×
Uislamu ni Dini ya Mola Mlezi wa viumbe

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Uislamu ni Dini ya Mola Mlezi wa viumbe

Nani Mola wako?

Hili ni swali zito katika maswali yote: Nalo ni swali muhimu, ni lazima kwa kila mtu kufahamu majibu yake.

Mola wetu Mlezi ni Yule aliyeziumba Mbingu na Ardhi, na akateremsha kutoka mawinguni maji kisha akaotesha kutokana na maji hayo matunda na miti ikiwa ni chakula kwetu sisi na kwa ajili ya wanyama tunaowatumia kama chakula,na ni Yeye ambaye amewaumba baba zetu, na akaumba kila kitu, na ni Yeye aliyeuweka usiku na mchana, na ni Yeye pia aliyeuweka usiku kuwa wakati wa kulala na kupumzika, na mchana kuwa ni wakati wa kutafuta chakula na maisha,na ni Yeye aliyetudhalilishia jua na mwezi na nyota na bahari, na akatudhalilishia wanyama tunaowala na tunaofaidika kutokana na maziwa yao na sufi zao.

Ni zipi sifa za Mola Mlezi wa viumbe?

Mola Mlezi ni yule aliyeumba viumbe, na ni Yeye anayewaongoza kwenye ukweli na uongofu, na ni Yeye anayeendesha mambo ya viumbe wote, na ni Yeye anayewapa riziki, na Yeye ni Mmiliki wa kila kitu kilichopo ndani ya maisha haya ya dunia na akhera, na kila kitu Yeye ndiye mmiliki wake na kisicho kuwa Yeye basi ni chenye kumilikiwa na Allah,na Yeye yupo hai ambaye hafi wala halali, na Yeye ndiye msimamiaji wa mambo yote ya wanadam ambaye kasimamia kila kilicho hai kwa amri yake, na ni Yeye ambaye rehema zake zimeenea kila kitu, na ni Yeye ambaye hakijifichi juu yake chochote ndani ya ardhi au mbinguni.Hakuna chochote cha kufananishwa naye na Yeye ni Msikivu Mjuzi, naye yupo juu ya mbingu zake Aliye jitosheleza kutohitajia msaada kwa viumbe wake, na viumbe ndio wenye kuhitajia kwake, haingii ndani ya kiumbe chake, na wala hakuna kitu katika viumbe wake kinachoweza kuingia ndani ya Dhati yake Aliyetakasika na Kutukuka,Mola Mlezi ndiye aliyeumba ulimwengu huu unaoonekana, kwa kila upangikaji wake unaolingana ambao hautofautiani, sawa sawa uwe ni mfumo wa mwili wa binadamu au mnyama, au mfumo wa dunia inayotuzunguka kwa jua lake na nyota zake na vingine vyote vinavyo ipamba dunia

Na kila kinacho abudiwa kinyume na Yeye Allah basi chenyewe hakiwezi kujipa manufaa au kujizuilia kupatwa na madhara, inawezekanaje kimiliki uwezo wa kumpa manufaa anayekiabudu, au kumuondoshea madhara.

Ni ipi haki ya Mola Mlezi kwetu sisi?

Hakika haki yake kwa watu wote wamuabudu peke yake na wasimshirikishe na chochote, na wala wasiabudu pamoja naye kiumbe au jiwe au mto au kisichokuwa na hisia, au nyota au kitu chochote kile, isipokuwa waifanye ibada ni mahususi kwa ajili ya Mola Mlezi wa viumbe.

Ni zipi haki za waja kwa Mola wao?

Hakika haki ya waja kwa Allah watakapo muabudu awape maisha mazuri ambayo watapata ndani yake utulivu na amani na kusalimika na ziada ya utulivu na kuridhia, na siku ya Kiyama awaingize ndani ya peponi na ndani yake kukiwa na neema za kudumu na kubakia milele, na wakimuasi na wakaenda kinyume na amri zake ayafanye maisha yao kuwa ya uovu na ubaya hata kama watadhani kuwa wao ni wema na wana utulivu, na siku ya Kiyama awaingize motoni wasitoke humo, na humo watakuwa na adhabu za milele, na kuishi moja kwa moja.

Ni yapi makusudio ya uwepo wetu? Na kwa nini tumeumbwa?

Hakika Mola Mtukufu ametueleza kuwa Yeye ametuumba kwa makusudio matukufu, nayo ni kumuabudu peke yake, na tusimshirikishe na chochote, na akatukalifisha kuimarisha dunia kwa mambo ya heri na yanayofaa, na atakaye abudu asiyekuwa Mola wake na Muumba wake huyo atakuwa hajatambua kazi aliyokalifishwa kuifanya.

Vipi tumuabudu Mola wetu?

