HUKU YA MUZIKI NA DALILI YA UHARAMU WAKE NA QAULI ZA WANACHUONI KUHUSU MUZIKI
Jamii ya vilivyomo
Full Description
حكم الغناء
أدلة تحريمه وأقوال بعض العلماء فيه
شيخ الإسلام ابن تيمية رحمه الله الإمام ابن القيم رحمه الله الإمام ابن القيم رحمه الله
HUKUMU YA MUZIKI DALILI ZA UHARAMU WAKE NA MANENO YA BAADHI YA WANACHUONI KATIKA HILO SHEIKHUL-ISLAM IBNU TAIMAYYA IMAM IBNUL-QAYYIM SHEIKH ABDUL-AZIZ BIN BAAZ ALLAH AWAREHEMU
KIMEFASIRIWA NA SHEKH YUNUS KANUNI KIMEREJEWA NA SHEKH YASINI TWAHA
Sifa njema zote zinamstahiki Allah, na Rehma na Amani zimwendee Mtume wa Allah. Ama baad.
Muziki pamoja na kuusikiliza ni haramu na ni uovu mkubwa, na ni miongoni mwa magonjwa ya moyo, na ukakamavu wa moyo. Na wameelezea baadhi ya wanachuoni juu ya makubalano ya uharamu wake.
DALILI ZA UHARAMU WA MUZIKI |
Dalili za kuharamisha muziki ni nyingi sana tutataja baadhi, na miongoni mwazo:
1-DALILI YA KWANZA: |
Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا أُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُهِينٌ (6) وَإِذَا تُتْلَى عَلَيْهِ آيَاتُنَا وَلَّى مُسْتَكْبِرًا كَأَنْ لَمْ يَسْمَعْهَا كَأَنَّ فِي أُذُنَيْهِ وَقْرًا فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ (7)}. (لقمان: 6-7).
Na miongoni mwa watu wapo wanao nunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu katika njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kufedhehesha.
Na (mtu kama huyo) anaposomewa Aya zetu huzipa mgongo kwa kujivuna, kama kwamba hakuzisikia, kama kwamba masikioni mwake kuna uziwi. Basi mbashirie kuwa atapata adhabu chungu (iumizayo). "Surat Luqman: 6-7.
Amesema Al-wahiid na wengineo: Kwamba wafasiri wengi wamesema juu ya (maneno ya upuuzi) hapo katika Aya kusudio lake ni Muziki. Ameyasema hayo Ibn Abas, na Ibun Masuud, na ndio kauli ya Mujaahid na Ikrima.
Na imepokelewa kutoka kwa Ibn Msuud kasema: Naapa kwa jina la Allah ambae hakuna Mola ila yeye, huo ni muziki yaani maneno ya upuuzi.
DALILI YA PILI: |
Ni kutoka katika Sunna: Kauli ya Mtume Swalla LLahu alayhi wa sallam.
(ليكونن من أمتي أقوام يستحلون الحر والحرير والخمر والمعازف)
Watatokea katika umma wangu watu (ambao) watahalalisha zinaa na hariri na pombe na ala (nyenzo) za miziki. Ameipokea Imamu Bukhari.
Cha kuzingatia katika dalili hiyo ni kwamba ala za miziki ndiyo nyenzo za mambo ya kipuuzi yote, wala hakuna utofauti baina ya watu wa lugha katika hilo.
Na kauli yake Mtume swalla LLahu alayhi wa sallam, "Wanahalalisha" maana yake ni jambo lilokua la haramu wakalifanya kuwa la halali.
DALILI YA TATU: |
عن أبي هريرة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «يمسخ قوم من هذه الأمة آخر الزمان قردة وخنازير»، قالوا: يا رسول الله أليس يشهدون ألا إله إلا الله وأن محمدًا رسول الله؟ قال: «بلى، ويصومون ويصلون ويحجون»، قالوا: فما بالهم؟ قال:«اتخذوا المعازف والدفوف والقينات فباتوا على شربهم ولهوهم فأصبحوا وقد مسخوا قردة وخنازير».
Kutoka kwa Abuu Hurayra radhi za Allah ziwe juu yake, ya kwamba Mtume (s.a.w) amesema: (Umma huu katika zama za mwisho kuna watu zitageuzwa kuwa nyani na nguruwe) wakasema ewe Mtume wa Allah: Hivi watu hao hawakiri ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad (s.a.w) ni Mtume wake? Akasema: (Wanakiri na wanafunga na wanaswali na wanahiji) wakauliza: Basi wana nini (watu hao)? Akasema (Wame zifanya ala (nyenzo) za miziki na ngoma nyimbo wakabobea katika ulevi wao huo upuuzi wao huo, wakajikuta wamegeuzwa kuwa manyani na manguruwe).
