×
No Description

ABU HURAIRA (ﷺ‬.a) SAHABA WA MTUME (S.A.W)

UTANGULIZI WA MTUNZI

Shukrani zote zimemthibitikia Allah Mola wa viumbe vyote, na Sala na Salamu zimshukie Bwana wetu Muhammad alieletwa kuwa ni Rehema kwa waja wote na ziwashukie jamaa na Masahaba wote, ama baada ya hayo

Hakika baadhi ya watu wamezowea ima kwa ujinga au kwa kufuata kwa wale kilichopekewa akili zao na matamanio ya nafsi juu ya kuwatukana Masahaba wa Mtume (S.A.W) walimuamini, waliojipatia hadhi kwa usuhuba wake wakamuunga nguvu na kumnusuru, wakashiriki pamoja nae kwa kila kilichotolewa juhudi katika kujenga maendeleleo ya umma huu, utukufu na historia yake waliojifakharishia, mataifa mengine yakajisifia kwayo, au sio wao baada matashi ya Allah Taala Uislamu usingelipatia ushindi, usingeea kwenye maeneo ya Ardhi, wala nuru yake kuenea kwenye anga, hivyo umma na kaumu zikaongoka juu ya tabia ndimi, rangi na asili zake, zikafanikiwa zilizofanikiwa juu ya nyenginezo, kwa sababu ya hayo mengine katika amali njema ambayo nafasi hii haitoshi kuyataja, Allah (S.W) aliwasifu, kuwaridhia kwake na malipo yake makubwa katika Aya nyingi katika Qur'ni Tukufu, na miongoni mwa hizo ni

Kauli yake Taala { Na waliotangulia wa awali katika Muhajirina na Ansari ambao waliwafuata kwa wema, Allah amewaridhia na wao wamemridhia na amewaandalia Pepo zinazopitiwa na mito chini yake waishi humo milele, huko ndiko kufuzu kuliko kukubwa }[At Tawbah 100]

Na kauli yake Taala {Hakika Allah ameshawaridhia waumini pale walipokupa ahadi ya utii chini ya mti hivyo Allah alishaelewa yaliyomo ndani ya nafsi zao akawateremshia utulivu juu yao na kuwalipa ushindi uliokaribu}[Al Fat-h 18].

Na kauli yaake Taala {Hawawi sawa miongoni mwenu yule aliehama kabla ya ukombozi na kupigana vita hao wanayo daraja kubwa kuliko wale waliotoka baadae na wote Allah amewaahidi malipo mema; na Allah kwa yale muyafanyayo ni Mwenye kuwa na habari} [Al Hadiid 10] Kama walivyostahiki sifa za Nabii (S.A.W), na kujitukuza kwa sababu yao na kuwafanya bora juu ya wengine kwa hadithi nyingi, miongoni mwao ni, kauli yake (.SA.W) ( Watu walio bora ni wa karne yangu, kisha wanaowafuatia wao, kisha ambao wanaowafuatia wao, kisha ambao wanaowafuatia wao) Hadithi [1]

Na kauli yake (( Musiwatukane masahaba wangu, naapa na yule ambae nafsi yangu iko mikono mwake lau mmoja wenu atatoa dhahabu mfano wa Uhud asingelifikia gao la mmoja wao wala nusu yake))[2]

Na kauli yake (Allah Allah katika masahaba wangu, musijewafanya malengo ya matusi, aliewapenda basi ni kwasababu ya mapenzi yangu na aliewachukia ni kwa sababu ya kunichukia mimi, na aliewaudhi basi ameniudhi mimi na alieniudhi mimi basi amemuudhi Allah na aliemuudhi Allah basi anakaribia kumnyakua)[3]

Na pamoja na mapenzi ya Allah Taala kwao na kuridhiwa nao, na kutukuzwa kwao na Nabii (S.A.W) na kuwafanya wabora kuliko wengine katika wana wa umma huu, lakini ndimi za bandia zimewatukana, na kalamu za mamluki, zimetilia nguvu juu ya idadi ya masahaba miongoni mwao waliotangulia mongoni mwao wa awali na wengineo.

Zikawasemea kwa wasiyoyasema, wakawanasibishia wasiyoyafanya, wakawasingizia kwa yale ambayo wao wametakasika nayo, bila ya kujali Aya za Qur'an zenye kuwatakasa na zenye kuwaridhia, na Hadithi sahihi za Mtume (S.A.W) zenye kunyanyua ubora wao, zikitegemea riwaya za kihistoria za kubuni, wanaojifanya waislamu wakaupaka matope kwazo toka kwa maadui zake, matamanio ya nafsi yakafanyia kazi kulikuza mpaka zikawa ni uhakika au kama zilivyowapitikia, pamoja na kwamba hayana asili kwenye, bali ni dhana mbovu na ubunifu tu, zilizochipuka toka kwenye fahamu mbovu na upelekeaji matokeo ya makosa.

Na katika nyaraka hizi nitazungumzia kuhusiana na mmoja wa Masahaba watukufu waliotafunwa na ndimi ovu na kuzushiwa uzushi waliopenda, na madai batili yaliojazwa uongo na ubaguzi na uadui. Huyo ni sahaba wa Mtume (S.A.W)(Abu Hurairah-ﷺ‬.a-) Sahaba, mtumishi wake na hafidhi wa Sunna zake (SAW).

Nitajitahidi kumuelezea, usuhuba wake na Mtume (S.A.W), na juhudi zake katika kuitumikia Sunna ya Nabii (S.A.W ), hivyo nitaonyesha uongo na shubuha zilizoenezwa dhidi yake, kwa lugha ya uwazi, na kuepusha kila ugumu, nitafanya ufupisho na kuwa mbali na urefushaji, ili kuweza kufahamika na kila mmoja kwa daraja yake, na nategemea msaada na tawfiqi ya kwa Allah kwa yote haya.

Doktori Harith bin Sulaiman

15 Muharram 1420H - 1/5/1999M

MLANGO WA KWANZA

MAELEZO YANAYOMUHUSU NA SIRA YAKE

Jina na Nasabu Yake[4]

Watu wametofautiana katika jina la Abu Huraira (ﷺ‬.a) kabla ya kusilimu kwake kwenye kauli kadha imesemwa Abdu Shams bin Sakhar, kasemwa Abdi Amr bin Abd Ghunum. Ikasemwa zaidi ya hiyo; kama walivyo tofautiana kwenye jina lake baada ya kusilimu kuna kauli mbali mbali, mashuhuri yao ni Abdurahman bin Sakhar. Imesimuliwa toka kwake kwamba amesema "Jina langu lilikuwa Abdu Shams, katika zama za ujahili, Mtume (S.A.W) akaniita Abdurahman[5] . Na lolote liwalo jina lake ni kwamba kun-ya yake Abu Huraira ndio limezidi jina lake, akawa hajulikani ila kwalo na sio jengine.

Imesimuliwa sababu ya kuitwa kun-ya hiyo, ni kwamba amesema "Nilikuwa nikichunga kondoo wetu, na nilikuwa na kipaka kidogo, basi nikawa usiku nakiweka kwenye mti, ukifika mchana kinanifuata na kucheza nacho hivyo nikaitwa Abu Huraira.

Ama nasabu yake wanahistoria wanasema anatoka katika kabila la Azdy la Kiyemen, alifariki Abu Huraira 57 au 58 au 59 Baada ya Hijra akiwa na umri wa miaka sabini na nane, na kauli ya mwisho ameidhoofisha AIhafidh Adhahabiy, na Ibn Hajar yeye pia kwa kutegemea kauli ya mwanzo, kifo chake kilikuwa Madinatu Munawara, na inasemekana Aqiiq, akabebwa mpaka Madina na kuzikwa Baqii na katika wasindikizaji wake walikuwa Abdullahi bin Omar, na Abu Said Alkhudriy(R.A).[6]

Kusilimu na Usahaba Wake

Abu Huraira alisilimu mwaka wa Khaibar katika mwezi wa Muharram mwaka wa saba Hijriya, na kushuhudia vita hivyo pamoja na Mtume (S.A.W). Kutoka kwa Said ibn Musayyib, toka kwa Abu Huraira amesema (Tulishuhudia pamoja na Mtume siku ya Khaibar…)[7] Toka kwa Abuilghaith, toka kwa Abu Huraira, amesema (Tulitoka pamoja na Nabii (S.A.W) kuelekea Khaibar Allah akatufungulia) Hadithi[8]

Kama alivyoshuhudia vita vyengine katika vita vilivyokuja baadae,na kwa hivyo akajipatia fadhila za Jihadi katika njia ya Allah zaidi ya ile hadhi ya usahaba wa Mtume (S.A.W), kwa vile alisuhubiana nae tokea siku hiyo mpaka kifo chake (S.A.W), na ni muda usiozidi miaka minne[9],alikamatana nae katika muda huo mkamatano uliokamilika alihama kwao kwa ajili ya kuchukua toka kwake na kusoma, hivyo mkono wake upo pamoja na mkono wa Mtume (S.A.W), anazunguka pamoja nae popote alipozunguka, anakwenda pamoja wala haachani nae popote nyumbani wala safarini, kwani hakushughulishwa na kuuza, kununua wala kuchunga mali.

Imesihi kwamba amesema "Hakika nyie mnadai kwamba Abu Huraira kazidi kwa mapokezi ya hadithi toka kwa Mtume (S.W.A) Wallahi ni ahadi, hakika mimi nilikuwa masikini aliyesuhubiana na Mtume (S.A.W) kwa kujaza tumbo langu, na Muhajirina walikuwa wakishughulishwa na kofi za sokoni, na Ansari nao wakishughulishwa kusimamia mali zao, mimi –siku moja-nilihudhuria majlisi ya Mtume (S.A.W) akasema ((Ni nani atakaetandika mtandio wake mpaka nimalize maneno yangu, halafu alikamate, asisahau kamwe alichosikia toka kwangu?. mimi nikatandika burda mpaka akamaliza mazungumzo yake kisha akalikamata kunipa, basi naapa na Yule Ambaye nafsi yangu iko kwenye Mikono yake sikusahau chochote nilichokisikia toka kwake baada ya hapo.)[10]

Na kwa hili, kwamba Abu Huraira (ﷺ‬.a) aligubikwa na baraka za usuhuba wake na Mtume (S.A.W), kukamatana nae, kumuhudumikia, na ndio akapata baraka ya usuhuba, Allah (S.W) akamruzuku hifadhi ya aliyoyasikia toka kwa Mtume (S.A.W) na kutosahau .

Mapenzi Yake Kwa Mtume (S.A.W) na Huduma Zake Kwake

Abu Huraira (ﷺ‬.a) alikua mwingi wa mapenzi kwa Mtume (S.A.W), aliitilia nguvu imani kwake, akajikurubisha kwake kwa lile linalomridhisha, hufurahi kwa furaha zake, akihuzunika kwa huzuni zake, akiumizwa na kutukanwa Mtume (S.A.W), hata yakiwa matusi yanatoka kwa mtu wa karibu zaidi kwake, imesihi toka kwake kwamba amesema "Nilikua nikimlingania mama yangu kwenye uislamu akiwa mshirikina, basi siku moja nikamlingania, akasema kuhusu Mtume (S.A.W) ninayoyachukia, hivyo nikamwendea Mtume (S.A.W) huku nalia, nikamwambia Ewe Mtume wa Allah nilikuwa nikimlingania mama yangu kwenye uislamu, lakini anakataa, leo nimemlingania akasema kuhusiana nawe yanayonikera, hebui muombe Allah amuongoe mama wa Abu Huraira"

Akasema Mtume (S.A.W) "Ewe Allah muongoe mama wa Abu Huraira".

Nikatoka nikiwa na furaha kwa dua ya Nabii (S.A.W.) nikenda mpaka mlangoni akawa mkali, akasikia sauti ya miguu yangu, akasema hapo hapo Ewe Abu Huraira na nikasikia, mchuruziko wa maji, akakoga na kuvaa nguo yake na kujitanda mtandio wake, haraka haraka akafungua mlango, na akasema Laa ilaaha illa Allah nashuhudia kwamba Muhammad ni Mtumwa wa Allah na Mtume wake.

Akasema;'Hapo nikarejea kwa Mtume (S.A.W), nikamjia nikilia kwa furaha, akasema nikamwambia Ewe Mtume wa Allah furahi, hakika Allah ametakabalia dua yako na amemuongoa mama wa Abu Huraira, amkashukuru Allah, na kumsifu, akasema kheri".Hadithi[11]

Hadithi hii inatuonesha hali ya mapenzi ya Abu Huraira (ﷺ‬.a) kwa Mtume (S.A.W) na kilio chake anapotukanwa,kwa kumtukuza Mtume (S.A.W) Aba Hurairah(ﷺ‬.a)kwa kumtekelezea ombi lake kwa dua ya kuongolewa mama yake alieongolewa na Allah kwa baraka ya dua,kitu ambacho kiliongeza furaha za Abu Huraira (ﷺ‬.a),na kufurahi na kulia kwake kwa hilo.

Alikua akiwasilisha mapenzi yake kwa Mtume (S.A.W) kwa mfano wa kauli yake 'Ameniusia kipenzi changu (S.A.W) juu ya mambo matatu, nisiyawache mpaka nitakapokufa kufunga siku tatu katika mwezi, sala ya dhuha na kulala baada ya witri'[12]

Na kauli yake nimemsika kipenzi changu akisema "Pambo la muislam litafikia pale udhu unapofikia'.[13]

Kama ambavyo akielezea pupa la kukamatana na Mtume (S.A.W), na utumishi wake kiasi kwamba hawachii fursa ya kumuhudumikia Mtume (S.A.W) ila akiichukua, katika hayo ni kwamba yeye alikuwa akimbebea Mtume (S.A.W) kiriba cha ngozi chenye maji kwa ajili ya udhu wake na haja yake, basi mara moja alipokuwa akimfuata na kiriba hicho, akasema nini huyu? Akamwambia Abu Huraira, akamwambia niletee mawe nistanjie, usiniletee mfupa, wala kinyesi cha mnyama, basi nikamletea mawe nabeba kwa ncha ya nguo yangu, mpaka nikayaweka pembeni mwake, kisha nikaondoka)..Hadithi. [14] Katika hayo ni yaliyosimuliwa na Abu Zuraa bin Amr bin Jariir toka kwa Abu Huraira, amesema “Mtume (SAW), aliingia chooni nikampelekea kitungi cha maji, basi akastanji, na akapangusa mkono wake ardhini, na nikampelekea kitungi chengine, akatawadhia' [15]

Katika hayo vilevile ni aliyosimulia Mujahid toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) amesema Alinipita Mtume wa Allah (S.A.W) akaitambua njaa kwenye uso wangu, akanita Ewe Abu Huraira? Nikamuitikia labaika ya rasulallahi nikaingia pamoja nae nyumbani akaona maziwa kwenye chombo, akasema 'Mumeyapata wapi haya? Akaambiwa "amekuletea Fulani", akasema "Ewe Abu Huraira nenda kwa watu wa Suffa ukawaite" Watu wa Suffa ni wageni wa uislamu, wasio na jamaa wala mali. Mtume wa Allah (S.A.W) akiletewa sadaka akiwapelekea, wala hachukui chochote, na akiletewa zawadi akitumia, na kuwashirikisha wao, basi nikachukizwa kunipeleka kwao, nikasema nilitarajia nipate maziwa haya yanitie nguvu, na ni maziwa kiasi gani haya kwa watu wa Suffa, na utiifu kwa Allah na Mtume wake ni lazima, basi nikawaendea wakaja na kuitikia wito, walipokwishakaa, akiniambia "Yachukue Abu Huraira uwape" basi nikawa nawapa, mtu-anakunywa mpaka kumtosha mpaka nikawaendea wote, na nikampa Mtume wa Allah (S.A.W) basi akanyanyua uso wake kwa tabasamu, akasema "Nimebakia mimi na wewe" nikawambia kweli Ewe Mtume wa Allah (S.A.W), Akaniambia "kunywa" basi nikanywa akaniambia "kunywa" nikanywa, basi hakuacha kuendelea anasema "kunywa" nakunywa mpaka nikasema "Naapa kwa yule ambae amekutuma kwa haki sina nafasi ya kuyaweka hivyo akayachukua akanywa yaliyobaki." [16]

Riwaya hizi na kabla ya hizi zinatuonesha pupa la Abu Huraira juu ya kumhudumia Mtume wa Allah (S.A.W) utii wake, kama zinavyotuonesha upeo wa kumtegemea kwake Mtume wa Allah (S.A.W) na kuwapendelea wao kuliko nafsi yake, kiasi kwamba hakunywa maziwa aliyopewa zawadi pamoja na kuyahitajia Mtume wa Allah (S.A.W) ila baada ya kunywa wao wote, na wakashiba kwa baraka za Mtume wa Allah (S.A.W) na hilo sio geni kutoka kiongozi, mwenye tabia adhimu.

Elimu na Ubora Wake

Abu Huraira alikuwa katika maulamaa wa Masahaba na wabora wao, hilo linashuhudiwa na riwaya za wengi miongni mwao waliosimulia toka kwake, na kwenda kwake katika Fatwa, kwani Masahaba waliosimulia toka kwake miongoni mwao ni, Zaid bin Thabit, Abu Ayoub Al- ansari, Abdullah bin Abbas, Abdullah bin Zubeir, Ubayya bin Kaab, Jabir bin Abdillaah, Aisha, Musawir bin Makhramah, Abu Musal Ash-ariy, Anas bin Malik, Abu Raafii muachwa huru wa Mtume wa Allah (S.A.W) na wengineo katika Masahaba (ﷺ‬,a); katika matabiina ni Qabiswa bin Dhuaib, Sai'd bin Al Musayyib,Urwa ibn Az ubair, Salim bin Abdillahi bin Omar, Abu Salamah bin Abdir Rahman, Abu Saleh Asamman, Ataa bin Abii Rabaah, Ataa bin Yasaar, Mujahid, Ashaabiy, Ibn Siryn Ikrimah, Naafii maula wa Ibn Omar, Abu Idris Al Khawlaniy. na wengineo katika Matabiina (ﷺ‬.a)[17] Amesema Bukhariy (ﷺ‬.a);'Wamesimulia toka kwake watu mia nane au zaidi.[18]

Kama walivyosimulia toka kwake, walikuwa wakimwendea kuuliza masuali na fatwa, na wengine wapo waliomtanguliza katika masuala hayo na kumuafiki katika aliyoyasema.

Amesema Al-shaafii (ﷺ‬.a) "Ametupa habari Maalik, toka kwa Maalik, toka kwa Yahya bin Saiid toka kwa Bukair bin Al Ashaji, toka kwa Muawiyah bin Iyaash Al Answari" Kwamba yeye alikuwa amekaa pamoja na Ibn Azubair, akaja Muhammad bin Al Bukair, akauliza kuhusu mtu aliewacha talaka tatu kabla ya kuingia ndani basi akampeleka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) na Ibn Abbas nasi tulikua kwa Aisha, akaenda akamuuliza ibn Abbas akamwambia Abu Huraira "Mpe fatwa Ewe Abu Huraira, amekujia akiwa na shida, akasema "Moja inamtenganisha nae na tatu zinamuharamishia, mpaka aolewe na mume asiekuwa yeye, na akasema Ibn Abbas mfano wa hayo[19]. Na toka kwa Azzuhriy, toka kwa Salim, kwamba amemsika Abu Huraira (ﷺ‬.a) [20]akisema "Kaumu wenye kuhirimia waliniuliza kuhusiana na wasiohirimia waliowapa zawadi kiwindwa, nikawaamrisha wakile.'

