VIPI ANATAKIWA AWE MWANAMKE MWEMA
Jamii ya vilivyomo
Full Description
بسم الله الرحمن الرحمن الرحيم
VIPI ANATAKIWA AWE MWANAMKE MWEMA?
Imeandaliwa na: Yunus Kanuni Ngenda
Imepitiwa na: Abubakari Shabani Rukonkwa.
Mwanamke mwema huimarisha ndoa yake kwa kutekeleza haki za mumewake, na hayo ndio maamrisho ambayo ameamrishwa na Allah mtukufu.
Chukua tahadhari ewe mwanamke wa kiislamu ili usiingie motoni!
Anasema Mtume s.a.w:-
عن عبد الله ابن أبي أوفى أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:"لو كنت آمراً أحداً أن يسجد لغير الله تعالى لأمرت المرأة أن تسجد لزوجها، و الذي نفس محمد بيده لا تؤدي المرأة حق ربها حتى تؤدي حق زوجها كله حتى لو سألها نفسها وهي على قتب لم تمنعه" (السلسلة الصحيحة1203 )
Kutoka kwa Abdullah bin abii awfaa Radhi za Allah ziwe juuyake, hakika Mtume
(Swalla Allaahu alayhi wasallam) alimesema:-
((Ningekuwa nimwenye kuamrisha mmoja wenu amsujudie asie kuwa Allah basi ningemuamrisha mwanamke amsujudie mumewe, Ninaapa kwa Allah ambae nafsi ya Muhammad iko mikononi mwake mwanamke hawezi kutekeleza haki za mola wake mpaka atekeleze haki zote za mume wake kwanza, hata akimuomba mumewe nafsi yake (akimuhitaji) akiwa jikoni mke hana haki yoyote yakukataa".
Subhana Allah! !
Subhana Allah! !.
Muogopeni Allah enyi wanawake Allah hakuwapa wanaume daraja hiyo ila nibaada yakuona shida na taabu ya majukumu ya kuitunza familia tulieni majumbani na muwatii waume zenu.
Mwanamke kukaa nyumbani na kumtii mumewe kwa kila jambo la halali basi mwanamke huyo analipwa thawabu za sawa na mtu aliyepigana jihadi.
Na miongoni mwa haki za mume kwa kwa mkewe:-
1-Ni mwanamke kuwa radhi pindi mumewe atakapo muhitaji (falagha) kitandani.
Anasema Mtume s.a.w:-
عن عبدالرحمن بن عوف رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:إذا دعا الرجل امرأته إلى فراشه فأبت فبات غضبان عليها لعنتها الملائكة حتى تصبح " البخار ومسلم.
Kutoka kwa Abdurahmani bin Aufi Radhi za Allah ziwe juu yake alisema:-
Alisema Mtume rehma na amani zewe juu yake: ((Pindi mume atakapo muita (atakapo muhitaji) mkewe kitandani kisha mwanamke akakataa, mwanaume akalala hali ya kua amekasirika kwa kitendo kile basi malaaika wanamlaani yule mwanamke mpaka asubuhi))
(Bukhari na muslim).
Inna lillahi wainna ilayhi rajiuna! Niwanawake wangapi walioko kwenye ndoa na kila siku wanalaaniwa na malaika?
Enyi kina mama wa kiislam hivi mnajua maana ya laana?
Maana ya laana ni mtu kufukuzwa (kutolewa) katika Rehma za Allah.
Sasa ukitolewa katika rehma za Allah utakuwa katika rehma za nani!?
Basi ni vema enyi kina mama wa kiislam kumuogopa Allah na kujitahidi kuzitekeleza haki za waume zenu kwani wao ni sababu kubwa ya nyinyi kuingia Peponi.
Anasema mtume (S.a.w):
جاء عَنْ أَبِى سَعِيدٍ الْخُدْرِىِّ رَضِىَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ : ( جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِىِّ صلى الله عليه وسلم بِابْنَةٍ لَهُ فَقَالَ : يَا رَسُولَ اللَّهِ ! هَذِهِ ابْنَتِى قَدْ أَبَتْ أَنْ تَزَوَّجَ . فَقَالَ لَهَا النَّبِىُّ صلى الله عليه وسلم : أَطِيعِى أَبَاكِ . فَقَالَتْ : وَالَّذِى بَعَثَكَ بِالْحَقِّ لاَ أَتَزَوَّجُ حَتَّى تُخْبِرَنِى مَا حَقُّ الزَّوْجِ عَلَى زَوْجَتِهِ . قَالَ : حَقُّ الزَّوْجِ عَلَى زَوْجَتِهِ أَنْ لَوْ كَانَتْ لَهُ قُرْحَةٌ فَلَحِسَتْهَا مَا أَدَّتْ حَقَّهُ ) زاد بعض الرواة : ( أَوِ انْتَثَرَ مَنْخِرَاهُ صَدِيدًا أَوْ دَمًا ، ثُمَّ ابْتَلَعَتْهُ مَا أَدَّتْ حَقَّهُ ، فَقَالَتْ : وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالْحَقِّ ، لا أَتَزَوَّجُ أَبَدًا ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : لا تُنْكِحُوهُنَّ إِلا بِإِذْنِهِنَّ).