Hakika Mola Aliyetukuka na Kutakasika hakutuumba kwa mchezo mchezo, na hakujalia maisha yetu kuwa ni upuuzi, isipokuwa amewachagua miongoni mwa viumbe kuwa mitume kwa watu wao, nao ni watu waliokamilika kimaumbile, na wenye nafsi zilizotakasika, na wenye mioyo iliyotakasika, na akateremsha juu yao ujumbe wake, na akaambatanisha ndani yake kila kilichokuwa ni lazima kwa watu kukitambua kunako Mola Mlezi Aliyetakasika, na namna watu watakavyo fufuliwa siku ya Kiyama nayo ni siku ya hesabu na malipo,na mitume waliwafikishia watu wao namna watakavyo muabudu Mola wao, na wakawabainishia namna ibada zilivyo na nyakati zake na malipo yake duniani na Akhera, na wakawatahadharisha na walivyo haramishiwa na Mola wao juu yao miongoni mwa vyakula na vinywaji na ndoa, na wakawaongoza katika tabia njema, na wakawakataza tabia mbaya.

Ni dini gani inayokubalika kwa Mola Mlezi Aliye Mtukufu?

Dini inayokubalika kwa Mola Mlezi ni Uislamu, nao ndio dini aliyowafikishia manabii wote, na Allah hakubali siku ya Kiyama dini isiyokuwa Uislamu, na kila dini waliyojivisha watu isiyokuwa Uislamu ni dini batili, na haina manufaa kwa mwenye kuwa nayo, isipokuwa anakuwa ni muovu duniani na Akhera.

Ni ipi misingi ya dini hii ya (Uislamu) na nguzo zake?

Dini hii aliyoifanya Allah kuwa nyepesi kwa waja wake, nguzo yake kubwa ni kumuamini Allah Mola Mwenye Uungu, na kuamini Malaika wake na vitabu vyake, na mitume wake na siku ya mwisho na kuamini makadirio, na ukubali ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah nakuwa Muhammadi ni mtume wa Allah, na usimamishe swala na utoe zaka kama utakuwa na mali ambazo zitakuwa ni lazima kutoa, na ufunge mwezi wa ramadhani nao ni mwezi mmoja ndani ya mwaka, na uitembelee nyumba (Makka) kwa ajili ya Allah nyumba kongwe ambayo ilijengwa na Ibrahim amani iwe juu yake kwa amri ya Mola wake, ikiwa njia ya kufanya hilo kwako ni jepesi.Na ujiweke mbali na uliyoharamishiwa na Allah juu yako, miongoni mwa hayo ni ushirikina, na kuuwa nafsi, na kuzini, na kula mali za haramu, na utakapomuamini Allah na ukafanya ibada hizi na ukajiweka mbali na mambo haya ya haramu wewe ni muislamu hapa duniani, na siku ya Kiyama Allah atakupa neema za kudumu na kuishi milele peponi.

Je Uislamu ni dini ya watu fulani au jinsia fulani?

Uislamu ni dini ya Mwenyezi Mungu kwa watu wote, hakuna ubora kwa yeyote juu ya mtu mwingine isipokuwa kwa kumcha Allah na kufanya matendo mazuri, na watu wote ni sawa.

Vipi watu watafahamu ukweli wa Mitume amani iwe juu yao?

Watu watafahamu ukweli wa Mitume kwa njia tofauti tofauti miongoni mwa hizo ni:

Yale wanayokuja nayo katika ukweli na uongofu yanakubaliwa na akili na maumbile yaliyo salama, na yanatolewa ushahidi na akili kwa uzuri wake, na asije yeyote na kitu tofauti na walichokujanacho Mitume.

Yale waliyokujanayo Mitume yanafaa kwa dini za watu na dunia yao, na kusimama sawa sawa kwa mambo yao na kujenga maendeleo yao na kuhifadhi dini zao na akili zao na mali zao na heshima zao.

Hakika Mitume amani iwe juu yao hawatafuti kutoka kwa watu ujira kwa kuwajulisha heri na uongofu, isipokuwa wanasubiri malipo kutoka kwa Mola wao.

Hakika waliyokuja nayo Mitume ni ukweli na yakini isiyo changanyika na shaka, wala haupingani wala haugongani, na kila nabii aliwakubali Manabii waliotangulia na akawaita watu kwenye mfano wa yale waliyowaita watu.

Hakika Allah anawapa nguvu Mitume amani iwe juu yao kwa alama za wazi na miujiza yenye ushindi ambayo Allah anaipitisha kupitia mikono yao; Ili iwe ni ushahidi na ukweli kuwa wao ni Mitume kutoka kwa Allah, na muujiza mkubwa wa Manabii ni muujiza wa Mtume wa mwisho Muhammad rehema na amani ziwe juu yake, nao ni Qur'ani Tukufu.

Qur'ani Tukufu ni nini?