Na toka kwa Ziyaad bin Maynaa, amesema "Walikua Ibn Abbas Ibn Omar, Abu Said, Abu Huraira na Jabir pamoja mfano wao, wakitoa Fatwa Madina toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W) Tokea alipokufa Othman mpaka walipokufa, na watano hao Fatwa ziliendelea.[21]

Nae Adhahabiy amesema "Na ikutoshe kwamba mfano wa Ibn Abbas anamuekea adabu na kumwambia "Ewe Abu Huraira toa Fatwa" [22]

Ibada na Taqwa Yake

Abu Huraira (ﷺ‬.a) alikua maarufu kwa ibada, taqwa, na kila lililomkaribisha kwa Allah (S.W), Vipi isiwe hivyo, wakati amesuhubiana na Kigezo Chema katika ibada, na kumuonyesha namna afanyavyo Jihadi nafsi yake kwenye ibada mpaka miguu yake ikavimba (S.A.W), hivyo alikua akifanya ibada kwa wingi miongoni mwa Sala, Saumu kusoma Qur'ani, na Sala za usiku. Toka kwa Hammaad toka kwa Abbaas Al Jaryriy amesema "Nimemsikia Aba Uthmaan An Nahdy Abu Huraira aliwaalika ugeni watu saba, basi akawa yeye, mkewe na mtumishi wao wanapokezana usiku sehemu tatu, huyu anasali na anamuasha huyu, halafu analala huyu, akasema, nikasema “Ewe Mtume wa Allah (S.A.W) wewe unafungaje? akasema ama mimi nafunga siku tatu katika mwanzo wa mwezi, iwapo nitatokewa na jambo huwa mwisho wa mwezi"[23]

Na toka kwa Ibn Jarir amesema amesema Abu Huraira (ﷺ‬.a) "Hakika mimi huugawa usiku wangu sehemu tatu, sehemu ya Quran, sehemu ya kulala na sehemu ya kukumbukia hadithi za Mtume wa Allah (S.A.W) [24]

Na imesihi kwamba amesema "Ameniusia kipenzi changu juu ya mambo matatu; Saumu siku tatu katika kila mwezi, rakaa mbili za dhuha na nasali witri kabla sijalala" [25]

Na kutoka kwa Hamaad bin Salamah, toka kwa Hisham bin Said bin Zaid Al Answariy, toka kwa Shurahbil kwamba Abu Huraira (ﷺ‬.a) alikuwa akifunga Jumatatu na Al Khamis.[26] Na zaidi ya hayo alikua mwingi wa Tasbiih na Alhamdu Lillahi Taala juu neema ya Uislamu na nyenginezo katika neema alizomneemesha Allah Taala, kama alivyokua mwingi kumuogopa Allah (S.W) mwingi wa kutahadharisha Moto –Allah atukinge nao-.

Toka kwa Maimun bin Maisarah amesema “ Kila siku Abu Huraira (ﷺ‬.a) alikuwa daima akipaza sauti mara mbili kwa kusema "Usiku umekwenda, na mchana umekuja, na jamaa wa Firaun wametiwa motoni basi hakuna atamsikie akisema hivyo ila atajikinga kwa Allah na moto".[27] Na imesimuliwa toka kwa Ibn Mubarak "Hakika Abu Huraira alilia katika maradhi yake, akaambiwa unalizwa na nini? Akasema "Silii juu ya dunia yenu hii, lakini juu ya yatakayokua baada ya yangu, na uchache wa zawadi zangu, na kwamba mimi nimeingiliwa na jioni katika kupanda juu, na maangukio yake ima ni juu ya Pepo au Moto, basi sielewi ni kwa ipi ya hizo nitachukuliwa , "[28]

Na imesimuliwa vile toka kwake Kwamba Abu Huraira (ﷺ‬.a) amesema "Muovu musimuonee choyo kwa neema, kwani walionyuma yake ni wenye pupa la kumtafuta; Jahannam kila inapopungua tunawazidishia Moto mkali." Na Ibn Kathir akasema " Kwa hakika Abu Huraira (ﷺ‬.a) alikua mkweli, mwenye hifadhi, dini, ibada, zaahid na mwenye amali kwa hali ya juu ,"[29]

Unyenyekevu, Ukarimu na Uzuri wa Tabia Zake

Abu Huraira (ﷺ‬.a) alijulikana kwa unyenyekevu wake wa kiwango kikubwa katika maisha yake, kamwe hakusahau wakati wake uliopita baada ya Allah kumpa neema ya elimu, cheo na ubora; kama watu wanavyogeuza yao ya kale, pale maisha yao yanapokua na wasaa, na kwamba alikua akikumbuka yake ya kale, na yale yaliompata katika shida na kunyimwa, ili amshukuru Allah (S.W) juu ya neema ya dini na neema nyenginezo na kutaka ziada katika neema zake Taala; imesimuliwa toka kwake kwamba amesema “Nimekulia uyatima, nikahama nikiwa maskini, nilikua muajiriwa wa Bint Ghazawaan kwa ajili ya chakula cha tumbo langu, na nguvu za miguu yangu nikiwasindikiza wanaposafiri, nikiokota kuni wateremkapo, hivyo shukrani zote zimemthibitikia Allah alieifanya dini kuwa ni yenye kutia nguvun, na Abu Huraira (ﷺ‬.a) kuwa imamu baada ya kuwa muajiriwa wa Bint Ghazawan kwa shibe ya tumbo lake, na kutia nguvu miguu yake "[30]

Amesema Adhdhabiy “Alikua mfuko wa elimu pamoja na utukufu, ibada na unyenyekevu."[31]Pamoja na unyenyekevu wake alikua mkarimu, na iweje isiwe hivyo wakati alimsahibu yule ambae ni mkarimu kuliko upepo ulioachiliwa (S.A.W), amesimulia Abu Nadhrat Abdiy toka kwa Altwaffaawiy amesema "Nilifika kwa Abu Huraira(ﷺ‬.a) akiwa Madina kwa kipindi cha miezi sita, basi sikumuona Sahaba yeyote wa Mtume wa Allah (S.A.W) mkarimu wala mkaribishaji mwema wa mgeni kulikoni yeye[32]

Na huenda alikusudia Masahaba wa Mtume wa Allah (S.A.W) kwa wale waliomkaribisha ugeni miongoni mwao, kama

inavyofahamika kutokana na kauli na sio wote, kwani miongoni mwao ni bahari zisiozoonekana fukwe zake katika ukarimu, na pamoja na unyenyekevu na ukarimu wake alikuwa mwepesi wa kiwiliwili, muwazi kwa anayoyasema, habebi chuki kwa yeyote yule, wala kuangalia kilicho kwa mwenginewe, mwenye kuridhika kwa alichonacho, mwenye kushukuru Allah kwacho.

Imesimuliwa toka kwake kwamba amesema "Shukrani zote zimemthibitikia Allah ambae ametushibisha mkate baada ya kutokua na chakula chetu ila vyeusi viwili tende na maji" [33]

Wema wake kwa mama yake na Mapenzi ya Watu Kwake

Abu Huraira alikua mwema kwa mama yake, alikuwa mtiifu kwake na katika wema kwa mama yake alifuatana wakati wa hijra kwenda kwa Mtume wa Allah (S.A.W) akiwa bado ni mshirikina, na kufikilia matarajio yake pale Mtume wa Allah (S.A.W) alipokubali ombi lake la kumuombea dua ya uongofu kwa mama yake kama ilivyotangulia, basi akaamini na akafurahi furaha kubwa sana zilizomliza kama ilivyotangulia.

Na katika wema kwake vile vile, ni ilivyosimuliwa toka kwake kwamba amesema" Siku moja nilitoka nyumbani kwangu nikawakuta watu, wakasema, “kitu gani kimekutoa?“ nikawambia njaa, wakasema nasisi Wallahi hatukutolewa ila na njaa, basi tukasimama, tukaingia kwa Mtume wa Allah (S.A.W), Akasema "Mmeletwa na nini saa hizi?" tukamueleza, basi akaja na sahani ndani yake zimo tende, akampa kila mtu kati yetu tendu mbili, akatwambia kuleni tende mbili hizi na muzinywelee maji, kwani zitakutoshelezeni siku yenu hii" basi nikala tende moja na nyengine kuificha, akasema " Ewe Abu Huraira kwanini umeichukua?" nikamwambia kwa ajili ya mama yangu. Akasema tutakupa tende mbili nyengine"[34] Na katika wema wake kwake ni yaliyosimuliwa na Ibn Shihaab Azzuhriy kwamba Abu Huraira (ﷺ‬.a) hakuwahi kuhiji mpaka alipokufa ili awe nae[35]

Imesimuliwa toka kwake katika kumuombea mama yake dua ya kusilimu, kwamba amesema "Nilisema, Ewe Mtume wa Allah (S.A.W) muombe Allah anipendezeshe mimi na mama yangu kwenye waja wake walioamini, nao awapendezeshe kwetu akasema "basi Mtume wa Allah (S.A.W) akasema "Allah kipendezeshe kitumwa chako hichi-yaani Abu Huraira (ﷺ‬.a)- na mama yake kwa waja wako walioamini, nao uwapendezeshe kwao walioamini" hadithi"[36] Na Ibn Kathir amesema, na hadithi hii ni katika dalili za unabii, kwani Abu Huraira alipendeza kwa watu wote, Allah ameufanya utajo wake uwe mashuhuri kwa kiwango alichokikadiria kiwe kutokana na riwaya zake[37]. Kwa maana kutokana na zile riwaya zilizosimuliwa toka kwake.

Pupa lake Juu Ya Kumfuata Mtume wa Allah(S.A.W)

Kutokana na mienendo yake ya kielimu yamedhihiri yale yanayojuilisha pupa lake kubwa la kumfuata Mtume wa Allah (S.A.W), na kumfanya kwake kuwa kigezo kwa yale aliyoyasema na alioyatenda akitekeleza kauli yake Taala.

{Na chochote alichokupeni Mtume basi kichukueni na alikukataze nacho basi kiwacheni} { Al Hashr 7}

Na akaitikia mlinganio wa mapenzi ya kweli kwa Mtume wa Allah (S.A.W) yalijaza nyoyo za Masahaba wake (ﷺ‬.a). na kumiliki kila huruma na viwiliwili vyao, na miongoni mwao ni Abu Huraira (ﷺ‬.a) aliyekua na pupa kubwa juu ya kumfuata (S.A.W ) namna alivyoweza, na huenda katika mifano ifuatayo yamo yanayotilia nguvu hayo. Na katika hayo ni yale yaliyosimuliwa kutoka kwake kwamba amesema " Ameniusia kipenzi changu mambo matatu saumu siku tatu katika kila mwezi, rakaa mbili za dhuha na witri kabla sijalala" [38] Na miongoni mwa hayo ni ile iliyosimuliwa toka kwake kwamba amesema " Mimi ndie mwenye kushabihiana wenu zaidi kwa Sala ya (S.A.W). Mtume wa Allah (S.A.W) alikua anaposema "samia llahu liman hamidah", akisema “Rabbanaa walakal hamdu" na alikua anatoa Takbira anaporukuu, na anaponyanyua kichwa chake, na anaposimama toka kwenye sijda mbili akisema "Allahu Akbar "[39]"

Na mesema Abu Huraira (ﷺ‬.a) "Hakika nilikua nikipiga mswaki kabla sijalala na baada ya kuamka, na baada ya kula, tokea nilipomsikia akisema aliyoyasema." [40] Na katika hayo vile vile ni ile aliyosimulia Saidul-Muqbiriy toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) Kwamba yeye alipita kwenye watu waliokua na mbuzi alieokwa, wakamwita akataa kula akasema. alitoka duniani na hakushibapo mkate wa ngano –shairi- [41] Na mifano iliotangulia ni dalili tosha juu ya upeo wa wafuasi wake (S.A.W) na kumuiga kwa kauli, vitendo na mwenendo.

Kauli na Hekima zake

Imesimuliwa toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) kauli na hekima zilizojaa mawaidha na maana zenye kujuilisha nguvu ya imani yake kwa Allah na Siku ya Kiama, na yale yatakayokuwepo katika hesabu, malipo na adhabu na njuu ya upana wa uelevu na fahamu yake ya mafunzo ya uislamu na upeo wake, na maarifa yake kuhusu dunia na zuhudi yake humo, na tutachagua baadhi ya kauli hizo, ili kuangalia yaliyomo katika maana ya kina na mawaidha ya hali ya juu

Katika hayo ni kauli ya Abi Salamah bin Abdirahman pale alipomtakia shifaa (kuponywa) "Ewe Abu Salamah, iwapo utaweza kufa basi kufa, naapa na yule ambaye nafsi ya Abu Huraira (ﷺ‬.a) ipo kwenye mkono wake umeshakaribia wakati maulamaa wakijiwa na mauti kuwa bora kwa mmoja wao kuliko dhahabu nyekundu, au wakati kukaribia kwa watu kujiwa na zama mtu kwendea kaburi la muislamu aseme ningependelea lau ningekua mwenye kaburi hili."[42]

Na kauli yake katika yale yaliyosimuliwa na Abdulmutawakil "Hakika Abu Huraira (ﷺ‬.a) alikuwa na mtumwa aliewachosha kwa kazi zake, basi siku moja akamnyanyulia bakora, akasema lau sio kisasi basi ningekuua lakini, nitakuuza kwa yule atakaenilipa thamani yako, nenda zako wewe ni -huru kwa ajili ya Allah. "[43]

Na kauli yake; "Hakika fagio hili ni lenye kuangamiza dunia na Akhera yenu. Akimaanisha mali na matamanio" Na katika yaliyosimuliwa toka kwa Muamar " Kwamba yeye alikuwa akipitiwa na jeneza akisema "Nendeni katika wakati wa jioni, na hakika sisi ni wenye kwenda asubuhi, au nendeni asubuhi sisi ni waendaji wa jioni, mawaidha ya hali ya juu, na sahau ya haraka, ya mwanzo inaondoka na ya mwisho inabakia haina mbadala." [44]

Na ile kauli yake pale alipoambiwa na mtu mmoja katika watu wa Madinah mwenye nyumba "Niandike nini juu ya mlango wa nyumba yangu?, basi akamwambia andika juu ya mlango wake, mtoto aliyeharibikiwa, mtoto wa mpoteaji, nakusanya kwa ajili ya mrithi “[45]

Na kauli yake " Hakuna maumivu yapendezayo zaidi kwangu kuliko homa, kwani inakipa kila kiungo sehemu yake ya maumivu, na kwamba Allah Taala hukipa kila kiungo sehemu yake ya malipo" [46]

Na kauli yake katika maradhi yake " Ewe Mola hakika mimi napenda kukutana na wewe, binafsi na Wewe pendelea kukutana nami"[47]

Na kauli yake kwa binti yake "Usivae dhahabu, kwani mimi nakuhofia moto"Alimkataza kuvaa dhahabu kwa sababu ya woga, na kwamba labda kuvaliwa kunapelekea maisha ya fakhari, ambayo mara nyengine hupelekea kuchoka kufanya ibada, na mapungufu katika utiifu, na vyenginevyo kujipambia mwanamke inajuzu, kwake yeye na kwa Masahaba wengine kama tunavyoelewa, mataabiina waliokuja baada ya wao katika maimamu kama tunavyoelewa, ikiwa sio kwa fakhari au kiburi, hivyo huharamishwa, kama yule anaeburura nguo yake kwa fakhari.[48]

Riwaya na Hifadhi Yake

Abu Huraira (ﷺ‬.a) alikua katika mahafidhi wa Masahaba wa Mtume wa Allah (S.A.W) pamesimuliwa toka kwake takriban hadithi 5374 zenye sanad,[49] na wingi wa riwaya zake na hifadhi inatokana na mambo hya -

1- Kusubihiana na Mtume wa Allah (S..W) kwa muda unaozidi miaka minne, ambao ni muda kwa kawaida unaotosheleza kwa kuhifadhi hadithi alizozihifadhi, bali zaidi ya hizo. Kwa yule aliyeacha shughuli zote kwa kuchukua na kuzihifadhi. Na nyingi ya riwaya hizo alizisimulia toka kwa baadhi ya Masahaba (ﷺ‬.a), na hasa zile ambazo zilimpita kuzisikia toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W) kabla ya kusilimu kwake kama vile Abi Bakr, Omar, Ubay bin Kaab, Usama bin Zaid na Aishah na wengineo (ﷺ‬.a).[50] Hivyo aliishi pamoja na hao, na wengineo katika Masahaba baada ya kifo cha Mtume wa Allah (S.A.W) kipindi sio kifupi, na hili linatujuilisha kwamba chanzo cha riwaya zake zote hakikuwa Mtume wa Allah (S.A.W) pekee, kama ambavyo muda wa kuzichukua haukufungika na muda wa usuhuba wake na Mtume wa Allah (S.A.W) kama wanavyodhani hivyo wasioelewa, isipokua uliendelea mpaka kipindi cha Masahaba walioishi baada ya kifo cha Mtume wa Allah (S.A.W)

2- Kujitenga kwake kwa ajili ya elimu na kuhifadhi, kama ilivyotangulia .[51]

3- Kifo chake kuchelewa mpaka baada ya mwaka 50H, na kama walivyokufa Masahaba wengi wa Mtume wa Allah (S.A.W) na Mahufadhi (ﷺ‬.a), na hawakubakia baada ya hapo ila kidogo kati yao, kama vile Abdullah bin Omar, Abdullah bin Abbas, Jaabir bin Abdillahi, Abuu Said Al Khudriy, Anas bin Malik, Aishah na wenginewe (ﷺ‬.a). Katika wakati ambao mahitajio ya elimu ya Masahaba (ﷺ‬.a) ilizidi kutokana na kutanuka kwa Dola ya Kiislamu, kuzidi kwa wanaoingia kwenye Uislamu, wingi wa watafutaji elimu katika watoto wa Masahaba na wengineo katika waliotoa kipao mbele kwenye elimu ya Masahaba kwa kuzingatia kwamba wao ndio marejeo pekee na salama ambayo yatawafikisha moja kwa moja mpaka kwa Mtume (S.A.W), na hasa wale waliojulikana miongoni mwao kwa kuhifadhi na kushikamana nae (S.A.W) kama vile Abu Huraira (ﷺ‬.a).

Shuhuda Ya Maulamaa kwa Hifadhi Yake

Kwa sababu ya mambo haya, baraka ya dua ya Mtume wa Allah (S.A.W) ya kuhifadhi alikuwa katika wahifadhi wakubwa wa Masahaba wa Mtume wa Allah (S.A.W) wingi wao wa hadithi. Amesimulia Al tirmidhiy toka kwa Abdullahi bin Omar (ﷺ‬.a) kwamba alimwambia Abu Huraira (ﷺ‬.a) "Ewe Abu Huraira wewe ulikuwa mwenye kuambatana zaidi kuliko sisi na Mtume wa Allah (S.A.W) hafidhi wetu zaidi wa Hadithi zake.[52]

Na vile vile amesimulia toka kwa Talha (ﷺ‬.a) kwamba amesema "Mimi sina shaka na kwamba yeye amesikia toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W) tusioyasikia" [53] Na Hakim amesimulia kwamba mtu mmoja alikuja kwa Zaid bin Thabit akamuuliza kuhusu kitu, akamwambia Nenda kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) na Fulani msikitini siku hiyo tunaomba na kumtaja Mola wetu akatoka Mtume wa Allah (S.A.W) mpaka akakaa nasi basi tukanyamaza, akasema "Yarejeni yale mliyokua mkiyatenda. Zaid akasema mimi na wenzangu wawili tukaomba kabla ya Abu Huraira, Mtume(ﷺ‬.a) akawa anasema aamin kwa dua zetu, halafu akaomba Abu Huraira "Ewe Mola hakika mimi nakuomba mfano wa waliokuomba wenzangu hawa wawili, na nakuomba elimu isiyosahaulika, basi Mtume wa Allah (S.A.W) akasema “aamin"Basi na sisi tukasema Ewe Mtume wa Allah (S.A.W) na sisi tunaomba elimu isiyosahaulika, akasema "Abu Huraira (ﷺ‬.a) amekutangulieni kwalo" Ad duusiy"[54]

Na Aamash amesema toka kwa Abi Saleh amesema "Alikuwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) katika wahifadhi wakubwa miongoni mwa Masahaba[55] . Amesema Al Shaafiy (ﷺ‬,a) "Abu Huraira (ﷺ‬.a) ndie hafidhi zaidi katika waliosimulia Hadithi katika wakati wake" [56]

Nae Ibn Abdil Barr amesema "Nae alikua hafidhi zaidi miongoni mwa Masahaba wa Mtume wa Allah (S.A.W), nae alikuwa akihudhuria wasimohudhuria Muhajirina kwa kushughulika kwao na biashara, na Ansaar kwa mashamba yao, nae Mtume wa Allah (S.A.W) amemshuhudia kwamba yeye ni mwenye pupa juu ya elimu na Hadithi"[57]

Na toka kwa Muhamad bin Amaari bin Amr bin Hazm kwamba yeye alikuwa amekaa kwenye majlisi ndani yake yumo Abu Huraira (ﷺ‬.a), na humo wamo mashekhe kumi na zaidi katika Masahaba wa Mtume wa Allah (S.A.W) basi akawa Abu Huraira (ﷺ‬.a) anawahadithia toka kwa Nabii (S.A.W) hadithi baadhi yao hawazielewi, kisha wanakumbushana kwenye hadithi hizo, baadhi yao wanazijua akawa anawahadithia hadithi hawaielewi baadhi yao, kisha akafanya hivyo mara kadha.Akasema "basi nikaelewa siku hiyo kwamba yeye ndie hafidhi zaidi wa watu toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W) " [58]

Nae Bukhaariy amesema "Wamesimulia toka kwake karibu maulamaa mia nane, nae alikuwa hafidhi zaidi wa waliosimulia Hadithi katika wakati wake. Amesema Abu Nuaim alikuwa hafidhi zaidi wa Masahaba kwa habari za Mtume wa Allah (S.A.W) na

alimuombea apendwe na walioamini [59] Hakim amesema "Hakika nimechunga kuanza katika fadhila za Abu Huraira (ﷺ‬.a), kutokana na hifadhi yake ya Hadithi za Mustafa (S.A.W) na kushuhudia kwa masahaba na matabiina kwake kwa hilo, kwani kila aliesoma Hadithi tokea enzi ya masahaba mpaka leo hii ni wafuasi wake na kundi lake kwa vile yeye ndie wa mwanzo wao na mwenye hadhi wao kwa jina la hafidhi ."[60]

Unatosheleza ushuhuda wa Masahaba hawa (ﷺ‬.a) na waliowafuatia katika vibendera vya maulamaa wa Ummah juu ya wingi wa riwaya na hifadhi yake ya Hadithi za Mtume wa Allah (S.A.W).

