram, na swala ilio bora bada ya swala za faradhi ni swala za usiku). Kapokea hadithi hii Imam Muslim (1163).

    Kapokea swahaba mtukufu Abahuraira kutoka kwa mtume Muhammad (s.a.w), ya kwamba swaumu bora kabisa katika swaumu alizo ziamrisha Mwenyezi Mungu ni swaumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mwezi wenye kheri nyingi sana na Baraka, kisha swaumu inayo fuatia kwa ubora ni swaumu katika mwezi wa Muharam (mwezi wa kwanza kiislamu). Mwezi ambao ndani yake kunapatikana swaumu ya Ashura, swaumu ambayo alikuwa nabii Muhammad (s.a.w), akiifunga na kuwaamrisha waisilamu waifunge, na mwezi wa Muharam nikatika miezi mine mitukufu, mwezi ambao Mwenyezi Mungu kamuangamiza fir-auli na kumuokoa nabii Mussa (s.a.w).

    3: Kutoka kwa Aba Huraira (ﷺ‬.a), amesimulia ya kwamba amekuja bedui kwa Mtume Muhammad (s.a.w), akasema: Ewe Mtume wa Allah: nionyeshe matendo ambayo nikiyafanya ntaingia peponi, akasema: (Unamuabudu Mwenyezi Mungu na wala usimshirikishi na chochote, na kusimamisha swala za faradhi, na kutoa zakka, na kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani), jamaa akasema: naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ambae nafsi yangu ipo mikononi mwake sintozidisha chochote kuhusu haya milele, na wala sinto punguza chochote, alipo ondoka akasema Mtume Muhammad (s.a.w): (Yeyote anaetaka kumuona mtu wa peponi amuangalie huyu).

    Kapokea hadithi hii Imam Bukhari fathulbari (3/1397), na Muslim (14), na tamshi ni la kwake.

    Anasimulia Aba Huraira (ﷺ‬.a), ya kwamba kaja bedui mtu asioishi mjini kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w), akimtaka elimu ya mambo akiyafanya itakua nisababu ya kuingia peponi, kiongozi wa umma Nabii Muhammad (s.a.w), akamwambia ya kwamba:

    Muabudu Mwenyezi Mungu pekeyake na wala usimshirikishe katika ibada zake na chochote, pia udumu katika ibada ya swala tano za faradhi, kwa sababu siku ya kiyama kitacho anza kuhesabiwa katika matendo ni swala, kisha matendo mengine.

    Pia akamwambia awe anatoa zakka katika mali yake ili Mwenyezi Mungu ailinde na kuihifadhi, na laity matajiri wa kiislamu wangelikua wakitoa zakka inavyo stahiki mafakiri na masikini katika jamii ya waislamu ingelipungua kiasi kikubwa sana, lakini wapowapi wenye kutekeleza nguzo ya zakka ni wachache mno, mwisho kibisa aliambiwa awe anafunga mwezi mtukufu wa Ramadhani mwezi wenye Baraka nyingi na kheri mbali mbali, mwezi wa Quran, mwezi wa taraweh, mwezi wa itikafu, mwezi wa lailatul-qadri, mwezi wakuachwa huru na moto wa jahannam. Bedui alipo sikia hayo kutoka kwa nabii Muhammad (s.a.w), akaondoka zake huku akisema: Ewe mtume wa Allah mambo ulio nambia tayafanyia kazi kama ulivyo nambia tafanya ibada kama alivyo amrisha Allah na wala sintomshirikisha katika ibada zake na kuswali kama ulivyo tufundisha na kutoa zakka pia kuufunga mwezi wa Ramadhani, bedui bada ya kuondoka kwake Mtume Muhammad (s.a.w), akasema kuwaambia maswahaba walio kuwepo pale ya kwamba yeyote anaetaka kumuona mtu wa peponi akiwa anatembea katika mgongo wa ardhi amuangalie huyu!!!.

    4: Kutoka kwa Abdullahi Ibn Omar (ﷺ‬.a), amesema: nimemsikia Mtume Muhammad (s.a.w), akisema: (Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano: Kushahidilia ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokua Mwenyezi Mungu Mmoja tu, na Muhammad (s.a.w), ni Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zakka, na kuhijji, na kufunga mwezi wa Ramadhani). Kapokea hadithi hii Imam Bukhari fat-hulbaari 1(8) na Muslim (16).

    Abdallah mtoto wa Omar (ﷺ‬.a), amemsikia Nabii Muhammad (s.a.w), akielezea nguzo za uislamu ni tano:

    1: Kukubali kwa moyo na kutamka kwa ulimi ya kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokua Mwenyezi Mungu Mmoja tu, hana mshirika katika uungu wake hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hafanani na chochote, na kukubali kwa moyo na kutamka kwa ulimi ya kwamba Nabii Muhammad (s.a.w), ni mja wake na mjumbe wake.