DALILI YA NNE: |
Ni kauli ya Allah Mtukufu:
{وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِنْدَ الْبَيْتِ إِلَّا مُكَاءً وَتَصْدِيَةً}
Na haikua ibada yao kwenye hiyo nyumba isipokua ni kupiga miunzi (miruzi) na makofi. Basi onjeni adhabu kwa yale mliyokua mkikufuru. (Surat Al-Anfaal: 35).
Amesema Ibn Abas na Ibn Omar na Atwiyyah na Mujaahid na Dhwihaak na Hassan na Qataada: Kwamba neno MUKAA katika hiyo Aya maana yake ni sauti za juu (fujo), na neno TASWDIYAH maana yake ni kupiga makofi.
BAADHI YA KAULI ZA WANACHUONI: |
Amesema Sheykhul Islam Bun Taymiyah: "Na katika mambo yanayotia nguvu hali za kishetani ni muziki na upuuzi, nazo ni nyimbo za washirikina. Anasema Allah Mtukufu:
{وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِنْدَ الْبَيْتِ إِلَّا مُكَاءً وَتَصْدِيَةً}
Na haikua ibada yao kwenye hiyo nyumba isipokua ni kupiga miunzi (miruzi) na makofi. Basi onjeni adhabu kwa yale mliyokua mkikufuru. (Surat Al-Anfaal: 35).
Amesema Ibn Abas na wengineo: Kwamba neno "TASWDIYAH" katika Aya hiyo ni kupiga makofi kwa mikono, na neno "MUKAA" maana yake ni sauti za juu (fujo), basi washirikina walikua wakifanya ibada hii. Ama Nabii wetu Muhammad (s.a.w) na Maswahaba wake Ibada yao ni ile aliyowaamrisha Allah waifanye, kama vile Swala, kusoma Qur'an, kufanya Dhikri na mfano wa hizo, na hakukusanyika Mtume (s.a.w) na Maswahaba zake kwaajili ya kusikiliza au kuimba nyimbo au muziki kamwe, siyo kwa kupiga makofi wala kwa kupiga ngoma (dufu).
Kisha akasema kwa mwenye kusikiliza nyimbo: Kwamba hali yake ya kwenda kinyume na kustarehe kwa kusikiliza nyimbo kunamfanya apunguze kusikiliza Qur'an na kupata nguvu ya kusikiliza (zumari) sauti za shetani, usiku anacheza na ukifika muda wa swala anaswali haliyakua amekaa au anadonoa katika swala kama kuku (anaswali haraka haraka), na mtu huyo huchukia kuisikiliza Qur'an tukufu na kuwa mbali nayo na inakua kwake ni mashaka (dhiki na tabu), anakua hana mapenzi na Qur'an wala hamu ya kuisoma wala kuisikiliza katika moyo wake, yeye anapenda kusikiliza sauti za nyimbo na makofi (muziki) na anavipenda kwa mapenzi ya moyoni mwake. Na hizi hali za kishetani tunazipata kama alivyosema Allah Mtukufu:
{وَمَنْ يَعْشُ عَنْ ذِكْرِ الرَّحْمَنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ قَرِينٌ}
Anaye yafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwakilishia Shetani kuwa ndiye rafiki yake. "Az-Zukhruf: 36.
Na akasema Ibnul Qayyimul Jauziyy Alla amrehem: Na miongoni mwa vitimbi vya adui wa Allah na mitego yake ambayo ametega mtu aliyepungukiwa na akili na elimu ya dini, na mitego hiyo imezinasa nyoyo za wajinga na wabatilifu: Ni kusikiliza nyimbo, ngoma na makofi na muziki kwa ala zilizoharamishwa ambazo zinazuia nyoyo kuisoma na kuisikiliza Qur'an tukufu, na kuziingiza katika kushiriki mambo ya ufasiqi na maovu. Basi hiyo ndiyo Qur'an ya Shetani na ni pazia nzito (uzio mkubwa kati ya wanaosikiliza miziki na wanaoimba, baina yao na Allah), nayo ni ngazi ya kufanyia liwatwi na zinaa, na kwa kupitia muziki anapata mtu mwovu kwa muovu mwenzie makusudio yao (uzinifu), Shetani amewafanyia vitimbi ndani ya nafsi zao kwa kupitia muziki na ameufanya muziki kuwa mzuri kwa vitimbi na kuwadanganya na akawafunulia batili na akaipendezesha na nyoyo zao zikakubali.