Uadilifu na Hifadhi Yake

Hakika uadilifu wa Mtume wa Allah (S.A.W) umethibiti kwa ufanwyaji uadilifu wa Allah na Mtume wa Allah (S.A.W) kwa Masahaba wa Mtume wa Allah (S.A.W), kwa Aya na Hadithi zilizotangulia na nyenginezo tusizozitaja kwa kuhofia kurefusha, na hivyo ni kutokana na ukweli wa imani yake na uzuri wa kukamatana na yale waliyoyatenda katika juhudi na kujitoa muhanga katika kuunusuru uislamu na kulinyanyua juu neno la Allah.

Amesema Al Khatib "Hata kwamba Allah na Mtume wa Allah (S.A.W) wasingeleta chochote katika tuliyoyataja hali waliokua nayo ya hijrah, jihadi kunusuru dini na kutoa nafsi, na mali' kuuwa mababa na watoto, unasihi wa dini, nguvu ya imani na yakini kukata juu ya uadilifu wao na kuitakidi utakaso wao, na kwamba wao ni bora kuliko wenye kufanywa waadilifu na kutakaswa ambao wanakuja baada yao.[61]

Kwa hivyo basi wamekubaliana maulamaa katika muhadithina na wengineo juu ya uadilifu wake pamoja na wenzake katika Masahaba (ﷺ‬.a), na kukubali riwaya zake zilizosihi kunasibishwa na yeye, ama zisizosihi kunasibishwa kwake basi hizo hazikubaliki, hazitolewi hoja kama riwaya nyengine zozote dhaifu na maudhui zilizonasibishwa na Sahaba mwengine yeyote yule katika Aalil Bait (Allah awe radhi nao).

Kutokana na hivyo basi hapazingatiwi utiliaji shaka wake au kwa zilizosihi kunasibishwa kwake katika riwaya toka kwa wale waliorithishana dhana mbaya dhidi ya Masahaba wa Mtume wa Allah (S.A.W), na wanarudiarudia uzushi wao katika wajinga wa sira ya Sahaba huyu mtukufu, na wanaodogosha cheo cha usahaba wake kwa Mtume wa Allah (S.A.W), na wakaleta yale yasioletwa na mfano wake au karibu yake kwa ajili ya dini hii wanaomsingizia yeye na wengineo katika watangulizi wa amani njema na maulamaa wenye ikhlasi .

Na iwapo uadilifu umehakikishwa kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) kwa kila kigezo kilichotangulia, basi pia pamehakikishwa hifadhi iliyokamilika kwa riwaya zake, hayo yameshuhudiwa na wanafunzi wake na wengineo waliochunguza hifadhi yake.

Amesimulia Imam Bukhariy kwamba, Muslim, Ahmad toka kwa Abi Hazim amesema "Nilikaa na Abu Huraira (ﷺ‬.a) miaka mitano nikamsikia anahadithia kutoka kwa Nabii (s.a.w) kwamba amesema Hakika Bani Israil walikua wakiongozwa na manabii, wote wakafariki Nabii nyuma ya Nabii, na kwa hakika hakuna nabii baada yangu",[62] hadithi inamaanisha kwamba hakuna kilichozidi wala kupungua katika hadithi hiyo katika muda wote uliotajwa.

Nae Hakim amesimulia toka kwa muandishi wa Marwani ibn Alhakam Amiri wa Madina amesema Kwamba "Marwan alimwita

Abu Huraira (ﷺ‬.a) akaniweka kitako nyuma ya kiti akawa anamuuliza, nikawa naandika mpaka ulipotimia mwaka kamili akamwita akamuweka kitako nyuma ya pazia, akawa anamuuliza kuhusiana na zile alizomuuliza mwanzo basi hakuongeza wala kupunguza, kutanguliza wala kuakhirisha"[63]

Kama hivyo ndivyo ulivyokua mtihani wa Marwani kwa hifadhi ya Abu Huraira (ﷺ‬.a) kama inavyoonesha, na hakuwa imla toka kwake kwa akielewa kuwa ataulizwa kama ilivyo wazi na katika yanayoshuhudia hifadhi na udhibiti wake ni ile ilotangulia toka kwa Ibn Omar " “Ewe Abu Huraira wewe ulikua mshikamanaji wetu zaidi wa Hadithi zake"[64]Na iliosimuliwa toka kwa Amaash toka kwa Abi Saleh amesema " Abu Huraira (ﷺ‬.a) alikua mwenye kuhifadhi zaidi wa Masahaba wa Mtume (S.A.W)"[65] Hivyo riwaya hizi na nyenginezo zilizotangulia zinajuilisha juu ya hifadhi yake iliyowafanya maulamaa waikubali hifadhi ya Abu Huraira (ﷺ‬.a), udhibiti wake, na kutolea umuhimu riwaya zake, ushughulikiaji wao wa riwaya zake na kulinganisha kwao baina ya sanadi zake kwa kuzingatia tofauti, kwa vile kauli kadha zimesimuliwa toka kwao. Imesemwa "Sanadi sahihi zaidi kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) Zuhriy toka kwa Said binil Musayyib toka kwake, na inasemekana Abu Zanaad toka kwa Aaraj toka kwake, nae imesemwa "Hamad bin Zaid, toka kwa Ayoub, toka kwa Muhammad bin Siyrin, toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a).“Na wakasema miongoni mwao " Hakika Sanadi sahihi zaidi ya Wayemen ni Maamar toka kwa Hamaam toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a). Na Ahmad bin Salih Amisriy akasema "Sanad iliyothabiti zaidi ya watu wa Madina; Ismail bin Hakiim, toka kwa Ubayda bin Sufiyan toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) ."

Nae Aba Bakril Burdijiy akasema "Wamekubaliana watu wa masimulizi juu ya usahihi wa hadithi za Zuhriy toka kwa Salim, toka kwa baba yake, toka kwa Said ibn al Musayyib toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a)"[66] Na vyovyote isemwavyo, hakika kauli hizi zinajulisha juu ya umuhimu wa riwaya za Abu Huraira (ﷺ‬.a), nakutoa umuhimu kwa muhadithina kuliko wazi, kuhifadhi, uzingatiaji na uandishi kiasi kwamba maimamu wa hadithi wameziweka kwenye vitabu vyao, hivyo vitabu sita na vyenginevyo katika vitabu mashuhuri na vilivyo kwenye mikono ya watu, vimetegemea riwaya za Abu Huraira (ﷺ‬.a) bila ya pingamizi kwao, hivyo inakaribia kuwa huoni mlango ila imo hadithi yake au zaidi.

NJIA ZAKE KATIKA RIWAYA

Hakika mwenye kuzingatia katika yale yaliyosimuliwa na Abu Huraira katika Hadithi atamuona kwamba amefata njia mbili kuuu katika kusimulia kwake,Njia yake ya mwanzo nayo ni riwaya tupu ya hadithi ya Mtume wa Allah (S.A.W). Nayo ni ile anayofupishia ndani yake kwenye ufikishaji wa yale aliyoyasikia toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W) katika kauli zake, au aliyoshuhudia katika vitendo au hali za wanafunzi wake au waulizaji wake kuhusu hadithi yenyewe kutokana na alivyoichukua toka kwake, au kuhakikisha kunasibishwa kwake na Mtume wa Allah (S.A.W) katika hiyo Na katika hizo ni Ile iliyosimuliwa na Abu Salamah bin Abdurahman toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) Amesema Mtume wa Allah (S.A.W) “ Mkamilifu wa walioamini kwa imani ni mzuri wao wa tabia, na mbora wao ni mbora wao kwa wake zake"[67] Nae Ikrima maula wa Ibn Abbas (ﷺ‬.a ) amesema "Niliingia nyumbani kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) nikamuuliza kuhusiana na Saumu siku ya Arafa huko Arafa, akasema amekataza Mtume wa Allah (S.A.W) Saumu siku ya Arafa huko Arafa"[68] .hivyo amefupisha katika kufikisha hadithi hizi mbili juu ya yale tu aliyomsikia Mtume wa Allah (S.A.W) kama ilivyo kawaida ya Muhadithina wa kisahaba, na waliokuja baada yao mataabiina na wengineo (ﷺ‬.a) katika kusimulia, na hii ndio ghalibu ya yaliyosimuliwa toka kwake katika Hadithi almarfuu'.

Njia ya Pili Ni Riwaya isiokua tupu

Nazo ni zile anazozisimulia pamoja na maneno yake akisherehesha humo riwaya, akitoa maana au hukumu inayopatikana, au katika riwaya nyengine katika jitihada zake na fahamu yake makhsusi kwa lengo la kufundisha na kueleza ambayo ni namna yake maalum iliyodhihiri kwenye uhai wake (ﷺ‬.a) wa kidaawa ambao aliupa umuhimu mkubwa kama tutakavyoona baadae. Na katika riwayo hizo kama mfano ni “Adhabu kali katika moto umevithibitikia visigino."[69]

Na ile iliyosimuliwa na Ahmad na Bukhariy toka kwa Salim bin Abdillahi amesema"sijui ni mara ngapi nilimuona Abu Huraira (ﷺ‬.a) amesimama sokoni akisema". Na kwa hili tunamuona kwenye riwaya hizi mbili ametanguliza maneno yake, pale alipoamrisha kutengeneza udhu kuhofia kuangukia kile alichokitahadharisha Mtume wa Allah (S.A.W), ni moto katika riwaya ya mwanzo .

Na katika riwaya ya pili akatanguliza kubainisha baadhi ya alama za Kiama, kama vile kuondolewa elimu , kudhihiri kwa fitina na kuzidi kwa mauaji, na hilo ni njia ya kutahadharisha kutokana na kuzama kwenye maasi, na kuwa mbali na utiifu wa Allah (S.W) na kumalizia kwa kutiliwa nguvu hilo na Mtume wa Allah (S.A.W).Na katika hadithi Iliyosimuliwa na Ahmad toka kwa Muhammad bin Ziyad, amesema "Nilimuona Mtume wa Allah (S.A.W) akipita kwenye watu wakitia udhu kwenye sehemu ya kutilia udhu akawambia " Tengenezeni udhu wenu Allah akurehemuni, hivi hamjasikia aliyoyasema Mtume wa Allah (S.A.W)".

Al-marfuu na Mawquuf katika riwaya za Abu Huraira (ﷺ‬.a)

Na kutokana na hali hii basi riwaya anazozileta kwenye mwanzo wa riwaya al-marfuu'(zinazonasibishwa na Mtume wa Allah (S.A.W) au mwisho wake baada ya mawquuf yake (iliyonasibishwa na Sahaba (ﷺ‬.a), kwani ni katika maneno yake yeye, sio katika al-marfuu, na ni ile ambayo akiulizwa mara nyengine,jee umeisikia toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W)? husema la hii inatoka mfukoni mwangu, au mfuko wa Abu Huraira .

Ama baadhi ya wasiokua na elimu ya Hadithi,au kuelewa njia za Abi Huraira katika riwaya kwamba anamaanishakwa kwa kauli yake hii, riwaya kwa vigawanyo vyake viwili (almarfuu na almawquuf) hakuna mawquuf maalum, hivyo husema kwa kutoelewa kwamba Abu Huraira husema yale anayoyasema yeye binafsi kwa Mtume wa Allah (S.A.W), na maneno haya yamesadifu nafsi za wenye maradhi, kwenye nyoyo zao, hivyo wanazirejearejea, huenda inawatilia nguvu katika wanayoyazua juu ya Sahaba huyu mtukufu.

Kutolea kwake Umuhimu Suala la Daawa na Kufikisha Elimu

Abu Huraira mmoja wa maulmaa wa Masahaba (ﷺ‬.a),ambao walijibebesha amana ya Daawa na kufikisha elimu walioipata toka kwa Mtume (S.A.W.) bali yeye alikuwa mwenye harakati zaidi katika uwanja huu, na hivyo ni kutokana na upana wa elimu yake toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W) na haja ya watu juu ya elimu yake katika wakati wake, kuwasomesha na woga wake wa adhabu ya kuficha elimu, imesimuliwa toka kwake kwamba amesema "Naapa na Allah lau sio Aya katika Kitabu cha Allah nisingekuhadithieni chochote abadani" kisha akasoma Aya {Hakika wale wanaoficha yale tuliyoyateremsha katika ubainishaji na Mongozo} [Al Baqarah 159]

Vile vile imesimuliwa toka kwake kwamba amesema Amesema Mtume wa Allah (S.A.W) "Yeyote alieulizwa kuhusiana na elimu akaificha atatiwa ujamu katika jamu za Moto siku ya Kiama"[70] Na imesimuliwa toka kwa Hassan toka kwake kwamba amesema Amesema Mtume wa Allah (S.A.W) " Hakuna mtu yeyote anaebeba katika yale Allah na Mtume wake aliohukumia neno moja au mawili au matatu au manne au matano akayaweka kwenye ncha ya nguo yake akayafanyia kazi au akayafundisha" Nikasema mimi nikatandika nguo yangu, basi Mtume wa Allah (S.A.W) akawa anahadithia mpaka hadithi yake ikamalizika, basi nikaiweka nguo yangu kwenye kifua change.[71] Na hivi Abu Huraira alifuata kila njia ya daawa iliyowezekana na kufikisha yale aliyoyachukua toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W) miongoni mwa elimu na maarifa, hivyo tunamuona anatoa mawaidha na kuhadithia kila pahala anapopata fursa ya kufanya hivyo, nyumbani, sokoni, msiktini na mwenginemo katika mwahala anamoweza kuhadithia na kutoa mawaidha.

Amesimulia Imam Ahmad toka kwa Ikrimah amesema "Niliingia nyumbani kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a), nikamuuliza kuhusiana na Saumu ya A'rafah Haditi hii iliyotangulia karibuni. Nae Hakim amesimulia toka kwa Aswim bin Muhammad toka kwa baba yake amesma "Nimemuona Abu Huraira (ﷺ‬.a) akitoka siku ya Ijumaa, Basi akakamata matovu ya membari akiwa amesimama huku akisema "Ametuzungumzia Abal Qaasim Mtume wa Allah (S.A.W), Mkweli Mwenye kuaminiwa (S.A.W) basi hakuwacha anahadithia mpaka akasikia –sauti ya –mlango kwa ajili ya kutoka Imamu kwa ajili ya Sala akakaa"[72] Abu Huraira (ﷺ‬.a) akasimama akawahadithia toka kwa Mtume (SAW) mpaka kukakucha. Nae Abu Huraira (ﷺ‬.a) hakutoshelezeka na kuhadithia na na mawaidha na kuongoza wanaume tu bali pia alifika kwa wanawake kuwahadithia na kuwapa mawaidha kwa wanayoyahitajia, na yanayoambatana na mambo yao,

Amesimulia Ahmad na Bukhariy toka kwa Salim bin Abdillahi bin Omar (ﷺ‬.a) amesema “sielelewi ni mara ngapi nimemuona Abu Huraira (ﷺ‬.a) akasimama sokoni akisema "Allah ataichukua elimu na fitina itadhihiri." Na kutoka kwa Mak-huul amesema "Watu waliweka ahadi ya kukusanyika Qubaa, wakakusanyika, basi Abu Huraira akahadithia, mawaidha na kuelekeza mpaka asubuhi"[73],

Imam Ahmad toka kwa Ubaid Maula wa Abdurahman, toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) "Kwamba alikutana na mwanamke aliejitia manukato kwa ajili ya Msikiti akamwambia umejitia manukato kwa ajili ya msikitini? akamwambia "naam". Akamwambia "Amesema Mtume wa Allah (S.A.W) Hakuna mwanamke yeyote aliejitia manukato kwa ajili ya Msikiti atakaekubaliwa sala yake na Allah (S.W) mpaka atakapokoga kwa ajili ya janaba, hivyo nenda ukakoge.[74]

Nae Al Awzai amesimulia toka kwa Ismail bin Ubaidilahi, toka kwa Karima binti Alhasan amesema nimemsika Abu Huraira (ﷺ‬.a) kwenye nyumba ya Ummu Dardaaiakisema "Mambo matatu ni katika kufuru Kwanza, kuchana nguo na kutia ila kwenye nasabu"[75] Namna hii ndio Abu Hurairah (ﷺ‬.a) alivyommbainishia mwanamke aliejitia manukato kutoruhusiwa kutoka kwake toka kwenye nyumba yake akiwa mwenye kujitia manukato mwenye kujipamba, hata kutoka kwake kukiwa kwa ajili ya kwenda kutekeleaza sala msiktini, na akamuamrisha arejee nyumbani kwake akoge kutokana na kujitia manukato atakapotaka kurejea msiktini, na tahadhari kubwa ilioje kwa wanawake wakiislamu leo hii lau wangechunga maelekezo haya ya kinabii, ili kuhifadhi nafsi zao kutokana na macho ya waovu, na nafsi zenye maradhi zilizopotea. Kama vile alivyowatahadharisha wale aliowakuta kwenye nyumba ya Ummu Dardaai taabiiya alie mbora, mke wa Abu Dardaai Sahaba mtukufu (ﷺ‬.a), kutokana na mambo matatu yanayofanywa sana na wanawake, nazo ni katika ada za kijahilia zilizoharamishwa na Uislamu na kufanywa sawa na ukafiri, kwani humpelekea aneyatenda kwenye Moto, kama kufuru inavyomfikisha mwenyewe kwenye Moto, nae hakika amefuata njia ya kimalezi ya kidaawa yenye kufanikiwa, pale alipowahutubia watu kwa njia zilizo mnasaba na wao, akiwa katika kazi hiyo njia ya kimalezi ya kidaawa ya mwanzo, ambayo nguzo zake zilisimamishwa na Mtume wa Allah (S.A.W) , nae (ﷺ‬.a) ametumia fani kadha wa kadha katika mbinu zake za Daawa kama ifuatavyo

Mbinu ya Kuhamasisha

Amesimulia Haithamiy toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) Kwamba alipita soko la Madina, akasimama, akasema. "Enyi watu wa soko nini kimekushindeni? wakasema ni nini hicho Ewe Abu Huraira? akawaambia ile mirathi ya Mtume (S.A.W) inagaiwa na nyie mpo hapa! Hamwendi kuchukua sehemu yenu? Wakasema Iko wapi? akawaambia iko msiktini, wakakimbilia mbio nae Abu Huraira (ﷺ‬.a) akasimama kuwangojea mpaka wakarejea akawaambia mmepata nini? wakasema "Tumekwenda na hatukupata chochote kinachogaiwa, akawaambia "na hamkumuona yeyote msikitini? Wakasema ndio tumewaona watu wanasali, wengine wanasoma Quran, kaumu wanakumbushana halali na haramu, Abu Huraira (ﷺ‬.a) akawaambia Na ni hiyo (mirathi ya Muhammad (S.A.W)) ,[76]Na kwa mbinu hii ya kidaawa madhubuti Abu Huraira aliwabanishia mirathi ya kikwelikweli, kwani hakurithiwa dirham wala dinar wala chengine chochote katika mali, ila aliwaachia Qura-n na Sunna, iliyo na aina mbali mbali za mwongozo, maarifa na mafanikio.