    2: Kusimamisha swala tano, Alfajiri, Adhuhuri, Laasiri, Magharibi, Ishaa, kila kipindi kwa wakati wake, kujitahidi kuswali kama alivyo kuwa akiswali Nabii Muhammad (s.a.w), na maswahaba zake.

    3: Kutoa zakka kwa wale wenye uwezo ili wawasaidie wasio kuwa na uwezo wajikimu kimaisha, masikini na mafakiri wapunguwe katika jamii ya waislamu.

    4: Na kwenda kufanya ibada ya Hijja kwa mwenye uwezo njia ipo wazi kabisa, muislamu ukiwa na uwezo nenda makkah ukatekeleze nguzo ya hijja uone namna watu wanavyo muabudu Mwenyezi Mungu.

    5: Kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani mwezi wa kheri na Baraka mwezi wakusaidiana sana mwezi wenye fadhila zaajabu mwezi wa kuhurumiana na kupendana mwezi wa taraweh na qurani, mwezi wakuachwa huru na moto wa jahannam.

    6: Kutoka kwa Bibi Aisha (ﷺ‬.a), amesema: Hamza ibn Amru aslamy alimuuliza mtume Muhammad (s.a.w), kuhusu kufunga safarini?. Akajibu:

    (Ukitaka funga na ukitaka fungua). Kapokea hadithi hii Imam Bukhari fat-hulbaari: 4 (1943), na Muslim (1121), na tamko nila kwake.

    Bibi Aisha (ﷺ‬.a), anasimulia ya kwamba mmoja katika maswahaba wa nabii Muhammad (s.a.w), akiitwa Hamza alimuliza mtume Muhammad (s.a.w), kuhusiana na hukumu ya kufunga ndani ya safari, Mtume Muhammad (s.a.w), akatoa ufafanuzi mzuri kabisa kwa kusema: ukitaka funga na ukitaka kula. Ndugu zangu msafiri afahamu ya kwamba kapewa kibali na Mwenyezi Mungu pamoja na nabii Muhammad (s.a.w), afahamu ya kwamba yupo huru akitaka anafunga na akitaka anafungua kwa maana anakula mchana wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kisha siku alizokula atazilipa bada ya Ramadhani.

    BADHI YA MAMBO YANAYO HARIBU SWAUMU:

    1: Kufanya tendo la ndo mcha wa mwezi wa Ramadhani, yeyote atakae fanya kitendo hicho nijuulake kafara nzito: kumuacha mtumwa huru, au kufunga miezi miliwi mfululizo, au kuwalishiza maskini (60).

    2: Kula kwa makusudi, yeyote alie funga akala kwa kukusudia swaumu yake nibatili, lakini akila kwa kusahua aendelee na swaumu yake itakua sahihi.

    3: Kunywa kwa makusudi, yeyote alie funga akanywa kwa makusudi swaumu yake nibatili, lakini akinywa kwa kusahau aendelee na swaumu yake itakua sahihi.

    4: Mwanamke aliefunga mwezi mtukufu wa Ramadhani kabla ya jua kuzama damu ya hedhi ikatoka, afahamu ya kwamba swaumu yake imeharibika.

    MANENO YA WANACHUONI KUHUSU FUNGA:

    1: Kutoka kwa Ally (ﷺ‬.a), amesema: (Kufunga sio kujiziwia na kula na kunywa, lakini ni kujiziwia na uongo na mambo ya batili na upuuzi).

    Muswannif libn abii shaiba: (2/422).

    2: Amesema Jabir bin Abdillahi (ﷺ‬.a): (Utapo funga basi nayafunge masikio yako na macho yako na ulimi wako kutokana na uongo na madhambi, na kuto muudhi mfanya kazi, nauwe na utulivu na upole wakati wakufunga kwako, na wala usijaalie siku ya kufunga kwako na siku ya kula kwako kuwa sawa). Bukhari fat-hu: 4(1947), na Muslim: (1116). Na tamshi nilakwake.

    MIONGONI MWA FAIDA ZA FUNGA:

    1: Ahadi na bishara na kufaulu kwa kuipata pepo.

    2: Husafisha nafsi na nikinga kwa mwili.

    3: Huvuna mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kumtii.

    4: Ni dalili ya mtu kuwa mwema na kuwa na msimamo.

    5: Funga ni ngao ya kumziwia mtu na kuto ingia katika mambo yaliyo haramishwa.

    6: Huleta unyenye kevu mbele ya Mwenyezi Mungu.

    7: Ndani yake kuna kupambana na shaitwani.

    8: Ndani yake kuna kuhisi maumivu yanayo mfika fakiri na mgonjwa.

    Haya ndio badhi ya mambo yanayo husiana na funga tumekusudia kukumbushana katika kurasa hizi chache, tunamuomba Mwenyezi Mungu kwa Rehma zake na Baraka zake atupe kila la kheri atuepushe na kila shari, atusamehe madhambi yetu atupe mwisho mwema awasamehe waislamu walio tangulia mbele ya haki ajaalie kaburi zao kua busatani za peponi. Aamin.