رواه ابن أبي شيبة في " المصنف " (3/556)، والنسائي في "السنن الكبرى" (3/283)
Imekuja kutoka kwa Abiy Said Alkhudriy Radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuja mtu kwa Mtume (s.a.w) na binti yake, akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Huyu binti yangu amekataa kuolewa. Mtume s.a.w akamwambia Yule binti (ewe binti) mtii baba yako. Yule binti akasema ninaapa kwa Mwenyezi Mungu ambae amekutuma kwa haki siolewi mpaka unieleze haki za mume kwa mkewe. Akasema Mtume S.a.w: haki za mume kwa mke wake nikwamba laiti angekuwa mume wako ana kidonda chenye usaha kisha mke akakilamba kile kidonda kwa ulimi wake basi asingekuwa ametekeleza mke haki yake kwa mumewe)
Wameongeza baadhi ya wapokezi :(laiti usaha au damu ingetapakaa kwenye midomo ya mke kisha akameza usaha au damu ya mume asingekuwa ametekeleza haki ya mume wake).
Akasema Yule binti: ninaapa kwa Mwenyezi Mungu ambae alie kutuma kwa haki kamwe sita olewa,
Akasema mtume S.a.w: Basi msiwaozeshe mabinti zenu ila kwa idhini yao).
(Ameipokea ibn Abii Shayba na Anasaai).
2-Mwanamke kutomuweka katika kitanda chake mwanaume asiekua mumewe.
Alisema Mtume s.a.w katika khutbatul-wadaa, khutba ya kuaga:-
))....أما بعد: أيها الناس إن لنسائكم عليكم حقا ولكم عليهن حق، لكم أن لا يواطئن فرشهم غيركم((...
Ama baada: Enyi watu hakika wake zenu wana haki kwenu na nyinyi mna haki kwao, (katika haki zenu kwao wake zenu) wasiwaweke katika vitanda vyao wanaume wasiokua nyinyi.
3-Mwanamke asimuingize ndani mtu yeyote ambae mumewe anamchukia.
Anasema Mtume s.a.w:-
((...ولا يدخلن أحدا تكرهونه بيوتكم إلا بإذنكم..))
Na wala wasiingize katika nyumba zenu mtu yeyote (katika watu) mnaowachukia.
4-Kutokufanya mambo machafu, (na maovu) kwani kufanya hivo kutapelekea kuhamwa kitanda nk.
Anasema Mtume s.a.w:-
(ولا يأتين بفاحشة، فإن الله قد أذن لكم أن تعضلوهن و تهجروهن في المضاجع و تضربوهن ضربا غير مبرح)
Na wala wasifanye mambo machafu (maovu kwasababu wakifanya hivo) hakika Allah ametoa idhini (amewaruhusu wanaume) kuwahama (wanawake hao) katika vitanda na kuwapiga kipigo kisichoumiza.
Hizo ni baadhi ya haki za mume juu ya mkewe, zipo haki nyingi sana za mke na mume ambazo kama wana ndoa watazizingatia kwa umakini basi misukosuko katika ndoa itakwisha na kutashamiri upendo, huruma, upole na ihsani.
Tambih, (Uzinduo)
Enyi wanawake wa kiislam mlio katika ndoa na nyinyi kina dada mnaotarajia kuingia katika ndoa, ni vema mkajitahidi kuzisoma ndoa zenu ili muweze kuzijua haki zenu kwa waume zenu na haki za waume zenu juu yenu hiyo itakua rahisi kwako kuzitekeleza.
Qur'ani iko wazi sana katika kuzielezea khabari hizi, na Sunna za Mtume s.a.w ziko wazi! Pia mnashauriwa akina mama wa kiislam kusoma vitabu na kusikiliza mawaidha mbalimbali yanayohusu mambo ya ndoa, maana mmekua wepesi kumtunza bibi harusi vyombo vya kupikia kuliko kumzawadia vitabu vya hukum za ndoa.
Ndoa ni nusu ya dini
Ndoa ni ibada yaqini
Ndoa ni utulivu makini
Ndoa hujaza mapenzi rohoni
Ndoa hueneza huruma moyoni
Anasema Allah s.w:-
(و من آياته أن خلق لكم من أنفسكم أزواجا لتسكنوا إليها و جعل بينكم مودة و رحمة)
((Na katika alama zake Allah (s.w) ni kwamba amewaumbia kutokana na nafsi zenu wake ili mpate utulivu utulivu kwao, na akajalia baina yenu mapenzi na huruma))
Tumuomba Allah ajaalie katika majumba yetu upendo, huruma, furaha na ucha Mungu.
Ewe Allah tunakuomba wajaalie wanawake wa kiislamu walio katika ndoa waweze kutekeleza haki za waume zao, na wao watekelezewe haki zao na waume zao. Ameeen!