Mbinu ya Kutisha

Kama alivyotumia njia ya kuhamasiha katika Daawa, pia alitumia mbinu ya kutisha kwenye Daawa.pamoja na walinganiwa waliokua wakifanya maasi kwa ujinga, au kukadiria vibaya yale yanayopelekea maasi hayo. Katika hayo ni yale mawaidha yake kwa wanawake yaliyopita, kwenye nyumba ya Ummi Dardaai (ﷺ‬.a) na kuwatahadharisha kwake kwanzai, kuchana nguo na kutia aibu nasabu, ambayo aliyahesabu katika ukafiri, kutoka na kupelekea kwake madhambi na adhabu kali.vile ni yaliyosimuliwa toka kwake kwamba amesema " Kamilisheni Udhu kwani mimi nilimsikia Abal Qaasim (S.A.W) Akisema "Adhabu kali kwa vifundo kutokana na Moto.[77]

Mbinu ya Kukabili na Uwazi

Toka kwa Qataada toka kwa Abi Umaril Ghadaniy, amesema nilikua kwa nimekaa, akasema akapita mtu katuka Bani Aamir Swaaswaa, akaambiwa Huyu ndie Aamiriy mwenye mali zaidi, akaambiwa na Abu Huraira (ﷺ‬.a) "Mrejesheni kwangu" basi wakamrejesha kwake, akamwambia nimepewa habari kwamba wewe ni mwenye mali nyingi, akasema Aamiriy "Ndio Wallahi, hakika mimi ninao ngamia mia wekundu, mia wa rangi ya udongo, mpaka akamaliza rangi za ngamia, fani za watumwa, na mazizi ya farasi, basi Abu Huraira akasema "Ole wako na kwato za ngamia na kwato za mbuzi, na kurejea hivyo mpaka rangi ya Aamiry ikageuka na kukoza, akamwambia na hivyo ni vipi Ewe Abu Huraira (ﷺ‬.a)? akamwambia; nilimsikia Mtume wa Allah anasema. Yule mwenye ngamia asitowe haki zake kwenye najdi na risli yao “Tukamwambia Ewe Mtume wa Allah nini najdi na risli yao? Akasema “ Kwenye tabu na raha zao" Hakika watakuja siku ya Kiama kama vile mwenye kupewa chakula zaidi walivyokua wakubwa mbele yao, mnene wao na mwenye nguvu wao, kisha watamchoma kwa pembe kali, wampondeponde kwa

kwato zao wa mwisho wao akimaliza anarejeshwa wamwanzo wao,siku ambayo kiwango chake ni miaka khamsini elfu, mpaka Allah atakapowahukumu watu aonyeshwe njia yake."

Hivyo Aamiriy akasema na ni ipi haki ya ngamia Ewe AbuHuraira? akasema utoe mzuri na uwape wengi ,utoe msaada wa kipando, unywesheze maziwa, na utoe madume ya kupandishia"[78]Na lau tutafuatilia juhudi za Abu Huraira (ﷺ‬.a) za kidaawa na usomeshaji na mbinu zake katika mambo hayo basi nafasi hii itarefuka, na kuzuwia tulizozileta katika dalili kutokana na ukubwa wa wa juhudi aliyoitoa,na kwa wingi wa waliofaidika toka kwake na wabebaji wa elimu yake(ﷺ‬.a)

Na Abu Huraira (ﷺ‬.a) alisimama mbali na khitilafu zilizotokea katika siku zake, na miongoni mwao ni ile fitina ilioenea baina ya Amiril Muuminiin Ali bin Abi Talib na Muawiya bin Abi Sufiyan wote(ﷺ‬.a), na kundi la Masahaba lilikuwa na msimamo huu ambao ni kujiepusha na fitina, kama vile Saad bin Abii Waqaas, Said bin Zaid bin Nufail, Abdillahi Omar bin Alkhatab, Muhammad bin Maslamah, Salama bin Al-akwa na wengineo (ﷺ‬.a).

Hapakupatikana cho chote kinachoonyesha kufungamana na upande wowote sio maneno wala vitendo, kama ambavyo hapakunukuliwa toka upande wowote kwamba ulitaka uungwaji wake mkono au asimame kwenye upande wake kwani kwake hakukua na maslahi yoyote kama mithali inavyosema (hana farasi wala ngamia) kama ambayo yeye anapendelea salama vyovyote inavyowezekana, wala hakutoka kwenye msimamo huo ila siku aliozingirwa Amiiril Mu-uminiin Othman (ﷺ‬.a), kutokana na fitina za kundi la waasi lililomuua kwa [79] dhuluma mwaka 35H.pale alipoingia kwake yeye kwa lengo la kumlinda, kama vile Hassan bin Ali bin Abi Talib, Abdillahi bin Omar na Abdillahi bin Zubeir na wengineo(ﷺ‬.a.)

Amesimulia Hakim toka kwa Musa bin Uqbah na ndugu zake Muhammad na Ibrahim wamesema "ametuhadithia Abu Hassan "Tulimshuhudia Abu Huraira na Othman wamezingirwa ndani kwenye nyumba na akamuomba ruhusa ya kusema, basi Abu Huraira akasema "Nilimsikia Mjumbe wa Allah akisema " Hakika ni fitina na khitilafu, au khitilafu na fitina, akasema tukamwambia Ewe Mjumbe wa Allah hivyo unatuamrisha nini?, akasema 'Ni wajibu wenu kumlinda kiongozi wa waislamu na watu wake na akaashiria kwa Othman" [80].

Hichi bila shaka ni kielelezo cha msimamo wa ujasiri wa Abu Huraira (ﷺ‬.a), kudhihirisha katika wakati tete usiojulikana matokeo ya kauli ya haki kwa mwenyewe, nae alibakia kwenye nyumba mpaka wakamshinda yeye na waliokua pamoja nae, na Othman akauawa akiwa shahidi (ﷺ‬.a) na Allah amlipe kheri kutokana na uislamu, ubora wa malipo wanayolipwa Siddiqiin, na Mashahidi, na bila shaka urafiki na watu hao ni kitu chema. Na Umawiyina waliuenzi msimamo huu na baadae kumpa hadhi, na huenda kuwa jambo hili ndilo lililopelekea balaa ya wenye matamanio ya nyoyo yakawapelekea kumzulia na kumvunjia heshima.

Abu Hurairah na Aalul Bait(ﷺ‬.a)

Abu Hurairah (ﷺ‬.a) alikuwa akiwapenda Ahlul Bait, kuwatukuza, kuelewa fadhila zao, mwenye kuenzi ujamaa wao na Mtume wa Allah, mzingatiaji wa wasia wa Mtume wa Allah (S.A.W) kwao wakisimulia riwaya nyingi katika fadhila na sifa zao, na mapenzi ya Nabii (S.A.W), na yafuatayo ni baadhi ya yaliyosimuliwa toka kwake kuhusiana na matendo yao mema (ﷺ‬.a)

Mwanzo –Yaliyosimuliwa toka kwake katika sifa za Ali (ﷺ‬.a)

1- Amesimulia Sahl bin Abi Saleh toka kwa baba yake toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) Kwamba Mtume wa Allah (S.A.W) alisema siku ya Khaibar "Kwa hakika bendera hii nitampa mtu anaependwa na Allah na Mtume wake, Allah atakomboa kwenye mikono yake "basi Mtume wa Allah akamwita Ali bin Abi Talib, akampa yeye na kumwambia 'Nenda wala usiangalie nyuma mpaka Allah akomboe juu yako" akasema "basi Ali akaenda kidogo, halafu akasimama na hakuangalia huku na kule, akasema nae kwa sauti kubwa Ewe Mtume wa Allah nipiganie watu juu ya nini? "akamwambia "Pigana nao vita mpaka washuhudie kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa ila Allah, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah, basi iwapo watafanya hivyo, wamejizuilia damu na roho zao ila kwa haki na hesabu yao kwa Allah"[81]

2- Na kutoka kwa Mujrir bin Abii Huraira toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) amesema " Nilikua pamoja na Ali bin Abi Talib pale alipopelekwa Makkah na kwa Bira-ah, akasema "Nini ulikua mukitangaza? akasema tukitangaza kwamba haingii Peponi ila Mu-min, asitufu Al Kaaba, na yeyote mwenye ahadi na Mtume (SAW) basi muda wake, au ameuongeza mpaka miezi minne, hivyo ikimalizika miezi minne, basi Allah atakua mbali na washirikna na Mtume wake, wala asihiji mshirikina baada ya mwaka huu, akasema "basi mimi nilikua nikitangaza mpaka sauti yangu ikakauka".[82] Nimeibainisha riwaya hii kwamba yeye alikua pamoja na Ali (ﷺ‬.a) katika kutekeleza jambo muhimu walilokalifishwa na Mtume (S.A.W). Na toka kwa Abii Raai amesema "Nilimwambia Abu Huraira (ﷺ‬.a) "Hakika Ali (ﷺ‬.a) akiwa Iraq kwenye Sala ya Ijumaa husoma Suratul Jumaa na Idhaa ja-akal munaafiquun, akasema "hivyo hivyo alikua akifanya Mtume wa Allah (S.A.W) .[83] Na katika riwaya hii anataja miongoni mwa fadhila za Ali Bin Abi Talib (ﷺ‬.a), nako ni kumfuata Mtume (S.A.W) katika masuala haya na kumfuata.

Pili- Yaliyosimuliwa toka kwake katika sifa za Ja'afar bin Abi Talib.

Imesimuliwa toka kwake (ﷺ‬.a) kwamba amesema "Na aliekua mbora wa watu katika kwa maskini ni Jaafar bin Abi Talib, nae alikua mara nyingi anatujia anatupa chakula kilichopo nyumbani mwake mpaka ikawa anatujia na akka[84] iliyokuwa kwake yenye kitu tunaipasua tunaipachika.[85] Na kutoka kwa Almuqbiry toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) amesema "Jaafar bin Abi Talib alikua akipenda maskini na kukaa nao na kuzungumza nao, na Mtume (SAW) alikua akimwita Abu masaakiin .[86]

Tatu- Yaliosimuliwa toka kwa kwake katika sifa za Hasan na Husein (ﷺ‬.a)

1- Imesimulia toka kwake kwamba "Mtume (S.A.W) alimuweka Hasan shingoni."[87] Na katika riwaya toka kwake toka kwa Nabii (S.A.W) kwamba alisema kuhusu Hasan "Ewe Mola hakika mimi nampenda basi mpende na mpendezeshe ampendae.[88]

2- Imekuja toka kwake kwamba amesema "Hakukua na yeyote kipenzi aliezidi kwangu kuliko Hasan bin Ali baada ya Mtume wa Allah (S.A.W) kusema alioyoyasema.[89]Na kutoka kwa Umeir bin Ishaq amesema "Nilikua nakwenda pamoja na Hasan bin Ali kwenye njia za Madina, tukakutana na Abu Huraira (ﷺ‬.a) basi akmwambia Hasan "Nikunjulie tumbo lako -nimejifanya kuwa fidia yako- mpaka nibusu pale nilipomuona Mtume wa Allah (S.A.W) anapabusu, akasema basi Hasan akakunjua tumbo lake na akapabusu".[90]

3- Na toka kwa Abdu rahman bin Masoud toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) amesema "Alitoka kuja kwetu Mtume wa Allah (S.A.W) akiwa pamoja na Hasan na Husein, huyu yuko kwenye bega lake na huyu yuko kwenye bega lake, akibusu mdomo wa huyu mara hii na mara nyengine huyu, mpaka akatufikia sisi, mtu mmoja akamwambia "Ewe Mtume wa Allah hakika wewe unawapenda akamwambia " Naam, na anewachukia basi huyo amenichukia mimi “ [91].

4- Na toka kwake (ﷺ‬.a) amesema "Sikumuona Alhassan bin Ali iIa macho yangu yalitoka machozi, na hivyo ni kwa sababu Mtume (S.A.W) mara moja alitoka akanikuta msikitini akachua mkono wangu, halafu akarejea nikarejea pamoja nae, mpaka tukafika soko la Bani Qainuqai, akasema Na hakunisemesha, akazunguka na akaangalia, kisha akarejea nikarejea pamoja nae, akakaa msikitini na kusimamisha miguu -kwa kuifunga nguo, akasema "Niitie Laka'a" akaja Husein mpaka akaangukia juu ya paja lake, akaingiza mkono wake kwenye ndevu za Mtume wa Allah (S.A.W), akawa Mtume wa Allah (S.A.W) anafungua mdomo wa Husein na kuingiza mdomo wake kwenye mdomo wake huku akisema "Ewe Allah hakika mimi napenda basi nawe mpende" [92]

Na inatosheleza tuliosimulia katika aliosimulia Abu Huraira (ﷺ‬.a) katika sifa zao, na yale aliyosimulia Abu Huraira (ﷺ‬.a) katika sifa za Aalil Bait (ﷺ‬.a), kuwa ni dalili tunazozitaka katika sifa juu ya uhusiano wa mapenzi kwao kutoka kwa Abu Huraira, mapenzi yake kwao na pupa lake juu ya kudhihirisha sifa zao, na kudhihirisha fadhila zao (ﷺ‬.a) na ni dalili ya kutoelewa kwa wale wanaojisemea kuhusiana na uhusiano huo, nayo ndio mapenzi ya kweli kwao. Na haya yakisemwa ni kwamba hapakuthibiti toka kwa yeyote yule katika Ahlil Bait linalojulisha utiaji ila wao kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a), au kumtukana isipokua imethibiti kwamba baadhi yao wamesimulia toka kwake, na kwamba wengi wa waaminifu (thuqaat) na wasimulizi toka kwao, wamesimulia toka kwake, na kwamba wengi wa waaminifu wa wanafunzi wao na wasimulizi toka kwao, wamesimulia toka kwake vilevile kwa sababu ya elimu yao bila ya upinzani toka kwa yeyote miongoni mwao, jambo linalojuilisha kumkubali kwao, na kukubali kwao riwaya zake, na anaetaka kuhakikisha tuliyoyaeleza, basi arejee kitabu cha (Difa'a 'an Abu Huraira (ﷺ‬.a) ) kilichoandikwa na Ustadh Abdil Munim Saleh Al Alii, humo ataona uhakika wa hayo.

MLANGO WA PILI

SHUBUHA ZA BATILI ZILIZOENEZWA DHIDI YAKE

Sehemu ya kwanza

shubuhati za batili zilizoenezwa dhidi yake

Usuhuba wa Abu Huraira (ﷺ‬.a), utumishi wake kwa Mtume wa Allah (S.A.W), uchukuzi wa Sunna zake, wala mwenendo wake mzuri, tabia zake tulivu, kusifiwa kwake na ndugu zake katika Masahaba (ﷺ‬.a) na kutukuzwa kwake na maulamaa wa umma baada yao katika Mataabiina na wengineo na kumpa kwao cheo, hayo yote hayakuwazuwia watu wa upotofu kumsema vibaya, na kumpakazia shubuhati batili, na miongoni mwao ni zile wasimulizi wake walizozikusudia, na maulamaa wakazirudi waliotangulia, na Muhadithiina na kubainisha uzushi na ubatili wao, na miongoni mwao ni yale ambayo wasimulizi wake walioangusha hadhi yake kwa ujumla, nasi tutajaribu kuzirudi aina hizi za shubuhati na kuonyesha uongo wake kwa kadiri Allah (S.A) atakavyotuwepesishia kiushahidi na dalili

Shubuha Ya Mwanzo

Wingi wa riwaya zake

Baadhi ya wasimulizi wanaona wingi wa riwaya zake pamoja na ufupi wa muda wa usuhuba wake kuwa ni jambo linalopelekea shaka katika kusihi kwa riwaya hizo, na shubha hii inajibiwa kwa njia zifuatazo

1-Kwamba wingi wa riwaya ni wingi kwa kulinganisha na wengine na sio wingi wa moja kwa moja kwamba yeye ndie Sahaba aliesimulia zaidi toka kwake katika Masahaba, na sio mwenye kuhifadhi zaidi toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W). Na linalotilia nguvu hilo ni kukiri kwake (ﷺ‬.a) kwamba yale yalio kwa Abdillahi bin Amri binl Al-asi (ﷺ‬.a) katika hadithi ni nyingi kuliko zilizo kwake, kwani Abdillahi kama alivyosema "alikua akiandika na yeye hakuwa akiandika, na ndilo aliloweka wazi Imamu Abu Bakri bin Khuzaimah kwa kauli yake " Alikuwa ndie mwingi Masahaba zake kwa riwaya toka kwake katika zile zilizoenea katika riwaya ama riwaya za wengine katika Masahaba zake (S.A.W) zimo kwenye Sihahi (Vitabu vya Hadithi Sahihi)[93]

Na ukosefu wa wingi wa riwaya kwa asiekua yeye katika waliorefukiwa na muda wa usuhuba wao pamoja na Mtume wa Allah (S.A.W) ni jambo lililohusiana na mtu mmoja mmoja, na sababu zake hurejea kwenye vifo vya mapema vya baadhi yao, kwa vile wapo baadhi yao waliofariki wakati wa Mtume wa Allah (S.A.W), wengine mara baada ya kifo chake (S.A.W), kama vile ambavyo wengine walikua na riwaya chache kwa sababu hawakua wakisimulia mpaka walipoulizwa, na katika hao walikua Makhalifa Rashiduun, wanne, Ubayya bin Ka'ab, Ibn Masoud, Abuu Said Al Khudriy, na wengineo.

2- Hakika ufupi wa muda wa suhuba wake na sio ufupi wa ujumla.Yaani kwa kulinganisha na yule ulierefuka usuhuba wao na Mtume wa Allah (S.A.W), kama kumi waliobashiriwa Pepo, na wengineo katika waliotangulia kwenye Uislamu miongoni mwa Masahaba (ﷺ‬.a) na vyenginevyo basi kwa uhakika sio muda mfupi kama zilivyo dhana hizo potofu, kwa vile ni zaidi miaka minne kama ilivyotangulia.[94] Nao ni muda unaotosheza kabisa kwa hayo aliyoyakusanya, na kusimulia aliyoyasimulia katika Hadithi, ikieleweka kwamba alikamatana nae mkamatano uliokamilika, nyumbani na safarini, akizunguka alipozunguka, alijitenga katika kipindi hicho kwa ajili ya elimu, hakushughulishwa na chochote katika vyenye kushughulisha katika biashara, kilimo, au kushughulikia familia yake au jengine lolote, ni mkamatano wasiouweza wengi wa Masahaba uliorefuka usuhuba wao na Mtume wa Allah (S.A.W) kutokana na kushughulika kwao na mambo ya lazima ya kimaisha, amesimulia Al baraa bin Aazib (ﷺ‬.a),“Sio kuwa sote tulisikia Hadithi za Mtume wa Allah (S.A.W), lakini tulikua na mashughuliko, ila watu siku hizo hawakua wakisema uongo, basi akihadithia alieshuhudia asiekuwepo.[95]

Na imesimuliwa kwamba mtu alikuja kwa Talha bin Ubaidulahi (ﷺ‬.a), akamwambia "Ewe Abu Abdallah, Wallahi hatuelewi Myemeni huyu ni mtaalamu zaidi kwa Mtume wa Allah (S.A.W) au nyie? Amemsemea Mtume wa Allah (S.A.W) asiyoyasema, akimaanisha Abu Huraira (ﷺ‬.a), Talha akasema "Wallahi hapana anaeshuku kwamba yeye amemsikia Mtume wa Allah (S.A.W) sisi tusioyasika ,na akaelewa tusiyoyaelewa, hakika sisi tulikuwa ni watu matajiri, tunazo nyumba na jamaa, tulikuwa tunakwenda kwa Mtume wa Allah (S.A.W) asubuhi na jioni na kurejea".

Nae Abu Huraira alikua maskini asiekua na mali, mke, wala mtoto, hakika mkono wake ulikua na mkono wa Mtume wa Allah (S.A.W), nae alikua akienda na Mtume wa Allah (S.A.W) popote aendapo, hatuna shaka kwamba alitenda tusioyatenda na kusika tusioyasika, hakuna aliemtuhumu ye yote katika sisi kwamba amemsemea Mtume wa Allah (S.A.W) asiyoyasema.[96]

Kama ambavyo vile vile wakishughulika na mambo ya Daawa, na kutekeleza kazi walizokua wakipewa na Mtume wa Allah (S.A.W), kama vile kutoka kwenye doria na vita, na kufikisha elimu, kupeleka barua kwa wafalme na viongozi waliokua majirani na Bara Arabu, mambo ambayo yalipelekea kusafiri na kuwa mbali na Mtume wa Allah (S.A.W) na kutokaa nae (S..A.W) na kuweko kwao mbali huweza kudumu masiku na miezi.