Na ukiwaona watu hao wanavyousikiliza muziki na kuunyenyekea na wakaacha kazi zao kwa kusikiliza muziki na nyoyo zao zikatulizana wakaanza kuucheza na kukata viuno, basi utawaona wanaume hao ni kama makhanithi na hawastahiki kuitwa wanaume kwasababu ya kujifananisha kwao na wanawake.
Nyoyo zao zimechanika kwa kumfuata shetani na wakatoa mali zao katika njia ya upotevu wakaumaliza umri wao katika starehe na matamanio ya haramu wakaifanya dini yao kuwa ni upuuzi,wanapenda kusikiliza sauti za shetani kuliko kusikiliza Qur'an, laity kama akisikiliza Qur'an mwanzo mpaka mwisho atatamani aweke pamba katika masikio yake ili asisikie, na akianza kusikiliza muziki utaona moyo wake unafurahi na viungo vyake vinatulia.
Ewe uliye fitinika na ukauza fungu lako kwa Mwenyezi Mungu kwa kununua fungu la shetani ambayo ni biashara yenye hasara, kwanini usipate starehe na moyo wako kutulia kwa kusikiliza Qur'an? Lakini hali ilivyo ni kwamba kila mtu anafuata wale anao fanana nao, na yeyote anaesikiliza muziki basi ajue kuwa anafanana na shetani aliyelaaniwa na Allah.
FAT-WA YA SHEKH ABDUL -AZIZ BUN BAZZ KUHUSU HUKUMU YA MUZIKI: |
Ni ipi hukumu ya muziki, je ni haramu au laa? Pamoja na kuwa nausikiliza kwa kujiliwaza, na niipi hukumu ya nyenzo za muziki wa zamani? Na ni ipi hukumu ya ngoma katika ndoa?
JAWABU: |
Akajibu Sheykh kwamba: kusikiliza miziki ni haramu na ni uovu, pia ni miongoni mwa maradhi ya moyo, na kususuwaa kwa moyo (yaani moyo kuwa mgum) na kumzuilia mtu katika kumtaja Mwenyezi Mungu na kuswali, wametafasiri wanachuoni wengi maneno ya Allah Mtukufu:
{وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ}
Na miongoni mwa watu wapo wanao nunua maneno ya upuuzi.
Kwamba ni miziki, na alikua Abdallah Bun Masuud (ﷺ.a) akiapa kwamba maneno ya kipuuzi ni muziki, na unapokua muziki umekusanya nyenzo kama vile gita, kinanda, ngoma, nai, zeze na mfano wa hivyo, basi uharamu wake ni mkubwa zaidi. Na wametaja baadhi ya wanachuoni kuwa nyimbo pamoja na nyenzo za kipuuzi za muziki ni haramu kwa makubaliano ya wanachuoni wote.
Basi niwajibu kujihadhari na vitu hivyo na kwa hakika imethibiti kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema ya kwamba:
(ليكونن من أمتي أقوام يستحلون الحر والحرير والخمر والمعازف)
Watatokea katika umma wangu watu (ambao) watahalalisha zinaa na hariri na pombe na ala (nyenzo) za miziki. Ameipokea Imamu Bukhari.
Nawausieni kufanya wingi wa kusoma Qur'an tukufu na kumtaja Allah Mtukufu, kama niwausiavyo kusikiliza idhaa ya Qur'an tukufu na idhaa mbalimbali za kiislam. Katika kuskiliza Qur'an kuna faida kubwa sana na nibora kuliko kusikiliza muziki.
Lakini katika ndoa inaruhusiwa kupiga dufu na kuimba nyimbo ambazo hazipelekei katika haramu wala kusifu mambo ya haramu wakati wa usiku, na hiyo ni kwa wanawake kwa ajili ya kuitangaza ndoa na kutofautisha baina ya ndoa na uzinifu kama ilivyothibiti katika Sunna kuhusu hilo kwa Mtume swalla LLahu alayhi wa sallam.
Ama ngoma haijuzu kupiga katika harusi wala katika mambo mengine bali inatosha dufu kupigwa katika harusi basi na ni kwa wanawake tu bila ya wanaume, na baada ya hayo yote (imekua kinyume) kwasababu waisilamu wengi leo wanahalalisha muziki ima ni kwa ujinga wao, na ndio wengi, ama kwa ubishi.
Tunamuomba Allah atujalie ni katika watu wenye kusikia maneno na kufuata yaliyo mazuri, hao ndio walioongozwa na Allah, na hao ndio wenye akili. Na rehma na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad na watu wake na maswahaba wake.