Qur'ani Tukufu ni kitabu cha Mola Mlezi wa viumbe, nayo ni maneno ya Allah, aliyateremsha Malaika Jibril amani iwe juu yake kwenda kwa Mtume Muhammad, na ndani yake kuna kila kitu alichokiwajibisha Allah kwa watu kukitambua kuhusu Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho na kuamini makadirio heri zake na shari zake,na ndani yake kuna ibada za lazima, na makatazo ambayo ni lazima kujiweka nayo mbali, na tabia njema na zilizo katazwa, na kila kinachofungamana na mambo ya watu na dunia yao, nacho ni kitabu na muujiza, Allah aliwatahini watu walete mfano wa hiyo Qur'ani, nayo imehifadhiwa mpaka siku ya Kiyama kwa lugha ya kiarabu ambayo Qur'ani iliteremka kwa lugha hiyo na hakuna hata herufi moja iliyopungua, na hakuna hata neno moja lililopungua.

Ni upi ushahidi wa kufufuliwa na kuhesabiwa?

Hivi huoni ardhi ilivyokuwa kame hakuna ndani yake uhai basi yanapoteremka juu yake maji inasisimka na kututumka na kumea kila namna ya mimea mizuri, hakika aliyeipa uhai ardhi hii ni muweza wa kukipa uhai kitu kilicho kufa,hakika yule aliyemuumba mwanadam kutokana na manii yatokanayo na maji madhaifu ni muweza wa kumfufua siku ya Kiyama kisha amuhesabu na amlipe malipo yatoshayo ikiwa heri atalipwa heri na ikiwa shari atalipwa shari,hakika yule aliyeumba mbingu na ardhi na nyota ni muweza wa kumrejesha mwanadam; hakika kurejesha umbo la mwanadam mara ya pili kuna wepesi zaidi kuliko uumbaji wa mbingu na ardhi.

Siku ya Kiyama kutakuwa na nini?

Mola Mlezi atawafufua viumbe kutoka kwenye makaburi yao, kisha atawahesabu kwa matendo yao, basi yule atakaye amini na akawakubali Mitume Allah atamuingiza peponi, ambayo ndiyo neema ya kudumu ambayo haijawahi kupita katika mawazo ya mwanadam kutokana na ukubwa wake, na atakayepinga Allah atamuingiza motoni, moto ambao adhabu zake ni za milele hakuna mwanadam anaweza kuzifikiria uhalisia wake jinsi zilivyo, na mwanadam anapoingia peponi au motoni basi hatokufa, ataishi milele na atadumu ndani ya neema au adhabu.

Atakapotaka mtu kuingia ndani ya Uislamu nini afanye, na je kuna maandalizi ya lazima ayafanye, au kuna watu lazima wampe idhini?

Mtu anapotambua kuwa dini ya kweli ni Uislamu, na kuwa Uislamu ndio dini ya Mola Mlezi wa viumbe, basi ni lazima kwake afanye haraka kuingia ndani ya Uislamu, kwakuwa akili inapobainikiwa na ukweli ni lazima aifanyie haraka, na asilicheleweshe jambo hili,na atakayetaka kuingia ndani ya Uislamu si lazima kwake kufanya maandalizi maalumu, na si lazima awe karibu na yeyote miongoni mwa viumbe, lakini kama itakuwa kuna uwepo wa muislamu au katika kituo cha kiislamu hilo ni bora zaidi, na kama si hivyo yamtosha kusema: (Nina kiri kwa moyo na ninatamka kwa ulimi kuwa: Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu) aseme hayo akiwa anajua maana yake na kwa kuyaamini, na kwa kufanya hivyo atakuwa ni muislamu: Kisha ajifunze yaliyobakia miongoni mwa sheria za Uislamu kidogo kidogo: Ili aweze kusimamisha yale aliyowajibishiwa na Mwenyezi Mungu juu yake.

Uislamu ni Dini ya Mola Mlezi wa viumbe

Nani Mola wako?

Ni zipi sifa za Mola Mlezi wa viumbe?

Ni ipi haki ya Mola Mlezi kwetu sisi?

Ni zipi haki za waja kwa Mola wao?

Ni yapi makusudio ya uwepo wetu? Na kwa nini tumeumbwa?

Vipi tumuabudu Mola wetu?

Ni dini gani inayokubalika kwa Mola Mlezi Aliye Mtukufu?

Ni ipi misingi ya dini hii ya (Uislamu) na nguzo zake?

Je Uislamu ni dini ya watu fulani au jinsia fulani?

Vipi watu watafahamu ukweli wa Mitume amani iwe juu yao?

Qur'ani Tukufu ni nini?

Ni upi ushahidi wa kufufuliwa na kuhesabiwa?

Siku ya Kiyama kutakuwa na nini?

Atakapotaka mtu kuingia ndani ya Uislamu nini afanye, na je kuna maandalizi ya lazima ayafanye, au kuna watu lazima wampe idhini?