Kama ambavyo miongoni mwao wamo waliokua hawakai na Mtume (S.A.W) Madina, hivyo haukua wepesi kwake kukutana na Mtume (S.A.W) wakati wowote atakaotaka. Kwa sababu hizi na nyenginezo haikua wepesi kushikamana kuliko kamilika kwa wengi wa uliorefuka usuhuba wao kwa Mtume (S.A.W), kama ilivyomuwepesikia Abu Huraira (ﷺ‬.a), nae Ibn Omar (ﷺ‬.a) anashuhudia hilo kwenye riwaya iliyosimuliwa toka kwake kwamba amesema, "Ewe Abu Huraira hakika wewe ulikuwa mwenye kushikamana na Mtume (SAW) zaidi Mtume wa Allah (S.A.W) na mwenye kuhifadhi zaidi Hadithi zake kuliko sisi .[97]

3- Pupa lake juu ya kupata na Dua za Mtume wa Allah (S.A.W) kwake ya kuhifadhi Abu Huraira (ﷺ‬.a) alikua mwenye kushughulikia elimu, mwenye pupa la kujifunza, hilo lilishuhudiwa na Mtume wa Allah (S.A.W), amesimulia Imam Bukhary toka kwa Saidil Muqbiry, toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a), Amesema "Nilisema Ewe Nabii wa Allah ni nani anaestahikiwa zaidi na Shufaa yako? Akasema "Nilidhani hatoniuliza Hadithi hii mwengine mwanzo kuliko wewe, kutokana na pupa lako la Hadithi"[98] Na inatosheleza kwa ushahidi huo, ushahidi juu ya pupa lake (ﷺ‬.a) juu ya elimu na kuitafuta na kwa hivyo tunaona Mtume wa Allah (S.A.W), anamshajiisha Abu Huraira (ﷺ‬.a) kutafuta elimu, kama alivyowashajiisha Masahaba wake wengine aliogundua akili, hamu na utayarifu wao kwa hilo. Kama vile Anas bin Malik, Ibn Abbas na wengineo.

Nae Mtume wa Allah (S.A.W) alimuombea Abu Huraira (ﷺ‬.a) kwa hifadhi na kutosahau, pale aliposema –amin- kwa dua yake kwa jambo hilo. Kutoka kwa Zaid bin Thabit (ﷺ‬.a), amesema Hakika mimi nilipokua nimekaa na Abu Huraira (ﷺ‬.a), na fulani msikitini siku hiyo tunaomba na kumtaja Mola wetu akatoka Mtume wa Allah (S.A.W) mpaka akakaa nasi, basi tukanyamaza, akasema yarejeeni yale muliokua mkiyatenda. Zaid akasema "mimi na wenzangu wawili tukaomba kabla ya Abu Huraira (ﷺ‬.a), Mtume akawa anasema –amin- kwa dua zetu, kisha akaomba Abu Huraira (ﷺ‬.a) "Ewe Mola hakika mimi nakuomba mfano wa waliyokuomba wenzangu hawa wawili, na nakuomba elimu isiosahaulika, basi Mtume wa Allah (S.A.W) akasema “-amin-" na sisi tukasema "Ewe Mtume wa Allah (S.A.W) na sisi tunaomba elimu isiosahaulika, akasema "Amekutangulieni kwalo Ad duusiy"[99] Na hivi inaonyesha namna (S.A.W) alivyokua akitilia umuhimu kufikisha kile alichokua akikibeba katika elimu na kuwafikishia wale waliokua tayari zaidi kuichuka na kuihifadhi katika vijana wa kisahaba (ﷺ‬.a), kila mmoja kwa mujibu wa kuwa kwake tayari na alivyowepesikiwa.

4- Masuala yake kwa Mtume (S.A.W) Ikiwa masuala kama ilvyosemwa ni funguo za elimu basi alikua katika waliozidisha, wenye kujijusurisha kwayo, kwani alikua akimuuliza Mtume wa Allah (S.A.W) katika yale alioyaona yanahitajia suala, kutafuta elimu, na kujizidishia maarifa toka kwenye chemchem yake iliyo safi, na chanzo chake cha mwanzo, na katika hayo ni suala lake kuhusiana na mtu mwenye kufanikiwa zaidi kwa Shufaa yake (S.A.W) siku ya Kiama kwa kauli yake "Ewe Nabii wa Allah ni nani anaestahikiwa zaidi na Shufaa yako? Akasema "Nilidhani asingeniuliza hadithi hii mwengine mwanzo kuliko wewe, kutokana na pupa lako la hadithi, mtu mwenye kufanikiwa zaidi kwa shufaa yangu siku ya kiama ni yule aliesema -Laa Ilaaha illa Allah- yenye ikhlasi ndani ya nafsi yake "[100]

Na kutoka kwa Ubay bin Ka'ab (ﷺ‬.a) amesema "Abu Huraira (ﷺ‬.a) alikuwa jasiri kwa Mtume wa Allah (S.A.W) anamuuliza mambo tusiomuuliza sisi"..

Na kutoka kwa Hudhaifa (ﷺ‬.a) amesema mtu mmoja alimwambia Ibn Omar "Hakika Abu Huraira (ﷺ‬.a) anazidisha Hadithi toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) katika amesema ,"Ibn Omar akasema "Namuomba Allah akuepushe kuwa na shaka katika anayokuja nayo lakini yeye alifanya ujasiri nasi tukafanya woga"[101].

Na zimethibiti (ﷺ‬.a) riwaya zake toka kwa Masahaba walio wengi (ﷺ‬.a), kama vile Abubakri, Omar, Al Fadhil bin Abbas,Ubay bin Kaab, Usama bin Zayd, Aishah, Sahl bin Saad As Saaidy, na Nadhwarata ibn Nadhwarata na wengineo. Ukiachia riwaya alizozisimulia toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W) moja kwa moja, mara nyengine alikuwa akisimulia toka kwa aliemchache zaidi wa riwaya kuliko yeye, amesimulia toka kwa Sahl bin Saa'd As Saai'dy, amesema Amesema Mtume wa Allah (S.A.W) "Mmoja wenu asimuelekezee upanga mmoja wake huenda shetani akamnyang'anya mkononi mwake, akaangukia kwenye shimo katika mashimo ya Moto" Akasema Abu Huraira (ﷺ‬.a) "Nimemsikia Sahl bin Saad As Saaidy toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W) [102].Na idadi alizosimulia toka kwa Masahaba zimechangia katika kuzidisha idadi ya hadithi zilizosimuliwa toka kwake, jambo ambalo hawalijui au wanajifanya hawalijui wanaomfanya Abu Huraira (ﷺ‬.a) amezidisha katika riwaya zake.

5- Kuchelewa kwa kifo chake na haja ya watu kwenye elimu yake, na wingi wa riwaya zake toka kwake. Alikua Abu Huraira (ﷺ‬.a) Masahaba wa Mtume wa Allah (S.A.W), ambao umri wao ulirefuka mpaka baada ya 50H, na watu wakawa wanahitaji na kumwendea kwenye mambo yaliowatatiza juu yao, na kwa kuwa alikuwa katika Masahaba waliohifadhi Hadithi nyingi zaidi za Mtume wa Allah (S.A.W) kuliko wengine, aliekusanya na mwenye kujiandaa kuzieneza, alikuwa na furaha kujiwa na watafutaji elimu na wenye hamu ya kupata maarifa, walinzi wa Dini katika Masahaba na Taabiina (ﷺ‬.a), kiasi kwamba wamesimulia toka kwake karibu Masahaba wakubwa na wadogo ishirini na nane kama vile Zayd bin Thabit, Abu Ayoubl Al-ansari, Ubay bin Kaab Abdullah bin Omar, Abdullah bin Abbas, Abdullah bin Zubair Ubay bin Kaab, Jaabir bin Abdullah, Anas bin Maalik, Aisha, na wengineo (ﷺ‬.a,) kama walivyosimulia toka kwake na kusoma mamia ya Taabiina, (ﷺ‬.a). Amesema Bukhary Wamesimulia toka kwake karibu watu 800 au zaidi.[103] Nae Haakim akasema "Idadi ya waliosimulia toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) katika Masahaba karibu watu 820, ama Taabiina basi hakuna kati yao mashuhuri wala mtukufu au mtaalamu kuliko wanafunzi wa Abu Huraira (ﷺ‬.a) na akawataja na katika pahala hapa kutajwa kwao kutarefusha kutokana na wingi wao.[104] Na ninavyoelewa idadi hii ya wasimulizi na wanukuuji wa elimu haikufikiwa toka kwa Masahaba haifikiwi na yeyote katika Masahaba toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W), na hapana shaka kwamba mfano wa wa idadi hii kubwa hakika imesaidia sana kunukuu riwaya zake na kuzibakisha zikiwa hai na zenye kupokelezaniwa baina ya idadi kubwa ya wasimulizi, na wenye kunukuu, mpaka zikaandikwa pamoja na nyengine katika riwaya nyengine za Hadithi kwenye vitabu vya Hadithi na juzuu zake kinyume na asiekua yeye katika Masahaba ambao riwaya zao zimepungua kutokana na vifo vyao kutangulia kwa ulinganisho, au kwa baadhi yao kutopendelea kusimulia, au kwa sababu nyengine tulizozitaja.

6- Njia za wasimulizi wake kua nyingi hakika njia za baadhi ya wasimulizi wake kwa kiwango fulani zimechangia idadi ilionasibishwa kwake (ﷺ‬.a), na aneangalia riwaya zake kwenye Musnad ya Imam Ahmad (ﷺ‬.a), ambazo kwa mujibu wa sherhe ya Ahmad Muhammad Shaakir (ﷺ‬.a) ni riwaya (3848) anaona kwamba karibu ya thuluthi yake riwaya zake zimejirudiarudia, kwa sababu ya ziada ya msimulizi au kubadilika kwa mfumo wa ufikishaji kwenye sanad, au ziada ya lafdhi katika Matini, hivyo hilo likapelekea kuhesabiwa kuwa ni riwaya moja katika hali halisi kuwa ni riwaya mbili au zaidi kulingana na idadi ya kujirudiarudia kwake, na hivi ndivyo walivyofanya watiaji nambari wa Musnad Ahmad, nao kwa hilo ni wenye kukubaliwa udhuru wao katika hilo, kutokana na sababu za kifani mashuhuri za kisasa kwa watu wa elimu hii.

7-kushirikiana nae Masahaba katika riwaya alizosimulia

Hakika mwenye kuangalia vitabu vya Hadithi vinavyotegemewa na vilivyoenea leo baina ya Waislamu, na humo kufatilia riwaya za Abu Huraira (ﷺ‬.a), ataona nyingi zao ameshirikiana na Sahaba mmoja au zaidi katika kuzisimulia, na hasa zile ambazo hutapakiziwa upuuzwaji au matusi toka kwa watu wa matamanio ya nafsi na bid-a, na wengineo wasiokua na utaalamu wa mambo yanayopelekea kusihi kwa Hadithi, na kutokusihi .

8-Wingi wa idadi ya wasimulizi toka kwake

Hakika riwaya za wengi toka kwake katika Masahaba, na mathiqa katika mataabiina (ﷺ‬.a) ambao idadi yao inazidi wasimulizi 800 kama ilivyotangulia karibuni, na kutegemewa riwaya zake baada yao na maulamaa wa Umma na mafuqahau wake na mujtahidina wake na zile zilizosihi kunasibishwa kwake na kwa Masahaba wengine (ﷺ‬.a) ni dalili tosha na ushahidi bora juu ya uadilifu wake (ﷺ‬.a), na amana tosha yake katika yale aliosimulia na kunukuu toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W), na yaliyotangulia anaelewa yule ambae undani wake umesafika, na nyoyo zao kuangazika, kwamba wingi ni wa ulinganisho wa riwaya zake zenye sanad zilizo sahihi, ni wingi wa kawaida, uliochangiwa kupatikana na kudhihiri kwake na sababu tulizozitaja katika kuirudi shubuha hii na nyenginezo katika sababu zenye kusaidia, ambazo yaliambatana na maisha yake na kukua kwa hadhi yake miongoni mwa usuhuba wake kwa Mtume (SAW) mpaka kifo chake (ﷺ‬.a).

Kama unavyodhihiri wazi uzushi wa shubuha hii, na kwamba kianzio chake iwapo sio ujinga wa wazi, basi ni matashi ya mapya au yote pamoja, nasi tunajikinga na hayo.

Shubuha ya Pili

Kupingwa na Baadhi ya Masahaba

Baadhi ya wasiokua na ujuzi wa namna Masahaba (ﷺ‬.a) wanavyorekebishana wamesema kwamba ni kudhoofishwa kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a), au kudhoofishwa hadithi zake khususan na hivyo ni kwa sababu kwamba amerekebishwa kutoka kwa Aisha na Ibn Omar (ﷺ‬.a).

Na shubuha hii hurudiwa kama ifuatavyo

1- Hakika kupingwa na Aisha na Ibn Omar (ﷺ‬.a) ni katika mambo yaliopelekewa na majadiliano ya kielimu, na kurudia (Hadithi) kunakotokea mara nyegine kwa Masahaba (ﷺ‬.a), kwani zaidi ya Sahaba mmoja alimrekebisha mwengine kiriwaya au masuala ya kielimu, akamkinaisha mwenzake kwa jambo hilo, na hili ni jambo maarufu kwa maulamaa, na hasa hasa muhadithina miongoni mwao, na hilo haliathiri chochote katika uadilifu wa alirekebishwa wala katika uaminifu wake, kama kusivyoathiri tofauti ya thiqa kwa thiqa mfano wake katika uadilifu wako, au katika riwaya wanazozisimulia. Na kudiriki kwa Aisha na Ibni Omar (ﷺ‬.a) juu ya Abu Huraira (ﷺ‬.a) kunakwenda kwenye namna hiyo.

2- Hakika kupinga kwa Aisha (ﷺ‬.a) juu yake kunafahamika kunatokana na ilivyosimuliwa kwamba yeye alimwita Abu Huraira (ﷺ‬.a) akamwambia "Ewe Abu Huraira ni hadithi zipi hizi zinazotufika kwamba unazihadithia toka kwa Nabii (S.A.W), hivi wewe (si) umesikia ila tulichokisikia, nae (si) umeona tulioyaona? Akamwambia "Ewe mama yangu hakika wewe ukielewa asemayo Mtume wa Allah (S.A.W) kwa kushughulishwa na vioo, wanja na kujipamba kwa ajili ya Mtume wa Allah (S.A.W) na mimi Wallahi sikughulishwa na chochote zaidi ya kuwa na yeye.[105]

Hivyo katika hadithi hii tunamuona Aba Huraira (ﷺ‬.a) anamjibu Aisha (ﷺ‬.a) juu ya kumuuliza kwake kwa jibu linalodhihirisha kwamba amemkinaisha, kwa vile hakurejesha jibu lolote au kuongezea chochote katika jibu hilo, kwa ule uwazi na hali halisi hali ambayo inamridhisha kila mwenye makusudio yalio salama na nafsi iliyo safi. Na hivyo inafahamika kwamba kumdiriki kwake hakukua na lengo lolote ila kutaka jibu tu, na akaelewa kuwa yale yasiokua kwake ni katika yale ambayo yeye hakuyasikia nae aliyasikia, hayo ni baada ya kujibiwa ailvyojibiwa na kwamba yeye aliona asiyoyaona kwa kuangalia mkamatano uliokamilika na Mtume wa Allah (S.A.W), nae kuwa alishughulika na yale yanayowashughulisha wanawake wenye waume kwa kawaida.

Na katika yanayotilia nguvu kutoshughulika kwake (ﷺ‬.a)na na kisichokua kumsiliza Mtume wa Allah (S.A.W) ni yale yaliotangulia toka kwa Talha bin Abdullah (ﷺ‬.a) kwamba mtu alikuja kwa Talha bin Ubaidillahi (ﷺ‬.a), akamwambia "Ewe Aba Abdillahi, Wallahi hatuelewi Myemeni huyu ni mtaalamu zaidi wa kwa Mtume wa Allah (S.A.W) au nyie? Amemsemea Mtume wa Allah (S.A.W) asiyoyasema, akimaanisha Abu Huraira (ﷺ‬.a ),,Talha akasema Wallahi hapana anaeshuku kwamba yeye amemsikia Mtume (SAW) sisi tusioyasika ,na akaelewa tusioyaelewa, hakika sisi tulikua ni watu matajiri, tunazo nyumba na jamaa, tulikua tunakwenda kwa Mtume (SAW) asubuhi na jioni kisha tunarejea. Nae Abu Huraira (ﷺ‬.a) alikuwa maskini asiekua na mali, mke, wala mtoto, hakika mkono wake ulikua na mkono wa Mtume (SAW), nae alikuwa akienda na Mtume (SAW) popote aendapo, hatuna shaka kwamba alitenda tusioyatenda na kusikia tusioyasika, hakuna aliemtuhumu yeyote katika sisi kwamba amemsemea Mtume (SAW) asiyoyasema.[106]

Ama kustadikiwa na Ibn Omar(ﷺ‬.a), ni kumhoji kwake katika Hadithi “ya kufuata Jeneza " na ni ile iliyosimuliwa kwamba alimpita Abu Huraira (ﷺ‬.a), nae anahadithia toka kwa Mtume (SAW) "Yeyote aliefuata jeneza basi anayo –malipo ya – qiiraat, akishuhudia kuzikwa kwake anazo qiraat mbili, qiraat ni kubwa kuliko (jabali la) Uhud" Akasema Ibn Omar Ewe Abu Huraira (ﷺ‬.a) angalia unachohadithia toka kwa Mtume (SAW), hivyo Abu Huraira (ﷺ‬.a) akasimama kumwendea mpaka kwa Aisha (ﷺ‬.a), akamwambia Ewe mama wa waislam nakuuliza Jee umemsika Mtume (SAW) akisema “Yeyote aliefuata jeneza basi anayo –malipo ya – qiiraat, akishuhudia kuzikwa kwake anazo qiraat mbili?"akasema "Allaahumma naam".

Akasema Abu Huraira "Hakika sisi hatukua tukishughulishwa na kupanda mimea ya mitende, wala kofi kwenye masoko, hakika mimi nilikua nikitaka neno toka kwa Mtume (SAW) anifundishe, au kula anilishe, hivyo Ibn Omar akasema "Ewe Abu Huraira ulikua mkamanataji wetu zaidi na Mtume (SAW) na mjuzi wetu zaidi wa Hadithi zake."[107] Na hili likendelea, Abu Huraira (ﷺ‬.a) hakua Sahaba pekee alivyopingwa na ndugu zake Masahaba, bali alistadirikiwa Ibn Omar na Aisha (ﷺ‬.a) na mwenginewe katika Masahaba, kama baadhi yao walivyopinga Aisha (ﷺ‬.a),na hili ni jambo maarufu kwa maulmaa na hapa sio pahala pa kutanua hili. Na katika hayo yaliyotangulia yanatutilia nguvu sisi kwamba, kurekebishana Masahaba wenyewe kwa wenyewe hakukupelekea kufanywa muongo alierekebishwa, wala kuharibu uadilifu wake, au kupunguza uaminifu wake, kama wajinga wanavyodhania dhana mbaya.

Shubha Ya Tatu

Kushughulika kwake na shibe ya tumbo lake

Wapo baadhi wanaomtuhumu Abu Huraira (ﷺ‬.a) kwa kushughulika na shibe ya tumbo lake, na kwamba hakusuhubiana na Mtume (SAW) ila kwa hilo, na kutumia kama hoja kwenye shubuha hii yaliyosimuliwa katika kauli yake "Nilikua nikisuhubiana na Mtume (SAW) kwa kujaza tumbo langu" “na kauli yake "Mimi nikitafuta neno toka kwa Mtume (SAW) anifundishe, au kula anilishe" na zenye maana ya hii katika ibara.

Na hii vilie vile ni tuhuma batili kwa namna

Mwenye shubuha hii kutofahamu muradi wa Abu Huraira (ﷺ‬.a) kutokana na kauli yake "Nilikua nikisuhubiana na Mtume (SAW) kwa kujaza tumbo langu" na yenye maana ya hiyo, na kutoelewa kwake kwa lililompelekea kusema kauli hii, na kwamba muradi wa Abu Huraira (ﷺ‬.a) wa kutaja shibe ya tumbo lake ni katika riwaya zilizotajwa ni ni kubainisha kujitenga kwake kikamilifu kwa ajili ya kujifungamanisha na Mtume (SAW), na kuhifadhi kwake alichokisika toka kwake, na kwamba hakuzuwiwa na jambo lolote lile asifanye hilo, hata tonge ya chakula ambayo wengine huwashughulisha,alipata kwa Mtume (SAW), na kwamba hilo hakulisema kipuuzi tu kama walivyodai wengine, bali alisema hilo ili kuwarudi waliosema "Hakika Abu Huraira (ﷺ‬.a) amezidi kusimulia toka kwa Mtume (SAW), na hili linafahamika toka kwenye kauli yake "Hakika nyie mnadai kwamba Abu Huraira (ﷺ‬.a) kazidi kwa Hadithi toka kwa Mtume (S. A. W) Wallahi ni ahadi, hakika mimi nilikuwa masikini nasuhubiana na Mtume (S.A.W) kwa kujaza tumbo langu, na Muhajirina walikua wakishughulishwa na kofi sokoni, na Ansari wao wakishughulishwa na kusimamia mali zao, mimi nilihudhuria majlisi ya Mtume (S.A.W) akasema ((Ni nani atakaetandika mtandio wake mpaka nimalize maneno yangu, kisha alikamate, asisahau kamwe alichosika toka kwangu?. mimi nikatandika yangu mpaka akamaliza mazungumzo yake kisha akalikamata kunipa, basi naapa na yule ambaye nafsi yangu iko kwenye mikono yake sikusahau chochote nilichokisikia toka kwake baada ya hapo.)[108] Na katika jibu lake lililotangulia karibuni juu ya ukosoaji wa Ibni Omar kwa kauli yake " Hakika sisi hatukua tukishughulishwa na kupanda mimea ya mitende, wala kofi kwenye masoko, hakika mimi nilikua nikitaka neno toka kwa Mtume (SAW) atufundishe, au kula atulishe"Lau ingekua hamu yake ni kushibisha tumbo lake basi angeweza kuitafuta toka kwa kiongozi yeyote katika viongozi wa Yemen, au raisi wa kabila katika makabila yake, afanye kazi ya kilimo kwake, kuchunga wanyama au kazi nyengine yoyote, na angetosheleka nafsi yake kutokana na tabu za safari na kuwacha familia, jamaa na nchi, kwa kuhama toka Yemen mpaka Hijaaz, kwenda kwa mtu asiekua mfalme, mwenye madaraka au mali wakati huo, na wala asiepukane na maadui zake watatu waliokua wakimvizia Mushrikina kule Makkah na sehemu nyengine, wanafiki Madina na pembezoni mwake, na mayahudi waliokua majirani zake ambapo uwezekano wa kushinda na kushindwa yote yaliwezekana kutokana na vipimo vya nyenzo za kibinadamu.

Na kamwe uwezekano huu haukuondoka kwenye akili ya kijana mwenye akili huyu wa Kiyemen mwenye hekima Abu Huraira, nae akimsisitiza mnyama wake kuelekea Madina, kuelekea kwenye mwangaza ulioangazia huko; akiitikia ulinganio wa haki, daawa ya Mtume (SAW), ulinganio wa kumuamini Allah mmoja aliepwekeka, na akashiriki kwenye vita vya Khaibar baada ya siku mbili au tatu pamoja na Mtume (SAW) [109].Nae akahudhuria pamoja nae kwenye vita, na kushikamana nae mpaka kifo chake, akahifadhi toka kwake wasioyahifadhi wengi asiekuwa yeye katika waliopata hadhi ya usuhuba wake (S.A.W), naam anamuhimiza mnyama wake akiwa anaelekea Madina huku akiimba

Ewe usiku unaotokana na urefu na matatizo yake,

Juu ya kwamba nimeokoka na nchi ya kufru[110]

4- Lau kama hamu yake ni shibe ya tumbo lake, basi angeliuacha mshikamano na Nabii na kumtafuta atakae mshibisha katika Masahaba wenye uwezo (ﷺ‬.a) au wenginewe katika watu wa Madina, kwa kufanya kazi au vyenginevyo kwa vile hakuweza kushiba katika siku zake nyingi alizofungamana na Mtume (SAW), kwani katika siku nyengine hakuweza kupata zaidi ya tende moja au mbili, au kunywa chubuo ya maziwa au karibu na hayo; imesimuliwa toka kwake kwmba amesema "siku moja nilitoka nyumbani kwangu nikawakuta watu, wakasema, “kitu gani kimekutoa? “nikawambia njaa, wakasema na sisi Wallahi hatukutolewa ila na njaa, basi tukasimama, tukaingia kwa Mtume wa Allah (S.A.W), Akasema "Mumeletwa na nini saa hizi?" tukamueleza, basi akatoka na sahani ndani yake zimo tende, akampa kila mtu kati yetu tende mbili, akatwambia kuleni tende mbili hizi na mnywe maji, zitakutoshelezeni siku yenu hii " basi nikala tende moja na nyengine kuificha, akasema "Ewe Abu Huraira (ﷺ‬.a) kwa nini umeichukua"? nikamwambia kwa ajili ya mama yangu. Akasema ile tutakupa tende mbili nyengine"[111]

Kama ilivyo toka kwake kwamba palitolewa zawadi ya kibuyu cha maziwa kwa Mtume (SAW) akamwamrishwa awaite watu wa Suffa nae alikua kiongozi wao-,basi akawaita mpaka walipokaa akamwambia “Yachukue Abu Huraira (ﷺ‬.a) uwape" basi nikawa nawapa,-mtu anakunywa mpaka anatosheka na nikawanywesheza wote, na nikampa Mtume wa Allah (S.A.W) basi akanyanyua uso wake kwa tabasamu, akasema " Nimebakia mimi na wewe" nikawambia "Kweli Ewe Mtume wa Allah (S.A.W)", akaniambia "kunywa" basi nikanywa akaniambia "kunywa" nikanywa, basi hakuacha kuendelea anasema "kunywa" “nikanywa mpaka nikasema "Naapa kwa yule ambae amekutuma kwa haki sina nafasi ya kuyaweka" hivyo akayachukua akanywa kutokana na yaliyobakia." [112]

Na riwaya hii inajulisha mambo makubwa, kama vile kuzidi kwa maziwa kwa sababu ya baraka ya Nabii (S.A.W), kuwaenzi kwake mafakiri wa Kiislamu na kuwatangulizia kunywa kabla ya yeye, na furaha zake kwa kushiba kwao, na kupigia kwake mfano wa thamani, na kwamba vilevile inaonyesha namna walivyokua wakipata shida ya njaa na haja toka kwao Abu Huraira (ﷺ‬.a) aliekua akishughulika na shibe ya nafsi yake, bali Nabii (S.A.W) hakushiba usiku mitatu mfululizo, imesihi toka kwa Aisha (ﷺ‬.a) kwamba amesema “Kamwe aila ya Muhammad (S.A.W) haikuwahi kushiba siku tatu mfulululizo mpaka alipofishwa, na kutoka kwake amesema ulikua ukija mwezi hatukoki moto, ila ni tende na maji -tu-"[113] Na kutoka kwa Saad bin Abi Waqaas (ﷺ‬.a) amesma " Hakika nilijiona wa saba katika saba pamoja na Mtume (SAW) na hatuna chakula ila majani ya miti, mpaka mafizi yetu yakafanya usaha" [114] Na ikiwa hiyo ndio hali ya Nabii (S.A.W) na aila ya nyumba yake, basi itakuaje hali ya Nabii (S.A.W) na mfano wake?, na iwe mfano wake katika hali hii atatuhumiwa kwa kujishughulisha na shibe ya tumbo lake? na kujishughulisha na hilo kutasaidia nini pamoja na kutokuepo au uchache anaowapelekea ili kushiba?

4- Lau angeka mwenye kujishughulisha na shibe ya tumbo lake au mambo mengine ya kidunia, basi angechukua kama mwengine we kitu katika ngawira ambayo Mtume alimpendekezea, toka kwa Saad bin Abi Hind toka kwa Nabii (S.A.W) kwamba Mtume wa Allah (S.A.W), alisema “kwa nini huniombi ngawira hizi ambazo wenzako wananiomba? nikamwambia "Mimi nakuomba unielimishe katika yale Allah aliokuelimisha! basi akaondoa nguo iliokua juu ya mgongo wangu, akaitandika baina yangu na yeye mpaka nikamuona mdudu chungu anakwenda juu yake, basi akanihadithia mpaka hadithi zake zikakamalika akasema "ikusanyie kwako" basi nikawa sipotezi herufi yoyote katika alionihadithia"[115] Hivyo iko wapi hamu ya Abu Huraira (ﷺ‬.a) ilioelekezwa kwenye kushibisha tumbo lake au kwenye elimu na maarifa? Allah ayalaani matamanio ya nafsi ikiwa yatampelekea mwenye nayo upofu wa macho yake kutoona haki na kauli yake.

5- Hakika utajo wake pale alipofikwa na matatizo ya njaa na ufakiri, ilikuwa vyema kukadiria, na sio kutafsiri tafsiri ya kimadia vyenye manufaa yasio na thamani, kutokana na yanayojulisha kutokana na hali halisi na kutokana yaliyopita, yaliyomsaidia juu ya unyenyekevu na kuelewa neema za Abu Huraira (ﷺ‬.a) juu yake, na shukrani zake juu yake baada ya Abu Huraira (ﷺ‬.a) kumpa neema, na kumnyanyulia jina lake, na kunyanyua cheo chake, kwa Uislamu na fadhila, kiasi ambapo tunamuona anakithirisha kumshukru na kumsifu sana Allah (s.w), katika hayo ni kauli yake "Shukrani zote zimemthibitikia Allah ambae ameijaalia Dini kusimama, na kumjaalia Abu Huraira (ﷺ‬.a) kuwa kiongozi, baada ya kua kibarua[116] "Shukrani zote zimemthibitikia Allah ambae amemfundisha Abu Huraira (ﷺ‬.a) Quran, amempa Abu Huraira (ﷺ‬.a) kwa shukrani za Muhammad (S.A.W)[117] .Na kwa hivi inatudhihirikia kubatilika kwa shubuha hizi, na kwamba Abu Huraira (ﷺ‬.a) hakusuhubiana na Nabii (S.A.W) kwa ajili ya shibe ya tumbo lake, kama wanavyodai wanaodai, bali amesuhubiana nae kwa ajili ya imani, mapenzi kwake, na kutaka kukusanya toka kwake na muongozo na nuru.

Shubha Ya Nne

Kuficha kwake Baadhi ya aliyoyapokea toka kwa Mtume (S.A.W)

Miongoni mwa shubuhati zilzotapatakazwa na baadhi ya wenye matamanio ya nafsi ni kuficha baadhi ya yale aliyopokea toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a), na hilo linahesabika kwamba ni kuficha Wahyi alioamrishwa Abu Huraira (ﷺ‬.a) na Mtume wake kufikishwa kwa watu, wakitegemezea katika hilo kwenye kauli yake iliyosihi toka kwake kwamba amesema "Nimehifadhi toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W) mifuko miwili ama mmoja wao nimaueneza kwa watu, ama mwengine lau ningeueneza koo hili lingekatwa[118] Na katika riwaya "Nimehifadhi toka kwa Mtume wa Allah (S.A.W) Hadithi nilizo kuhadithieni, na lau ningelikuzungumzieni hadithi moja tu katika hizo mungenirembea kwa mawe.[119] Na shubuha hii hujibibiwa kama ifuatavyo

1- Kwa hakika Abu Huraira (ﷺ‬.a) alikusudia mifuko miwili na ilio katika maana yake, sehemu au makundi mawili katika Hadithi, la kwanza nalo ndilo kubwa ni lile alilolisimulia na kulieneza kwa watu, nalo ni lile lililo wajibu kufikishiwa, na la pili nalo ni dogo, na huenda kwa wingi halizidi hadithi moja au mbili, nalo ni lile alilolificha na hakulihadithia kwa watu, na hilo ni lilesilohitajiwa kufanyiwa kazi, linaweza kueneza fitina, kupelekea watu kujibweteza kutofanya amali, kupata maudhi kutokana nalo, kukadhibishwa kwa anaesimulia, au jambo jengine, amesema Adh Dhahabiy "Hivi ni kuchukulia kujukuzu kuficha baadhi ya Hadithi ambazo huhemua fitina kwenye mambo ya msingi (Tawhiid) au matawi (Fiqhi), au sifa au kuponda. Ama hadithi inayoambatana na halali au haramu, hiyo sio halali kufichwa kwa hali yoyote ile, kwani hiyo ni katika ubainishaji na muongozo.[120] Anamaanisha ni wajibu kuibainisha kwa watu wala haijuzu kufichwa. Amesema Haafidh Ibn Kathir "Na mfuko huu aliokua haudhihirishi ni fitina, mitihani na yaliyotokea baina ya watu miongoni mwa vita, mapigano, na yale yatakayotokea, na haya lau angeyatolea habari kabla ya kutokea kwake, wengi wa watu wangekimbilia kumfanya muongo.[121]

2- Abu Huraira hakuwa Sahaba pekee alieficha baadhi ya aliyopokea toka kwa Mtume (SAW), kwani imethibiti kwamba baadhi ya Masahaba walificha baadhi ya waliyopokea toka kwa Mtume (SAW) katika Hadithi, na miongoni mwao alikua Muaadh bin Jabal, amesimulia Muslim toka kwake amesema "Nilikua nyuma ya Mtume (S.A.W) juu ya punda aitwae Aafiir, akasema kuniambia" "Ewe Muadh unaijua ni ipi haki ya Allah juu ya mja?, na nini haki ipi ya mja juu ya Allah?" nikasema "Allah na Mtume wake ndio wanaoelewa, akaniambia "Basi hakika haki ya Allah juu ya waja ni kumuabudu Allah na kutomshirikisha na chochote na haki ya mja juu ya Allah Azza wa Jalla ni kutomuadhibu yeyote asiemshirikisha na chochote, akasema nikamwambia "Ewe Mjumbe wa Allah niwabashirie watu, akasema "usiwabashirie wakajibweteza"[122] Na miongoni mwao ni Ubaada bin Saamit (ﷺ‬.a) imesihi toka kwake kwamba alisema kwenye maradhi ya mauti yake "Hakuna Hadithi yoyote niliyoisikia toka kwa Mtume (SAW) yenye kheri kwenu ila nimewahadithia, isipokua hadithi moja leo nitawahadithia, na nafsi yangu imezingirwa, nimemsikia Mtume (SAW) akisema " Yeyote alieshuhudia kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa ila Allah na kwamba Muhammad ni mjumbe wa Allah, Allah atamuharimishia Moto"[123] Amesema Kadhi Iyadh. "Na mfano wa hili toka kwa Masahaba (ﷺ‬.a) ni mengi katika kuacha kuhadithia yasiohitajia kufanyiwa amali, wala kupelekea umuhimu, au zile zisizoweza kubebwa na akili za wote au kuhohofia madhara juu ya msemaji wake au msikilizaji wake."[124]

3- Wito wa Masahaba wakubwa wa kupunguza kusimulia Hadithi, na msisitizo wao juu ya hilo, kutokana na sababu walizoziona zinazopelekea upunguzaji wa kusimulia. Imesimuliwa toka kwa Omar kwamba alisema "Punguzeni kusimulia toka kwa Mtume (SAW) ila kwa yale ya kufanyiwa amali Amesema Ibn Kathir "Na hili linachukuliwa toka kwa Omar kwamba alihofia hadithi ambazo watu wanaweza kuziweka kwenye mwahala musimo mwao, kwamba wanasema kwenye yaliyomo ndani ya hadithi za ruhusa, na kwamba mtu iwapo atazidisha kusimulia huenda akaangukia kwenye hadithi zake baadhi ya makosa, watu wakiyabeba toka kwake.[125] Na imesihi toka kwa Ali bin Abi Talib (ﷺ‬.a) kwamba " wahadithieni watu kwa wanayoyaelewa,na wacheni wasiyoyaelewa,hivi nyie munapenda akadhibishwe Allah na Mtume wake?"[126] Kama ilvyosihi toka kwa Abdullah bin Masoud (ﷺ‬.a) kwamba "Wewe hutoihadithia kaumu hadithi isiofika akilini mwao ila itakuwa fitina kwa baadhi yao"[127] Na kwa hili inadhihiri wazi kwamba yale yale yaliyofichwa na Abu Huraira (ﷺ‬.a) hayatoki kwenye sababu walizofichia kwazo baadhi ya Masahaba (ﷺ‬.a) baadhi ya riwaya, na kwamba hakua mfichaji wa yale ambayo Allah ameamrisha kufikishwa, na Mtume wake (S.A.W.) kutokana na mnasaba wake kinyume na wenye dhana mbovu wanavyodhania .

Shubha Ya Tano

Kuuzuliwa toka kwenye uongozi wa Bahrein na Omar (ﷺ‬.a)

Na katika shubha zilizotapakazwa na baadhi ya watu wa matamanio ya nafsi vile vile, ni kauli yao "kwamba kuuzuliwa kwake toka kwenye uongozi wa Bahrein na Omar binil Khattab kunaeneza shaka katika uaminifu wake. Nayo ni shubha batili kwa sababu zifuatazo

1- Pale Omar alipomuuzulu toka kwenye uongozi wa Bahrain hakuwa ni mwenye mashaka na uaminifu wa Abu Huraira (ﷺ‬.a), Ila ilikuwa ni kutokana na kuombwa kwake kufanya hivyo ili kukata maulizo kuhusiana na mali alioikuza baada ya kuwa kwake kiongozi wa Bahrein, japo kwamba mali hiyo ni kidogo, lakini kama mfano unavyosema "Fakiri avaapo nguo mpya huulizwa nani aliekupa hii?" na hata kwa kuchukulia kwamba alikua na mashaka nae katika uaminifu wake, basi shaka hii ilimuoondokea baada ya kumuuliza kuhusiana na chanzo cha mali hiyo, na jibu lake lenye kukinaisha juu ya suala lake.Toka kwa Ayoub As Sakhtiyaniy, toka kwa Muhammad bin Siyriin." Hakika Omar alimuajiri Abu Huraira (ﷺ‬.a) juu ya Bahrein akaja na elfu kumi, akaulizwa na Omar "Umejiwekea mali hii ewe adui wa Allah na adui wa kitabu chake?" Abu Hurairah (ﷺ‬.a) akasema nikamwambia "mimi sie adui wa Allah wala adui wa kitabu chake, lakini ni adui wa anaemfanyia uadui Allah na Kitabu chake, akaniambia basi imetoka wapi? nikamwambia farasi amezaa, mtumwa wangu akawa na bei ya juu, na mishahara iliyofuatana, akasema "wakaangalia wakaona kama alivyosema" Na katika yanayotilia nguvu kukinai kwa Omar kwa jibu lake, na kuondokwa na shaka yake kwenye uaminifu wake, ni kumwita tena kwa ajili ya uongozi wa Bahrein.

Imekuja kwenye riwaya hiyo hiyo “kwamba baada ya hapo, Omar alimwita kwa ajili ya kumpa uongozi wa Bahrein mara nyengine, akakataa, akamwambia "unakataa kazi, na ameomba kazi aliekua mbora kuliko wewe, Yusuf (A.S)?", akamwabia "Yusuf ni Nabii mtoto wa Nabii, na mimi ni Aba Huraira mtoto wa Umaima, na naogopa matatu na mawili "akamwambia "basi kwanini usiseme matano", "naogopa kusema bila ya elimu, kuhukumu bila ya upole, kupigwa mgongo wangu, kunyang'anywa mali yangu, na kutukanwa hadhi yangu" " [128]

Na riwaya hii ndio riwaya sahihi zaidi katika maudhui ya kuuzuliwa na Omar kwenye uongozi wa Bahrein, kutokana na kukubalika kwa wasimulizi wake, na sanad zake kuwa nyingi kufikia kwa Taabii mtukufu Muhammad bin Siriyn (ﷺ‬.a,) nayo inajulisha kwamba kuuzuliwa kwake hakukua kwa khiana, upungufu wa uaminifu wake, au mapungufu katika wajibu, na vyenginevyo basi unautafsiri vipi wito wa Omar kwa ajili ya kumpa uongozi mara ya pili?."

2- Siasa ya Omar (ﷺ‬.a) ilikuwa ya aina yake katika uongozi, kufuatilia viongozi kazi zao na kuwauliza, japo kwa jambo dogo tu analopelekewa au lisemwalo dhidi yao, vyo vyote vyeo vyao vitakavyokua, na vyeo vyao kutukuka katika kutangulia kwenye Uislamu, na hili ni katika ubora wake, hivyo tunamuona anamuhesabu Abu Huraira (ﷺ‬.a), alie chini yake na kumuhesabu alie na ngazi ya juu na ubora, kuliko yeye, kama vile Saad bin Abi Waqqas (ﷺ‬.a), mmoja ya waliotangulia kwenye Uislam na mmoja wa waliobashiriwa Pepo, na mwenye kukubaliwa maombi yake miongoni mwao[129], nae Omar alikua amemuuzulu uongozi wa Al-kuufa, nae akasema baada ya hapo kwenye wasia wake kwa watu wa Shura " ukifika uongozi kwa Saad basi ni mahala pake, na vyenginevyo basi yule ambae atakaetawala atake msaada wake kwani mimi sikumuuzulu kwa sababu ya kushindwa au khiana"[130] Na Umair bin Saad bin Umair Ubaid Al Ansariy, ambae anaitwa Umair mfumaji pekee ", inasemekana aliemsifu kwa wasfu huu ni Omar (ﷺ‬.a) na imesimuliwa toka kwa Ibn Omar (ﷺ‬.a) kwamba alimwambia Abdulrahman bin Saad “Sham hakukua na mbora kuliko baba yako"[131]

Na pamoja na hayo basi amesimulia Tirmidhiy toka kwa Abi Idriisil Khawlaniy kwamba Omar alimuuzulu toka kwenye uongozi wa Himsi na kumtawalisha Sahaba mwengine.[132] Na juu ya hivyo, Omar kuwauliza viongozi wake, mara nyengine kuwauzulu, ilikua ndio siasa yake kama tulivyotanguliza na sio lazima kudogoka kwa aliowauzulu, na huenda alitaka kuwawekea njia kwa Makhalifa na Maamiri waliokuja baada yake yeye.

Shubuha Ya Sita

Kutuhumiwa Kwake kwa Kuwaunga Mkono Bani Umayyah

Wenye matamanio ya nafsi hawakutoshelezeka na shubuha zilizokwishatangulia ambazo walizitapakaza kwa uzushi juu ya Abu Huraira (ﷺ‬.a), na kwamba wao wanacho kisasi au haki ya mali juu yake, kiasi cha kudai kwamba alikuwa akiwaunga mkono Bani Umayyah, na kumzushia hadithi Muawiya katika kumtukana Ali bin Abi Talib (ﷺ‬.a), dai ambalo halina dalili yoyote, wala msingi wa kusihi kwa sababu zifuatazo

1- Tunavyoelewa hapakuja hadithi yoyote ile iliyodaiwa kuzushwa kwenye vitabu vya hadithi vyenye kutegemewa na jamhuri ya waislam, sio katika Sahaba wala vyenginevyo, na anaedai ni juu yake kuthibitisha anayodai iwapo ni mkweli, na wapi atapata hilo?

2- Vipi waovu hao wagundue uzushi wa hadithi wa Abu Huraira (ﷺ‬.a), wawe hawakugundua hivyo waliosimulia toka kwake katika Masahaba, na mataabiina waadilifu, na waliokuja baada yao miongoni mwa maulmaa wa Jarhu na Taadil, ambao hawakumpaka mafuta yeyote nyuma ya chupa juu ya hesabu ya dini yao na Sunna za Nabii wao (S.A.W).

3- Itakuaje Abu Huraira (ﷺ‬.a) azue hadithi nae ndie msimulizi wa hadithi “Yeyote alienizulia uongo kwa makusudi basi atayarishe makaazi yake kwenye Moto" ambayo karibu Masahaba arobaini walishirikiana nae katika kuisimulia.

4- Ni zipi hizo hadithi alizozizua kwa ajili ya Muaawiya? na idadi yake ni ngapi? na ni vipi vitabu vilivyosimulia?, ili tuelewe kipimo chake mbele ya wenye elimu ya hadithi.

5- Vitabu vya hadithi vingi vinavyotegemewa vimetusimulia riwaya nyingi sahihi na hasan toka kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a). Katika sifa za Abu Huraira (ﷺ‬.a) wakitanguliwa na Ali bi Talib (Abu Huraira (ﷺ‬.a) na Aalil Bait) ambazo zinatutosheleza na kuzirejea tena hapa, wakati ambapo hapakusimuliwa chochote kile katika fadhila za Muawiya, au yeyote katika Bani Umayyah kwa mujibu tunavyoelewa.

6- Hapakuthibiti kwamba yeye alipewa kazi wakati wa Muawiyah au kujulika chochote kinachothibitisha shubuha hii, ila kile kilichosimuliwa kuwa alitawalia uamiri wa Madina kwa niaba ya Marwan ibn Al-Hakam kwa ajili ya baadhi ya haja zake.

Nao ni uamiri usiozidi mipaka ya kumuwakilisha kwenye Sala, khotuba na unaokaribiana na hayo, kutokana na kufaa kwake kwa hilo, na kukubalika kwake na watu kwa hilo, sio kwa ajili ya mapenzi yake kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a), kutokana na tofauti zilizokuwepo baina yao na kutofautina kwao kuliko wazi kwenye misimamo kadha .

Na katika hayo; ni ule uliosimuliwa toka kwa Al Waliid bin Rabaah amesema "nimemsikia Abu Huraira (ﷺ‬.a) akimwambia Marwaan "Wewe sio kiongozi hakika uongozi ni wa Mwengine, akimaanisha pale alipotaka kumzika Hassan pamoja na Mtume (SAW), lakini wewe unaingilia yasio kuhusu, hakika wewe unataka hivyo ili umridhishe alie mbali na wewe. Marwan akamgeukia katika hali ya kughadhibika, akamwambia. "Ewe Abu Huraira (ﷺ‬.a) hakika watu wamesema umezidisha hadithi toka kwa Mtume (SAW)", akamwambia nimekuja na Mtume (SAW) yupo Khaibar na mimi siku hiyo nimeshazidi miaka thelathini na sita, nikakaa nae mpaka akafariki, nazunguka pamoja nae kwenye nyumba za wake zake, napigana, nahiji pamoja nae, na ninasali nyuma yake basi Wallahi nikawa mjuzi wa watu kwa hadithi zake.[133]

Na katika riwaya; "Kwamba Abu Huraira (ﷺ‬.a) alimwambia Marwan "hakika mimi nilisilimu nikahajiri kwa khiari yangu, nikasuhubiana na Mtume (SAW) kwa mapenzi makubwa sana, na nyie ni watu wa nchi na pahala mlipomtoa mlinganiaji kwenye nchi yake, mkamuudhi yeye na Masahaba wake, na kusilimu kwenu kukachelewa kuliko kwangu basi mimi ni mjuzi zaidi wa maneno yake na mchaji wake.

Na katika hayo; ni yale yaliyosimuliwa toka kwake kwamba amesema "Naapa na Yule ambae nafsi yangu imo kwenye mikono yake, unakaribia kuja wakati kuwa kikundi kidogo cha mbuzi kinakuwa bora kwa mwenyewe kuliko nyumba ya Marwan[134]

Na katika haya umo upinzani uliowazi kwa Marwan lakini kwa haja ya hukumu ambayo sababu yake inajulikana. Kamwe hakuelemea kwenye upande wowote ule kwenye tofauti zilizotokea baina ya Ali bin Abi Talib na Muawiyah (ﷺ‬.a), nae alijiepusha na fitina iliyotokana na tofauti baina yao pamoja na kundi la Masahaba wenzake (ﷺ‬.a), akakaa Madina baada ya kurejea kutoka Bahrein kabla ya mwaka 20H, akabakia humo mpaka alipofariki mwaka 56H kama tulivyotanguliza kusema, na hata tukikubali uzushi wa wazushi, na uongo wa watu wa batili, ambao walimsemea asiyoyasema, na katika hayo ni maneno ambayo yanasema "Sala nyuma ya mkamilifu, akiwa ni mzushi hivi ni iwapo mzushi wake haelewi hilo, ama akiwa mjuzi kwalo basi inaelekea kuwa huyo amekengeuka toka kwenye msingi wa kiislamu usemao {Hakika huzua uongo wale ambao hawamini Aya za Allah na hao ni makafiri} [ Annahl 105 ]

Hakika kaelekea kwenye rai ya Mikaviyl asemae 'Lengo huondosha njia ya kufikia'. Uchukivu wa mtu kwa mwengine hukubalisha uongo na uzushi juu yake ili kuridhia matamanio ya nafsi, kwa ajili ya kukubali hadaa za shetani, na hichi ndicho chanzo cha msingi cha kila kilichotapakaziwa kwa Sahaba huyu mtukufu na riwaya zake miongoni mwa shubuhati na madai ya batili.

Allah amrehemu aliesema

Ewe mtafutji elimu na riwaya =Hakika riwaya ni zenye magonjwa

Ndugu yangu usichukue elimu toka kwa alietuhumiwa ila kwa yule mwenye shada za Ijaza.Muridhiapo amana toka kwake na Dini zizungukeni amana[135]

MLANGO WA TATU

Sababu za Kuenezwa Shubuha kuhusu dhidi yake (ﷺ‬.a )

Shubuha kuhusina na Abu Hurairah (ﷺ‬.a) zimeenezwa ikiwa ni pamoja na kampeni ya ujumla ya kuwatapakazia Masahaba, na hasa hasa wasimulizi, kama vila Imran bin Huswain, Al Barrau bin Aazib, Jaabir bin Abdullah na wengineo, kutokana na vikundi na watu mmoja mmoja, katika wazandiki, wazushi na wengineo na maadui wa kiislam na wenye chuki nao katika mulhidina na mustashrikina na wengineo miongoni mwa waliokereka na jengo madhubuti la Uislamu, huduma za watoto wake na ulinzi wao kwayo, wametilia nguvu yaliyosimuliwa toka kwenye vikundi hivi.

Wakaongeza kwenye shubuha za waliowatangulia yale yaliyopelekewa na chuki zao za urithi na fahamu yao iliyopotea na wakawa wanarejearejea shubuha za hawa na wale, baadhi ya watu wa sasa miongoni mwa walio chukiwa na umati huu kwa sababu kadha, nyingi zao zenye kurejea kwenye matamanio ya nafsi, ujinga na kupenda ushindi tu mara nyengine, na hayo ni kwa gharama za kizazi bora cha Umma huu na waaminifu wao juu ya dini yake, mirathi ya Nabii wake, nae Abu Huraira amepata sehemu kubwa katika matangazo hayo ya kidhulma na khiana kwa sababu kadha miongoni mwake

1-Kuwa ni mwenye kusimulia hadithi nyingi zaidi toka kwa Mtume (SAW) .

2-Umuhimu wa yaliyomo kwenye hadithi zake, kuwa ni mjuzi wa fani nyingi za dini katika Tawhid, ibada, muamalat, tabia na kadhalika.

3-Kusimulia kwake Hadithi zinazoambatana na baadhi ya tofauti, zilizotegemewa na Jamhuri kwenye tofauti zao pamoja na wengineo na hoja ikawa ni yao.

4-Hadithi zake kusimuliwa na maimamu kwenye vitabu vyao wakiongozwa na maimamu wawili Bukhariy na Muslim(ﷺ‬.a).

Na malengo muhimu wanayoyakusudia ni

Mwanzo Kutia shaka kuhusiana nae.

Pili -Kutia shaka kwenye hadithi zake.

Tatu -Kutia shaka kuhusu vitabu vilivyosimulia riwaya zake hizo, na hilo ndilo lengo kuu linalotafutwa na maadui wa Sunna na wanaowasindikiza katika waliohadaika na waajiriwa wa zamani na wa sasa.

Nne - Kutoelewa historia ya maisha yake na namna na ya kukusanywa kwa riwaya zake na utayari wa anaetambua hili, na hili ni kwa mujibu wa wenye nia zilizosafika, iwapo ni katika wale wabebeshwa (upotevu huu) miongoni mwa waliotengenea nia zao.

Hapa ni muhimu kwetu kuleta yale aliyonukuu Al Haakim Abuu Abdillahi toka kwa Al Haafidh Abui Bakr bin Khuzaimah kuhusiana na sababu za kumtia ila kumsema vibaya Abu Huraira (ﷺ‬.a) na riwaya zake, pale aliposema haya tunayofanya muhtasari wake "hakika humsema Abu Huraira (ﷺ‬.a) ili kukimbiza Hadithi zake wale ambao Allah ameshawapofua nyoyo zao, hivyo hawafahamu maana ya Hadithi, ima hao ni wapingaji wa Kijahamiyyah wanaosikia habari zake anazosimulia kinyume na madhehebu yao, basi wanamtukana Abu Huraira (ﷺ‬.a) na kumsingizia kwa yale Allah aliomtakasia wakidai kiupofu kwamba habari zake hazithibitishi hoja, au ni Makhawaarij wanaposikia habari kinyume na madhehebu yao hawakupata hila za kupinga Hadithi zake kwa hoja na dalili maangukio ya fazaa yanakua kwa Abu Huraira (ﷺ‬.a), au Qadariy waliowakufurisha waislamu ambao wanafuata qadari zilizotangulia, Allah alizozikadiria na kuziamua kabla ya kuchumwa na viumbe waangaliapo riwaya za Abu Huraira (ﷺ‬.a) alizosimulia toka kwa Mtume SAW katika kuthibitisha Qadar hawapati hoja inayotilia nguvu kusihi kwa kauli yao, hoja yao huwatoka kwenye nafsi yake kwamba riwaya za Abu Huraira (ﷺ‬.a) hazijuzu kutolewa hoja, au mjinga achukuae Fiqhi na kuitafuta toka kwenye mwahala musimokua mwake, anaposikia habari za Abu Huraira katika zile zinapingana na madhehebu alioyapata na hadithi zake kwa kufuata bila ya hoja wala dalili na amesema Abu Huraira na kupinga Hadithi zake zinazokwenda kinyume na madhehebu yake-mpaka aliposema "Na baadhi ya vikundi hivi vilipinga Hadithi za Abu Huraira (ﷺ‬.a) wasizozielewa maana zake"[136]. Na inaonyesha wale aliowataja Imam Ibn Khuzaimah walikua waliowatangulia baadhi ya watu wa leo ambao wanakana baadhi ya Hadithi wasiozingatia usahihishwaji wa wenye elimu yake na kuzikubali, kwa kuwa tu hawakuzifahamu maana zake, au akili zao hazikuzikubali, bila ya kujituma kurejea kwenye kauli za maulamaa, na maelekezo yao kuhusiana na Hadithi hizo, lakini Imam Yahya bin Maaiin alikua makini pale aliposema "Muahammad bin Abdullah Answaariy alikuwa akifaliwa na uqadhi, akaambiwa Ewe Aba Zakaria hadithi? akasema

Vita vina wenyewe walioumbiwa

Na kwa maofisi ni wanamahesabu na wahazili.

MWISHO

Baada ya hayo kwa hakika imetubainikia katika utafiti huu wa haraka haraka wa maisha ya Abu Huraira (ﷺ‬.a) kwamba Yeye alikuwa na sifa zilizowazi zilizochangia katika kujenga heshima yake na kunyanyua hadhi yake na ueneaji wa elimu yake, na sifa hizo ni katika mambo kadha, muhimu yao ni

1-Kusilimu na ushuba wake na Mtume (SAW) kwa muda uliozidi miaka minne na kujifungamanisha nae katika muda wote huo, na kukusanya kwake kiwango kikubwa cha elimu na aina za uongofu na maarifa kwa fadhila ya kujifungamanisha kwake huko.

2-Mapenzi yake kwa Mtume wa Allah (S.A.W) na pupa lake la kumfuata na kumuiga, kimaneno, kimatendo na kitabia, hayo yalidhihiri toka kwake kwenye nyanja kadha za tabia na amali.

3-Ibada na uchaji wake, kukumbuka kwake sana mauti, woga wake wa siku ya Kiama na kujikinga kwake na Moto na yanayokaribisha kwenye Moto.

4-Unyenyekevu wake mkubwa, ukarimu wake, tabia zake njema, ibada zake, uwazi na mapenzi ya watu kwake.

5- Kueneza kwake elimu, kuelekeza umuhimu wa daawa katika dini, kuliko mpelekea awe mlinganiaji mzuri miongoni mwa masahaba katika wakati wa uhai wake Mtume (SAW) na baada ya mauti yake (SAW).

6-Wingi wa riwaya zake na kusihi kwake, umadhubuti wa hifadhi yake, na ukamilifu wa udhibiti wake.

7-Kuthibiti uadilifu na usuhuba kwake, hivyo hivyo uadilifu wa riwaya kiasi kwamba wamesimulia Masahaba wengi (ﷺ‬.a) toka kwake, na baadhi yao kusifu hifadhi na elimu yake, kama ambavyo wamesimulia toka kwake mamia ya Mataabiina kumsifu na kumkubali, vile vile akakubaliwa na waliokuja baada yao katika maulamaa wa Umma huu miongoni mwa wale ambao kauli zao zinakubalika na kutegemewa kwenye elimu hii.

8-Kutoelemea kokote kwenye tofauti zilizotokea katika siku zake baina ya Masahaba (ﷺ‬.a).

9-Mapenzi yake kwa Aalbait (ﷺ‬.a) na riwaya zake za nyingi za sifa zao na fadhila zao, na kutothibiti wao kutoridhika nae kama uzushi unavyoenezwa.

10-Kuthibitika ubatili wa anayotapakaziwa katika shubuhati za uzushi, na kubainisha sababu muhimu zilizojificha nyuma ya utapakazaji wa shubuha hizo na madai ya batili .

11-Baadhi ya wenye matamanio ya nafsi kuzua hadithi, kwa kutilia nguvu bidaa zao kwa upande mmoja, na kutia shaka kuhusiana na yeye na riwaya zake kwa upande mwengine, na hivyo ni kuwa kwake na khitilafu zilizo wazi kwa uhakika wa dini na mafunzo yake yenye kuangaza, nazo ni maarufu kwa wenye elimu hii.

Katika yaliyotangulia ni jumla yasifa njema za maisha yake (ﷺ‬.a) zinazotosheleza kutolea dalili juu ya utukufu wa cheo chake na ukubwa wa hadhi yake, na juu ya uharamu wa kumtukana au kumsema vibaya, au mwengine yeyote katika Masahaba (ﷺ‬.a), kutokana na kuwemo kwa kuwatendea maovu kwa, kutowafanyia mema, kutokana na juhudi zao njema katika kuunusuru Uislamu na Mtume wake (S.A.W), na kunukuu kwao elimu na kuwafikishia waliokuja baada yao, mpaka kutufikia sisi bila ya tabu na bila ya malipo.Kutokana na dalili za aya tukufu na Hadithi Tukufu zilizokuja katika ubainishaji wa fadhila zao, na zilizotahadharishwa kutukanwa na udhalilishaji wa usuhuba wao na Mtume (SAW), kwani ubora wa sahibu unatokana na ubora wa aliesuhubiwa. Ama katika ufikishaji huu kwa mwenye moyo au alietega sikio nae akiwepo, na Allah anasema Haki nae anaongoa njia na ndie mtoshelezaji wetu na msimamizi wetu alie bora.

KIAMBATISHI

Yaliyosemwa Kuhusiana na Abu Huraira Katika Mashairi

Kwa Sahaba

Mshairi mahiri Ustadh Mahmud Daliliy Aal Ja'afaril Hadithiy (Mmoja katika washairi wa kiislam wa Iraq )

Kwa ajili ya ujumbe wa uongofu wa kiislam alijizuwia

Na kutokana na utamu wa chem chem akanywa .

Moyo mtukufu hisia kali

Hima ya utukufu wa Wahyi anasifiwa.

Kwa kusonga mbele na woga wa Dini hii unamfunika.

Unaipandisha juu,unaimiliki,unaimiliki……..

(Abu Huraira) huyu ndie niliejua kwa sababu yake

Kupenda Sharia kwenye siri zake za dhamana.

Unaufata uongofu kwenye shauku na kwenye shida

Na akenda kwenye chem chem yake kufyonza

Moyo hukamatana na umpendae unamfata

Hiyo ndio siri roho inokuanayo

Yeyote anokwenda nyuma yaTaha mwendoni mwake

Basi mwendo wake hauna shaka wote unayo hadhi

Ulezi wa Ujumbe katika subra na ukakamavu

Huenda ikawa tabu kwa hayo anaesifu

Akawa anaidharau dunia na furaha zake

Kamwe raha kumhadaa wala tamaa

Ni katika nyota ziloangaza zing'arazo

Akapanda maisha na kwenye maisha hakuna tofauti

Kazi zake ziko wazi kwa wenye akili

Na kamwe mwenye chuki ubora hakiri

Naionea ajabu kaumu wamtusi

Matunda ya elimu toka kwake wachuma

Hamtukani ila alokodiwa asukumwae

Na roho ya ria, movuni aliezama

Ewe uliekunywa toka kwa msamehevu ulofungamana

Na mwendo uliosawa kwayo umelisha walokuja baadae

Umehami Qura-n kuihami kwelikweli

Na kila alotujia na tabia zilokengeuka.

Wamekuja wafanyia uadui Uislamu

Na siri (ya ulinganio wo) tumeshatambua.

Na wabomoaji wa jahazi lao ndio mwendo wetu

Na mwenye chuki huishia vitimbi vilokunjika.

Siasa mbaya mno fikira zinowachochea

Kiganja cha (mamluki) kamwe walotangulia haokoki

Unyenyekevu wa utukufu hatutowacha kwendelea kwa nyundo zetu

Twagonga na wasokua sisi wamesimama nyuma yetu

ABU HURAIRAH HISTORIA YA KUJIFAKHARISHA

MSHAIRI USTADH ABDIL JALIIL RASHIID

Nadona ukumbusho wako mdono wa ndege mafichoni

Na kuchukua mwongozo toka kwenye tarekhe yako nzuri

Nakumbuka kurasa zako njema huzikunjua

Kuangazia kwenye njia mazingatio na fikira.

Sura inang'aa na mwangaza wake kuenea

Wangapi wamevutika na uzuri wa sura

Nilizungumzia nafsi yangu kuhusiana nayo ikaishangaa

Nkasema Ewe nafsi hapa ndo pahala pa ibra

Na kuhusiana na Jihadi bendera za mipago zikanyanyuka

Hukunja tambarare na kunyanyua yalopatikana

Na walojitolea mhanga kwa mitihani kamwe hawakufanya ubakhili

Na toka kwenye kurasa umo mwenendo bora.

Natolea fidia nafsi yangu historia yao ilotangulia

Kwa makarama yasokumbukwa, ua jema

Nawe Ewe bwana wangu umendelea kukalia

Watulizana, wahifadhi kwenye mazingatio na hadhari

Hizi Hadithi wahifadhi na kukusanya

Uzuri ulioje ulopata toka kwenye athari bora

Umelinda hazina ya uongofu

Ukilinda vitimbi vibaya vya shari

Ulikua mlinzi zaidi kuliko mama juu ya mtoto

Na muhifadhi zaidi wa shamba na mjini

Umezingatia kila umakini katika kuzungumza nae

Na kila tendo toka kwake ni lenye kukimbiliwa

Allah kakuombea usisahau kheri zake

Vipi usahau nawe umthibiti wa habari

Ukarusha mshale ukampata mwenye chuki

Nawe kusimama kurejesha mishale mtoni

Ukasimama kilimani kwelekea nyuso zao

Ukiihami Sunna teule isipate madhara

Wakafanya uhudi za chuki kama kwamba

Mwenendo wao uko hasarani

limewachukiza kuona bendera za Sunna yetu zikipaa

Wakati riwaya zao zimeangamia.

Abu Huraira wa pekee katika tabia

Na mwenendo mlima ulopaa juu

Basi hivi vipaka vyake kwenye upole vyashuhudia

Na yamtoshea sifa ya upole kwenye paka

Hivyo ambae sirini upole kashuhurika

Kamwe uzushi haujulikani kwenye habari

Hivyo ambae sirini zuhudi kashuhurika

Kweli takua na haja kukusanya mamali?

Wangapi walodhihiri kisha Allah kavunja chuki zao

Basi kwani alivuna tunda zaidi ya kutengwa?

Kundi Allah alotutahini jambo lao leo hii

Hivyo tumche Allah kwa maisha ya baadae

Abu Huraira (ﷺ‬.a) historia yampamba

Marashi ya uongofu yamiminikia sasa

Hakuna ubaya kwa ubaya wake

Na sio ubaya kufichua alojificha

Kiza cha kufru hakifichi mwanga wa Sunna yetu

Kwani mwezi mdande wang'aa zaidi ya kiza totoro

NURU ZA SAHABA WA MUSTW'AFA

MSHAIRI USTADH SWALIH H'AYYAAWY

Lau ungesimulia hadithi zenye habari za

yazdajir leo ungekua mteule

Dhambi yako ilikua ipi ulipomzungumzia muulizaji wao

kuhusiana na uhakika mpaka kelele wakapiga

Na watu wakipenda kufuru huwatosha

Wakikataa chuki zao hubanwa na moto

Abu Huraira (ﷺ‬.a) historia wamzulia

Nahukumalizia mzushi ila kuwa nayo aibu

Na kwenye kiungo mshale umerushiwa kwa yale

alosimulia kwenye taa aibu imefikilia

Ewe Sahaba wa Mustwafa maneno na mashairi

yanokupa hadhi kwani jitihada ni ushujaa

Abu Huraira (ﷺ‬.a) lau wakati ungewarejea

munahadithi na hakuna pazia kwa watu

Kamwe hawasisalimishi kwa kauli wasoiafiki

Wala kufanyia ibada ila kwa ile ya walopita

Nani huyo mashakili kadha yalompata

Dan-dana zao na hamu ni dinari

Na mfano wake hudai elimu na maarifa

Njia kapotea na kupinga hakumsaidii

Kakutana na upotovu kwenye kauli

Kwa wenye ghafiliko kama elimu ni mzigo

Moto, chuki uwakop kwa mbebaji wake

Na madhehebu ya chuki kwamba watu wako huru

Dhamana ya Allah dhamana ni ya baba yenu vipi niwaone

huruma ukweli wa hadithi

Tafsirini mpendavyo chuki za matendo yao

Na waovu ta-a-wili imezidi kufuru za waovu

Ewe Sahaba wa Mustafa nuru zimekuzunguka

zafunika macho, macho maovu hayakuoni

Kauli yangu kamwe haifichui siri

Ilojificha na siri haikukuzunguka

Lakini mate natema kwenye

kufichua uzushi kwa jina utafiti

Shetani kawapambia uongo maandishi yao

Mtia sumu kwenye samli, ni mkhaini

Kamwe harejeikua uongo iswe kazi yao

madamu uongo mauzoni unabei

basi tonge ya rushwa ina kauli iza ta-a-wili

apendavyo mweyewe, rushwa inao wafanya biashara

Hivi ndivyo rizki kwenye hadhi chake mwanzo wake

Upondaji na kugonga heshima na kukana?



[1] -Al Bukhary 35/3 Kitaabu Fadhw'aailus Swa'haaah, na Muslim 185/7

[2] Al Bukhary 21/7, Muslim 188/7…………………….

[3] Ibn Maajah 189/8

[4] At Tirmidhiy katika As Sunan 350/5 na Al Hakim katika Mustadrak 506/3

[5]Al Hakim katika Mustadrak 507/3,Ibn Hajar katika Iswaba 202/4 na lbn Abdil Barr katika Al Istiia'ab ,Hamish ya Iswaba.205/4 na baada ya hapo.

[6] Al Hakim katika Mustadrak 508/3 na Adh Dhahabiy kwenye Siyar Aa'laam An Nubalaa 262-267,A Ibn Hajar katika Iswaaba 210/4, lbn Abdil Barr katika Al Istiiaab ,Hamish ya Iswaba.209-210/4. na A'qiiq ni umbali wa Meli kumi toka Madina,

[7] AlBukhariy 74/5.

[8] AlBukhariy katika Fat-h 225/6, Muslim Sherhun Nawawiy 42-43/1,na Ahmad 225/1

[9] Muslim Sherhun Nawawiy128/2

[10] AlBukhariy 248/4-Al Buyuu'u,Muslim Sherhun Nawawiy 52-56/16 Fadhwaailus Swahaabah, na matamshi ni ya Bukhaariy.

[11]Muslim Sherhun Nawawiy 51-92/16,Fadhwaailus Swahaabah,na Ibn H'ibbaan 142/8, na lafdhi ni ya Muslim.

[12] AlBukhariy 54/2na Muslim 158/2 na matamshi ni ya Bukhaariy

[13] Ahmad;Al Musnad 27/17,na muradi wa pambo ni nuru.

[14] Bukhariy 240/,

[15] Ahmad : Al Musnad 239 /15

[16] Adhdhahabiy As Siyar Aa'laam An Nubalaa 591-592/2, asili ya riwaya hii imo kwenye Bukhary 179-180/7. Kitaab:Ar Riqaaq , na As Suffa ni pahala alipopaandaa Mtume wa Allah (S.A.W) kwa ajili ya mafukara wa Kihajirina.

[17] na Al Haakim :Al Mustadrakm 513/3, Adhdhahabiy: As Siyar Aa'laam An Nubalaa 580 -585/2

[18] Adh Dhahabiy:Tadhkirat ul Huffaadh'36/1,na Ibn Hajar :Al Isw'aabah205/4

[19] Maalik :Al Muwattw'a na As Shaafi'i: AL Musnad36/3.

[20] Maalik :Al Muwattw'a 351-352/1

[21]Adhdhahabiy AsSiyar Aalaam An Nubalaa 606-607

[22] Adhdhahabiy AsSiyar Aalaam An Nubalaa 609/2

[23] Ahmmad :Al Musnad 260/ 16

[24] Ibni Kathiir:Al Bidaayah wa An Nihaaya 133/8

[25] Adhdhahabiy AsSiyar Aalaam An Nubalaa 611/2 na Ibni Kathiir:Al Bidaayah wa An Nihaaya 113/2

[26] Adhdhahabiy AsSiyar Aalaam An Nubalaa 610/2

[27] Adhdhahabiy AsSiyar Aalaam An Nubalaa 611/2

[28] Kitabu kilichotangulia620/2.

[29] Ibn Kathiir:Al Bidaaya wan Nihaayah 113/8

[30] Adhdhahabiy As Siyar Aalaam An Nubalaa 611/2 na Ibn Kathiir:Al Bidaaya wan Nihaayah 113/2

[31] Adhdhahabiy:Tadhkirul Huffaadh34/1 na huenda alikusudia kwa kauli yake imamu,kiongozi wa elimu na Fatwa.

[32] Adhdhahabiy:Tadhkirat ul Huffaadh'35/ na As Siyar Aalaam An Nubalaa 593/2, na Tw'affaawi:ni Sahaba katika watu wa As Suffa Nua'im :Al Hulyah 375/375.

[33] Adhdhahabiy; As Siyar Aalaam An Nubalaa 610/2.

[34] Ibn Saa'd:Twabaqaat 329/4, na Adhdhahabiy; As Siyar Aalaam An Nubalaa 592/2

[35] Ibn Isaad:Twabaqaat 329/4

[36] Muslim kwa sherhe ya Nawawiy 52/16

[37] IbnKathiir: Al Bidaaya 108/8.

[38] Takhriji yake imetangulia.

[39] Ahmad :Al Musnad111/16

[40] Ahmad :Al Musnad16/18

[41] Al Bukhaariy 205/6-Kitaabul Atw'imah.

[42] Ibni Saad:At Tw'abaqaat 337/4

[43] Abu Nuaim :Al H'ulyah 384/2 ;na Ibnil Jawziy:Swifatus Swaf-wah692/1

[44] Ibn Kathiir :Al Bidaayah114-115/8 Abu Nuaim :Al H'ulyah 384/2

[45] Abu Nuaim :Al H'ulyah 385/2

[46] Ibnil Jawziy:Swifatus Swafwah692/1

[47] Adhdhahabiy; As Siyar Aalaam An Nubalaa 625/2.

[48] Adhdhahabiy; As Siyar Aalaam An Nubalaa 629/2.

[49] Adhdhahabiy; As Siyar Aalaam An Nubalaa 632/2.

[50]Ibn Hajar :Al Iswaabah 205/4

[51] Imetangulia kwenye kusiimu na Usuhuba wake.

[52]At Tirmidhiy As Sunan 348/5 na Al Haakim :Al Mustadrakm 511/3,

[53] At Tirmidhiy As Sunan 348-349/5

[54] Al Haakim :Al Mustadrakm 513/3,

[55] Ibn Hajar :Al Iswaabah 208/4

[56] Adhdhahabiy:Tadhkirul Huffaadh36/1 na Ibn Hajar :Al Iswaabah 205/4

[57] Ibni Abdil Barr,Al-Istiiaaa'b kwa Haamish 208 -209/4

[58] Al Bukhaariy At Taariikh!/187.

[59] Adhdhahabiy:Tadhkirul Huffaadh34/1

[60] Al Haakim :Al Mustadrakm 512/3,

[61] Al Khatw'iib : Al Kifaayah 94.

[62] Al Khatw'iib : Al Kifaayah 94.

[63] Al Haakim :Al Mustadrakm 510/3, na aksema sanad yake ni sahihi , na kuwafikiwa na ad Dhahabiy.

[64] At Tirmidhiy As Sunan 348/5 na Al Haakim :Al Mustadrakm 511/3,kwa lafdhi na mjuzi wetu kwa masimulizi.

[65] Al Haakim :Al Mustadrakm 509/3,

[66]Al Haakim :ﷻ‬'luumil Hadiith 55,na As Suyuutw'y:Tadriibur Raawiy 46-48/1

[67] na Ahmad 133/13 na At Tirmidhiy As Sunan 304/2 na akasema ni Hasanun Swahiih.

[68] Ahmad 225/1 na At Tirmidhiy As Sunan 180/5 na Abu Daawud 2440.

[69] Ahmad 222/14

[70] Ahmad 5/4 na Abu Daawud 321/3

[71] Ahmad : Musnad147/8 na Hasn ni Al Baswary .

[72] Al Haakim :Al Mustadrakm 511/3,na akasema :Hadithi ni yenye Sanad Sahihi,na kuwafikiwa na Dhahabiy.

[73] Adhdhahabiy; As Siyar Aalaam An Nubalaa 599/2.

[74] Ahmad :Al Musnad107-108/1,na Ibni Maajah:As Sunan1326/2,na lafdhi ni ya Ahmad.

[75] Adhdhahabiy; As Siyar Aalaam An Nubalaa 586/2.

[76] Al Haythamy :majmaa'z Zawaaid 123-124/1

[77] Ahmad:al Musnad 125/19.

[78] Muslim Sherhun Nawawiy 64-66/7,na Ahmad:Al Musnad 72-73/20 na lafdhi ni ya Ahmad.

[79] Al Hakim;Musadrak98/3,na akasema:Hadithi ni yenye sanad sahihi,na akawafikiwa na Adhdhahabiy.

[80]Al Haakim :Al Mustadrakm 98/3,na akasema :Hadithi ni yenye Sanad Sahihi,na kuwafikiwa na Dhahabiy.

[81] Muslim121/7,Kitaabu Fadw'aails Swahaaba, na Ibn Hibbaan : as Swahih43/8,Na lafdhi ni ya Muslm.

[82] Ahmad:Al Musnad 133-134 /1.

[83] Ibn Hibaan:As Swahiih104/4.

[84] Aina ya tunda

[85] Bukhaary,Kitaabul Fadw'aa-lis Swahaabah.

[86] Ibn Hibaan:As Sunan138/5.

[87] Al Bukhaary216/2 manaaqibil Hasn na Hal Husain (ﷺ‬.a)

[88] Muslim 7/129, Ahmad:Al Musnad 128/14

[89] Ibn Hibaan:As Swahiih 56/8.

[90] Ahmad:Al Musnad 195 /14 na Ibn Hibbaan:As Swahiih 57/8.

[91] Al Haakim :AlMustadrak195/14 166/,nae akasema:Hadithi Swahih,na ameafikwa na Adhdhahabiy

[92] Al Haakim :AlMustadrak178/14,nae akasema:Hadithi Swahih na ameafikwa na Adhdhahabiy.

[93] Al Haakim :Al Mustadrakm 112/3

[94] Imetangulia kwenye kuslimu na usuhuba wake.

[95] Al Khatw'iib:AlKifaayah548 na Suyuutw'y:Miftaahul Jannah 22';

[96] Al Haakim :AlMustadrak 511-512/3,nae akasema:Hadithi Swahih.

[97] Takhriji yake imetanguliakwenye Riwaya na Hifadhi yake.

[98] Ahmad :Al Musnad 35-36/17, na Al Bukhariy katika Fat-h 193/1 na lafdhi ni ya Ahmad.

[99] Al Haakim :AlMustadrak 508/3.

[100] Ahmad :Al Musnad 35-36/17, na Al Bukhariy katika Fat-h 193/1 na lafdhi ni ya Ahmad.

85Al Haakim :AlMustadrak510/3

[101] Al Haakim :AlMustadrak 512-513/3

[103]Adhdhahabiy:Tadhkirul Huffaadh36/1 na Ibn Hajar :Al Iswaabah 205/4

[104] Mustarakul Haakim 513/3

[105] Ahmad :Al Musnad 121/19, 597/2. Al Haakim :Al Mustadrakm 509/3,na akasema :Hadithi ni yenye Sanad Sahihi,na kuwafikiwa na Dhahabiy.

[106] Al Haakim :AlMustadrak 511-512/3,nae akasema:Hadithi Swahih.

[107] Al Haakim :Al Mustadrakm 511-512/3,

[108] AlBukhariy 248/4-AlBuyuu'u,Muslim Sherhun Nawawiy 52-56/16 Fadhwaailus Swahaabah, na matamshi ni ya Bukhaariy.

[109] Al –Bukhaary 74/5.

[110] Abu Nua'aim :Al Hulyah379/1, na Ibni Kathiir:Al Bidaayah wa An Nihaayah 107/8.

[111]Adhdhahabiy; As Siyar Aa'laam An Nubalaa 592/2

[112] Adhdhahabiy AsSiyar Aalaam An Nubalaa 592/2 ,asili ya riwaya hii imo kwenye Bukhary 179-180/7. Kitaab:AR riqaaq , na As Suffa ni pahala alipopaandaa M kwa ajili ya mafukara wa Kihajirina.

[113] Al Bukhaary181/7

[114] Abu Nuai'am : Al Hilyah 93/1

[115] Abu Nuai'am : Al Hilyah 93/1

[116] Ibni Kathiir:Al Bidaayah wa An Nihaayah 113/8.

[117] Abu Nuai'am : Al Hilyah 381/1 na Adhdhahabiy; As Siyar Aalaam An Nubalaa594.

[118] Ai Bukhaariy:192-193,Kitaabul I'lm.

[119] 597/2. Al Haakim :Al Mustadrakm 509/3,na akasema :Hadithi ni yenye Sanad Sahihi,na kuwafikiwa na Dhahabiy.

[120] Adhdhahabiy; As Siyar Aalaam An Nubalaa

[121] Ibn Kathiir:Al Bidaayah wa An Nihaayah109/8.

[122] Muslim Sherh An Nnawawiy232/1

[123] Muslim Sherh An Nnawawiy 229/1

[124] Nawawiy: Sherh Muslim 229/1

[125] Ibn Kathiir:Al Bidaayah wa An Nihaayah79/8 na Al Iswaabah 33/2

[126] Al bukhaary 199/1,Kitaabul I'lmi.

[127] Muslim :al Muqaddimah Bisharhin Nawawiy76/1

[128] Adhdhahabiy; As Siyar Aalaam An Nubalaa 612/2.

[129] Ibn Kathiir:Al Bidaayah wa An Nihaayah79/8 na Al Iswaabah 33/2

[130] Ibn Kathiir:Al Bidaayah wa An Nihaayah79/8 na Al Iswaabah 33/2

[131] Al Iswaabah 32/3

[132] At Tirmidhiy: As Sunan

[133] Adhdhahabiy; As Siyar Aalaam An Nubalaa 605/2.

[134] Adhdhahabiy; As Siyar Aalaam An Nubalaa 610-611/2.

[135] Al Khatw'iib : Al Kifaayah 133.

[136] Al Haakim :Al Mustadrakm 519/3.